Simu ya Samsung Galaxy A05s ni simu ya daraja la kati ambayo bei yake ya GB 64 inauzwa shiling laki tatu na nusu
Bei yake ni ndogo ukilinganisha na toleo la Samsung Galaxy S24 kwani Galaxy A05s haina vitu vingi ukifuatilia sifa zake
Hata hivyo ni moja ya simu nzuri za bei nafuu kutoka samsung ambayo ilitoka mwaka 2023
Fuatilia sifa zake zote zilizoorodheshwa ufahamu vipengele vyenye ubora kiundani.
Bei ya Samsung Galaxy A05s ya GB 128
Samsung Galaxy A05s yenye GB 128 inauzwa shilingi laki nne (400,000)
Ukubwa ni mzuri kwa mtumiaji anaetarajia kuhifadhi vitu vingi ndani ya simu
Na vizuri ukawa na toleo la memori kubwa kwa mantiki ya kwamba app kama whatsapp zinahifadhi mafaili ndani ya simu
Kwa maana kadri unavyoweka mafaili mengi ndivyo memori ya simu inazidi kujaa
Sifa za Samsung Galaxy A05s
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | IPS LCD, Refresh rate:90Hz |
Softawre |
|
Memori | eMMC 5.1,128GB,64GB na RAM 6GB,4GB |
Kamera | Kamera tatu
|
Muundo | Urefu-6.7inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 400,000/= |
Upi ubora wa Samsung Galaxy A05s
Simu inakuja na kioo kizuri hasa kwa kucheza gemu
Bei yake ni nafuu ukilinganisha na samsung za matoleo ya juu
Kamera zake zinapiga picha vizuri ukilinganisha na simu nyingi zilizopo kwenye kundi moja
Inaweza kujaza betri kwa haraka
Betri yake ni kubwa na ukaaji wake wa chaji ni wa kuridhisha
Memori yake inaweza kuhifadhi vitu vingi
Kuelewa ubora na udhaifu kwenye kila kipengele soma hii posti yote,
Kabla ya hapo, vipi kuhusu uwezo wake wa network?
Uwezo wa Network
Hii simu inasapoti mpaka mtandao wa 4G kama kiwango cha juu cha network
Aina ya 4g simu inayosapoti ni LTE Cat 13
LTE Cat 13 spidi yake ya juu kabisa ya kupakua vitu inafika 350mbps
Wakati spidi yake ya juu kabisa ya ku-upload ni 150Mbps
Kwa sasa kasi hii hapa Tanazania unaweza kuipata kwenye mtandao wa 5G
Ila kumbuka Galaxy A05s haina 4G
Hata hivyo kasi kubwa inakulazimu kulipia zaidi
Eneo lingine ambalo lina ubora kiasi fulani ni kioo cha hii simu
Ubora wa kioo cha Samsung Galaxy A05s
Kioo cha Samsung Galaxy A05s ni cha aina ya IPS LCD chenye resolution 1080×2400 pixels
Kwa simu mfano wa Tecno Spark 10 pro resolution yake ipo chini ya hii
Kwa maana hiyo wa vitu kwenye galaxy a05s ni mzuri zaidi
Japokuwa kioo chake hakitumii teknoljia ila refresh rate kubwa inayofika 90Hz
Inafanya simu kuwa na uharaka hasa wakati wa kuperuzi na nzuri kucheza magemu
Nguvu ya processor Snapdragon 680 4G
Simu ya galaxy A05s inatumia processor ya snapdragon 680 4g ambayo kwa sasa ina muda kidogo
Imegawanyika katika sehemu mbili kama ilivyo kwa chip nyingi za simu ya Android
Uwezo wake kiutendaji ni wa wastani hivyo gemu nyingi zinaplay kwa ustadi kama ukiseti muonekano wa chini wa picha (Low Resolution)
Hii chip inapata alama 409 kutoka kwenye app inayotumika kupima nguvu ya processor
Ni alama ndogo ukilinganisha na processor kwenye simu za iPhone, Google pixel ama Samsung S-series
Hata kwa mtumiaji wa kawaida anaweza asione tofauti
Uwezo wa betri na chaji
Betri ya Samsung Galaxy A05s ina ukubwa wa 5000mAh ila ukaaji wake wa chaji ni wa wastani
Kutoka GSMArena, Galaxy A05s inaweza kukaa na chaji kwa takribani masaa 10 ukiwa unaperuzi intaneti
Kwa mfano, kama unatafuta vitu kwenye google muda wote basi simu inaweza kuhimili kukaa na chaji muda huo
Kwa mantiki hiyo, kwa mtumiaji sana wa simu muda wote atalazimika kuchaji simu mara mbili kwa siku
Chaji yake inaweza kupeleka chaji mpaka wati 25 kama kiwango cha juu
Kiwastani, chaji yake inajaza 43% ndani ya nusu saa
Hivyo simu inaweza kujaa ndani ya masaa mawili kwa asilimia mia
Ukubwa na aina ya memori
Kuna matoleo ya aina mbili kwenye upande wa memori
Kuna ya GB 64 na GB 128 na RAM zipo za GB 4 na GB 6
Wazo zuri ni kuchukua yenye RAM kubwa na memori kubwa
Hii itakusaidia kuhifadhi vitu vingi na pia kufungua mafaili mengi kwa wakati mmoja hasa ukiwa unacheza magemu
Uimara wa bodi ya Samsung Galaxy A05s
Bodi ya hii simu upande wa nyuma ni ya plastiki
Na upande wa mbele imewekewa kioo
Hii simu haina viwango vya IP, hivyo haipaswi kutumia ama kuizamisha kwenye maji
Kwani ukichelewa kuitoa maji yanaweza penya ndani ya simu
Kama unahitaji simu yenye waterproof Samsung Galaxy A54 ni chaguo zuri la bei nafuu
Ila unafuu wake ni kwa kulinganisha na simu zingine zenye waterproof kama iPhone 15
Kwa maana A54 bei yake ni kubwa kidogo
Ubora wa kamera
Hii simu inakuja na kamera zipatazo tatu huku kamera kubwa(wide) ina megapixel 50
Tuiangazie hii kamera.
Usahihi wa rangi ni wa kuridhisha ila moja ya kitu nimekiona kutoka kwenye picha zilizopigwa na hii simu kuna kuongezeka kwa rangi kidogo
Yaani kama rangi nyekundu kuna mkorezo wa ziada upande wa texture
Hata hivyo kwa ubora wa kawaida na ukizingatia bei ya hii simu, ubora wa kamera ni mzuri hasa kwenye mwanga mwingi
Hii simu inaweza kurekodi video za Full hd kwa kiwango cha 30FPS
Kamera za hii simu zinakosa OIS na PDAF
Ubora wa Software
Samsung Galaxy A05s inakuja na Android 13 na mfumo wa One UI core 5.1
Hakuna uhakika kama hii simu itapata toleo la Android 14
Mfumo wa One UI Core 5.1 hutumika kwenye simu za samsung zenye nguvu ndogo
Ila chip ya snapdragon 680 4G nguvu yake sio ndogo kiasi hiko
Ingeweza kufanya kazi kwa ustadi kama ingewekewa One UI yenyewe
Kwa sababu One UI Core huondoa baadhi ya vitu kama secure folder
Washindani wa Samsung Galaxy A05s
Mshindani wa kwanza wa toleo hili la samsung ni Oppo A96 ambayo ina miaka takribani miwili tangu itoke
Bei ya hizi simu zinaneandana na zote zinatumia processor moja
Kitu cha ziada kutoka oppo ni uwepo wa IP rating ambayo inamaanisha oppo ina uimara fulani wa kuzuia maji
Mshindani mwingine ni Tecno Spark 10 Pro. Ndio ni tecno
Mtu mwingine anaweza kushangaa “Samsung vs Tecno”? mbigu na ardhi.
Ila kumbuka spark 10 pro na samsung galaxy a05s ni simu za madaraja ya kati, kiubora hakuna tofauti kubwa
Pia bila kusahau toleo la Redmi 12C ama Redmi 10C zenye bei ya chini zaidi
Hitimisho
Kwa wale wanaohitaji kumiliki samsung kwa bajeti ndogo hili ni toleo zuri
Japo hutopata vitu vilivyomo kwenye toleo jipya la Samsung S24
Ila sio simu mbaya kuwa nayo
Maoni 16 kuhusu “Bei ya Samsung Galaxy A05s na Sifa Zake Zote”
Nahitaji iyo samsung A05s kwa bei ya Tsh 350,000 ahsante.
Nahitaji hiy simu
Je naweza letewa mi nipo Arusha Tanzania
Upo uwezekano
Samsung ni simu nzuri ila mnafeli upande wa betry na netwek sehemu ukiws mbali kidogo na minara utaona zile baa zake zinasinzia
Simu ya Samsung galaxy A05s ina uwezo wa kubeba flash yenye BG ngapi
Kwann samsung a05s zinakuja bila chaji na airfon
Kwann sim aina ya samsung a05s zinakuja bila chaji na airfon hamuoni kama mnatupa usumbufu wateja kununua cm na kununua chaji na chaji tunazo nunua tunajuaje kama ni salama kwa cm
Wenyewe wanadai kuhifadhi mazingira
Nzuur kwa ujaaji wa chaji ni wa haraka
Jmn mm ninayo sasa nkadownload app zote mbil yn cpu x na cpu z …kwny upande wa proccessor kweny cpu z inanmbia ni snapdragon 636 while cpu x inasma 680 of which Selew nn niamin lkn apoapo nlvyodownload io cpu x mwanzo haiku na iko kipengele cha proccessor ckuiona ila kwa bdae kdg ndo nikaona sa napo nashndwa kuelewa …af pia ni android version 14 akat nmefuatlia hzi cm ni version 13 kwamb hakna uhakka wa kua na version 14 ..kwaio nlkua nahitaj angalau maelezo mafupi kulingana a na ilo jambo
CPU X ndio IPO sahihi
Sasa vip kuhs io version yao mana walsema ni 13 na hakna uhakka kama kuna android vision 14 na yang ni version ya 14
Android version 14 IPO sasa inawezekana simu iliupdatiwa
Ni kweli kabisa sifa xote hizo inazo
Hata mimi ndo naitumia hii SAMSUNG A05
Je nilirudia password ya simu ikajifunga Kwa masaa Sasa nifanyaje ili nifunguee