Kampuni ya infinix iliingiza sokoni simu ya Infinix hot 20i mnamo mwezi septemba 2023
Hivyo bado simu changa na ni bei ya infinix hot 20i ni ndogo kwa sababu ni ya daraja la mwisho
Sifa zake nyingi ni za kawaida ambazo kwa mtumiaji mwenye matumizi ya kawaida bado inafaa
Ila kwa mtu anaelenga kuitumia simu kwa mambo mengi sana itamlazimu kutafuta simu mbadala
Bei ya Infinix Hot 20i ya GB 64
Kwa hapa Tanzania Infinix Hot 20i yenye ukubwa uliotajwa inauzwa shilingi 285,000/=
Bei yake inatokana na kutumika kwa vitu vichache vyenye ubora mkubwa amabvyo huchangia gharama kuwa kubwa
Kuanzia processor, kioo, network, aina ya chaji vyote vina ubora wa kawaida
Hivyo ubora wa simu unaendana kwa kiasi kikubwa na kiwango cha pesa kinachohitajika kuipata hot 20i
Kwa mantiki hiyo kuna vitu vizuri na vingine vina ubora hafifu hivyo usitarajie makubwa sana kama ya simu ya Redmi Note 12
Sifa za Infinix Hot 20i
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | IPS LCD |
Softawre |
|
Memori | eMMC 5.1, 128GB,64GB na RAM 2GB,6GB,3GB,4GB |
Kamera | Kamera tatu
|
Muundo | Urefu-6.6inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 285,000/= |
Upi Ubora wa simu ya infinix hot 20i
Ubora mkubwa wa hii simu ni kukaa na chaji muda mrefu
Ikizingatiwa mfumo wake hauna vifaa vinavyotumia nguvu kubwa sana
Inakuja na memori kubwa inayokupa uwezo wa kuhifadhi mafaili mengi
Ni moja ya simu ya 4G inayouzwa kwa bei nafuu
Mengineyo ni ya kawaida
Uwezo wa Network
Hot 20i inasapoti mpaka mtandao wa 4G pekee
Aina ya 4G inayotumia ni LTE Cat 7 ambayo kasi yake ni 300Mbps sawa na 37.5MBps
Kwa maana kama unapakuwa app ya whatsapp kutoka playstore simu inaweza chukua sekunde mbili kumaliza
Ila 300Mbps sio kubwa ukilinganisha na 4G ya LTE Cat 24 ambayo kasi yake inafika 2000Mbps(kwenye samsung s23 ipo)
Hata hivyo kwa hapa nchini si rahisi kupata kasi hizo(300Mbps na 2000Mbps) kwa sasa japo kwa 5G inawezekana
Lakini hii sio ya 5G
Ina masafa matano tu ya 5G ila ni masafa yote yanayotumika na mitandao ya hapa nchini Tanzania
Kwa maana kila mtandao utafanya kazi pasipo na shida
Ubora wa kioo cha Infinix Hot 20i
Kioo cha infinix hot 20i ni cha ips lcd chenye resolution ya 720 x 1612 pixels
Kwa viwango vya sasa hii ni resolution ndogo ukizingatia kioo chenyewe ni cha ips lcd
Zingatia kuwa bei ya hii simu ni ndogo, haiwezi kuwa na kioo cha amoled
Amoled huwa na mkolezo mzuri wa rangi na resolution huwa kubwa
Muonekano wa vitu ni wa kuvutia ukilanginisha na kioo cha LCD
Uangavu wa kioo kwenye hii simu unafika nits 500
Simu itaweza kuonyesha vitu ukiwa juani japo si kwa mwanga mkubwa sana
Nguvu ya processor Mediatek Helio G25
Chip ya Helio G25 ina idadi ya core(sehemu) zipatazo nane zinazotumia muundo wa Cortex A53
Muundo wa Cortex A53 huwa una nguvu ndogo kiutendaji na mara nyingi zinatumika kwa kazi zisizohitaji nguvu kubwa
Hivyo kiutendaji chip ya mediatek helio g25 ina uwezo mdogo kiutendaji
Kwa maana kama unacheza sana magemu utakumbana na changamoto ya simu kukwama kwenye gemu kubwa
Kwa mfano gemu kama PUBG Mobile inaweza isicheze ukiweka resolution kubwa(Ultra high settings)
Ila kwa mambo mengine ya kawaida itaendelea kudunda
Ndio maana app ya kupima ubora ya geekbench inaipa alama 135 ambayo ni ndogo ukilinganisha na chip ya Helio G85 inayofika alama 300
Kwa sababu processor inatumia nguvu kidogo hivyo inakula umeme kidogo kitu kinachorefusha maisha ya betri
Uwezo wa betri na chaji
Simu inakuja na betri ya ukubwa wa 5000mAh aina ya Li-Po
Kama unatumia mara kwa mara kwa kazi za kawaida betri inaweza chukua hata siku kuisha
Chaji yake inapeleka umeme wa wati 10
Ni kiwango kidogo na betri itachukua muda mpaka kujaa
Ukubwa na aina ya memori
Infinix Hot 20i imegawanyika katika matoleo matano upande wa RAM na memori
Ila kwenye memori kuna toleo la 64GB na 128GB na RAM inaanzia 2GB mpaka GB 6
Kiushauri ram ya GB 4 ndio inafaa zaidi na memori kubwa kwa ajili ya kuweza kuhifadhi na kufungua mafaili mengi
Aina ya memori inayotumiwa na hii simu ni eMMC 5.1 ambazo spidi sio kubwa kama memori za UFS
Uimara wa bodi ya infinix hot 20i
Bodi ya hii simu ni ya plastiki upande wa nyuma
Haina viwango vya aina yoyote vya IP vinavyoashilia uwezo wa simu kuzuia maji na vumbi
Hivyo simu ikiingia kwenye maji inaweza kuharibika tofauti na simu ya iphone 14 pro max
Ni vizuri ukawa makini na kuweka skrini protekta kama njia ya kuilinda simu
Na pia kutumia kava kuepusha kupungua kwa ubora wa rangi ya plastiki
Ubora wa kamera
Hot 20i ina jumla ya kamera zipatazo tatu
Kamera kubwa ina kubwa ina megapixel 13 wakati kamera zingine zina resolution ndogo sana na za kizamani
Bila kuzama kiundani ni kuwa kwenye nyanja ya kamera simu haina kamera nzuri kiujumla
Si kwa sababu ya kuwa na 13MP bali ni kukosekana kwa vitu vingine muhimu kama ulengaji wa PDAF na kutokuwepo kwa HDR
Upande wa video kamera zinarekodi video za full hd pekee kwa kiwango cha 30fps
Kwa kuwa hina OIS ni lazima urekodi kwa kutuliza mkono ili video itokee vizuri kama ukirekodi huku ukiwa unatembea
Ubora wa Software
Simu inakuja na toleo la Android 12 na mfumo wa XOS 10.6
XOS 10.6 inakuja na app nyingi za simu baadhi unaweza usizutumie
Moja ya kitu utakachokutana nacho ni matangazo
Na Android 12 ina maboresho ya kuisalama ambapo kama app inatumia kamera kuna icon ya kijani inatokea
Kwa hiyo inakuwa rahisi kujua kama kuna app inatumia baadhi ya vitu pasipo ridhaa yako
Hitimisho
Kwa muhitaji wa simujanja na mwenye bajeti ndogo infinix hot 12i ni moja ya chaguo zuri
Ila inapaswa kuwekwa akilini kuwa kuna vitu vinakosekana na hata hivyo haishangazi kutokana na bei yake
Kama kamera na utendaji ni muhimu sana basi huna budi kutazamia kuongeza bajeti yako ya kununua simu
Zingatia kuwa simu nzuri iliyo kamiri kila idara haiwezi kuuzwa kwa bei ya chini sana
Maoni 3 kuhusu “Bei ya Infinix Hot 20i na Sifa Zake Muhimu”
naitaji simu samsung garaxy s23ultra nakaa mbeya
Nataka namna ya kutumia kamera zote za hii simu nafanyeje
Na nikipiga picha itokee ikiwa vizuri na yenye kupendeza.
Simu nzuri sana