Kwenye hii posti kuna ufafanuzi na orodha ya simu kumi za sony xperia na bei zake kwa mwaka 2022.
Utazifahamu simu za sony ambazo zimetoka kati ya mwaka 2017 mpaka 2021
Ufafanuzi utakujulisha sababu ya simu za sony kuwa na bei kubwa
Lakini pia utaelewa kiundani ubora wa simu aina ya sony experia unaotofautina na simu nyingi za android
Sony Xperia 1
Simu ya Sony Xperia 1 ni simu ya android ambayo ilitoka mnamo mwaka 2019.
Pamoja na kuwa sokoni muda mrefu, sony xperia 1 ni simu yenye utendaji unaozishinda simu mpya nyingi za android za mwaka 2022
Ubora wa simu aina ya sony xperia unachagizwa na processor yenye nguvu ya Snapdragon 855
Pia kioo chake chake cha OLED ambacho kina uwezo wa kuonyesha rangi zaidi ya bilioni moja.
Sony Xperia 1 ni moja ya simu yenye camera nzuri.
Kwa sababu kamera zake mbili kati ya tatu zina teknolojia nzuri ya ulengaji(autofocus) matata aina ya predictive dual pixel pdaf na predictive pdaf.
Na pia kamera zake zinatumia OIS(Optical Image Stabilization) kutuliza video wakati wa kurekodi.
Changamoto kubwa ya sony xperia ni betri yake kukaa na chaji masaa machache.
Hili linachangiwa na betri yake ndogo ya 3330mAh
Simu ya Sony Xperia haipitishi maji kwa muda wa nusu saa kama ikiingia kwenye maji ya kina cha mita moja na nusu
Bei ya Sony Xperia 1
Bei halisi ya sony xperia 1 yenye ukubwa wa 64GB na RAM ya 6GB ni shilingi 555,675.00/=
Hii ni bei inayopatikana aliexpress.
Ubora wa simu hii ya sony unaifanya bei yake kuwa ni nafuu sana.
Sony Xperia Pro-I
Simu ya Sony Xperia Pro-I ni simu ya sony ambayo ina kamera nzuri sana
Xperia Pro-I inakuja na android 11 na ni simu inayokubali mtandao wa 5G
Kioo cha sony xperia pro-i kinaonyesha picha kwa ubora wa juu sababu ya ni kioo cha OLED chenye resolution ya 1644 x 3840 pixels
Betri yake ina ukubwa wa 4500mAh japokuwa simu inakaa na chaji kwa masaa machache.
Utendaji wa xperia pro-i unaweza kusukuma gemu kubwa za simu kwa resolution ya ultra hd bila shida
Inatokana na simu kuwekewa chip ya Snapdragon 888 5G
Sony Xperia Pro-I ni simu yenye uwezo wa kutopitisha maji kwani ina viwango vya IP67
Kamera zake zinaweza kurekodi video mpaka za 4k kwa spidi ya 120fps na full hd kwa spidi ya 240fps
Bei ya Sony Xperia Pro-I
Bei ya sony xperia Pro-I yenye ukubwa wa 512GB ni shilingi 2,741,175.00/=
Gharama kubwa ya simu inasababishwa na processor yenye nguvu na aina ya kioo ambaccho simu inatumia.
Vitu vingi vya sony xperia pro-I vina uimara na ubora mkubwa
Sony Xperia 1 III
Sony Xperia 1 III ni simu ya android 11 inayokubali toleo jipya la Android 12
Xperia 1 III ni simu ya 5G inayokubali network bands za 4G zipatazo 25
Kwa maana simu inaweza kutumika na mitandao yote ya 4G hapa Tanzania
Kioo cha sony xperia 1 iii ni aina ya OLED kinachoongezewa ubora wa kuwa na resolution na refresh rate kubwa.
Refresh rate ya kioo chake ni 120Hz, inafanya simu kuwa nyepesi
Xperia inaweza kucheza gemu zote kubwa kwa ubora wa ultra hd kwa sababu simu ina processor yenye nguvu ya Snapdragon 888 5g
Simu ina kamera nne, tatu zina ulengaji mzuri zaidi sababu zimewezeshwa teknolojia ya dual pixel pdaf
Sony inashika nafasi ya 65 kwa kamera nzuri (Kwa mujibu wa DXOMark)
Ukaaji wa chaji wa xperia 1 iii si mkubwa pamoja na kuwa na betri ya 4500mAh.
Na ina chaji inayopeleka umeme mwingi wa 33W
Bei ya Sony Xperia 1 III
Bei ya sony xperia 1 iii yenye ukubwa wa 256GB na RAM ya 12GB ni shilingi 1,915,769.51/=
Bei yake ni kubwa kwa sababu processor ya simu ina nguvu kubwa
Na kioo cha sony xperia ni vioo vinavyoonyesha picha kwa ubora kitu kinachofanya bei ya kioo kuwa kubwa pia
Sony Xperia XZ3
Simu ya sony xperia xz3 ni toleo la android la mwaka 2018.
Ni simu ya muda mrefu inayoweza kushindana na simu mpya za redmi, oppo, vivo na hata samsung za matoleo mapya ya kati.
Ubora wa sony xperia xz3 unachangiwa na processor ya snapdragon 845 yenye nguvu kubwa.
Ubora wake pia unachagizwa na uwezo wa simu kutopitisha maji kwani xperia xz3 ina ip65 na ip68
Kioo cha sony xperia xz3 ni cha p-oled ambacho kimeongezewa uzuri na resolution ya 1440 x 2880 pixels
Kamera ya simu ya xperia xz3 zinaweza kurekodi video za 4K
Uwezo wa sony xperia xz3 kukaa na chaji ni mdogo.
Kwa sababu betri yake ina ukubwa wa 3300mAh
Bei ya Sony Xperia XZ3
Bei ya sony xperia xz3 ya 64GB na RAM ya ukubwa wa 4GB ni shilingi 1,250,199.33/= za Tanzania
Kisifa simu inaendana sana na sony xperia 1
Hivyo unaweza kuchukua xperia 1 iwapo utaona bei ya xz3 kuwa kubwa.
Sony Xperia 5 III
Sony xperia 5 iii ni toleo la sony linalokubali mtandao wa 5G.
Xperia 5 III ni moja ya simu bora ya mwaka 2021.
Ubora wake upo kwenye nyanja za processor, kioo, ugumu wa bodi, network, kamera na uwezo wa kukaa na chaji.
Processor ya simu aina ya sony xperia 5 III ni Snapdragon 888 5G.
Hii ni chip inayoipa simu nguvu kubwa ya kiutendaji
Simu inatumia kioo cha oled chenye refresh rate kubwa ya 120Hz
Simu ina betri ya 4500mAh inayoweza kukaa na chaji masaa 100 simu ikiwa haitumiki mara kwa mara
Sony xperia 5 III ni simu isiyopitisha maji hata ikidumbukia kwenye kina cha mita moja
Ni sony ya macho matatu yenye mfumo mzuri wa kamera unaweza kuekodi mpaka video za 4K
Bei ya sony xperia 5 iii
Bei ya sony xperia 5 iii ya ukubwa wa 128GB na ram ya 8GB ni shilingi za Tanzania 1,487,976.32/=
Bei ya simu inaendana na sifa zake kwani simu zenye snapdragon 888 5g huuzwa kwa bei inayozidi milioni.
Sony Xperia XZ2
Sony xperia xz2 ni toleo la simu la mwaka 2018
Ni simu yenye uwezo wa kawaida lakini inazizidi simu nyigi mpya za infinix za bei rahisi na bei kubwa
Simu ya sony xperia xz2 ni sony ya kawaida kutokana na aina ya kioo, chip, betri, na chaji
Kioo cha sony xperia xz2 ni cha ips lcd ambacho kiubora kinazidiwa na kioo cha oled
Betri ya hii simu ni ndogo kwani ukubwa wake ni 3180mAh
Simu ina kamera moja inayoweza kurekodi video za 4K kwa spidi 30fps
Bodi yake haipitishi maji kwani ina ip68
Bei ya Sony Xperia XZ2
Sony Xperia XZ2 ya ukubwa wa 64GB ni shilingi 882,493.65/=
Uwezakano ni kuwa bei yake inaweza kushuka zaidi kwa sababu simu ni ya muda mrefu
Ila inaendana na wakati huu.
Sony Xperia 10 III
Simu ya sony xperia 10 III ni simu ya toleo la mwaka 2021 inaweza kupokea toleo jipya la android 12
Hii ni simu ya daraja la kati inayotumia kioo aina ya oled
Simu inakubali mtandao wa 5G
Na ina utendaji mkubwa kwa sababu ya kutumia processor ya Snapdragon 690 5G
Ina betri ya ukubwa wa 4500mAh hivyo ukaaji wa chaji ni wa kuridhisha
Simu inatumia kioo cha oled chenye rangi zaidi ya bilioni
Ni simu ambayo haipitishi maji kwani ina IP68
Sony xperia 10 III ina macho matatu zenye ubora wa wastani
Bei ya xperia 10 iii
Bei ya xperia 10 iii ya ukubwa wa 128GB na 6GB ni shilingi 1,022,983.72/=
Kiushandani simu inaendana na Redmi note 11 pro plus 5G
Ila xperia ina bei kubwa inayosababishwa na ubora wa ziada unaokesakana kwenye redmi
Sony Xperia 5
Sony Xperia 5 ni simu ya mwaka 2019 inayoweza kukubali android toleo la 11
Utendaji wa simu ni mkubwa kwa sababu ina processor yenye nguvu ya Snapdragon 855
Ukaaji wa chaji sio mkubwa kwa sababu simu inatumia betri ndogo ya 3140mAh
Kioo cha sony xperia ni cha oled kinachoonyesha picha kwa ustadi mkubwa
Simu ni ngumu na haipistishi maji
Simu ina kamera tatu zenye ulengaji wenye usahihi mzuri sababu kamera zinatumia predictive Dual Pixel PDAF
Bei ya sony xperia 5
Sony xperia 5 ni simu ya bei nafuu ya sony
Kwani bei yake ni shilingi 544,041.34/=
Japokuwa ni simu ya 2019 lakini ni mara chache kupata simu ya ubora huu kwa chini ya laki sita kwa sasa
Sony Xperia XZ1
Simu aina ya sony xperia xz1 ni toleo la sony la mwaka 2017.
Ni takribani miaka mitano tangu simu imetoka.
Lakini kiubora inaweza kuzishinda simu mpya nyingi.
Kwa mfano, ni simu chache za daraja la kati na chini zinaweza kuzuia maji kupenya
Ila xperia xz1 haipitishi kwani ina viwango vya IP68
Kasoro kubwa ya simu ya xz1 ni betri ndogo ya 2700mAh
Lakini kamera yake inatoa picha bora kutokana na kuwa na Laser AF
Kioo cha sony xperia xz1 ni cha ips lcd ambazo kimeboreshwa na hdr10
Hivyo ubora wa picha kiasi fulani ni mzuri
Bei ya simu ya sony xperia xz1
Bei ya sony xperia xz1 inapaswa iwe chini ya shilingi laki mbili na nusu
Kwa sababu kwa sasa utapata simu hii used na sio mpya
Sony Xperia 10 III Lite
Sony Xperia 10 III Lite ni simu ya mwaka 2021 yenye android 11
Ina utendaji wa wastani kwa sababu simu ina chip ya Snapdragon 695 5G
Kioo cha sony xperia 10 III lite ni aina ya OLED kilicho na ubora zaidi ya kioo cha IPS LCD
Simu ina betri kubwa lenye ujazo wa 4500mAh
Ni simu ya 5G inayokubali network bands za 4G nyingi ikiwemo zote zinazopatikana Tanzania
Bei ya sony xperia 10 iii lite
Bei ya sony xperia xperia 907,007.36/=
Hii ni bei ya sony ya GB 64 na RAM ya GB 6
Maoni 40 kuhusu “Simu za Sony Xperia na Bei Zake Tanzania (2022)”
Nataka simu naipaje
Natka son xperea 1 bei gani
Hizi Kwa sasa nyingi ni used na unaweza pata Kwa 750,000
Son xprea 1
Nina xz1 inafumuka tuu kioo je shida ni nilivo idondosha au Kuna changamoto nyingne ndani???
Uwezekano kuwa kioo kimelegea
Jamn nina sony xperia839a cjajua bei yake naomba niijue
Ok tutakuangalizia
Naomba kujua bei ya kioo cha sony experia xz2
Sony Xperia pro 1 inauzwaje
Naitaji SONY XPERIA 10
Naipataje npo Dodoma
Sony xperia 10 naipataje,nipo mkoani tabora
Nauza sony
Nina sony xperia xz3 na imepasuka kioo kidogo je naweza pata kioo chake na ni bei gani
Nina sony xz1 imezima ghafula wakati ipo kwenye chaji sijui tatizo nini
mimi battery ya sony Xperia sk-o3 imekufa sijui napata wapi
AliExpress zinaweza kuwepo
Kuna simu nilikuwa naitaji sijui naweza kuipataje
Ya Aina gani?
Kiyoo cha Sony xperia so-05k shingapi
Naomba kujua bei ya kioo cha sony xz3 alafu tuwasiliane nijue nakipata vipi niko dar es salaam tafadhali msaada nahitaj sana
Mimi nasimu ya Sony ila kioo nimeambiwa bei sana
Mm nataka simu ya Sony naipataje
Nataka simu Sony nipo dare saslam
Sony Toleo lipi
Naomba Bei ya kioo cha Sonny experia 10 11 (ten two )
Mawasiliano 0782473137 nipo dodoma
Vioo vya Sony ni changamoto nitakuulizia na kukutaarifu
Kiukweli niwapongeze sana kampuni hii inayotengeneza simu aina ya sony kwa simu nzuri na zenye ubora mzuri mimi natumia sony xperia xz1 lakini hiyo simu toka ninunue kwa mtu 150000 yenye gb 64 kiukweli najivunia sana kwa kuwa na simu nzuri ikiwa yenye ubora kwenye kamera na vitu vingine vingi nimetokea kuwapenda kwa ubora wa simu zenu mpaka sasa ninahamasika ninunue nyingine sony mpyaaaaa dukani huku nikivua magamba mimi mwenyewe
Kwanini sony zinabanduka vioo?????
Kama sijaelewa
Nataka kujua bei ya kioo cha Sony Xperia xz1
Sifahamu bei za vioo vya sony
Mambo vipi sony Xperia xz3 inauzwa iko njema sana haina shida location ni dodoma mjini mawasiliano
0679148184
Nataka kioo cha Sony Xperia xz1 number 0776682119 nipo kibaha
Naomba kujua Bei ya simu ya Sony toleo la mwaka 2014
Hizi sifahamu Kwa sasa
Samahani kaka nahitaji plotecta ya Son xperia xz2 Naipataje niko mara Tarime
naweza pata Sony ya laki na nusu
nahitaji sony ya laki na nusu
Hazipo kiongozi