Katika pitapita zangu na kuchunguza simu bora za bei ndogo na ya chini nimekuja kugundua kitu cha kustahajabisha kidogo
Wapenzi wa iPhone wenye bajeti ndogo wananunua iphone used hazipokei maboresho ya mfumo endeshi mpya wa IOS
Aina hii ya simu haipokei Whatsapp mpya na zingine kuanzia mwakani hazitokuwa zinapokea whatsapp mpya
Basi hii posti inaorodhesha simu za iphone za bei rahisi zinazofaa kununuliwa kwa mwaka 2024 kwenda mbele
Iwapo unataka kumiliki yenye kupokea iOS mpya basi fuatilia hapa
iPhone nzuri za bei ya chini
Usiishie hapo, fuatilia posti yote uone vitu vya muhimu vilivyopo kwenye hizi simu.
Apple iPhone 8
iPhone 8 ni simu ya mwaka 2017 ambayo bei yake ni shilingi 300,000 ya GB 64
Utendaji wa iPhone 8 unazipiku simu nyingi mpya za madaraja ya chini na ya kati
Kwani processor yake ya Apple A11 Bionic ina alama 935 kwenye ya Geekbench, alama ambazo hazifikiwi na chip ya Helio G99 iliyotumika kwenye simu za tekno spark za 2023.
Inapokea mfumo endeshi mwisho wa iOS 16.7.5, kumbuka iOS mpya ni iOS 18
Hata hivyo kiasi iOS 16 inakupa uhakika wa kuendelea kupata maboresho ya apps kwa miaka mingi
Betri yake sio kubwa kwani ina mAh 1821, ukaaji wa chaji sio wa kuridhisha pia chunguza kipengele hiki unaponunua kwa mtu
Kitengo cha kamera simu inaweza kurekodi video za 4K
Ila ubora wa picha sio mkubwa kivile.
Unapoikuza picha kuna chengachenga zinaonekana kwa wazi halafu kuna mwangaza mwingi(overexposure)
Hata hivyo kwa viwango vya simu za daraja la kati za sasa simu inapiga picha nzuri
Apple iPhone 8 Plus
Simu ya iPhone 8 Plus ilitoka mwaka 2017 kama iliyvo mtangulizi wake
Kwa sasa bei ya iPhone 8 Plus ya GB 64 ni shilingi 350,000
Na yenyewe inatumia chip ya Apple A11 Bionic hivyo utendaji ni mzuri pia
Yaani inaweza kusukuma gemu nyingi pasipo kukwama kwama
Pia inapokea mpaka toleo la iOS 16.7.5
Ina kamera moja tu na ina OIS pia inatumia PDAF
Ubora wa picha pia ni wa kawaida, picha ni nzuri ila kuna changamoto zilezile za iphone 8
Apple iPhone X
iPhone X ilitoka rasmi mwezi novemba 2017 ikiwa ni boresho la matoleo ya iphone 8
Vitu vilivyoboreshwa ni skrini(kioo) , betri na kamera kama utakavyoona
Bei ya iPhone X ni laki sita ya GB 64 na unaweza ipata chini ya hapo
Inapokea hadi toleo la iOS 16 na haipokei toleo jipya la iOS 18
Kumbuka iOS 16 inatosha sana kuipa simu thamani kwa miaka ijayo
Betri yake ni kubwa kidogo, ina mAh 2716
Simu za zamani afya ya betri hupungua kadri muda unavyoenda
Kuna maboresho makubwa sana kwenye kamera
Kwani kwa mara ya kwanza apple walianza kutumia ulengaji wa dual pixel kwenye kamera kuu
Hata hivyo ubora wa picha hauna tofauti kubwa na iPhone 8 au iPhone 8 Plus
Apple iPhone XR
Simu ya iPhone XR ni toleo la iPhone la mwaka 2018
Bei ya iPhone XR ni shilingi laki saba ila kwa mtu unaweza ipata hata kwa laki tano
Kwenye utendaji iPhone XR inaitoa inachuana na Samsung Galaxy A55
Hii inatokana na iPhone XR kutumia processor ya Apple A12 Bionic yenye alama 1290 kwenye Geekbench
Kwa maana iphone xr inaendana kiubora na matoleo yaliyotoka kati ya 2023 hadi 2024 ya daraja la kati
iPhone XR inapokea mpaka toleo jipya kabisa la iOS 18,thamani yake bado inaridhisha
Betri yake ni kubwa ya kukaa na chaji muda mrefu kwani ina mAh 2900
Ina kamera moja upande wa ubora maboresho yapo hasa kiwango cha noise ni kidogo
Apple iPhone XS
iPhone XS iitoka mnamo mwaka 2018
Bei yake ni shilingi laki sita ila kwa bei ya mkononi unaweza ipata kwa chini ya hapo
Utendaji una nguvu ya kufanya vitu kwa ufanisi kutokana na kutumia chip ya Apple A12 Bionic
Upande wa software, iPhone XS inaweza kupokea hadi iOS 18
Betri yake sio kubwa kama iPhone XR, ukubwa wake ni 2600mAh
Kamera yake inaweza kurekodi video za 4K
Hata hivyo ubora wa kamera ni mzuri ila sio wa kiwango kikubwa
Maana ukiikuza picha kuna chengachenga zinaonekana
Apple iPhone XS Max
Apple iPhone XS Max na yenyewe ilizinduliwa mwaka 2018, ni toleo bora kati ya matoleo ya iPhone X
Bei yake ni shilingi laki saba kwa hapa Tanzania
Processor inayotumia ni Apple A12 Bionic, nguvu yake ya utendaji ni kubwa
Inapokea hadi toleo la iOS 18 hivyo basi hata matoleo mapya ya app simu itakuwa inayapata kwa miaka mingi
Betri ya iPhone XS Max na lenyewe sio kubwa kwani lina ukubwa wa 2600mAh
Ina kamera mbili zinazotumia ulengaji wa dual pixel pdaf na uwezo wa kurekodi video za 4K
Ubora wa picha ni mzuri japo noise zipo hata kwenye mwanga mwingi
Apple iPhone 11
Simu ya iPhone 11 ilitoka rasmi mwaka 2019, hili toleo lina ubora zaidi ukilinganisha na matoleo ya nyuma
Bei ya iphone 11 kwa mwaka 2024 ni shilingi laki nane yenye GB 128 na ikiwa ni used
iPhone 11 ina nguvu kubwa sana ya kuweza kufungua app ya aina yoyote bila kukwama
Hii inatokana na simu kutumia processor yenye nguvu, chip hiyo ni Apple A13 Bionic
Kuna app za kupima nguvu za processor ambazo ni Antuntu na Geekbench
Kwenye antuntu Apple A13 Bionic ina alama 870K, na geekbench inaonyesha chip inaweza kufungua kurasa 87 kwa sekunde bila kuganda
Hii ni namba kubwa, simu nyingi mpya za daraja la kati hazifikii kiwango hiki
Simu inapokea toleo jipya la iOS 18 na itapokea toleo litakalofuata
Ina betri yenye ukubwa wa 3110mAh
Kamera zake zinapiga picha nzuri na inajitahidi kuonyesha rangi kwa usahihi mkubwa
Apple iPhone 11 Pro
Apple iPhone 11 Pro na yenyewe ilitoka mwaka 2019 ikiwa na kamera tatu
Bei ya iPhone 11 Pro ni shilingi laki tisa na elfu ishirini
Utendaji wake una nguvu kwa sababu inakuja na chip ya Apple A13 Bionic
Kama ilivyo kwa iphone za mwaka 2018 kwenda mbele, iPhone 11 Pro inapokea toleo hadi la iOS 18
Betri yake ina ukubwa wa 3046mAh
Kamera ya iphone 11 Pro inatoa picha nzuri hata katika ya mwanga hafifu
Moja ya kamera yake inatumia chip ya dual pixel pdaf na inaweza kurekodi za 4K kwa kiwango cha 60fps
Apple iPhone 11 Pro Max
Apple iPhone 11 Pro Max ni simu ya daraja la juu kwa mwaka 2019
Hivyo bei yake kwa wakati huo ilikuwa kubwa ila kwa sasa imeshuka
Bei yake pia inachagizwa na uwepo wa processor ya Apple A13 Bionic
Bei ya iphone 11 pro max ni milioni moja na laki tatu ila wapo wanaouza hadi laki tisa
Hii ikiwa na ukubwa wa GB 256
Ni iphone ya mwanzo kuja na betri kubwa
Betri yake ina ukubwa wa 3969mAh
Ubora wake wa kamera ni mkubwa ukizingatia moja lenzi yake ni ya optical lenzi
Hitimisho
Hizi ndizo iphone za kumiliki kwa sasa epuka kununua iphone ambayo haipokei maboresho ya iOS
Simu za iphone ni tofauti sana na simu za Android kutokana na kuwa na restrictions nyingi
Kwa kifupi acha kununua iphone inayoishia na mfumo endeshi wa iOS 12, UTANISHUKURU.
Maoni 5 kuhusu “iPhone za bei rahisi za kumiliki kwa sasa(2024-2027)”
Nimeipenda
Ni i phone ni simu nzur san
Nimeipenda hy 11 pro max
Bado ni simu yenye ubora
I phone 11 pro Max