Google Pixel 11 Pro imewasili
Lakini kuna jambo moja litakalokufanya ufikilie kununua hii simu.
Jambo hilo ni bei yake.
Bei ya Google Pixel 11 Pro ni shilingi milioni 3 kwa bei ya kimataifa
Kwa pesa kama hiyo, tayari unaanza kujiuliza:
Pixel 11 Pro ina nini cha kipekee kiasi cha kustahili pesa ya kiwanja?
![]()
Je kamera ina ubora kiasi gani, utendaji, betri, kioo, na mifumo ya software vina thamani hiyo
Na je vina ubora unaokulazimisha kulipa milioni tatu?
Hebu tuichambue Pixel 11 Pro kipengele kwa kipengele na tuone kama hii ni simu ya kulipia milioni 3—au ni pesa nyingi kwa jina la Google tu.
Bei ya Google Pixel 11 Pro GB 256
Kwa Tanzania bei ya Google Pixel 11 Pro inafika milioni 3.5
Ukubwa wa RAM ni GB 12
Kiwango hiki kinakuhakikishia matumizi yasiyo na mkwamo
Kwa maana simu inakuwa smooth
Pia kuna matoleo ya ukubwa wa GB 512 na hata 1TB (GB 1000)
Uwezo wa network
Google Pixel 11 Pro inasapati aina zote za network
Ni simu ya laini mbili
Ila moja utalazimika kuweka ya eSIM
Haya hapa maaelezo ya eSIM
Ubora wa kioo
Ujue kuna vioo vya simu rangi zake sio halisi kihivyo
Kwa maana vinakuwa na kina kidogo cha rangi
Lakini kuna vioo vina utajiri mkubwa wa rangi na hivyo vitu kuonekana kwa ustadi
Mfano kioo cha Google Pixel 11 Pro
Kioo cha hii simu ni aina ya OLED na resolution ni kubwa
Na kimeboreshwa kwa uwepo wa HDR10+
Ila hii hdr10+ ni kitu gani, majibu yake haya hapa
Nguvu ya utendaji
Google Pixel 11 Pro ina nguvu ya kufanya vitu vingi bila shida
Na imeboresha mifumo yake ya kupooza simu inapopata joto
Lakini kuna jambo Google Pixel kama wamekwama
Ni hivi
Ukifananisha utendaji na simu za apple, na zile za Qualcomm ama mediatek. Google ipo nyuma
Simu za iPhone 17 Pro, Xiaomi 17T Pro na Honor 600 Pro zimeonyesha utendaji mkubwa zaidi
Hata hivyo hakuna tofauti kubwa kiasi cha kuleta shida katika matumizi ya kila siku
Uimara wa bodi
Tukianza na uimara wa kioo
Simu ina kioo kilichoongezwa tabaka gumu a kuzuia kuchunika
Na pia kioo kimeundwa kuhimili kupasuka ikianguka usawa wa kimo cha kiuno cha mtu mzima
Ukiwa umeingusha kwenye ndoo ya maji Pixel itaweza kuzuia maji
Kwa maana ina cheti IP68
Kiujumla simu ni imara
Lakini umakini unahitajika bila kujali simu ina uimara aina gani
Ubora wa kamera
Google Pixel 11 Pro ina bonge la kamera
Simu inapiga picha zenye rangi halisi pasipo kukoleza rangi
Hata mazingira ya mwanga hafifu ubora wa picha bado unabaki kuwa mkubwa
Unaweza kuzitazama hizi picha mbili hapa chaini

Kiujumla simu ina kamera zipatazo tatu
Na kamera kubwa ina megapixel 50
Uwezo wa chaji na betri
Google Pixel 11 Pro ina betri kubwa na chaji yenye kasi
Betri yake ina ukubwa wa mAh 4850
Ila ukilinganisha na simu ya Oppo Find X9 Pro, Google Pixel ipo nyuma sana kwenye utunzaji wa chaji
Ifuatalie hapa Oppo Find X9 Pro
Maana Oppo Find X9 Pro ina bonge la betri la 10,000mAh
Ubora wa software
Simu inakuja na Android 17
Hii simu mfumo wake umejikita sana kuifanya Gemini kuwa AI inayotumika zaidi
Maana kwenye “home screen” kuna AI ya gemini
Kiasi cha kwamba mtumiaji wa Pixel 11 Pro anaweza akawa anaitumia ChatGPT mara chache
![]()
Google wamefanya app kuweza kuwasiliana
Mfano app ya message na calendar zinabadilishana taarifa
Washindani
Simu za China zinazotumia prosesa za Snapdragon 8 Elite na Mediatek dimensity 9500
Hizi simu zina bei ndogo kuliko pixel
Wakati huo kiutendaji na ukaaji wa chaji simu za kichna zimekuwa vizuri sasa hivi
Lakini pia simu za iPhone zinauobonda mwingi
Kwa hiyo ni chaguo lako kuona ipi inafaa na kuiependa
Neno la mwisho
Ujio wa Google Pixel 11 Pro umekuja na hisia tofauti
Wapo wanaoiponda hii simu
Kwa mimi, sioni haja ya kuwa na hii simu kama una Google Pixel 10 Pro
Kuna tofauti ndogo sana