SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

Bei ya Simu ya Vivo Y21 na Sifa Zake (2022)

Sifa za simu

Sihaba Mikole

April 14, 2022

Kama unahitaji kumiliki Vivo ya bei rahisi kwa mwaka 2022 Vivo Y21 inaweza ikawa chagua zuri.

Ila linapokuja ubora wa simu, utendaji wake ni wa chini kwa kuzingatia memori na chip

vivo y21 upande wa mbele na nyuma

Simu ya Vivo Y21 ina memori kubwa hata hivyo.

Baadhi ya sifa zake zinakidhi pakubwa mahitaji ya mtumiaji wa simu

Pitia taarifa zote zilizopo kwenye post hii uifahamu vizuri simu.

Bei ya vivo Y21 Taznania

Bei ya vivo y21 inatofautiana kulingana na ukubwa wa memori na ram

Vivo y21 ya gb 64 inauzwa shilingi 410,000/= mpaka 450,000/=

Ni bei ya maduka ya simu kariakoo mitaa ya agrey

Na vivo y21 ya gb 128 bei yake inafika 490,000/=

Bei inaonekana ni kubwa kwa Tanzania ukilinganisha bei ya simu nchini India

Kwani India bei ya juu kabisa ni shilingi 426,884/=

Kiuhalisia sifa za vivo y21 zinaifanya bei yake kuwa kubwa kuliko ubora wa simu yenyewe

Sifa za Vivo Y21

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g, 4g
Processor(SoC)
  • CPU – Mediatek Helio P35 
  • Core Zenye nguvu(4) – 4×2.35 GHz Cortex-A53
  • Core Za kawaida(4) – 4×1.8 GHz Cortex-A53
  • GPU-PowerVR GE8320
Display(Kioo) IPS LCD,
Softawre
  • Android 11
  • Funtouch 11.1
Memori eMMC 5.1, 128GB,64GB na RAM 4GB
Kamera Kamera mbili (macho mawili)

  1. 13MP,PDAF(wide)
  2. 2MP(macro)
Muundo Urefu-6.51inchi
Chaji na Betri
  • 5000mAh-Li-Po
  • Chaji-18W
Bei ya simu(TSH) 450,000/=

Upi ubora wa Simu ya Vivo Y21

Simu ina betri kubwa inayoweza kukaa na chaji kwa masaa mengi ya kutosha

Memori yake inaweza kuhifadhi mafaili mengi

taarifa za vivo y21 kwa njia ya picha

Mfumo wake wa gps una aina nne za gps

Simu ina sehemu ya memori kadi na pia ina redio

Katika nyanja zingine ubora umegwanyika kama utavyoona.

Ni vizuri ukaielewa simu ya Y21 kwa kuzingatia mahitaji yako

Uwezo wa Network

Simu hii ya Vivo inauwezo wa kukubali mtandao wa 4G

Aina ya 4G yake ni LTE Cat 7

network ya vivo y21

4G ya LTE cat 7 inaweza kudownlod faili kwa spidi ya juu inayofikia 300Mbps

Endapo mtandao wa simu unakupa spidi hii, basi vivo y21 itadownload faili la 13ooMB kwa sekunde 39

Si laini zote za simu Tanzania zinakubali intaneti ya kasi(4G) kwenye hii simu.

Kwa sababu ina bands za 4G saba pekee

Ubora wa kioo cha Vivo Y21

Kioo cha vivo y21 ni aina ya IPS LCD.

Kiubora, kioo cha ips lcd kinaundwa na rangi chache.

Kitu kinachofanya baadhi ya vitu kuonekana kwa rangi zisizo halisi hasa rangi nyeusi

Resolution yake ina ukubwa wa kawaida(standard)

Kwani ina pixels 720×1600, vitu vitaonekana kwa ubora mzuri

Nguvu ya processor ya Helio P35

Processor ya Helio P35 ina core nane

Katika core nane kuna core nne zenye spidi kubwa na core nne zenye spidi ndogo

Spidi kubwa inafikia 2.35GHz, na ndogo inafikia 1.8GHz

processor ya helio p35 inayotumia na samsung galaxy a03s

Core zote zina muundo wa Cortex A53

Kiuhalisia muundo wa cortex a53 ni kwa ajili ya kufanya kazi ndogndogo

Kwa hiyo vivo y21 ni simu yenye utendaji wa chini sana kwenye kurekodi video za resolution kubwa.

Na hata kucheza magemu ya simu yenye graphics nyingi(tegemea simu kupata moto)

Uwezo wa betri na chaji

Chaji ya vivo y21 inaweza kupeleka umeme kwa kasi inayofikia wati 18

Hii ni kasi ya wastani.

Kwa umeme huo betri yake inaweza kujaa kwa masaa yanayofikia matatu.

Kwa sababu betri yake ina ukubwa wa 5000mAh

Hivyo ukilinganisha nguvu ya chaji na ukubwa wa betri, itachukua dakika nyingi sana simu kujaa chaji

Ukubwa na aina ya memori

Vivo y21 ina memori aina eMMC 5.1

Kabla ya mwaka 2015, memori za eMMC 5.1 ndio memori zilizokuwa na kasi zaidi.

Lakini baada ya ujio wa aina mpya ya UFS, zimeifanya eMMC kupitwa na wakati

Kuna aina mbili za Y21 upande wa memori

Ipo vivo y21 ya 64GB, RAM 4GB na 128GB, 4GB RAM

Uimara wa bodi ya Vivo Y21

Bodi ya vivo y21 imetengenezwa kwa plastiki.

Bodi za plastiki huwa ni nyepesi kupasuka iwapo simu ikianguaka kwa kimo cha mita mbili.

Na ni bodi zenye changamoto ya rangi kuchunik kadri muda unavyokwenda

Kuongeza ulinzi mtumiaji atalazimika kuweka kava na screen protectot.

Simu ni ndevu na nyepesi kubeba

Kwani uzito wake unafikia gramu 182

Ubora wa kamera

Kuna kamera mbili tu kwenye simu ya vivo y21

Kamera kuu ina sensa ya megapixel 13

Wakati kamera ya macro ina 5MP

kamera ya vivo y21

Kamera aina ya macro hutumika kupiga picha au video ya kitu cha karibu sana na kamera.

Kwa mfano ukitaka kumpiga picha sisimizi na aonekane kwa ukubwa basi kamera  ya macro ndio inafaa zaidi

Na kamera yake kubwa ina ya teknolojia ya ulengaji ya PDAF ambayo si nzuri sana kama multdirection pdaf

Ubora wa Video

Kamera ya hii simu inaweza kurekodi video zenye ubora wa aina moja pekee

Kama unarekodi video utapata video zenye ubora wa full hd(1080) kwa spidi ya 30fps

Hivyo usitarajie kupata video za 4k na 8k kwa spidi ya 60fps

Sababu kubwa ya kushindwa kurekodi video za 4k ni nguvu ndogo ya processor ya simu

Ubora wa Software

Vivo y21 ni simu ya android 11 yenye software ya vivo Funtouch 11.1

Mfumo wa android 11 una applikesheni ya kurekodi screen ya simu,

Ukiwa nayo utapunguza gharama ya bando la kudownload applikesheni za kurekodi screen.

Wakati functouch 11.1 inaiwezesha simu kuongeza ukubwa wa memori ya ram.

Funtouch ina muundo wa kuvutia wa multi tasking(kutumia app nyingi kwa wakati mmoja)

Kwani inazipangilia apps kwa muundo wa row(grids)

Inatengeneza urahisi wa kuhama kutoka app moja mpaka nyingine

Yapi Madhaifu ya Vivo Y21

Kwa kutazama bei yake na sifa zake, simu inakosa vitu vingi sana ambavyo vipo kwenye simu nyingi za laki nne mpaka laki tano.

Kwanza, uwezo wa processor ni wa chini na utendaji wake una nguvu ndogo.

Kioo chake kina resolution  ndogo kwani simu ya bei hii hutumia resolution za Full HD Plus(1080×2600)

Chaji yake inapleka umeme kidogo wakati simu ya redmi note 10 inapeleka umeme wa 33W

Bodi ya simu ni ya plastiki na simu haina viwango vya IP53(kuzuia vumbi)

Kamera zake hazirekodi video zenye resolution kubwa zaidi

Kioo chake kina refresh rate ya kawaida na hakina teknolojia ya HDR10

Neno la Mwisho

Bei halisi ya vivo y21 ilipaswa iwe chini ya 300,000 au isizidi 350,000 kama samsung a03s

Kama utapata chini ya hapo utakuwa umeipata kwa bei stahiki

Lakini kuuzwa juu ya laki nne inaifanya kuwa simu ya gharama sana kuliko ubora

Hiyo ni bei ya simu ya redmi note 10 ambayo ina utendaji mkubwa kuliko y21

Lakini sio mbaya kujaribu kitu tofautii(uzuri wa Functouch)

 

Maoni 3 kuhusu “Bei ya Simu ya Vivo Y21 na Sifa Zake (2022)

  • Sim n nzur sana kiukwel ila je kama kioo cha kamera kimechafuka camera inaonekana kama Haina ubora je unaweza kubadilisha kioo cha camera mfano mm cm yang camera ya nyuma ikipiga picha unakua na ukungu sana je naweza kubadisha kioo cha camera ya nyuma ya mbele ipo saw.

  • Naweza kubadili kioo cha camera ya nyuma maana nikioiga picha inatoka yenye ukungu nahic n kioo cha camera kimechafuka je uweza wa kubadili upo?

Maoni na Maswali

Email yako haitochapishwa, kwenye alama * lazima pajazwe ili ukomenti

Fuatilia Zaidi

No Featured Image

Simu 14 mpya za Vivo za ubora mkubwa na bei zake (2024)

Tangu mwishoni mwa mwaka 2023 mpaka mwaka huu 2024 Vivo imeachia matoleo mengi ya simu Katika matoleo hayo yapo ya bei ndogo, bei ya kati na bei kubwa Kwa maana […]

simu mpya

Simu mpya kali 20 na bei zake kwa mwaka 2024

Hii ni orodha ya simu mpya ambazo zimetoka mwaka 2024 ama mwishoni mwa mwaka 2023 kutoka kwa kampuni zipatazo 11 Ni orodha inayohusisha simu za daraja la kati na la […]

vivo y02t

Bei ya Vivo Y02t na Sifa Zake

Vivo Y02t ni simu ya bei nafuu ambayo imetoka katikati ya mwaka 2023 Bei ya vivo y02t haizidi laki tatu kwa hapa Tanzania kutokana na aina ya sifa ambazo simu […]

Jinsi ya Kutumia GPS kwenye Simu (Hatua kwa Hatua)

GPS kirefu chake ni Global Positioning System, ni mfumo wa utambuzi wa maeneo ambao unasimamiwa na Marekani Simujanja karibu zote zina huu mfumo Una faida kubwa sana hasa kama unajua […]

SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

E-mail : simunzuriblog@gmail.com

Simu: +255 683 420 543

Whatsapp: +255 756 077 262

Kabila, Magu

Mwanza, Tanzania

Company

Find Us On

FB Twitter Instagram