Simu ya Samsung Galaxy Note 20 Ultra ni samsung ya mwaka 2020
Japo ina miaka ipatayo mitatu tangu itoke ila ni moja samsung kali mpaka wakati huu wa sasa
Bei ya Samsung Galaxy Note 20 Ultra 5G kwa sasa inazidi milioni ikiwa used
Kwa Tanzania kuna changamoto ya kuipata ikiwa mpya, nyingi ni used
Hata hivyo utofauti wa bei yake unategemea na ukubwa wa memori
Bei ya Samsung Galaxy Note 20 Ultra 5G ya GB 128
Kwa sasa hapa Tanzania simu hii inapatakana kwa kiasi cha shilingi 1,200,00 yaani milioni moja na laki mbili
Hii ni bei ya note 20 ultra ambayo imetumika bila kujali imetumika wapi
Kama utalinganisha galaxy note 20 ultra na matoleo mapya ya daraja la kati utaona kuwa note inaziacha kwa kiwango kikubwa
Ikiwemo yale matoleo ya samsung a54 au samsung a14, bado samsung note 20 ultra ni kiboko
Na wala haishangazi bei yake kuendelea kuwa kubwa hata kwa miaka itakayofuata
Sifa za Samsung Galaxy Note 20 Ultra 5G
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g and 5g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | Dynamic AMOLED 2X, Refresh rate:120Hz |
Softawre |
|
Memori | UFS 3.0,256GB,128GB,512GB na RAM 8GB,12GB |
Kamera | Kamera tatu
|
Muundo | Urefu-6.9inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 1,200,000/= |
Upi ubora wa Samsung Galaxy Note 20 Ultra 5G
Ina utendaji mkubwa kutokana na kutumia chip yenye nguvu kubwa
Inakuja na kioo chenye uoneshaji wa kiwango kikubwa cha rangi
Memori yake ina kasi kubwa ya kusafirisha data
Ni simu ndefu inayoweza kuonyesha vitu kwa upana mzuri na kuonekana kwa ustadi
Betri yake ni kubwa
Kamera yake inatoa picha vizuri hata kwenye mazingira yenye mwanga mdogo
Ni simu inayiosapoti 4G zenye kasi kubwa ya kupakuwa vitu
Uwezo wa Network
Galaxy Note 20 5G inasapoti mitandao yote ikiwemo 5G kama jina lake linavyojieleza
Kwenye upande wa 5G inasapoti masafa yote matatu kwa maana masafa ya kati, mafupi na marefu
Na pia inakubali 5g za NSA na SA, NSA ni 5G ambayo hutumia miundombinu ya 4G
Aina ya 4G simu inayotumia ni LTE Cat 24 yenye kasi inayofika 7350Mbps kwenye kudownload
Ni kasi kubwa ambayo huwezi kuipata kwenye mitandao ya 4G kwa hapa Tanzania
Kwa sasa 5G inapatikana kwenye mitandao ya Airtel, Vodacom na Tigo kwa baadhi ya maeneo ya Dar Es Salaam
Hivyo ukiwa kwenye eneo zuri stahiki utaweza kutumia mtandao huu wenye kasi zaidi
Ubora wa kioo cha Samsung Galaxy Note 20 Ultra 5G
Kioo cha samsung galaxy note 20 ultra 5G ni aina ya Amoled 2X ambavyo hutengenezwa na samsung wenyewe
Kioo cha hii simu kina resolution ya 1440 x 3088 pixels ambayo ni kubwa
Ufanisi katika kuonyesha vitu vizuri unachangiwa na uwepo HDR10+
HDR10+ inaongeza kiwango cha rangi hivyo kioo kuwa na uwezo wa kuonyesha vitu kwa rangi zinazoendana na uhaisia kwa kiwangio cha juu
Pia ina refresh rate inayofika 120Hz kitu kinachofanya kuperuzi kuwa ni kuzuri
Kuifupi, ubora wa kioo cha samsung ni mkubwa
Kama kioo kikiharibika inabidi uwe tayari kuingia gharama kupata kioo orijino
Maana bei ya kioo cha samsung note 20 ultra 5g ni kubwa
Nguvu ya processor Exynos 990
Samsung Galaxy Note 20 Ultra 5g inatumia processor ya Exynos 990 kufanya kazi zake
Hii ni chip ambayo imegawanyika katika sehemu tatu huku sehemu zenye nguvu kubwa sana zikiwa zinatumia muundo wa Mongoose M5
Mongoose M5 huweza kuchakata kazi sita kwa wakati mmoja kwa kila mzunguko
Na mizunguko ya hii core ni 2.7GHz(yaani mizunguko bilioni mbili nukta saba)
Ndio maana app inayopima ubora wa processor iitwayo Geekbench inaipa exynoss 990 alama 900
Na pia uchezaji wa magemu ni mzuri kutokana na aina hii ya utendaji
Kwa mfano gemu ya armajet 2020 inacheza kwa kiwango cha 60fps, yaani muonekano wa gemu unakuwa mzuri bila kuganda ganda
Wakati huo samsung a54 ya mwaka 2023 inacheza gemu ya pubg mobile kwa kiwango cha 36fps huku galaxy note 20 ni 30fps
Hii inamaanisha Samsung Galaxy Note 20 Ultra 5G ina nguvu kubwa ya utendaji
Uwezo wa betri na chaji
Betri ya hii simu ina ukubwa wa 4500mAh
Kutoka gsmarena, ni kuwa simu inadumu masaa 11 ikiwa ipo kwenye intaneti muda wote na refresh rate ikiwa 120Hz
Ila kama refresh rate umeiseti kuwa ndogo betri hutunza chaji mpaka masaa 13
Sio kiwango kikubwa sana ukilinganisha na simu zenye mabetri ya ukubwa wa 5000mAh
Ila ni muda unaoweza kutumia kufanya vitu hata ukiwa mbali na maeneo yenye umeme
Uzuri chaji inapeleka umeme mwingi wa kiwango cha wati 25
Hii chaji inaweza kujaza betri kwa kiwango cha 48% kwa muda wa nusu saa
Hivyo ndani ya dakika 80 simu inaweza kujaa kwa 100%
Ukubwa na aina ya memori
Upande wa memori simu zipo za aina tatu huku kubwa zaidi ikiwa na GB 512
Na ram pia zipo kwenye mgawanyo wa sehemu tatu
Yenye ram kubwa na memori kubwa bei yake inaongezeka kiasi
Aina ya memori inayotumiwa na hii ni simu UFS 3.0 ambayo kasi yake inafika 2400MBps kusafirisha data
Maana yake ni kuwa simu inauwezo wa kufungua apps kwa haraka na kwa sekunde chache
Uimara wa bodi ya Samsung Galaxy Note 20 Ultra 5G
Galaxy Note 20 Ultra ina viwango vya IP68 vinavyoashiria uwezo wa kuzuia maji kupenya
Iwapo simu ikizama kwenye kina cha mita 1.5 maji hayatoingia kwa muda wa nusu saa
Pia imewekewa skrini protekta aina ya kioo kutoka kwa kampuni ya gorilla
Na upande wa nyuma pia kuna kioo cha gorilla victus
Kiujumla simu ina bodi imara isiyopoteza ubora wake kwa muda mrefu
Ubora wa kamera
Simu ina idadi ya kamera zipatazo tatu
Kuna kamera ya kupiga picha vitu vya mbali sana, eneo pana na kamera ya kawaida
Kamera mbili zinatumia teknolojia ya ulengaji ya PDFA na kamera kubwa pia ina Laser AF kwa ajili ya usiku
PDAF ulengaji sio wa haraka kama dual pixel pdaf
Kama unakipiga kitu kinachokimbia kwa kasi kiwango cha kamera kurekodi kwa utulivu ni wa taratibu
Hata hivyo ubora wa picha ni wa kiwango cha kuvutia
Kuna kiwango kidogo cha noise hata picha ukiikuza kuwa kubwa
Usahihi wa rangi unajitahidi kuonyesha rangi sahihi za mazingira ya hiko kitu
Utofauitishaji wa rangi ni mkubwa na kamera haiathiriwi na mwangaza mwingi wakati wa mchana
Hata kwenye mwanga hafifu vitu vingi vinaweza kuonekana kwa uzuri bila kuathiriwa na kiwango kikubwa cha giza
Ubora wa Software
Samsung Galaxy Note 20 Ultra 5G ilitoka mwaka 2020 hivyo inakuja na android 10
Hata hivyo, simu inakubali kupokea toleo jipya Android 13
Android 13 ndio toleo la sasa kabisa, hivi karibuni android 14 itakuja kuchukua nafasi yake
Kitendo cha simu kuweza kupokea matoleo ya android yanaipa simu thamani zaidi
Washindani wa Samsung Galaxy Note 20 Ultra 5G
Mshindani wa kwanza ni iPhone 12 Pro Max
iPhone 12 Pro Max inakuja na masafa mengi zaidi ya 5G na utendaji wake ni mkubwa kuliko galaxy note 20 ultra 5g
iPhone ina kamera yenye ulengaji dual pixel pdaf yenye uweza wa kukitambua kitu kwa ustadi
Kwa bahati mbaya bei ya iphone 12 pro max inaizidi kiasi samsung
Mshindani mwingine ni Xiaomi 13 Ultra
Xiaomi 13 Ultra ni mpya ina vitu vya kisasa ambavyo vingine havipo kwenye galaxy note 20
Bei pia bei yake ni kubwa ila inatoa ushindani unaoweza mshawishi mtu kuacha kununua note20
Neno la Mwisho
Kwa muhitaji wa simu za viwango vya juu na hana bajeti kubwa, samsung galaxy note20 ultra 5G ni mbadala mzuri
Hakuna tofauti kubwa sana na matoleo mengi ya daraja la juu ya hivi karibuni
Zingatia kuwa simu nyingi za hii galaxy kwa hapa nchini kwetu ni used
Simu used zinapunguza gharama kama ukipata nzuri
Maoni 6 kuhusu “Bei ya Samsung Galaxy Note 20 Ultra 5G na Sifa Zake 2023”
Nahitaji kioo original mana imemeguka kidogo ilidondoka jana
Daah unajua ku
zichambua
aise Daah unajua ku
zichambua
Kati galaxy s20 5g na note 20 5g ipi nzuri kutumia
Note 20 5g ni nzuri zaidi japo kiuwezo hazitofautiani
Vp kwa mkopo
siwez nikapat