Simu mpya ya samsung galaxy a73 5g ni simu iliyoingia sokoni mnamo aprili 2022.
Ubora mkubwa wa galaxy A73 ni utendaji wa juu wa kusukuma kila aina ya gemu kwa resolution kubwa na kwa urahisi.
Hii ni simu ambayo iko kamili kwenye nyanja karibu zote.
Na mapungufu machache yanaifanya kuwa simu bora ya daraja la kati ya 2022
Kuelewa ubora wa samsung galaxy a73 itakupasa kujua sifa zote za simu na bei yake.
Bei ya Samsung Galaxy A73 5G
Bei ya samsung galaxy a73 5g haipo moja kulingana na memori na ukubwa wa Ram
Galaxy A73 5g ya GB 128 na Ram GB 8 inauzwa shilingi 1,286,295.79/=
Na samsung galaxy a73 5g ya gb 256 na ram gb 8 inauzwa shilingi 1,378,174.06/=
Hizi ni bei za India, kwa Tanzania bei ya simu inaweza ikazidi zaidi ya hapo ikizingatiwa ni simu mpya kabisa
Hakuna swali la kujiuliza kwa kuwa bei inaweza ikawa isiwe rafiki kwa watanzania wengi
Ila ukipitia ubora wa kila nyanja ulioanishwa humu utaona kuwa samsung a73 ni simu bora
Kizuri ni gharama.
Sifa za simu mpya ya Samsung Galaxy A73 5G
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g and 5g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | Super AMOLED Plus, Refresh rate:120Hz |
Softawre |
|
Memori | 128GB,256GB na RAM 8GB,6GB |
Kamera | Kamera nne
|
Muundo | Urefu-6.7inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 1,286,295.79/= |
Upi ubora wa Samsung Galaxy A73 5G
Samsung galaxy a73 5g ina kioo chenye refresh inayoifanya simu kuwa nyepesi wakati wa kuperuzi na kucheza magenu ya simu
Kamera yake ina sensa kubwa inayofaa zaidi wakati wa kuzoom
Simu inatunza chaji muda mrefu sababu ya kuwa na betri lenye ujazo mkubwa
Mfumo wake wa chaji unapeleka umeme wa kasi unaojaza betri ndani ya dakika chache
Simu imewezeshwa na matoleo mapya ya android.
Na itaweza kupokea kila toleo jipya la android kwa miaka minne mfululizo
Uwezo wa Network
Uwezo wake wa network kwa kuzingitia spidi ni wa kasi
Intaneti yake inawezeshwa na modem ya Snapdragon X53 5G Modem-RF yenye uwezo wa kupakua faili kwa spidi inayofikia 1200Mbps(LTE Cat 24)
Japokuwa kwa Tanzania ni ngumu kupata mtandao wa simu unaokupa spidi kubwa kama hiyo
Simu ina uwezo wa kukubali bands karibu zote za 4G, ila kuna network bands 18 za 4G
Kila laini ya simu itakubali kutumika kwenye simu ya samsung galaxy a73 5g kwa ajili ya intaneti ya 4G
5G yake inakubali network bands chache
Ubora wa kioo cha Samsung Galaxy A73 5G
Simu inatumia vioo vya amoled aina super amoled plus.
Mara ya mwisho kwa vioo hivi kutumika ni mwaka 2012
Tangia hapo, amoled ya kawaida ndio kimekuwa kioo cha simu mpya ya samsung kwa miaka mingi.
Kikubwa ni kwamba vioo vya super amoled vinazarisha rangi nyingi sana kwa sababu ya contrast kubwa.
Na uzrui kioo kina refresh rate inayofikia 120Hz.
Refresh rate 120Hz inasaidia kuperuzi kwa kasi kitabu, majina, sms, na kucheza magemu kwa urahisi
Resolution ya simu ni nzuri kuonesha vitu kwa ubora.
Kwani ina 1080 x 2400 pixels, hii hufahamika kama Full HD Plus
Nguvu ya processor Snapdragon 778 5G
Snapdragon 778 5g ni processor ya simu ya daraja la kati ambayo utendaji ni wa hali ya juu.
Kwenye app ya antutu snapdragon 778 ina alama 526,758
App ya geekbench processor ina alama 770 kwenye core moja
Hii inamaanisha simu mpya ya samsung galaxy a73 5g ina utendaji mkubwa kuliko galaxy a53 5g na a33 5g.
Processor inakuja na core nane ambazo zipo core kubwa na core ndogo.
Uwezo wa core kubwa na ndogo unatambulisha utendaji wa processor na ulaji wa umeme wa betri ya simu
Uwezo wa core kubwa
Core zenye nguvu kubwa zipo nne zenye spidi ya 2.4GHz kila moja
Na zimeundwa kwa muundo wa Kryo 670 Gold
Kryo 670 Gold ni muundo wa Cortex A78 ulioboreshwa
Cortex A78 inatumia umeme kidogo kufanya kazi kubwa.
Na ni muundo unaosaidia simu kusukuma gemu ya aina yoyote.
Kwa mfano, simu zenye processor ya cortex A78 zinacheza gemu ya Call of Duty: Mobile kwa resolution kubwa ya UHD na kwa wastani wa 42fps
Gemu ikiwa na resolution kubwa sana baadhi ya simu huchemka na kushindwa kulicheza kwa urahisi
Uwezo wa core ndogo
Kuna core nne zenye nguvu ndogo.
Hizi huwa ni maalumu kwa ajili ya kazi ndogo ndogo simu inazozifanya.
Kwa mfano ukipiga simu, chip hutumia hizi core pekee yake.
Core ndogo zina spidi ya 1.8GHz kila core na zina muundo wa Cortex A55
Cortex A55 huwa inatumia chaji kidogo sana ukilinganisha na A53
Uwezo wa betri na chaji
Samsung A73 inatumia betri aina ya Li-Po lenye ukubwa wa 5000mAh
Samsung wanadai kuwa betri inakaa na chaji kwa masaa 17 simu ikiwa inatumia intaneti masaa mengi mfululizo
Hii simu haiji na chaji
Hivyo utalazimika kununua fast chaji ya samsung ya wati 25
Inaweza chukua chini ya masaa mawili kwa chaji ya wati 25 kujaza betri la 5000mAh
Ukubwa na aina ya memori
Chipset ya snapdragon 778 inasapoti memori za aina mbili.
Yaani UFS 3.0 na UFS 3.1
Yoyote ambayo ipo kwenye galaxy a73, hizo ni memori zenye kasi kubwa ya kusoma(read) na kuandika(write) faili(data)
Memori za UFS husaidia simu kufungua app kwa haraka
Ukiwasha simu ndani ya sekunde chache simu inawaka
Zipo aina tatu za samsung galaxy a73 kwenye memori
- 128GB, RAM 6GB
- 128GB, RAM 8GB
- 256GB, RAM 8GB
Simu inakupa machaguo makubwa ya memori kulingana na matumizi yako
Uimara wa bodi ya Samsung Galaxy A73 5G
Bodi ya samsung galaxy a73 haipitishi maji hata punje kama simu ikizama kwenye kina cha mita moja kwa muda wa nusu saa.
Gorilla glass 5 inaipa ulinzi screen.
Vioo vya gorilla glass 5 vinaweza kuzuia simu kupasuka pindi inapoanguka kwa kimo cha mita 1.2
Uzito wa simu ni gramu 181, ni simu nyepesi kubeba.
Urefu na upana wake unafikia inchi 6.7
Ubora wa kamera
Simu ina kamera nne.
Ni kamera moja tu yenye teknolojia ya OIS inayotuliza video pindi anayerokodi akiwa anatembea.
Teknolojia ya autofocus iliyotumika ni pdaf.
Pdaf haina ulengaji mzuri wa kamera ukilinganisha dual pixel pdaf.
Kwa baadhi ya picha nilizoziona youtube, picha za samsung galaxy a73 zinapiga vizuri wakati wa mchana na usiku.
Inabalansi rangi vizuri na wala huwezi ukaona noises kwenye mwanga mwingi
Kitu kizuri ni kwamba simu inaweza ikatumia kamera tatu kwa wakati mmoja
Hiyo inawezeshwa na ISP ya snapdragon
Ubora wa video
Simu inaweza kurekodi video za aina mbili
- 4k(uhd) kwa 30fps
- 1080(fhd) kwa 30fps au 60fps
Pia kamera zake zinatumia gyro-EIS kutuliza video wakati wa kurekodi.
gyro-EIS inatofautiana na OIS(itafafanunuliwa kwenye makala zingine)
Ubora wa Software
Hii simu ni samsung yenye android 12 na software ya One UI 4.1
One UI 4.1 inasaidia kuongeza ram ya simu
Unaweza ukaongeza ukubwa wa ram mpaka GB 8
Wakati android 12 imeboresha namna ya ku-screen shot
Kwa maana unaweza ukascreen shot kurasa kwa urefu unaoutaka
One UI ni software inayosifiwa kuwa nyepesi na haina matangazo kama MIUI ya xiaomi au HIOS ya tecno
Yapi Madhaifu ya Samsung Galaxy A73 5G
Samsung Galaxy A73 5G haina sehemu ya kuweka earphone.
Hivyo utalazimika kununua adapta kama utahitaji kutumia earphone au earphone za bluetooth
Na haina sehemu ya kuweka memori kadi
Samsung hawajatumia autofocus ya dual pixel pdaf
Display yake haina HDR10 inayorekebisha muonekano wa vitu hasa vilivyopigwa kwenye mwanga mdogo
Kibaya zaidi, utalazimika kununua chaji kwa sababu simu haiji na chaji
5G ya galaxy a73 5g ina bands chache sana, japo nchini mwetu bado hatujaanza kutumia 5g
Neno la Mwisho
Ukiachana na kutekuwepo earphone na chaji, simu ya samsung a73 ni simu bora ya daraja la kati
Mshindani mkubwa wa hii simu ni simu ya xiaomi 12x
Bei ya xiaomi 12x inaizidi kidogo sana a73 5g
Ila ubora wa kioo, network, utendaji, kamera, spidi ya chaji,
Xiaomi 12x inaizidi pakubwa Galaxy A73
Xiaomi inapatikana kwa bei ya 1,393,200/=
Maoni 9 kuhusu “Ubora wa Simu Mpya ya Samsung Galaxy A73 5G[na bei yake]”
Ahsante kwa elimu nzuri bila ada
Ni kweli nzur ila yangu imepata mistar ya kijan inaweza kuondoka nikiianza upya
Mistari ya kijani inaonesha kioo kimepata hitilafu, factory reset haiwezi saidia
Mimi yangu ina green line wala sijaiangusha nimeamka tuu asubuhi nakuta green line ilianza na moja sasa ishafanya kumi
Kioo kimearibika ulinunua sehemu gani?
Mimi yangu ina green line wala sijaiangusha nimeamka tuu asubuhi nakuta green line ilianza na moja sasa ishafanya kumi tatizo nini ila sijaipeleka kwa fundi inanitia uchungu kweli natumia hivohivo
Sasa nifanye nini au nibadidishe kioo
Kaisa, badirisha kioo kitakuwa kimearibika
Kioo cha a735g shiling ngap