Samsung Galaxy S10 5G ni simu ya mwaka 2019 iliyopo kwenye kundi la daraja la juu kwa wakati huo
Ni simu ya mwanzo kuja na teknolojia ya 5g.
Japokuwa ina miaka minne tangu iingie sokoni ila bado ni simu shindani kwa simu za mwaka 2023
Ndio maana bei ya samsung galaxy s10 5g inaendana na bei za simu mpya za madaraja ya kati
Hii inatokana na sifa zake nyingi kuendelea kuwa kubwa hata kwa sasa
Bei ya Samsung Galaxy S10 5G ya GB 256
Kwa Tanzania, Samsung Galaxy S10 5G inauzwa shilingi 770,000
Hii simu ina utendaji wa kuridhisha unaoziacha matoleo mengi ya sasa
Pia vitu vingine vinavyoifanya simu na bei hii ni ubora wa kamera, kioo na uwezo wa kupokea matoleo mapya ya android
Kitendo cha simu kukubali toleo lingine la android kunaipa simu thamani mpya hata kama inakuwa na muda mrefu tangu imetoka
Kwa kuangalia sifa zake zote utapata picha kiundani juu ya ubora wa samsung s10 5g
Sifa za Samsung Galaxy S10 5G
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g and 5g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | Super Amoled |
Softawre |
|
Memori | UFS 2.1, 256GB,512GB na RAM 8GB |
Kamera | Kamera tatu
|
Muundo | Urefu-6.7inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 770,000/= |
Upi ubora wa Samsung Galaxy S10 5G
Galaxy S10 5G inakuja na kioo chenye ubora wa kuonyesha rangi nyingi kwa ustadi
Ina mfumo mzuri wa kamera unaopiga picha nzuri
Inatumia muundo wa memori unaosafirisha data kwa kasi
Utendaji wake mkubwa kutokana na aina ya chip iliyotumika
Inakubali kupokea matoleo mengine ya android mbali na toleo inalokuja nalo
Betri yake inadumu n chaji kwa masaa kwa sababu ni kubwa
Chaji yake inapeleka umeme unaowahi kulijaza betri kwa muda mfupi
Uwezo wa Network
Hii ni simu ya 5G lakini ina masafa machache ukizingatia 2019 5g haikusambaa sana
Kuna uwezakano wa kutopata 5g kwa baadhi ya mitandao ya simu hapa nchini
Mbali na hivyo simu ina mtandao wa 4G aina ya LTE Cat. 20
Aina hii ya 4G inaweza kudownload faili kwa kasi inayofika 2000Mbps
Kwa bahati mbaya kwa hapa Tanzania kiwango hiko kinabaki kuwa ni namba
Kwani hakuna mtandao wa simu unaotoa kasi hiyo kwa sasa
Kikawaida mitandao mingi nchini ikienda sana ni 75Mbps (bado ni kubwa hata hivyo)
Ubora wa kioo cha Samsung Galaxy S10 5G
Kioo cha samsung galaxy s10 5g ni aina ya super amoled chenye resolution kubwa ya 1440 x 3040 pixels
Kioo cha super amoled kina muundo unaoifanya kuonyesha rangi nyingi kwa usahihi
Mfano ni muonekano wa rangi nyeusi, kwenye super amoled rangi hukolea na kuonekana kuwa halisi tofauti na vioo vya ips lcd.
Na ubora wa kioo chake unachagizwa na uwepo wa HDR10+
HDR10+ ina ongeza kioo uangavu na uwezo wa kuonyesha rangi nyingi zinazidi bilioni 12
Hivyo skrini hujitahidi kuonyesha vitu kwa muonekano halisi kama vinavyoenakana kwenye mazingira yake duniani
Uwepo wa HDR10+ inamaanisha kioo kina uangavu mkubwa
Nguvu ya processor ya Exynos 9820
Exynos 9820 ndio processor inayoipa uwezo samsung s10 5g kufanya kazi zake
Imeundwa katika sehemu nane huku sehemu zenye nguvu kubwa ya kiutendaji zipo nne (mbili zina nguvu kubwa zaidi)
Zenye nguvu zinatumia muundo wa Cortex A75 na Mongoose M4
Utendaji wa hizi ni mkubwa kiasi fulani na ulaji wake wa umeme ni wati 2
Japokuwa hizi core za mongoose zilizoonyesha udhaifu hivyo samsung waliamua kuachana nazo
Kwenye app zinazocheki nguvu za utendaji wa processor exynoss 9820 ina alama 800 ambazo ni nyingi
Kwani inaizid processor ya mediatek dimensity 800 ambayo ipo kwenye simu ya Oppo A94 5G
Uwezo wa betri na chaji
Simu inakuja na betri yenye ukubwa wa 4500mAh
Japo siku hizi betri huwa na ujazo wa 5000mAh ila 4500mAh ni kubwa
Kwa mfano samsung s10 5g inakaa na chaji kwa muda wa masaa yanayozidi 12 simu ikiwa kwenye intaneti
Chaji yake ina ukubwa wa 25W ambayo ndani ya dakika 80 inajaza simu kwa 100%
Hivyo simu inakaa muda mfupi kuijaza
Hii samsung inasapoti wireless charge(kuchaji bila kutumia waya)
Unaigusisha simu na kifaa fulani kisha chaji inaanza kuingia
Ni nadra kwa simu za nyingi za matoleo ya kati kwa sasa kuwa na mfumo huu
Japo tecno wameweka kwenye Tecno Camon 20
Ukubwa na aina ya memori
Samsung Galaxy S10 5G zipo za matoleo mawili kwenye upande wa memori
Kuna ya GB 256 na ya GB 512
Zote zinatumia memori zenye muundo wa UFS
Hivyo kasi ya kusafirisha data ni nzuri kwani spidi yake inafika 1200MBps
Upande wa RAM zote zina GB 8
Kwenye simu za android RAM kubwa ni kitu cha msingi
Maana kama unacheza gemu sana sehemu kubwa ya RAM hujaa kitu kinachofanya simu kuwa nzito kiutendaji
Uimara wa bodi ya Samsung Galaxy S10 5G
Bodi ya samsung galaxy s10 5g ina uwezo wa kuzuia maji kupenya kwani ina viwango vya IP68
IP68 humaanisha kuwa simu inaweza kustahimili kutopitisha maji kama ikizama kwenye kina cha mita 1.5 kwa muda wa nusu saa
Kwenye skrini kumewekwa kioo cha Gorilla glass 6
Kwenye majaribio kioo cha gorilla glass kinaweza kuepuka kupasuka kama simu ikianguka kwa kimo cha mita 1.6
Hata hivyo simu kuotpasuka kunategemea na uso pamoja na asili ya eneo hivyo majaribio ya maabara pekee hayatoshi kutoa hitimisho
Ubora wa kamera
Ubora wa kamera wa Samsung Galaxy S10 5G hauna tofauti na ule S10 zingine
Ina jumla ya kamera tatu zote zina megpixel 12
Megapixel 12 inatosha kupiga na kurekodi picha nzuri ukizingatia tayari simu ina teknolojia zinazohitajika kupiga picha vizuri
Kamera zake zote zina dual pixel pdaf zinazosadia kamera kulenga kitu kwa ustadi hivyo kukusanya data za kutosha cha kitu kinachopigwa picha
Ubora wa picha ni mkubwa na kiwango cha noise nyakati sio rahisi kuweza kukiona kwa macho
Kmaera inajitahidi kutoa rangi zenye muonekano halisi
Kama kitu ni cheusi kitatokea kwa jinsi kinavyoonekana na sio kwa kuongeza mng’ao
Upande wa video simu inaweza kurekodi mpaka video za 4K na kwaa kiwango cha HDR10+
Si kawaida kuikuta kamera ya daraja ya kati ya mwaka 2023 kuwa na uwezo huo
Ubora wa Software
Wakati inatoka ilikuwa inakuja na android 9, kwa sasa inakubali mpaka toleo la android 12
Toleo jipya ni android 13 ambalo kwenye hii haipokei sapoti ila unaweza kuliweka kama ukiwa mtaalamu
Na pia inaweza kutumia mfumo wa One UI 4.1 ambapo toleo la sasa ni One UI 5
Hata hivyo software za android 12 na One UI 4.1 zina vitu karibu vyote vya muhimu vinavyohitajika na mtumiaji yoyote wa simu
Washindani wa Samsung Galaxy S10 5G
Kununua samsung galaxy s10 5g kwa mwaka 2023 itakulazimu kuangalia matoleo mapya ya simu za daraja la kati
Kwa sababu teknolojia imesogea mbele zaidi na inapatakana kwa bei nafuu
Mshindani wa kwanza kabisa ni simu ya Oppo Reno8 5G
Reno8 inaizidi kila kitu galaxy s10 5g isipokuwa kwenye kamera na bei ya oppo reno8 inakaribia laki tisa
Simu kali nyingine itakayokuja akilini ni Tecno Camon 20 Pro 5G
Camon 20 Pro 5G ina kioo chenye refresh rate inayogusa 120Hz na kamera ya 4K
Ambapo bei ya camon inaenda kwenye laki saba
Mshindani mwingine ni Redmi Note 12 5G
Neno la Mwisho
Simu ya Samsung Galaxy S10 5G bado ni simu nzuri kwa mwaka huu na miaka mingi ijayo
Bei yake inaendana na sifa zake na ni shindani kwa matoleo mapya ya daraja la kati
Lakini kumbuka bei hiyo inaweza kukupa simu nzuri zaidi
Maoni 2 kuhusu “Bei ya sasa ya Samsung Galaxy S10 5G na Sifa Zake”
Shida kubwa ya samsung ipo kwenye betry haikai na chaji????????
Nikweli kabisa simu ya samsung haikai nachaji yaani Hilo nitatizo