Simu ya samsung galaxy a03s ni simu ya daraja la chini iliyotoka mwaka 2021.
Simu nyingi za daraja la chini huundwa na vitu vichache vyenye ubora mkubwa.
Na bei za simu za daraja la chini huwa zipo chini pia.
Ndio maana bei ya samsung galaxy a03s ni chini ya laki nne.
Hilo linatokana na sifa zake kuanzia utendaji, nguvu ya processor, kioo nk
Bei ya Samsung Galaxy a03s Tanzania
Baadhi ya maduka ya simu ya kariakoo samsung galaxy a03s inauzwa kwa bei ya shilingi 350,000/= mpaka 360,000/=
Ni bei ya Samsung A03s ya GB 64
Ila nchi zingine duniani bei yake ni shilingi 340,000/=
Ni samsung ya bei rahisi ila ina sifa nyingi ambazo haziifikii samsung za gharama
Sifa za Samsung Galaxy A03S
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | IPS LCD, |
Softawre |
|
Memori | eMMC 5.1, 32GB,64GB na RAM 2GB, 4GB, 3GB |
Kamera | Kamera tatu (simu ya macho matatu)
|
Muundo | Urefu-6.5inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 350,000/= |
Upi ubora wa Samsung Galaxy A03S
Ubora wa simu ya samsung a03s unapatikana kwa kiasi kikubwa kwenye betri na software
Software kwa maana ya skin ni nyepesi na rahisi kutumia
Betri yake ni kubwa inayowaza kukaa na chaji muda mwingi
Spidi ya chaji yake haiwezi kuharibu betri
Lakini ubora wa vitu vingine si mkubwa, endelea kusoma hii makala na kuelewa nini ninachokimaanisha
Uwezo wa Network
Simu ya samsung galaxy inakubali mtandao wa 4G aina ya LTE Cat 7
LTE Cat 7 ni aina ya 4g yenye spidi ya kasi inayofikia 300Mbps
Zipo aina nyingi za 4G zenye spidi mara ya nne ya hii.
Kwa kiasi kikubwa ni spidi inayoperuzi na kudownload mafaili kwa kasi
Uzuri wa galaxy a03s ni kuwezeshwa network bands zinazokubali mitandao yote ya simu Tanzania
Ila simu haina 5G, kwa sasa hakuna laini ya simu inayokubali 5G Tanzania
Ubora wa kioo cha Samsung Galaxy A03S
Kama ilivyo kwa simu ya vivo y21, kioo cha samsung galaxy a03s ni cha IPS LCD
IPS LCD ni vioo vizuri lakina havina rangi nyingi.
Kitu kinachosababisha screen kuonyesha baadhi ya vitu kwa rangi zisizo halisi ukilinganisha na vioo vya amoled
Simu haina resolution kubwa sana.
Resolution yake ina ukubwa wa 720 x 1600 pixels
Pia galaxy a03s haina teknolojia inayoboresha rangi zaidi aina ya HDR10
Nguvu ya processor ya simu
Simu ya samsung galaxy a03s inapewa nguvu na processor ya MediaTek Helio P35
Ni processor yenye core nane ambazo zimetofautiana spidi.
Core nne za mwanzo spidi yake inafikia 2.35GHz
Na core nne zingine spidi yake inafikia 1.8GHz
Uwezo wa processor ya MediaTek Helio P35 kiutendaji ni mdogo
Inapata alama chache kwenye app zinazopima nguvu ya processor
Antutu kwa mfano, inaipa alama 100,496
Na GeekBench inaipa alama 171 kwenye core moja
Nguvu ndogo ya chip hii inasababishwa na kutumia muundo wa Cortex A53 kwenye core zote
Cortex A53 ni muundo kwa ajili ya kufanya kazi ndogo.
Hivyo simu hii inapata shida kwenye kucheza magemu yanayohitaji nguvu kubwa ya processor
Uwezo wa betri na chaji
Chaji ya samsung galaxy a03s inapeleka umeme wa wastani wa wati 15
Kiasi cha umeme ambacho kitachukua masaa zaidi ya matatu kujaza betri.
Hilo linasababishwa na betri yake aina ya Li-Po yenye ujazo wa 5000mAh
Simu yenye ujazo wa 5000mAh hukaa na chaji muda mrefu.
Kikawaida ni zaidi ya masaa 13 simu ikiwa muda wote kwenye intaneti
Ukubwa na aina ya memori
Kasi ya memori ya samsung galaxy a03s si kubwa sana.
Kasi ndogo inatokana na aina ya memori ya eMMC 5.1 iliyotumika kwenye hii simu.
Moja ya kitu kinachoathiri utendaji wa simu ni spidi ya memori kwenye kuandika na kusoma data
Samsung a03s zipo za aina nne kwenye memori
- Samsung A03s ya GB 32, RAM GB 2
- Samsung A03s ya GB 32, RAM GB 3
- Samsung A03s ya GB 32, RAM GB 4
- Samsung A03s ya GB 64, RAM GB 4
Kama utakuwa unahitaji kuhifadhi mafaili mengi samsung ya gb 64 ndio inafaa zaidi
Uimara wa bodi ya Samsung Galaxy A03S
Bodi ya samsung galaxy a03s imeundwa kwa plastiki
Hizi bodi huchunika rangi kadri muda unavyoenda
Na zinaweza kupasuka kirahisi simu ikianguka kwa kimo cha mita mbili kutoka juu.
Ni jambo la msingi kuweka kava na screen protector kuipa simu ulinzi wa ziada
Simu ni nyepesi kubeba kwani uzito wake ni gramu 196
Ubora wa kamera
Samsung galaxy a03s ni simu ya macho matatu ya bei nafuu.
Kamera kuu ina ukubwa wa 13MP yenye teknolojia ya ulengaji(autofocus) ya kawaida sio pdaf
Na kamera nyingine ya macro mahsusi kwa kupiga vitu kwa ukaribu ina resolution ndogo ya 2MP
Na kamera nyingine hutumiwa na simu kupima umbali kati ya kamera na kinachopigwa simu
Hizi huitwa kamera za depth, huisaidia simu kujua ukubwa wa eneo linalopaswa kutokea kwenye simu.
Sio kamera muhimu sana sababu ni kitu kinachoweza kufanywa na software
Kamera zake zinarekodi video zenye ubora wa aina moja tu (full hd)
Ubora wa Software
Simu ya samsung galaxy a03s ni simu nyingine ya android 11 inayotumia software ya One UI 3.1 Core
One UI Core ni mfumo wa samsung unatumika kwenye simu zenye nguvu ndogo kiutendaji.
Ni mfumo ambao umeondoa baadhi ya app na kuacha applikesheni za msingi zinazohitajika mara kwa mara.
Kwa mfano Samsung S22 Ultra ina programu ya kufungua magemu, lakini kwenye A03S haipo
Mtindo huu unaongeza utendaji wa simu kiasi fulani
Yapi Madhaifu ya Samsung Galaxy A03S
Simu ya samsung galaxy a03s ina nguvu ndogo kiutendaji.
Ni simu isiyofaa kucheza gemu nzito na kufungua applikesheni nyingi kwa wakati mmoja
Kamera zake hazina OIS wala dual pixel pdaf
Na haziwezi kurekodi video za resolution kubwa
Simu haiwezi kuzuia maji kupenya.
Na bodi yake si imara kupasuka inapodondoka kimo kirefu
Memori zake ni ndogo na zinasafarisha data kwa kasi ndogo
Chaji yake inapeleka umeme mdogo
Neno la Mwisho
Kwa kuzingatia bei, samsung galaxy a03s ni simu ya bei nafuu inayofaa kumilikiwa
Ila unapaswa ujue, zipo simu za laki tatu na nusu zenye utendaji mkubwa kuliko hii.
Mfano ni simu ya Redmi 9T ina processor yenye nguvu na inaweza kusukuma magemu mengi kwa urahisi
Samsung galaxy a03s inamfaa zaidi mtu anayetumia smartphone kwa mara ya kwanza.
Maoni 6 kuhusu “Ubora na bei ya Samsung galaxy a03s (Na sifa zake)”
Bei ya kiyoo cha Samsung’s A03s
30,000 unapata
Wapi unapatikana
Kioo og A03s bei gani?
Nawaze kupata
Unaweza kupata simu.pia napatikana Boko chasimba