Hii ni listi(orodha) ya simu zenye kamera nzuri kwa wakati
Kiuhalisia hizi simu zinaenda kutamba hata mwaka 2027
Kwa hapa tutaorodhesha simu tano (5) tu
Orodha kamili ya simu zote 15 zipo katika hii video
Orodha hii imetokana na tovuti ya DXOMARK na uchambuzi niliofanya kwa kutazama ubora wa picha na video wa simu zipatazo hamsini
Twende kazi
1-Huawei Pura 80 Ultra
Huawei Pura 80 Ultra ina kamera zipatazo nne
Kamera kubwa zaidi ina megapixel 50, kwa asiefahamu anaweza shangaa maana zipo za 200MP
Kitu kikubwa zaidi hii simu ina sensa kubwa sana
Hii sensa imeafanya simu kutoa picha nzuri katika mazingira yote
Itazame moja ya picha iliyopigwa na hii simu kwenye hiyo video juu
Kamera inaweza kuonyesha vitu kwa uhalisia wake
Hivyo eneo ambalo lina mwanga mdogo halijaweza kuzuia vitu visionekane kwa namna inavyotakiwa
Na hata mazingira ya mwanga kamera inatoa kila kitu kwa ubora ule ule
Na haina chengechenga kabisa mpaka uizoom mara nyingi
Bei ya huawei pura 80 ultra ni shilingi milioni tatu na nusu (3,500,000)
2-Motorola Signature 27
Hii ina kamera tatu na sensa zake ni kubwa vilevile
Bei yake ni shilingi milioni na laki sita (4,600,000)
Kwenye video hapo juu kamera yake imerekodi eneo la uwanja
Katika picha vitu ambavyo vipo mbali na kamera vinaweza kutambulika hata ukiizoom
Rangi ya uwanja haina tofauti kabisa na jinsi inavyoonekana na macho ya binaadamu
Hii simu kamera yake inaweza kuonyesha vitu hata katika mazingira ya mvua kubwa
Noises(chengachenga) zinaweza onekana kwenye kiza kingi na kwa kuikuza sana picha
3-Apple iPhone 18 Pro
iPhone 18 Pro ukubwa wa sensa yake inafanana na motorola
Lakini iPhone ina mapungufu kidogo kwa picha za kwenye hafifu
Vitu ambavyo vipo karibu na kamera vinaonakana vizuri na kwa utofauti wa rangi sahihi
Hii na kwa nyakati za usiku
Laki vile vitu ambavyo vimeathariwa sana na giza kunakuwa na kiwango kidogo cha chengachenga
Ndio maana hii ipo katika nafasi ya tatu
Na bei yake ni shilingi milioni tatu na nusu
4-Vivo X300 Pro
Kwenye video na picha niliyoichunguza sana ni ile iliyopigwa usiku ukumbini
Kutoka kwenye hiyo video hapo juu utaona mdada analinganisha hii simu na simu nyingine
Hii simu inaweza kurekodi kitu ambacho kipo mbali sana na kikatambuliko
Yaani mtu anayelengwa anaonekana
Na kitu ambacho kipo mbali na gizani kinaweza kutambuliko
Japo ukiikuza picha hasa za kwenye kiza kuna ubora unaopungua
Bei ya
5-OPPO Find X9 Ultra
Bei ya Oppo Find X9 Ultra kwa Tanzania ni shilingi milioni tatu na nusu
Upande wa kamera zipo nne
Uangavu wa picha ni mkubwa hasa kwenye mazingira ya mwanga mwingi
Na pia ina kiwango kidogo sana cha chenge chenga iwapo utaizoom picha mara nyingi