Samsung wameendelea kuachia matoleo mapya kwa mwaka 2023 kwenye upande wa matoleo ya A-Series
Toleo mojawapo ni Samsung Galaxy A54 5G yenye Android 13
Hii ni simu ya daraja la kati kitu kitakochasababisha simu kuwa na bei iliyochangamka kiasi
Kwa masoko ya ulaya ya ulaya bei ya Samsung Galaxy A54 5G inazidi shilingi milioni moja kutegemeana na ukubwa wa memori
Ubora wake unashawishi kwa kiwango kikubwa kuinunua kwa bei tajwa
Bei ya Samsung Galaxy A54 ya GB 128
Tangu kuzinduliwa mwezi machi bei yake ya GB 128 inaanzia shilingi 1,300,000/=
Kwa Tanzania kuna uwezekano bei ikaongezeka kidogo
Ukiangalia aina ya screen, memori, chip, bluetooth na vifaa vingine utagundua kuwa ni simu tofauti sana na Samsung Galaxy A04
Ila kuna sifa zinazoendana kwa kiasi fulani na simu ya Samsung Galaxy Z Fold 4 hivyo bei yake haiwezi kuwa nafuu
Pitia sifa zote zilizoainishwa humu kufahamu ubora wake kiufasaha
Sifa za Samsung Galaxy A54 5G
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g and 5g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | Super Amoled, Refresh rate:120Hz |
Softawre |
|
Memori | 256GB,128GB na RAM 8GB,6GB |
Kamera | Kamera tatu
|
Muundo | Urefu-6.4inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 1,300,000/= |
Upi ubora wa Samsung Galaxy A54
Galaxy A54 ina kioo kizuri kwenye uoneshaji wa vitu kwa usahihi
Ina utendaji unaoweza kufungua applikesheni yoyote bila kukwama
Inakuja na chaji yenye kujaza simu kwa haraka
Ina toleo la jipya la android na inaweza kupokea toleo jipya
Maji hayawezi kupenya kwenye hii simu kwa urahisi
Betri yake ni kubwa hivyo kuna uhakika wa simu kustahimili muda mrefu kwenye ukaaji wa chaji
Uwezo wa Network
Samsung Galaxy A54 ni simu ya daraja la kati yenye 5G
Inakubali aina zote za 5G ikiwemo mmWave ambayo hutumika sana kwa USA
Kitendo cha simu kuwa na uwezo wa kupokea mmWave inamaanisha kasi yake ni kubwa kwenye mtandao
Kwa sasa hutakiwi kuwanza kuhusu mtandao, 5G ya Tigo inaweza kufika mpaka 1Gbps ni tofauti na ile ya Vodacom
Na upande wa 4G simu inasapoti LTE Cat 18 kwa maana kama kuna mtandao wenye kasi ya 3790Mbps basi inaweza kuchakata kiwango hiko cha data
Ila kiuhalisia hii ni kasi ya 5G
Kama hupendelei kuwa na laini za simu, Galaxy A54 inaweza kufanya bila kuwa na laini
Hii inatokana na kuwezeshwa kwa eSIM(embedid SIM) ambayo haihitaji laini zile za plastiki kabisa
Airtel wameanzisha huu mfumo hapa Tanzania
Ubora wa kioo cha Samsung Galaxy A54
Galaxy A54 ina kioo cha Super Amoled
Vioo vya amoled huwa havitegemei mwanga wa taa bali ni vioo vinavyozalisha mwanga wenyewe
Kitendo hiki hufanya amoled kuzalisha rangi nyeusi halisi tofauti na vioo vya IPS LCD
Faida ya vioo hivi ni kuwa na uwezo wa kuzalisha rangi nyingi zinaweza fika bilioni
Kitendo cha kuwa na rangi nyingi huchangia rangi za vitu kuonekana kwa rangi halisi na kukolea vizuri
Ndio maana huwa ni vioo vyenye bei
Na pia resolution yake ni full hd+ na kikiwa na refresh rate ya 120Hz
Hivyo simu inakuwa nyepesi wakati wa kutachi
Nguvu ya processor Exynos 1380
Kitu chochote ambacho simu inakifanya huwa kinachakatwa na processor
Processor ikiwa na nguvu ndio utendaji wa simu unakuwa mkubwa
Samsung inatumia chip ya Exynos 1380 ambayo imegawanyika katika sehemu
Kila sehemu ina idadi ya core(sehemu za processor) nne
Kuna core zenye nguvu sana kwa ajili ya kufanya kazi kubwa na zile zenye nguvu ndogo
Core zenye nguvu kubwa zinatumia muundo wa Cortex A78 na zile ndogo ni Cortex A55
Cortex A78 inaweza kufanya mizunguko zaidi ya bilioni tatu na kila mzunguko ukwa unachakata kazi 4 kwa sekunde
Huu utendaji unaifanya simu kuweza kucheza kia aina ya gemu ama kutumia applikesheni nyingi kwa wakati mmoja pasipokuwa na tatizo
Uwezo wa betri na chaji
Ukubwa wa betri ya galaxy a54 5g ni 5000mAh
Huu ni ujazo unaofanya simu kukaa muda mrefu na chaji
Chaji yake inakuja na kasi ya wati 25 hivyo betri hii kubwa itajazwa kwa haraka bila tatizo
Lakini ukaaji wa chaji unategemea sana na aina ya matumizi
Ila kwenye simu zingine za samsung zenye 25W, ujazaji wa chaji ni wa kiwango kidogo ukilinganisha na simu zenye wati 33 au wati 120
Ukubwa na aina ya memori
Kuna matoleo mawili ya Samsung Galaxy A54 5G linapokuja swala la memori
Kuna zenye GB 128 na pia zile zenye GB 256
Simu za bei ya juu siku hizi huwa haziji na sehemu ya kuweka memori ya ziada
Ila simu hii inakuja nayo
Hivyo memori kama ikijaa utaweza kuongeza memori kadi kuhifadhi mafaili zaidi
GB 128 sio memori kubwa sana kama unapakuwa na kurekodi sana video
Simu inaweza kujaa ndani ya muda mfupi
Uimara wa bodi ya Samsung Galaxy A54
Bodi yake haiwezi kupitisha maji kama simu ikidumbukia kwenye kina cha mita 1.5 kwa muda wa nusu saa
Simu ina viwango vya IP67 vinavyooshiria kuwa maji na vumbi haviwezi kupenya ndani
Kuwa na bodi ngumu ya namna inasaidia simu kukaa muda mrefu
Na ni msaada mkubwa kwa ambaye ana shughuli zinazomfanya ashinde sana kwenye mvua
Ubora wa kamera
Simu ina kamera tatu zinawezoweza kupiga picha kwenye eneo pana sana na kitu cha karibu
Kamera kuu ina ukubwa wa 50MP ambayo ina OIS na ulengaji wa PDAF
OIS husaidia utulivu wakati wa kurekodi video huku ukiwa unatembea
Inafanya video kutokutikisika tikisika
PDAF hufanya kamera kukitambua kitu kinachopigwa kwa haraka japo inazidiwa na dual pixel pdaf
Hii simu inaweza kurekodi mpaka video za 4K kwa kiwango cha 30fps
Ubora wa Software
Ukiinunua ikiwa mpya kabisa utakutana na Android 13 na mfumo wa One UI 5.1
One UI 5.1 ni mfumo mwepesi na hauji na matangazo kama baadhi ya mifumo mingine
One UI 5.1 ina kitu kinaitwa image clipper
Image Clipper inakuwezesha kukikopi kitu chochote kutoka kwenye picha na kukitengenezea picha nyingine
Kwa mfano umepiga picha nyuma ya gari na gari ikatokea
Kama unataka picha ya gari kutoka kwenye picha uliyoipiga basi hapo utatumia hiyo image clipper
Kuna mengi unawe yapata, pitia hapa
Yapi Madhaifu ya Samsung Galaxy A54
Mfumo wake wa kamera si wa kuvutia sana ukilinganisha na simu za samsung galaxy s23
Simu haina sehemu ya kuweka earphone kama ilivyo kawaida ya simu za siku hizi
Hivyo mbadala ni kutumia earphone za bluetooth
Na kwa wapenzi wa redio pia hii simu inaweza isiwafae kwa sababu haina redio
Neno la Mwisho
Wale ambao wana mfuko ulionona hii ni moja ya simu ya kuwa nayo
Japokuwa bei yake inaingia kwenye ushindani na simu za xiaomi 13 pro na OPPO Reno 5G
Ila bei yake inaendana na ubora wake kwa kiasi kikubwa
Maoni 9 kuhusu “Bei ya Samsung Galaxy A54 5G na Upekee Wake”
Asante sana kwa kutuelimisha kuhusu simu hiyo,je ni simu gani nyingine iliyo nasifa kama hizo Samsung A54 lkn yenye bei nafuu kuanzia tsh500,000
Google Pixel 5
Kwenye hiyo bei akuna punguzo
Bajeti yako ngapi
Naweza pata Samsung A54 kwa mkopo au s23 kwa mkopo
Kwa sasa hiyo Samsung A54, gb128 inatembea kwa sh nhapi
Nimeipenda naenda kununua
Nikitaka simu ya samsang kwa 400000 je napata aina gan
Samsung Galaxy A15 4G