SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

Bei ya Samsung Galaxy A05s na Sifa Zake Zote

Sifa za simu

Sihaba Mikole

January 29, 2024

Simu ya Samsung Galaxy A05s ni simu ya daraja la kati ambayo bei yake ya GB 64 inauzwa shiling laki tatu na nusu

Bei yake ni ndogo ukilinganisha na toleo la Samsung Galaxy S24 kwani Galaxy A05s haina vitu vingi ukifuatilia sifa zake

Hata hivyo ni moja ya simu nzuri za bei nafuu kutoka samsung ambayo ilitoka mwaka 2023

Fuatilia sifa zake zote zilizoorodheshwa ufahamu vipengele vyenye ubora kiundani.

Bei ya Samsung Galaxy A05s ya GB 128

Samsung Galaxy A05s yenye GB 128 inauzwa shilingi laki nne (400,000)

Ukubwa ni mzuri kwa mtumiaji anaetarajia kuhifadhi vitu vingi ndani ya simu

Na vizuri ukawa na toleo la memori kubwa kwa mantiki ya kwamba app kama whatsapp zinahifadhi mafaili ndani ya simu

Kwa maana kadri unavyoweka mafaili mengi ndivyo memori ya simu inazidi kujaa

Sifa za Samsung Galaxy A05s

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g, 4g
Processor(SoC)
  • CPU – Snapdragon 680 4G
  • Core Zenye nguvu(4) – 4×2.4 GHz Kryo 265
  • Core Za kawaida(4) – 4×1.9 GHz Kryo 265 Silver
  • GPU-Adreno 610
Display(Kioo) IPS LCD, Refresh rate:90Hz
Softawre
  • Android 13
Memori eMMC 5.1,128GB,64GB na RAM 6GB,4GB
Kamera Kamera tatu

  1. 50MP,AF(wide)
  2. 2MP(macro)
  3. 2MP(depth)
Muundo Urefu-6.7inchi
Chaji na Betri
  • 5000mAh-Li-Po
  • Chaji-25W
Bei ya simu(TSH) 400,000/=

Upi ubora wa Samsung Galaxy A05s

Simu inakuja na kioo kizuri hasa kwa kucheza gemu

Bei yake ni nafuu ukilinganisha na samsung za matoleo ya juu

Kamera zake zinapiga picha vizuri ukilinganisha na simu nyingi zilizopo kwenye kundi moja

Inaweza kujaza betri kwa haraka

Betri yake ni kubwa na ukaaji wake wa chaji ni wa kuridhisha

Memori yake inaweza kuhifadhi vitu vingi

Kuelewa ubora na udhaifu kwenye kila kipengele soma hii posti yote,

Kabla ya hapo, vipi kuhusu uwezo wake wa network?

Uwezo wa Network

Hii simu inasapoti mpaka mtandao wa 4G kama kiwango cha juu cha network

Aina ya 4g simu inayosapoti ni LTE Cat 13

LTE Cat 13 spidi yake ya juu kabisa ya kupakua vitu inafika 350mbps

Wakati spidi yake ya juu kabisa ya ku-upload ni 150Mbps

Kwa sasa kasi hii hapa Tanazania unaweza kuipata kwenye mtandao wa 5G

Ila kumbuka Galaxy A05s haina 4G

Hata hivyo kasi kubwa inakulazimu kulipia zaidi

Eneo lingine ambalo lina ubora kiasi fulani ni kioo cha hii simu

Ubora wa kioo cha Samsung Galaxy A05s

Kioo cha Samsung Galaxy A05s ni cha aina ya IPS LCD chenye resolution 1080×2400 pixels

Kwa simu mfano wa Tecno Spark 10 pro resolution yake ipo chini ya hii

Kwa maana hiyo wa vitu kwenye galaxy a05s ni mzuri zaidi

Japokuwa kioo chake hakitumii teknoljia ila refresh rate kubwa inayofika 90Hz

Inafanya simu kuwa na uharaka hasa wakati wa kuperuzi na nzuri kucheza magemu

Nguvu ya processor Snapdragon 680 4G

Simu ya galaxy A05s inatumia processor ya snapdragon 680 4g ambayo kwa sasa ina muda kidogo

Imegawanyika katika sehemu mbili kama ilivyo kwa chip nyingi za simu ya Android

Uwezo wake kiutendaji ni wa wastani hivyo gemu nyingi zinaplay kwa ustadi kama ukiseti muonekano wa chini wa picha (Low Resolution)

Hii chip inapata alama 409 kutoka kwenye app inayotumika kupima nguvu ya processor

Ni alama ndogo ukilinganisha na processor kwenye simu za iPhone, Google pixel ama Samsung S-series

Hata kwa mtumiaji wa kawaida anaweza asione tofauti

Uwezo wa betri na chaji

Betri ya Samsung Galaxy A05s ina ukubwa wa 5000mAh ila ukaaji wake wa chaji ni wa wastani

Kutoka GSMArena, Galaxy A05s inaweza kukaa na chaji kwa takribani masaa 10 ukiwa unaperuzi intaneti

Kwa mfano, kama unatafuta vitu kwenye google muda wote basi simu inaweza kuhimili kukaa na chaji muda huo

Kwa mantiki hiyo, kwa mtumiaji sana wa simu muda wote atalazimika kuchaji simu mara mbili kwa siku

Chaji yake inaweza kupeleka chaji mpaka wati 25 kama kiwango cha juu

Kiwastani, chaji yake inajaza 43% ndani ya nusu saa

Hivyo simu inaweza kujaa ndani ya masaa mawili kwa asilimia mia

Ukubwa na aina ya memori

Kuna matoleo ya aina mbili kwenye upande wa memori

Kuna ya GB 64 na GB 128 na RAM zipo za GB 4 na GB 6

Wazo zuri ni kuchukua yenye RAM kubwa na memori kubwa

Hii itakusaidia kuhifadhi vitu vingi na pia kufungua mafaili mengi kwa wakati mmoja hasa ukiwa unacheza magemu

Uimara wa bodi ya Samsung Galaxy A05s

Bodi ya hii simu upande wa nyuma ni ya plastiki

Na upande wa mbele imewekewa kioo

Hii simu haina viwango vya IP, hivyo haipaswi kutumia ama kuizamisha kwenye maji

Kwani ukichelewa kuitoa maji yanaweza penya ndani ya simu

Kama unahitaji simu yenye waterproof Samsung Galaxy A54 ni chaguo zuri la bei nafuu

Ila unafuu wake ni kwa kulinganisha na simu zingine zenye waterproof kama iPhone 15

Kwa maana A54 bei yake ni kubwa kidogo

Ubora wa kamera

Hii simu inakuja na kamera zipatazo tatu huku kamera kubwa(wide) ina megapixel 50

Tuiangazie hii kamera.

Usahihi wa rangi ni wa kuridhisha ila moja ya kitu nimekiona kutoka kwenye picha zilizopigwa na hii simu kuna kuongezeka kwa rangi kidogo

Yaani kama rangi nyekundu kuna mkorezo wa ziada upande wa texture

Hata hivyo kwa ubora wa kawaida na ukizingatia bei ya hii simu, ubora wa kamera ni mzuri hasa kwenye  mwanga mwingi

Hii simu inaweza kurekodi video za Full hd kwa kiwango cha 30FPS

Kamera za hii simu zinakosa OIS na PDAF

Ubora wa Software

Samsung Galaxy A05s inakuja na Android 13 na mfumo wa One UI core 5.1

Hakuna uhakika kama hii simu itapata toleo la Android 14

Mfumo wa One UI Core 5.1 hutumika kwenye simu za samsung zenye nguvu ndogo

Ila chip ya snapdragon 680 4G nguvu yake sio ndogo kiasi hiko

Ingeweza kufanya kazi kwa ustadi kama ingewekewa One UI yenyewe

Kwa sababu One UI Core huondoa baadhi ya vitu kama secure folder

Washindani wa Samsung Galaxy A05s

Mshindani wa kwanza wa toleo hili la samsung ni Oppo A96 ambayo ina miaka takribani miwili tangu itoke

Bei ya hizi simu zinaneandana na zote zinatumia processor moja

Kitu cha ziada kutoka oppo ni uwepo wa IP rating ambayo inamaanisha oppo ina uimara fulani wa kuzuia maji

Mshindani mwingine ni Tecno Spark 10 Pro. Ndio ni tecno

Mtu mwingine anaweza kushangaa “Samsung vs Tecno”? mbigu na ardhi.

Ila kumbuka spark 10 pro na samsung galaxy a05s ni simu za madaraja ya kati, kiubora hakuna tofauti kubwa

Pia bila kusahau toleo la Redmi 12C ama Redmi 10C  zenye bei ya chini zaidi

Hitimisho

Kwa wale wanaohitaji kumiliki samsung kwa bajeti ndogo hili ni toleo zuri

Japo hutopata vitu vilivyomo kwenye toleo jipya la Samsung S24

Ila sio simu mbaya kuwa nayo

Maoni 5 kuhusu “Bei ya Samsung Galaxy A05s na Sifa Zake Zote

Maoni na Maswali

Email yako haitochapishwa, kwenye alama * lazima pajazwe ili ukomenti

Fuatilia Zaidi

No Featured Image

Simu Mpya za Samsung 2024 (za bei rahisi na ghari)

Kuna simu zaidi ya tisa zilizotengenezwa na kampuni ya Samsung kutoka Hapa kuna orodha ya simu kumi mpya za samsung ambazo zimetoka mwishoni mwa mwaka 2023 hadi mwaka 2024 Ni […]

Bei ya Samsung Galaxy A25 na Sifa zake

Simu ya Samsung Galaxy A25 ilitoka rasmi mnamo mwezi desemba 2023 Ni simu ya daraja ambayo bei yake kwa Tanzania ni shilingi laki saba (700,000/=), hii ikiwa ni bei ya […]

samsung galaxy a15 thumbnail

Bei ya Samsung Galaxy A15 na Sifa Muhimu

Mwezi wa desemba 2023 ni mwezi ambao Simu ya Samsung Galaxy A15 ilizinduliwa Ni simu ya daraja la kati ambayo ina vitu vichache vinavyopatikana kwenye samsung za bei kubwa Ndio […]

samsung a55 showcase

Bei ya Samsung Galaxy A55 na Ubora wake

Samsung Galaxy A55 imetoka mwezi machi mwaka 2024 na ni simu ya daraja la kati Bei ya Samsung Galaxy A55 kwa Tanzania ni shilingi milioni moja na laki moja na […]

SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

E-mail : simunzuriblog@gmail.com

Simu: +255 683 420 543

Whatsapp: +255 756 077 262

Kabila, Magu

Mwanza, Tanzania

Company

Find Us On

FB Twitter Instagram