Tecno mpya za Camon 2022 zinaweza kuwa ni simu za Tekno zinazoweza kushindana na matoleo mengi ya Android daraja la kati
Mfano simu ya Tecno Camon 19 Pro ina sifa nzuri upande wa kamera na utendaji kama ilivyo Tecno Camon 19 Pro 5G
Kitu kinachofanya bei ya Camon 19 Pro kuwa zaidi ya laki sita
Japokuwa kuna vitu vya msingi vinavyoweza kuifanya simu isiwe shindani
Hii inatokana na bei na sifa zake kupatikana kwa baadhi ya simu ambazo zinauzwa bei sawa na Camon 19 Pro
Bei ya Tecno Camon 19 Pro ya GB 256
Simu inauzwa kwa bei ya shilingi laki sita na nusu (650,000/=) kwa maduka ya Kariakoo
Uwezekano wa kuipata chini ya hapo pia upo
Ila sifa za hii simu kwenye display (kioo) ina ukakasi kwa kuzingatia bei
Baadhi ya simu zinazoendana bei hututmia vioo vya amoled
Ukitizama sifa zake kwenye jedwari utagunduoa jinsi camon 19 inavyoachwa nyuma na simu ya Realme 9 Pro
Japo Realme 9 Pro ina memori NDOGO ila bei hazitofautiani sana
Sifa za Tecno Camon 19 Pro
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | IPS LCD, Refresh rate:120Hz |
Softawre |
|
Memori | 256GB,128GB na RAM 8GB |
Kamera | Kamera TATU
|
Muundo | Urefu-6.8inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 650,000/= |
Ni upi ubora wa simu ya Tecno Camon 19 Pro
Tecno Camon 19 Pro ina mfumo mzuri wa kamera ambao unaifanya simu kurekodi na kupiga picha vizuri
Inakuja na memori kubwa inayoweza kuhifadhi vitu vya kutosha
Ina chaji inayojaza simu kwa dakika chache
Betri yake inaweza kukaa na chaji masaa mengi
Ina kioo kizuri kwa kucheza gemu kwa sababu ya kuwa na refresh rate kubwa
Hata RAM pia ni kubwa kitu kinachohitajika kwenye simu nyingi za android
Kwenye vipengele vya Network mpaka Software kuna ubora na kasoro kadhaa pia
Fuatilia uvifahamu kiundani.
Uwezo wa Network
Camon 19 Pro ni simu ya 4G
Na 4G inayotumia ni LTE Cat 13
LTE Cat 13 ina spidi ya kudownload inayofikia 390Mbps
Kwa maana kama simu inadownload kitu cha ukubwa wa 960MB basi simu itadownload kwa sekunde ishirini
Spidi hii ingewezekana kama unatumia mtandao wa USA kama AT& T
Spidi ya AT&T kwa USA inafika 280Mbps
Lakini kwa Tanzania bado mitandao ya simu ina spidi ndogo
Camon 19 Pro haina mtandao wa 5G
Japokuwa kwa 5G bado haijatua nchini ila serikali imeshaanza taritibu za kuweka mtandao huo
Unaweza pitia hii habari: Vibali vya 5G
Ubora wa kioo cha Tecno Camon 19 Pro
Kwa kuangilia resolution, kioo cha Tecno Camon 19 Pro kinaoonyesha vitu vizuri
Hii inachangiwa na simu kuwa resolution kubwa ya 1080 x 2460 pixels
Uwepo wa refresh rate inayofikia 120Hz kunaoongeza ulaini(smoothness) wa kioo kuonyesha vitu kwa ustadi
Kwa maana kama unaperuzi sehemu inayooleza picha zilizopo kwenye simu basi ukiwa unatachi kwa kupekeleka kidole juu picha zinakuwa zinabadirika haraka na wepesi
Refresh rate kubwa huwa inatumia umeme mwingi wa betri
Lakini hii simu ina betri kubwa hivyo inaweza isiwe tatizo
Kwa bahati mbaya Tecno Camon 19 Pro ina kioo cha IPS LCD na sio LTPO Amoled
LTPO Amoled inajua ni mazingira yapi ya kutumia refresh rate ya 120Hz
Na mazingira yapi ya kutumia refresh rate ya kawaida yaani 60Hz
Nguvu ya processor Mediatek Helio G96
Camon 19 Pro inatumia chip ya mediaatek helio g96 katika kufanya kazi zote za simu inazofanya
Ni processor ya simu daraja la kati hivyo utendaji wake ni wa kuridhisha
Hii ni processor inayoweza kucheza gemu kubwa kama Genshin Impact kwa spidi ya 23fps kwenye resolution ndogo
App ya geekbench inayopima nguvu za processor inaipa Helio G96 alama 540
Hivyo uwezo wa Camon 19 Pro kiutendaji unaendana na Redmi Note 10 kwa kiasi kikubwa
Nguvu kubwa ya processor inatokana na chip kutumia muundo wa Cortex A76 kwenye core kubwa
Cortex A76 huwa inaweza kufanya kazi nne kwa kila mzunguko kwa sekunde moja
Kumbuka Spidi ya core kubwa ni 2.05GHz(mizunguko bilioni 2.05)
Uwezo wa betri na chaji
Simu ina betri aina ya Li-Po yenye ukubwa wa 5000mAh
Kuifahamu li-po pitia: ufafanuzi wa betri aina ya lipo kwa sisi hapa sio wanakemia hatuwezi kuielezea kiundani tofauti ya Li-Ion na Li-Po
Simu nyingi zenye betri za 5000mAh zinakaa na chaji masaa yanayozidi 14 simu ikiwa kwenye intaneti
Chaji ya simu ikiwa inapeleka umeme mdogo betri lazima ichelewe kujaa ikizangatiwa ni kubwa
Lakini Tecno Camon 19 Pro chaji yake inapeleka umeme wa wati 33.
Huu ni umeme unaoweza jaza simu ndani ya dakika 65
Kama ukiwa una haraka inakuhitaji dakika chache tu simu kujaa
Waya wake wa chaji ni ule wenye kichwa kipana hujulikana kama USB Type-C 2.0 na sio ule mdogo (micro usb)
Ukubwa na aina ya memori
Camon ina matoleo ya aina mbili upande wa memori
Kuna ya ukubwa GB 128 na GB 256
Haifahamiki kama ni memori za UFS au eMMC
Ila kama ni UFS itakuwa nzuri zaid kwani zina kasi kubwa ya kusafirisha data
Kwneye RAM zipo za aina moja pekee ambazo ni GB 8
RAM ikiwa kubwa inaipa simu nafasi ya kuweza kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja
Uimara wa bodi ya Tecno Camon 19 Pro
Simu ina bodi ya plastiki na haijatumia vioo vya gorilla
Uzito wa simu ni gramu 204 (Na kazito kidogo)
Camon hii haina viwango vinavyoonyesha uwezo wa simu kuzuia maji na vumbi
Hivyo ni muhimu kununua kava ya simu na screen protekta
Itasaidia simu kutoka kwenye mikwaruzo na kupasuka pindi inapodondoka
Ubora wa kamera
Tecno Camon 19 Pro ni tecno macho matatu
Kwa maana ina kamera kubwa (wide) yenye resolution ya 64MP
Kuna kamera kwa ajili ya kupiga vitu vilivyopo mbali , hii huitwa telephoto na ina megapixel 50MP
Na kamera nyingine ni depth yenye 2MP ambayo hutumika kupiga mahesabu kujua kitu kinachostahili kutokeo kwa sehemu kubwa kwenye picha
Ndio kamera inayotumika kutengeneza ukungu kwa nyuma ya kitu kinachopigwa picha (hufahamika kama bokeh effect)
Kamera zake zimeboreshwa na uwepo wa OIS, PDAF na Laser AF bila kusahau HDR
Pitia: Jinsi ya kujua kamera nzuri ya simu ili ufahamu umuhimu wa hivyo viyu vilvyotaja
Tecno Camon ya 19 Pro inaweza kurekodi video za full hd pekee
Ubora wa Software
Tecno Camon 19 Pro inakuja na Android toleo la 12 na mfumo wa HIOS 8.1
HIOS 8.1 ina mpangalio muziri wa setting ambao unamrahishia mtu kufikia kile anachokitafuta
Na pia kwenye mpangilio wa phonebook una muonekano unaovutia macho
HIOS 8.1 ina applikesheni unayoweza kuitumia kuficha baadhi ya app ambazo hutaki watu wengine wazitumie
Yapi Madhaifu ya Tecno Camon 19 Pro
Udhaifu wa kwanza ni simu kutumia kioo cha IPS LCD na sio AMOLED
AMOLED ni vioo vinavyoweza kuonyesha rangi nyingi
Kitu kinachofanya vitu kuonekana kwa rangi zake halisi kwa asilimia kubwa ukilinganisha na LCD
Kamera yake haiwezi kurekodi video za 4k ambazo huwa zina resolution kubwa
Utendaji wa processor ni wa wastani na unazidiwa na processor ya Snapdragon 695 5G
Ikizingatiwa simu zenye Snapdragon 695 5G zina bei sawa na Camon 19 Pro
Kioo chake hakina HDR10 wala Doldy Vision ambazo huboresha muonekano wa vitu
Neno la Mwisho
Tecno kwa miaka ya karibuni wamekuwa wakitoa simu nzuri ikiwemo hii inayozungumziwa hapa
Kitu kinachoweza kufanya mtu kusita kununua simu hii ni bei
Mfano, bei ya tecno camon 19 pro na pro 5g zinaweza nunua simu za Realme 9 Pro au Redmi Note 11 Pro 5G
Realme 9 Pro na Redmi Note 11 Pro 5G zinatumia chip ya Snapdragon 695 5g
Snapdragon 695 5g inaiacha pakubwa kiutendaji chip Helio G96 iliyomo kwenye camon 19 pro
Ila kiujumla, Tecno Camon 19 Pro ni moja ya simu bora ya daraja la kati kwa mwaka 2022
Wazo moja kuhusu “Bei ya Simu ya Tecno Camon 19 Pro na Sifa Muhimu”
Nahitaji simu zenye ubora zaidi