Mwishoni mwa 2022 Kampuni ya Xiaomi ilitoa toleo la simu ya Redmi 12C
Ni simu ya daraja la chini hivyo bei yake ni ndogo hata kwa ambazo memori zake ni kubwa
Hivyo basi tarajia bei ya redmi 12c kuanzia laki mbili na nusu na kuendelea mbele
Kwenye hii post zipo sifa zinazofafanua ubora na vitu vingine vinavyoihusu hii simu
Bei ya Redmi 12C ya GB 128
Redmi 12C yenye RAM GB 6 na memori ya GB 128 inapatakana kwa shilingi 350,000/= kwa Tanzania
Yenye GB bei yake ni ndogo zaidi ambayo ni shilingi 290,000/= ila inakuwa na ram ndogo
Bei ndogo inatokana na simu kuwa na vitu vichache vyenye ubora mkubwa
Hivyo vitu vichache vinaifanya bei kuendana na ubora wa simu
Inachuana na simu ya tecno spark 10 pro kiutendaji
Sifa za Simu ya Redmi 12C
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | IPS LCD, |
Softawre |
|
Memori | eMMC 5.1, 128GB,64GB,32GB na RAM 3GB,6GB,4GB |
Kamera | Kamera mbili
|
Muundo | Urefu-6.71inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 350,000/= |
Upi Ubora wa Redmi 12C
Simu inakuja na machaguo mengi ya memori na inakupa nafasi ya kuipata kwa pesa kidogo
Mbali na hivyo pia utunzaji wa chaji ni wa kiwango cha kulidhsisha
Ukizingatia kuwa inatumia chip ambayo ina matumizi madogo ya chaji
Kamera yake pia ni nzuri kiasi fulani japo si sana
Baadhi ya matoleo yana ram kubwa muhimu kwa kufungua app nyingi kwa wakati mmoja
Yote ya yote ni kuwa usitarajie makubwa sana ukizingatia bei yake ni ya chini
Ila ina vitu ambavyo kwa simu zingine hufanya bei kuwa ya juu zaidi
Uwezo wa Network
Simu inasapoti mtandao mpaka wa 4G si zaidi ya hapo.
Ina jumla ya masafa ya 4G yapatayo tisa ikiwemo yanayotumika na mitandao ya simu nchini
Aina ya 4G simu inayosapoti ni LTE Cat 7 ambayo kasi ya kupakua ni 300Mbps sawa na 37.5MBps na kupakia(upload) ni 100Mbps sawa na 12.5Mbps
Kwa bahati mbaya ni ngumu kwa maeneo mengi Tanzania kupata 4G inayofika 300Mbps mara nyingi utachezea kwenye 75Mbps kama kiwango cha juu
Hata kwa kulinganisha na Redmi Note 12 utaona kuwa kasi ya hii simu sio kwenye uwezo wa Network
Ubora wa kioo cha Redmi 12C
Kioo cha Redmi 12C ni aina ya IPS LCD ambacho resolution yake ni ndogo (720 x 1650 pixels)
Simu ina uangavu unaofikia nits 500
Sio kiwango kikubwa sana cha kuonesha vitu vizrui ukiwa unaitumia simu juani
Kiwango cha refresh rate ni cha kawaida hakifiki 90Hz
Kiujumla ubora wa kioo sio mkubwa ukizingatia kuwa ips lcd huzidiwa pakubwa na vioo vya Amoled
Hasa kwenye uonyeshaji wa rangi nyeusi
Amoled huonyesha rangi nyeusi iliyokolea, yaani inakuwa halisi.
Nguvu ya processor Mediatek Helio G85
Redmi 12C inatumia processor ya Helio G85 ambayo ina core mbili zenye nguvu na core sita zenye nguvu ndogo
Utendaji wake sio mkubwa hasa kama ukiwa ni mpenzi wa magemu makubwa
Itacheza ila unaweza kushuhudia kukwama kwa baadhi ya magemu
Hivyo itakulazimu kucheza kwa kuweka settings ndogo za muonekano wa picha za gemu
Kwenye app ya kupima nguvu za processor ya Geekbench, Helio G85 ina alama 360
Kwangu mimi, chip ikiwa na alama chini ya 500 naiona kuwa ni dhaifu
Hata hivyo ulaji wa chaji sio mkubwa, utaitumia simu kwa muda mrefu
Uwezo wa betri na chaji
Simu inakuja na betri ya ukubwa wa 5000mAh na chaji ya kasi ya 10W
Na kichwa chake cha chaji ni Micro USB (zile ndogo) wakati kwa sasa simu nyingi huja na USB Type C(zile pana)
Kama ilivyotanguliwa kuelezwa kuwa, bei ya simu hii ndogo hivyo usitarajie makubwa
Betri yake inaweza kukaa masaa zaidi ya 14(kwenye intaneti) ikitegemea namna ambavyo unatumia simu husika
Ila wati 10 kwenye chaji itajaza betri kwa masaa zaidi ya matatu
Kwani ina kasi ndogo japo wenyewe xiaomi wanaita kuwa ni fast chaji
Ukubwa na aina ya memori
Kuna matoleo matano ya Redmi 12C upande wa memori
Yenye memori ndogo bei yake ndio inakuwa ndogo zaidi
Aina ya memori ya Redmi 12C ni eMMC 5.1
eMMC 5.1 inasafirisha data kwa kasi ndogo ukilinganisha na memori za UFS 2.1
Hivyo kuna kauzito utakumbana nacho wakati utakopokuwa unafungua vitu vingi kwa wakati mmoja
Japo simu ina mfumo huo wa memori ila processor ya simu inasapoti ufs 2.1 ila redmi hawakuweka
Kwenye Ram utakutana na yenye 3GB, 4GB na 6GB
Ni vizrui ukachukua yenye RAM na memori kubwa kuhifadhi vitu vingi kwenye simu na kuepuka kukwama kwama
Uimara wa bodi ya Redmi 12C
Simu imeundwa kwa bodi za plastiki kama ilivyo kawaida ya simu za daraja la chini
Pia kwenye skrini hakujaainishwa uwepo wa protekta
Inambidi mtumiaji kununua skrini protekta na pia kutumia kava mara kwa mara ili ubora wa simu uwendelee kudumu
Na haina viwango vya IP kitu kinachoashiria kuwa Redmi 12C haina uwezo wa kuzuia maji kupenya ndani
Kiujumla umakini unahitajika pindi utumiapo hii simu kwenye mkusanyiko wa maji au kwenye mvua
Ubora wa kamera
Redmi 12C haina mfumo mzuri wa kamera kama utafananisha na simu zenye kamera nzuri
Fuatilia, orodha ya baadhi za simu zenye kamera bora 2023 uone ubora wa picha na vitu vilivyopo kwenye hizo simu.
Redmi 12C ina kamera mbili ila kiuhalisia ni kamera moja tu ndio inayofanya kazi
Teknoloji ya ulengaji iliyotumika ni PDAF kwenye kamera ya megapixel 50
Inaweza kurekodi video za full hd pekee kwa kiwango cha 30fps ambapo simu za daraja la kati zinakupa zaidi ya hiyo
Ila kwa kulinganisha na bei inayouzwa na simu zilizopo kundi moja, hii ina kamera nzuri vilevile
Utakachokosa kwenye kamera zake ni kukosekana kwa kamera za ultrawide na telephoto
Ubora wa Software
Hii simu inakuja na MIUI 13 ikiwa inatumia mfumo wa Android 12 ambapo kwa sasa tupo kwenye Android 13
MIUI 13 ina vitu vizuri vingi kwa mfano uwezo wa kuscreenshot peji kwa kiwango unachotaka wewe
Kalkuleta yake inatoa chaguo la kutazama mabadilishano ya fedha za kigeni
Ila MIUI inakera kwenye swala la matangazo
Ukifungua app ya file manager unakutana na matangazo
Na pia MIUI ni nzito kiasi fulani, ila bado ni mfumo mzuri
Washindani wa Redmi 12C
Mshindani wa kwanza wa hii simu ni Pixel 3a ambayo kwa sasa unaweza kuipata kwa bei ya chini ya laki tatu
Pixel 3a ni simu inayotoa picha nzuri upande wa kamera na ina kioo kizuri chenye resolution kubwa
Mshindani mwingine ni simu ya Samsung Glaxy A04 na yenyewe ina bei ndogo kuliko Redmi
Na chaguo linigne linalotoa ushinda kwa simujanja hii Tecno Spark 10 Pro
Spark 10 pro ina utendaji unaoendana japokuwa tecno ina bei ya juu kidogo
Lakini ukiwa na tecno unaenda kupata kioo chenye refresh rate inayofika 90Hz
Neno la Mwisho
Kwa wanaotamani simu ya ubora wa kati huku wakiwa na kiwango kidogo Redmi 12C ni chaguo bora kwa sasa
Sio rahisi kupata simu ya GB 128 na RAM ya GB 6 kwa kiwango cha chini ya laki nne
Na pia ni ngumu kupata kupata simu yenye kamera ya wastani kwa bei hii
Na kama bajeti inabana zaidi hii simu inakupa simu mpaka ya memori ya GB 32 japo kwa sasa ni kiwango kidogo
Maoni 8 kuhusu “Bei ya Redmi 12C na Sifa Zake Muhimu”
Nahitaji kuuza redmi yangu ya 12C je niuze kwa sh.ngapi ili ninunue pixel 4a hii simu ni mpya bado ndo kwanza ina mwezi Tu. Naomba ushauri
Hata 320,000 wewe ulinunua sh ngapi?
Natumia Redmi 12C
Nahitajii kubadilii simu yangu aina ya Infinix Smart 7HD NIPATE Redmi 12c 64gb ,unawezekana kubadili??
Kwetu Sisi haiwezekani, Ila yapo maduka ya hivyo mwanza
Nataka redmi 12A GB 128 ram 6 xhingapi mkuu
Naomba kuuliza,nna redmi 13, changamoto iliyopo ni kushindwa Ku download baadhi ya application.Hasa zile za betting.ina download APK zake but kwenye Ku install inagoma.sijajua changamoto yake ni nini?0710801987
Haujaruhusu external source(nje ya playstore) kuweka app kwenye simu