iPhone 18 Pro imetoka tangu mwezi wa tisa
Imebadilika maeneo machache sana
Kiasi cha kwamba unaweza usione tofauti na toleo la iPhone 17 Pro
Hata hivyo bei ya iPhone 18 Pro imekuwa zaidi
Kikubwa tupitie sifa zake muhimu halafu tutathmini iwapo inafaa kuimiliki
Bei ya iPhone 18 Pro GB 256
iPhone 18 Pro inauzwa shilingi milioni nneĀ na laki tano
Hii ni yenye ukubwa wa GB 12
Bei ni ya kushtua ila kwa nini hii simu ina bei kubwa sana

Kupata jibu inatubidi tuangalie sifa zake muhimu
Lakini sio sifa pekee zilizosababisha bei kubwa kuna sababu zingine
Tufuatilie sifa zake kwanza
Sifa za iPhone 18 Pro
| Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
|---|---|
| Network | 2g, 3g, 4g, 5g |
| Processor(SoC) |
|
| Display(Kioo) | LTPO Super Retina XDR OLED, Refresh rate:120Hz |
| Softawre |
|
| Memori | NVMe, 256GB, 512GB, 1TB na RAM 12GB |
| Kamera | Kamera TATU
|
| Muundo | Urefu-6.3inchi |
| Chaji na Betri |
|
| Bei ya simu(TSH) | 4,500,000/= |
Uwezo wa network
Kwa mara ya kwanza apple wameweka modem yao
Kila simu ina modem ambayo hutumika kuingia kwenye intaneti
Lakini kwenye Pro Max bado modem ya qualcomm inatumika
Inasapoti aina zote za mtandao wa 5G aina zote
Kuna baadhi ya watumia wa iPhone wanalalamika C2 imepungua spidi
Unaweza kufuatilia mjadala hapa
Nguvu ya utendaji
iPhone 18 Pro ina utendaji mkubwa sana
Imetengenezwa kuhimili mifumo ya AI inayoambatana na simu
Kwa maana hii simu itakuwa inaweza kutumia vizuri AI za offline

Yote haya yamesababishwa na iPhone 18 Pro kutumia prosesa yenye muundo mpya
Prosesa hiyo inaitwa Apple A20 Pro
Muundo wake umifanya kuwa na nguvu sana na utumiaji mdogo wa umeme
Ubora wa kioo
Kioo chake ni cha aina ya OLED
Kama vioo vya miaka iliyopita

Kiujumla muonekano wa vitu upo “deep” sana
Ubora wa kamera
iPhone 18 Pro ina kamera tatu
Ambazo ni telephoto, ultrawide na kamera kuu
Maboresho ya kamera yapo kwenye muundo wa kamera

Kamera ya sasa hivi unaweza kuamua kiasi cha mwanga kamera ipate
Hii inafaa zaidi kwa watu wanaojishughulisha na upigaji wa picha
Mambo mengine ni AI inayosaidia kuondoa vitu usivyovihitaji vitokee kwenye picha
Uwezo wa betri na chaji
Kimakadirio iPhone 18 Pro inadumu na chaji takribani masaa 14
Huu ni muda simu ikiwa inaperuzi intaneti muda wote
Ni tofauti na simu za China kama Realme P4 Power
Realme P4 Power inamaliza masaa 24 kwa kuperuzi
Apple iPhone 18 Pro inasapoti mpaka wati 25 upande wa chaji
Kwa nyakati hizi ni kiwango cha kawaida sana
Hata hivyo betri yake inawahi kujaa sababu ina ukubwa wa 4056mAh
Uimara wa bodi
iPhone 18 Pro ni himilivu sana inapoanguka
Inahitaji mazingira mabaya mpaka ipasuke kiasi cha kutotumika
Ukichunguza baadhi ya video za Youtube utaona watu wanaziangusha simu kwenye kimo kirefu

Na baada ya kuanguka tachi ya simu bado inafanya kazi
Lakini ifahamike ni muhimu kuwa makini
Maana simu inaweza kuharibika mazingira usiyoyatarajia kabisa
Ubora wa software
iPhone 18 Pro inaendeshwa na mfumo wa iOS 26
Mfumo wa iOS 26 imeipa matumizi mengi sana ya AI hii simu

Moja ya kitu ambacho kipo ni kunnunua bidhaa mtandaoni kwa kuskani picha
Na kitu kingine ni uwezo wa kutengeza shortcut
Kwa mfano kama kuna aina ya setting iko mbali iOS 26 inakupa fursa ya kutengenezea shotcut yake
Washindani
Kwangu mimi naziona iPhone 17 Pro na Samsung Galaxy S26 Pro
iPhone mpya ina bei kubwa sana
Na maboresho makubwa yapo kwenye software
Na kwa bahati nzuri mtumiaji wa iPhone 17 Pro atapata iOS 26
Ni ngumu kuhamia kwenye iPhone hii mpya
Neno la mwisho
Simu za iPhone kiujumla bado ni simu bora
Lakini hakuna ule ubunifu mkubwa wa kimapinduzi kama ilivyokuwa nyuma
Bado mabadiliko ni ya kiwango cha kawaida