SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

Simu za OPPO za Bei Rahisi na Ubora wake (Simu Kumi)

Bei Nafuu

Sihaba Mikole

April 24, 2022

Hii ni orodha ya simu kumi za oppo za bei rahisi za madaraja ya chini na kati

Bei za oppo zilizopo ni zile zinazouzwa chini ya laki tano

Utaziona simu za oppo ambazo zimetoka kuanzia 2017, 2018 hadi 2022

Ukiijua ubora wa kila oppo ya bei rahisi itakusaidia kuchagua oppo nzuri inayokidhi mahitaji yako ya simu

Simu ya OPPO A16K

Simu ya oppo a16k ni simu ya bei nafuu ambayo imetoka mwishoni mwa mwaka 2021

Ubora wa oppo a16k ni kuwa na kioo kigumu cha aina ya gorilla glass 3

Simu ina utendaji wa chini kwa sababu ina processor ya Helio G35

simu ya oppo a16k

Kioo chake si cha kuvutia kwani ni cha IPS LCD kilichowezeshwa resolution ndogo ya 720×1600 pixels

Simu inakuja na Android 11 na haiwezi kupokea anadroid mpya

Betri lake linatunza chaji muda mrefu kwa sababu lina ukubwa wa 4230mAh

Ni oppo yenye 4G inayokubali mitandao yote ya simu nchini Tanzania

Bei ya OPPO A16K Tanzania

Bei ya OPPO A16K yenye memori ya ukubwa wa GB 32 na RAM ya 3GB ni shilingi 305,000/=

Kwa upande wa maduka ya simu ya mwanza na kariakoo bei yake inaweza kuzidi laki tatu na nusu

Japokuwa ni simu yenye ubora wa vitu vichache

Simu ya OPPO A15

Simu ya oppo a15 ni simu ya macho matatu ya bei nafuu ya mwaka 2020

Ubora wa oppo a15 upande wa kamera ni wa chini

Kwa maana kamera zake hazina dual pixel pdaf na ois wala hazirekodi mpaka video za 4k

simu ya oppo a15

Utendaji wa simu ni mdogo kwa sababu inatumia processor ya Helio P35 na memori aina ya eMMC

Betri yake ina ukubwa wa 4230mAh hivyo simu inakaa na chaji masaa mengi

Kioo chake cha IPS LCD na kina resolution ndogo

Na simu imeundwa kwa bodi ya plastiki upande wa nyuma

Bei ya OPPO A15 Tanzania

Bei ya oppo a15 yenye memori ya 32GB ni shilingi 305,000/=

Ni oppo inayofanana vitu karibu vyote na oppo a16k

Simu ya OPPO A33 2020

Simu ya oppo a33 ni simu ya macho matatu ambayo imetoka mwaka 2020

Kamera zake zina ubora wa chini kwani zina PDAF bila OIS

Simu ina betri kubwa la 5000mAh

Hivyo ukaaji wa chaji unaweza kuchukua masaa zaidi ya 14 ikiwa kwenye intaneti.

simu ya oppo a33

Ukaaji wa chaji wa muda mrefu pia unachangiwa na utendaji mdogo wa simu.

Kwani oppo a33 inatumia processor yenye nguvu ndogo aina ya snapdragon 460

Simu ina kioo ambacho ni chepesi kutachi kutokana na kuwa na refresh rate ya 90Hz

Lakini pia ina kioo cha aina IPS LCD

Bei ya OPPO A33 Tazania

Bei ya oppo a33 ya ukubwa wa 32GB ni shiling 305,000/=

Memori ya oppo a33 ina kasi kwani ni aina ya UFS 2.1

Hivyo bei yake ni nafuu pia

Simu ya OPPO A71

Simu ya oppo a71 ni simu iliyotoka mwaka 2017 hivyo bei yake ipo chini zaidi.

Ni simu yenye kioo kigumu kinacholindwa na gorilla glass 3

Kioo cha oppo a71 ni cha aina ya ips lcd, na simu ni fupi kwa kimo cha inchi 5.2

simu ya oppo a71

Utendaji wa processor ni wa chini sana kwani inatumia chip dhaifu ya Mediatek MT6750

Hii ni simu yenye ubora mdogo wa kamera na betri

Kwani betri yake ina ukubwa wa 3000mAh

Na kamera yake moja inaweza kurekodi video za aina moja tu za full hd

Bei ya OPPO A71 Tanzania

Bei halisi ya oppo a71 kwa sasa ni shilingi 213,388.76/=

Na bei yake inapaswa iwe chini ya laki mbili.

Kwa sabab kuna aina za simu za madaraja ya chini zenye nguvu zaidi na zinauzwa kwa bei nafuu mfano ni itel a58

Simu ya OPPO K10

Simu ya oppo k10 ni oppo mpya ya bei nafuu ambayo imetoka mwezi machi 2022

Ubora wa oppo k10 ni kuwa na utendaji wenye nguvu, kamera zenye lens kubwa, betri imara, kioo chenye uangavu mkubwa na chaji yenye kasi kubwa ya kujaza betri kwa dakika chache.

Kioo cha oppo k10 ni cha aina ya IPS LCD ambacho kina resolution kubwa ya 1080×2412.

simu ya oppo k10

Utendaji wa simu ni wa kuridhisha kwani inatumia processor ya Snapdragon 680 4G

Betri yake inakaa na chaji masaa ya kutosha na spidi yake ya kuchaji inafika umeme wa wati 33

Aina hii ya chaji hujaza betri chini ya dakika 85

Oppo k10 ni simu ya macho matatu ambayo inatumia PDAF kwenye ulengaji

Simu inatumia toleo la android 11 japo ni simu ya mwaka 2022

Bei OPPO K10 Tanzania

Bei halsi ya oppo k1o yenye memori ya GB 128 ni shilingi 457,261.63/=

Ila maduka ya Tanzania wanaweza kuiza kwa bei ya juu kidogo.

Hivyo unaponunua hii simu kwenye maduka ya kariakoo au mwanza inabidi uwe na shilingi 500,000/= kwenda juu

Simu ya OPPO A55

Oppo a55 ni simu ya bei nafuu ambayo imetoka mwishoni mwa mwaka 2021.

Utendaji wa simu ni wa chini kwa sababu inatumia processor ya Helio G35

Inatumia kioo cha IPS LCD ambacho kina resolution ndogo ya 720×1600 pixels

Ni simu ambayo inaweza kuzuia maji yanayotiririka

simu ya oppo a55

Ina kamera tatu, kamera moja(50MP) inatumia PDAF kwa ajili ya ulengaji

Uwezo wa kamera si mkubwa kwani inarekodi video za aina moja tu yaani full hd pekee

Betri ya oppo a55 ni kubwa kwa saizi ya 5000mAh hivyo ukaaji wa chaji ni wa muda mrefu

Ni simu inayokuja na Android 11

Bei ya OPPO A55 Tanzania

Bei halisi ya oppo A55 ya ukubwa wa GB 64 na RAM ya 4GB ni shilingi 457,000/=

Kwa Tanzania tegemea bei kuzidi laki tano hasa maduka ya simu kinondoni na kariakoo

Simu ya OPPO A16

Simu ya oppo a16 ni simu ambayo imetoka katikati ya mwaka 2021.

Kiutendaji simu ina utendaji wa chini kutokana na kuwa na memori za aina ya eMMC na chip ya Helio G35

Betri ya simu ya oppo a16 ina ukubwa wa 5000mAh.

simu ya oppo a16

Hivyo simu itakaa na chaji masaa mengi ikizingatiwa pia ina nguvu ndogo ya utendaji

Kioo cha oppo a16 ni cha aina ya IPS LCD chenye resolution ndogo ya 720×1600 pixels

Ni oppo ya macho matatu yenye kamera zenye resolution ndogo zisizokuwa na OIS

Utendaji wa simu si mkubwa kwani inatumia chip ya MediTek Helio G35 na memori za aina ya eMMC 5.1

Bei ya Oppo A16 Tanania

Kwa Tanzania bei ya oppo a16 inaweza kuzidi laki nne na nusu.

Lakini bei yake halisi kwa masoko mengi duniani ni shilingi 3962,93.41/=

Hivyo kama unaweza kuagiza nunua kwa njia ya mtandao

Simu ya OPPO A54

Oppo A54 ni simu ya macho matatu yenye ubora katika sehemu chache sana.

Kioo cha oppo a54 ni cha IPS LCD chenye resolution ndogo

Simu haina nguvu kubwa kwani inatumia chip ya MediaTek Helio P35

Ni simu inayokaa na chaji masaa mengi kwani ina betri kubwa la 5000mAh

simu ya oppo a54

Oppo A54 ni simu ya mwaka 2021 yenye toleo la android 11

Inakubali mtandao wa 4G wa mitandao yote ya simu nchini

Chaji yake inapeleka umeme wa wastani wa wati 18.

Hivyo betri haitochukua muda mrefu sana kujaa

Bei ya OPPO A54

Bei halisi ya oppo a54 ya ukubwa wa GB 64 ni shilingi 381,051.35/=

Kama ilivyo kawaida kwa Tanzania bei yake inazidi laki nne na inaweza kufika laki nne na nusu

Simu ya OPPO A54s

Simu ya oppo a54s ni simu ya mwaka 2021 yenye kamera tatu

Inafafa kwa kiasi kikubwa na oppo a54 ila kamera oppo a54s natoa picha nzuri zaidi.

simu ya oppo a54s

Oppo A54s ipo ya toleo la aina moja tu lenye memori ya 128GB

Vitu vingine simu inafanana na oppo a54

Bei ya Oppo a54s

Bei halisi ya oppo a54s ni shilingi 486,777.31/=

Bei itakuwa kubwa zaidi kutokana na mkoa ulipo ila kwa Dar Es Salaaam simu inaweza kuzidi laki tano

Simu ya OPPO A31

Oppo a31 ni simu ya mwaka 2019 yenye toleo la android 9

Betri yake si kubwa sana lakini linastahamili kukaa na chaji masaa mengi kwani ukubwa wake ni 4230mAh

Ni simu tenye kioo kigumu kuchunika kwani inatumia kioo cha Gorilla Glass 3

simu ya oppo a31

Kioo cha oppo a32 ni cha aina ya IPS LCD chenye resolution ngodo

Ni simu yenye macho matatu na kamera zenye ubora wa kawaida kama si wa chini

Utendaji wa simu ni wa uwezo wa chini kwa sababu inatumia chip ya Helio P35 na memori aina ya eMMC 5.1

Bei ya OPPO A31 Tanzania

Bei ya oppo a31 ni shilingi 396,293.41/= kwa masoko ya India

Na kwa upande wa Tanzania bei ya simu inaweza ikawa ni pungufu ya hapo

Kwani ni simu ya zamani isiyopokea toleo jipya la android

Maoni 38 kuhusu “Simu za OPPO za Bei Rahisi na Ubora wake (Simu Kumi)

Maoni na Maswali

Email yako haitochapishwa, kwenye alama * lazima pajazwe ili ukomenti

Fuatilia Zaidi

thumbnail oppo

Simu mpya 12 nzuri za Oppo na bei zake 2024

Tangu mwishoni mwa mwaka 2023 mpaka sasa 2024 tayari kampuni ya OPPO toka china wametoa simu zaidi ya 15 za madaraja mbalimbali Hapa utakutana na orodha ya simu mpya za […]

simu mpya

Simu mpya kali 20 na bei zake kwa mwaka 2024

Hii ni orodha ya simu mpya ambazo zimetoka mwaka 2024 ama mwishoni mwa mwaka 2023 kutoka kwa kampuni zipatazo 11 Ni orodha inayohusisha simu za daraja la kati na la […]

No Featured Image

Bei ya sasa ya Oppo A17K na Sifa Zake

Oppo  A17K ni simu iliyotoka mwishoni mwa mwaka 2022 mnamo mwezi oktoba Ni simu ya daraja nafuu ambayo haihitaji bajeti kubwa kuimiliki Kwani bei ya oppo A17K haizidi laki tatu […]

iphone feki 2

Simu Origino ni Zipi na Unazitambuaje? (Hatua za kufuata)

Matoleo ya simu yamekuwa yakitoka mara kwa mara yakiwemo yenye bei kubwa na zinazotamaniwa na watu wengi Aina hizi ya simu huvutia watu wasio waaminifu kutengeneza simu feki zenye ufanano […]

SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani
TUFUATE
Youtube Facebook Instagram twitter

E-mail : simunzuriblog@gmail.com

Simu: +255 683 420 543

Whatsapp: +255 756 077 262

Kabila, Magu

Mwanza, Tanzania

Company