SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

Sifa na ubora wa simu ya OPPO A76 (Na bei yake)

Sifa za simu

Sihaba Mikole

April 7, 2022

Simu ya oppo a76 ni toleo jipya la mwaka 2022 kutoka oppo.

Ubora wa oppo a76 upande wa processor unashindana na simu mpya ya Samsung Galaxy A23.

Ni moja ya simu inayokaa na chaji muda mrefu sababu ya kuwa na betri kubwa

Sifa za Oppo a76 zinazizidi mbali sana oppo a92,a55 na a31 kama utakavyoona kila sifa ya a76 baadae.

Japokuwa bei ya oppo a92 ni rahisi kuliko oppo a76

Ipi ni bei ya Oppo A76 Tanzania?

Bei ya oppo a76 ya GB 128 na RAM GB 6 inaanzia shilingi 534,329.92/= kwa masoko ya dunia.

Kwa Tanzania, baadhi ya madauka ya ilala na kariakoo wanaiuza simu ya oppo a76 ya 128GB kwa shilingi  600,000/=

simu ya oppo a76

Swali la kujiuliza,

Kwa nini A76 ina bei kubwa

Sifa zake za kiujumla zinaweza zikakupa jibu na maamuzi sahihi ya kununua ama kutokununua hii simu.

Sifa za oppo a76

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g, 4g and 5g
Processor(SoC)
  • CPU – Snapdragon 680 4G
  • Core Zenye nguvu(4) – 4×2.4 GHz Kryo 265 Gold
  • Core Za kawaida(4) – 4×1.9 GHz Kryo 265 Silver
  • GPU-Adreno 610
Display(Kioo) IPS LCD, Refresh rate:90Hz
Softawre
  • Android 11
  • ColorOS 11.1
Memori UFS 2.1, 128GB na RAM 8GB,6GB,4GB
Kamera Kamera nne

  1. 13MP,PDAF(wide)
  2. 2MP(depth)
Muundo Urefu-6.5inchi
Chaji na Betri
  • 5000mAh-Li-Po
  • Chaji-33W
Bei ya simu(TSH) /=

Upi ubora wa simu ya Oppo A76?

Oppo a76 inatumia memori zinazosafirisha data kwa kasi

Simu ina betri inayosaidia simu kutumika kwa masaa mengi bila kuisha

Chaji ya oppo a76 inapeleka umeme kwa kasi,

Umeme unaojaza betri kwa dakika chache

Kioo chake ni chepesi pale unapatachi simu

Simu ni ndevu na display yake ina resolution kubwa

Kwa kifupi ubora wa oppo a76 upo kwenye display, betri, chaji na memori kwa kiasi kikubwa

Ubora wa Network

Oppo inayozungumziwa hapa ni simu ya 4G.

Pia inakubali mtandao wa 3G na haina 4G

4g ya oppo hii inakubali mitandao yote yenye network ya 4g Tanzania.

Ina network bands kumi(10) za 4g

Bands hizo ni 1,3,5,7,8,20,28,38,40 na 41

Mitandao ya voda, tigo, halotel, ttcl na airtel inatumia bands hizo kwa ajili ya intaneti ya 4g

Ubora wa kioo cha oppo A76

Kioo cha oppo a76 ni cha aina ya IPS LCD

Bei ya kioo cha IPS LCD huwa ni ndogo ukilinganisha na vioo vya amoled

Ila kiubora, vioo vya amoled huwa vina rangi nyingi zaidi

Kioo cha simu hii ni chepesi na kina kasi pindi unapotachi.

Hii inasababishwa na refresh rate inayofikia 90Hz.

Japokuwa refresh rate kubwa hula chaji nyingi lakini inasaidia kuscroll kwa haraka unapokuwa unaperuzi majina(phonebook) ya kwenye simu

Nguvu ya processor Snapdragon 680 4G

Processor ya snapdragon 680 4g ndio ubongo wa oppo a76.

Snapdragon 680 4g ni chip yenye utendaji wa kiwango kati

Si processor ya simu yenye nguvu sana ama nguvu ndogo.

Ni chip yenye core nane na uwezo wa kugfungua kila aina ya app bila kukwama

Chipset ya snapdragon 680 imegawanyika mara mbili.

Kuna upande wenye core kubwa.

Na upande wenye core ndogo

Uwezo wa core kubwa

Kuna core nne zenye nguvu kubwa.

Hizi ni aina ya core zinazotumika pindi simu ikiwa inafanya kazi kubwa.

Kwa mfano ukiwa unacheza gemu ama kurekodi video za 8k au kutumia app nyingi kwa wakati mmoja,

Basi core kubwa hutumika.

Kila core ina spidi inayofikia 2.4GHz

Na core zote zimeundwa kwa muundo wa Kryo 265 Gold

Utendaji wa Kryo 265 Gold ni wa kiwango cha chini ukulinganisha na processor ya Snapdragon 695 5g

Snapdragon 695 5g imeundwa kwa core aina ya Kryo 660

Pitia: simu ya redmi yenye snapdragon 695 5g

Uwezo wa core ndogo

Processor ina core ndogo nne.

Kila core ina spidi inayofikia 1.9GHz

Core zote zimeundwa kwa muundo wa Kryo 265 Silva

Simu inatumia core ndogo inapokuwa inafanya kazi zinazotumia nguvu ndogo

Kazi kama kupiga simu na kutuma sms smartphone haitumii nguvu kubwa

Kiutendaji na matumizi Kryo 265 Silva zinazidiwa na Kryo 660 silva ya snapdragon 695

Uwezo wa betri na chaji

Betri ya oppo a76  ni aina ya Li-Po yenye ukubwa wa 5000mAh

Chaji yake inapeleka umeme kwa kiasi cha 33W

Ni umeme mwingi ila simu ikikalibia kujaa spidi ya chaji hupungua

Chaji nyingi za 33W zinaweza kujaza simu yenye betri la 5000mAh chini ya dakika 80

Kutokana na kutumia chip ya simu yenye nguvu ndogo, oppo a76 inaweza kukaa na chaj masaa zaidi ya 13 simu ikiwa inatumia intaneti muda wote.

Ukubwa na aina ya memori

Moja ya kitu kinachotambulisha uwezo wa smartphone ni aina ya memori.

Memori aina ya UFS 2.1 husafirisha data za simu kwa spidi inayofikia 850MBps

Spidi inayowasha simu kwa haraka na app kufunguka ndani ya sekunde chache

Oppo a76 ina memori aina UFS 2.1

Na zipo simu za aina tatu upande wa memori

  1. Oppo a76 GB 128 na RAM GB 4
  2. Oppo a76 GB 128 na RAM GB 6
  3. Oppo a76 GB 128 na RAM GB 8

Uimara wa bodi ya oppo a76

Oppo ni simu ndefu na sio simu ndogo kama iPhone SE 2022.

Urefu wa oppo unaofikia 6.5inchi unajaa kwenye kiganja cha mkono kwa asilimia kubwa

Simu imeundwa kwa plastiki upande wa nyuma.

Bodi za simu zenye plastiki zina kawaida ya kuchunika rangi

Screen yake haijalindwa na vioo vya gorilla victus kama simu ya xiaomi 12 pro

Hivyo kuna umuhimu wa kutumia kava za simu na screen protector zilizo imara

Ubora wa kamera

Kuna kamera mbili tu kwenye hii simu.

oppo-a76-camera

Kamera ya depth na kamera kuu(wide)

Kamera ya depth hupima umbali kati kamera na kinachopigwa picha.

Umbali uliopimwa unaisadia kamera kuamua upana unaopaswa kutokea kwenye picha

Lakini kuna aina hii ya kamera bora zaidi ya hii kama TOF ya simu ya samsung galaxy s20

Ubora wa picha wa kitu kinachotembea kwa kasi utakuwa mdogo kwenye oppo a76.

Hilo linasababishwa na kamera kukosa teknolojia nzuri aina ya dual pixel pdaf

Ubora wa video

Simu inakosa kamera yenye teknolojia ya OIS

Hivyo mkono unapaswa kutulia pindi simu ikiwa inarekodi video wakati unatembea

Kamera zake zinarekodi aina moja tu ya video kwa spidi ya 30fps.

Aina hiyo ni full hd(1080).

Ulimwengu wa sasa, video za 4k zinatoa video zinazoonyesha picha zenye ubora wa juu zaidi

Ubora wa Software

Oppo a76 ni simu ya android inayotumia android 11

Matarajio ni kuwa simu ilipaswa ije na toleo jipya zaidi la android

Sio mbaya hata hivyo kwa sababu software ya ColorOS 11.1 ina mambo mazuri mengi.

Kwanza ina emoji zilizoboreshwa.

Ukiwa na hii simu hauhitaji app ya ziada kuhamisha mafaili kwa njia ya wifi kutoka kwenye kompyuta kwenda kwenye simu na kinyume chake.

Yapi Madhaifu ya oppo a76

Simu inatumia kioo ambacho kinaenda kupitwa na wakati.

Vioo vya IPS LCD huwa na rangi chache.

Oppo a76 haitumii teknolojia ya HDR10 kurekebisha muonekano wa vitu vilivyopigwa picha

Processor yake haina nguvu kubwa

Network ya hii simu inasapoti bands chache za 4g

Hii inamaanisha simu haitoweza kutumika kwenye baadhi ya nchi na mitandao mengine duniani.

A76 haina kamera kwa ajili ya kupiga eneo pana sana(ultrawide)

Smartphone ya A76 haiwezi kuzuia maji kupenya ndani sababu haina viwango vya IP67 au IP68

Neno la Mwisho

Washindani wakubwa wa simu ya Oppo A76 ni simu zinazotumia processor ya snapdragon 695 5g na MediaTek Dimensity 800

Simu zenye snapdragon 695 5g na MediaTek Dimensity 800 zinaendana na oppo tunayoijadili

Kwa mfano Redmi note 11 pro 5g bei yake inaanzia 600,000/=

Na imekamilika idara nyingi

Kama mtu anapenda kamera na utendaji basi oppo a76 haitofaa na bei yake ni kubwa.

Lakini kwa wapenzi wanaopenda simu zinazotunza chaji basi hii ni simu ya kuwa nayo.

 

Wazo moja kuhusu “Sifa na ubora wa simu ya OPPO A76 (Na bei yake)

Maoni na Maswali

Email yako haitochapishwa, kwenye alama * lazima pajazwe ili ukomenti

Fuatilia Zaidi

thumbnail oppo

Simu mpya 12 nzuri za Oppo na bei zake 2024

Tangu mwishoni mwa mwaka 2023 mpaka sasa 2024 tayari kampuni ya OPPO toka china wametoa simu zaidi ya 15 za madaraja mbalimbali Hapa utakutana na orodha ya simu mpya za […]

simu mpya

Simu mpya kali 20 na bei zake kwa mwaka 2024

Hii ni orodha ya simu mpya ambazo zimetoka mwaka 2024 ama mwishoni mwa mwaka 2023 kutoka kwa kampuni zipatazo 11 Ni orodha inayohusisha simu za daraja la kati na la […]

No Featured Image

Bei ya sasa ya Oppo A17K na Sifa Zake

Oppo  A17K ni simu iliyotoka mwishoni mwa mwaka 2022 mnamo mwezi oktoba Ni simu ya daraja nafuu ambayo haihitaji bajeti kubwa kuimiliki Kwani bei ya oppo A17K haizidi laki tatu […]

iphone feki 2

Simu Origino ni Zipi na Unazitambuaje? (Hatua za kufuata)

Matoleo ya simu yamekuwa yakitoka mara kwa mara yakiwemo yenye bei kubwa na zinazotamaniwa na watu wengi Aina hizi ya simu huvutia watu wasio waaminifu kutengeneza simu feki zenye ufanano […]

SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani
TUFUATE
Youtube Facebook Instagram twitter

E-mail : simunzuriblog@gmail.com

Simu: +255 683 420 543

Whatsapp: +255 756 077 262

Kabila, Magu

Mwanza, Tanzania

Company