Mwezi wa desemba 2023 ni mwezi ambao Simu ya Samsung Galaxy A15 ilizinduliwa
Ni simu ya daraja la kati ambayo ina vitu vichache vinavyopatikana kwenye samsung za bei kubwa
Ndio maana bei ya Samsung Galaxy A15 ya GB 128 ni shilingi laki nne na nusu kama kima cha juu kabisa
Kwenye eneo lenye ubora mkubwa zaidiĀ ni upande wa kioo
Japo sifa zingine zipo zenye ila skrini yake ni nzuri zaidi kama utakavyoona
Sifa za Samsung Galaxy A15
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | Super Amoled, Refresh rate:90Hz |
Softawre |
|
Memori | 256GB,128GB na RAM 8GB,6GB,4GB |
Kamera | Kamera TATU
|
Muundo | Urefu-6.5inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 450,000/= |
Uwezo wa Network
Hii ni simu ya 4G haiji na uwezo wa mtandao wa 5G na haisapoti eSIM
Kuna Galaxy A15 yenye laini moja na nyingine zinakubali laini mbili
4G yake inakubali mitandao yote ya simu hapa Tanzania
Aina ya 4G yake ni LTE Cat 13 ambayo kasi yake ya kupakua faili mtandaoni inaweza fika 650 iwapo mtandao wa simu unasapoti kasi hii ya 4G
Kasi hii inaweza kudownload vitu kwa sekunde chache hata mafaili makubwa hayachukui muda kumalizika
Hata hivyo sio rahisi kupata kasi ya 4G ya kiwango kikubwa hiki kwa sehemu kubwa hapa Tanzania
Ubora wa kioo cha Samsung Galaxy A15
Samsung Galaxy A15 inatumia kioo cha Super Amoled chenye resolution ya 1080 x 2340 pixels
Resolution kubwa kwenye kioo cha super amoled kinaongeza uwezo wa kioo kuonyesha vitu kwa ufanisi
Kioo cha hii simu kama kioo cha Samsung Galaxy A55
Kwani chenyewe kinakosa HDR10+ ambayo huboresha muonekano wa vitu
Ila utapata refresh rate inayofika 90Hz ambayo ni kubwa
Hii inafanya kioo kuwa fasta unapokuwa unatachi
Nguvu ya processor Mediatek Helio G99
Mediatek helio G99 ndio chip inayotumika katika kufanya kazi mbalimbali kwenye hii simu
Ina core mbili zenye muundo wa Cortex A76 yenye mizunguko 2.2GHz
Hii speed 2.2GHz inaweza kufikiwa iwapo simu inafanya kanzi nzito sana kama kucheza gemu
Ila mara nyingi ni nadra app za simu za kawaida kufika kiwango hiko
Kiujumla utendaji wa Mediatek helio G99 ni wa kuridhisha
Yaani hata gemu zinazotumia nguvu kubwa zinacheza kwa graphics zenye resolution kubwa
Uwezo wa betri na chaji
Betri ya hii simu ina ukubwa wa 5000mAh
Ukaaaji wa chaji wa Galaxy A15 ni mkubwa kwani kwa mchangachiko wa matumizi inaweza chukua masaa karibu 15
Kwenye kuperuzi intaneti ukaaji wa chaji unatumia karibu masaa 12
Ila magemu yanakula chaji kwa kiwango kikubwa kwani smu inachukua masaa 7 tu mpaka kuisha
Hii simu inasapoti chaji yenye kupeleka umeme wa wati 25
Na unapoichaji hii simu na chaji ya wati 25, simu inajaa ndani ya dakika 81
Huu ni muda mdogo kwa kiasi fulani, japo siku hizi kuna chaji zinajaza betri kwa dakika 17 tu
Ukubwa na aina ya memori
Siku hizi simu nyingi za daraja la kati huja na memori za ukubwa wa GB 128 kwenda mbele
Hivyo hata Samsung Galaxy A15 zipo za GB 128 na GB 256
Mgawanyo wa RAM ni GB 4, 6 na 8
Kiushauri RAM ndogo haifai kwa mtumiaji anayefanya vitu kwenye simu kwa wakati mmoja
Kwa mfano ukiwa unacheza gemu kama ya Dream Soccer ram inajaa nyingi kwa haraka
Hivyo inapelekea simu kuganda ganda
Hivyo basi chukua yenye RAM kubwa kama bajeti yako inaruhusu
Uimara wa bodi ya Samsung Galaxy A15
Bodi ya Samsung Galaxy A15 imeundwa kwa plastiki haina kioo nyuma wala mbele
Hii simu haina waterproof, kwani hakuna kiwango chochote cha IP kilichoainishwa
Ikizama kwenye maji uwezekano wa simu kuathirika ni mkubwa kama hujaiwahi
Kwa hiyo ni lazima kuwa makini unapokuwa na simu kwenye mazingira ya mvua au maeneo yanye maji
Na pia ni muhimu kuweka
Ubora wa kamera
Ubora wa kamera wa Galaxy A15 ni wa kawaida sio mkubwa kama Galaxy A55
Kwa mfano ubora wa picha nyakati za usiku yaani kwenye mwanga mdogo unaathiriwa na kiwango kikubwa cha chengachenga(noise)
Ila kwenye mwanga mwingi muonekano niĀ mzuri japo sio kiivyo
Kamera ya hii simu haiwezi kurekodi video za 4K bali inarekodi video za full hd pekee kwa kiwango cha 30fps
Pia inakosa teknolojia ya OIS, inabidi kutuliza mkono sana wakati ukirekodi huku ukiwa unatembea
Tembelea hapa kuona picha zilizopigwa na Samsung Galaxy A15
Ubora wa Software
Samsung Galaxy A15 inakuja na toleo la Android 14 na One UI 6
Hii ina uhakika wa kupata matoleo mapya ya android kwa kipidi cha miaka mitatu
Kwa maana hiyo Galaxy A15 itapata hadi Android 17
Simu inapopata maboresho ya namna hii kwa inaongeza maisha ya simu kutumika muda mrefu
Na pia inaimarisha usalama na pia kupata vitu vipya ambavyo havipo kwenye matoleo ya nyuma
Washindani wa Samsung Galaxy A15
Kama ilivyo ada washindani wakubwa wa Samsung ni simu za kampuni kutika china
Siku hizi kampuni za china pia zinatengeneza simu nzuri za madaraja ya kati
Simu ya kwanza ni Redmi Note 13 ambayo inapatikana kwa laki nne aliexpress
Kioo cha Redmi Note 13 ni kizuri na chaji yake ina kasi kubwa
Pia kuna simu za iQOO na zenyewe zipo za bei ndogo ya hii zenye kuendana kisifa
Kwa bei ya Samsung Galaxy A15 inatoa fursa kwa muhitaji wa simu kuona machaguo mengi mbadala
Neno la Mwisho
Simu ya Samsung Galaxy A15 ni ya bei nafuu yenye ubora wa ziada unaokosekana kwenye matoleo ya Samsung A05
Angalau hii simu ina baadhi ya vitu vya S24 kwa bei nafuu
Kwa wahitaji wa simu wanaotaka kujaribu simu mpya yenye kutoa matoleo mapya ya Android kwa muda mrefu basi hili ni moja ya Chaguo sahihi
Maoni 6 kuhusu “Bei ya Samsung Galaxy A15 na Sifa Muhimu”
Nifanyaje ili kupunguza simu kupata moto samsung A15 au nitafute simu yenye wat sawa na betr
Simu yangu ni samsung A15 lakini inachelewa kujaa tofauti na mwanzo na nishabadilisha chaji
Inawezekana Betti imeanza haribuka au chaji, jaribu kutumia fast charge nyingine
Bei ya Samsung Galaxy a15 ni shingapi
Nifanye nin ili smu yangu iache kupata moto
Punguza idadi ya app zinazorun in background kama manotification mengi, pili punguza mwanga ama kutumia Sana simu kwenye mazingira ya juani