Ukilinganisha na Tecno Camon 40, Camon 50 imeboreshwa upande wa betri, uimara wa bodi na kioo
Hizi ndizo kubwa sifa ambazo zimetengeneza utofauti wa bei ukiondoa utofauti wa kimuonekano
Ukishaiona bei ya Tecno Camon 50 na sifa zake kuu inaweza kukushtua
Ila ni muhimu ukafahamu kwa uzuri sifa zote na washindani ujue kama ni bei sahihi kwako
Bei ya Tecno Camon 50 ya GB 128
Kwa Tanzania Tecno Camon 50 inauzwa shilingi laki nane na nusu (850,000)
Hii ikiwa na ukubwa wa RAM wa GB 8
Ukubwa wa RAM unaashairia Camon 50 kuwa ni simu ya utendaji mkubwa
Kwa maana hiyo sifa zingine sio ndogo
Bei yake inakupasa upitie kila sifa ili ujilidhishe iwapo inakufaa
Sifa za Tecno Camon 50
| Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
|---|---|
| Network | 2g, 3g, 4g |
| Processor(SoC) |
|
| Display(Kioo) | Super AMOLED, Refresh rate:144Hz |
| Softawre |
|
| Memori | 128GB, 256GB na RAM 12GB, 8GB |
| Kamera | Kamera mbili
|
| Muundo | Urefu-6.7inchi |
| Chaji na Betri |
|
| Bei ya simu(TSH) | 850,000/= |
Uwezo wa network
Tecno Camon 50 inasapoti mpaka mtandao wa 4G
Inatumia laini za kawaida na haisapoti laini za eSIM
Pia kama unataka 5G hii simu haina bali toleo lingine
Ukija kwenye 4G, kasi yake inafika hadi Mbps 600
Kama mtandao unakupa kasi hii basi itatumia sekunde 15 kupakua faili la GB 1
Lakini mitandao mingi kwa Tanzania kasi huwa chini ya 100Mbps
Ubora wa kioo
Kioo cha hii simu ni cha amoled
Huwa kina kikubwa cha rangi na hoonyesha rangi za vitu kwa usahihi mkubwa
Na kitu kizuri zaidi kioo hiki kina refresh rate kubwa ya 144Hz
Kwa kifupi ni kioo kizuri japo hakina teknolojia ya hdr
Nguvu ya utendaji
Tecno Camon 50 ina utendaji wa wastani
Karibu kila aina ya gemu kubwa inaweza kucheza kwenye hii simu
Lakini utendaji wake hauwezi kusukuma gemu vizuri kwenye graphics zenye uangavu wa 1080p
Lakini kwa vitu vingine simu ni himilivu
Kwa sababu prosesa ya Mediatek Helio g200 ultimate inajitahidi kiasi chake
Uimara wa bodi
Tecno Camon 50 ina waterproof
Waterproof inaweza kuzuia maji hata simu ukiizamisha kwenye kina cha mita 2
Uvumilivu huu unadumu kwa muda wa nusu saa
Hata hivyo unahitajika kuwa makini hasa ikizama kwenye kina kikubwa zaidi
Simu haijaanishwa kama ina screen protekta ila ni vizuri kununua hata kama inayo
Ubora wa kamera
Kamera za hii simu zinapiga nzuri
Japo ina kamera mbili aina ya wide na ultrwide
Haina kamera ya kulenga vitu vilivyo mbali
hivyo mtumiaji atalazimika kui-zoom simu kwa kiwngo fulani
Hii simu ina rekodi video za uangavu wa full hd
Na hairekodi video 4K na pia inakosa OIS kwa ajili ya kutuliza kamera ukiwa unarekodi video huku unatembea
Uwezo wa betri na chaji
Camon 50 inakuja na bonge la betri la ukubwa 6150mAh
Kwa hiyo ina ongezeko la muda wa ukaaji chaji
Ila uwezo wa kuchai inabaki kuwa ni wati 45
Hii pia inajaza betri ndani ya muda mfupi kama dakika 60
Ubora wa software
Tecno Camon 50 inatumia mfumo wa Android 16 ukiendesha mfumo wa HIOS 16
Hakuna kitu kikubwa sana ukiondoa mifumo mbalimbali ya AI
Na hii simu itakuwa inapokea matoleo mapya ya Android kwa miaka mitatu
Kupata matoleo mapya kunaisadia simu kuondoa kasoro zilizopo na kuiboresha simu na vitu vipya
Simu Mbadala
Kwa mtumiaji wa Tecno Camon 40 anaweza asishawishike kununua Camon 50
Vitu vingi kwenye hizi simu mbili havina tofauti
Mshindani mwingine ni Samsung Galaxy A17 5G
Hii inakupa laini ya eSIM na mtandao wa 5G pia bei yake ipo chini
Na simu nyingine ni Redmi Note 15 ambayo ina sifa nyingi zaidi nzuri
Na bei yake ni shilingi laki saba
Neno la mwisho
Tecno Camon 50 ni simu nzuri
Ila kwa bei yake ilipaswa ije na vitu vya ziada
Hasa kwenye utendaji
Simu nyingi za laki nane huwa na 5G na kioo chenye hdr10+