Kisifa Samsung Galaxy S24 Plus ina sifa nyingi zinazoendana kwa kiasi kikubwa na Samsung Galaxy S24 Ultra
Kwa maana Galaxy S24+ ubora wake unazipita simu nyingi na mkubwa, hivyo bei yake imechangamka pia
Kwa Tanzania, bei ya Samsung Galaxy S24 Plus ni shilingi milioni mbili na nusu, hii ni bei ya Samsung yenye ukubwa wa GB 256
Bei hii ni kubwa kuliko Infinix Hot 40 Pro ya GB 256 na kinachofanya bei ya Samsung kuwa ni sifa zake ambazo ni kubwa sana
Kuanzia kamera, utendaji, kioo na uimara wa simu bila kusahau software huwezi kukuta kwenye simu za daraja la chini
Sifa za Samsung Galaxy S24+
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g and 5g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | Dynamic LTPO AMOLED 2X, Refresh rate:120Hz |
Softawre |
|
Memori | UFS 4.0, 256GB,512GB na RAM 12GB |
Kamera | Kamera tatu
|
Muundo | Urefu-6.7inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 2,500,000/= |
Uwezo wa network
Samsung Galaxy S24+ inasapoti mpaka mtandao wa 5G kama ilivyo kwa samsung ultra
Aina ya 4G ambayo simu inayo ni ile inayoweza kufika kasi ya 10000Mbps kwa kupakuwa mafaili
Kwa hapa nchini kasi kubwa utaipata kama unatumia mtandao wa 5G
Kwa bahati mbaya 5G bado haijasambaa maeneo mengi ya nchi
Kwa wakazi wa Dar Es Salaam kwenye baadhi ya maeneo unaweza pata teknolojia hii ya mawasiliano
Ubora wa kioo
Kioo cha Samsung Galaxy S24 Plus ni cha aina ya amoled
Ila amoled yake ni ile inayoitwa Dynamic LTPO Amoled chenye resolution ya 1440 x 3120 pixels
Hii simu kioo chake kinauwezo wa kuonyesha rangi nyingi kutokana na uwepo wa HDR10+
Uangavu wa kioo unafika mpaka nits 2600
Uangavu huu unasaidia kioo kuweza kuonyesha vizuri kwenye mazingira yoyote
Kama ujuavyo ukiwa juani inakubidi uongeze mwanga ili skrini ioneshe vizuri
Nguvu ya processor Snapdragon 8 Gen 3
Simu ya Samsung Galaxy 8 Gen 3 inatumia chip ya snapdragon 8 gen 3 kwa matoleo ya Marekani
Wakati nchi nyingine zinakuja na processor ya Exynos 2400 ambayo huundwa na kutengenezwa na samsung yenyewe
Kimuundo hizi chip mbili hazitofautiani sana na kwa kiasi kikubwa zipo sawa
Kwa hapa, tutaizungumzia Snapdragon 8 Gen 3
Kwenye app ya Geekbench 5 inayotumiwa kupima nguvu za processor, snapdragon 8 gen 3 inaonyesha kuwa na nguvu kubwa kuliko hata processor nyingi za Apple
Kama unavyojua kwa miaka mingi chip za apple zimekuwa kinara kwenye utendaji mkubwa
Ila kwa matoleo mapya ya Snapdragon yamepunguza hii tofauti kwa kiwango kikubwa
Kwa mtumiaji wa kawaida anaweza asione tofauti ya wazi
Uwezo wa betri na chaji
Betri ya hii simu ni kubwa na ina mAh zipatazo 4900
GSMArena tovuti kubwa ya udadisi kuhusu sifa za simu inasema kuwa wastani wa simu kukaa na chaji ni masaa kumi na mbili
Kwenye kucheza gemu, intaneti na hata kuangalia video
Utofauti wa muda hautofautiani sana na Samsung Galaxy S24 Ultra
Ila inazidiwa kwa mbali sana na Apple iPhone 15 Pro Max na OnePlus 12
Cha kushangaza ni kwamba betri ya iphone sio kubwa kama Samsung
Upande wa chaji simu inasapoti chaji yenye kasi mpaka wati 45
Chaji ni nzuri hasa kipindi cha umeme unaokatika mara kwa mara
Kwani ndani ya nusu betri inajaa kwa asilimia 75
Kwa mtumiaji mkubwa sana wa simu ataichaji galaxy s24 plus mara mbili tu kwa siku
Ukubwa na aina ya memori
Samsung hii ina matoleo matatu upande wa memori na zote zina RAM ya GB 12
Mfumo wa memori unaotumiwa na hii simu ni UFS 4.1
Kasi yake ya kusoma na kuandika data kwenye memori ni mara mbili ya mfumo wa UFS 3.0
Hii kasi inaipa simu nguvu ya ziada katik utendaji wake wa kazi mbalimbali
Kwa kifupi kuna Samsung Galaxy S24+ ya GB 256 na 512
Na zote hazina sehemu ya kuweka memori kadi kama ilivyo simu nyingi za daraja la juu zinazotoka miaka hii
Ukubwa huo unatosha kuhofadhi mafaili na app nyingi
Uimara wa bodi ya Samsung Galaxy S24+
Hii ni simu yenye waterproof kwa maana haiwezi pitisha maji kama ikizama kwenye kina fulani
Ukiizamisha kwenye kina cha mita 1.5 kwa muda wa nusu saa maji hayawezi kuingia
Pia ina uwezo wa kuzuia maji tiririka kama mvua hivyo hutokuwa na wasi ukiwa upo mvua kubwa ambayo imenyesha ghafla ukiwa njiani
Uimara wa Galaxy S24 Plus haupo tu kwenye waterproof bali ugumu wake pia inapoanguka
Upande wa skrini simu ina kioo cha Gorilla Glass Victus 2 ambacho kina uvumilivu wa kutopasuka pindi ikidondoka kwenye kina cha mita mbili
Hata hivyo kioo ni kioo tu hivyo umakini ni kitu cha msingi
Upande wa nyuma ya simu kuna kioo cha Gorilla Glass Victus 2 vile vile
Ubora wa kamera
Kamera za Samsung Galaxy S24+ zipo tatu ambapo kamera kubwa zaidi ina megapixel 50 na zinatumia ulengaji wa dual pxiel pdaf
Kiujumla kamera za hii simu zinatoa picha nzuri na zenye usahihi wa rangi
Tofauti na kamera ya Samsung Galaxy S24 Ultra ni kuwa nyakati za usiku utaona kiwango fulani cha noise ukiikuza picha kwenye hii simu ya Samsung Galaxy S24+
Kiwango ambacho ni ngumu kugundua kwenye Galaxy Ultra
Mambo mengine yapo sawa ikiwemo kurekodi mpaka video za 8K kwa maudhui ya HDR10+
Ni ngumu kukuta HDR10+ kwenye simu za daraja la kati
Pitia hapa kujua: Maana ya HDR na umuhimu wake
Ubora wa Software
Kwa mara ya kwanza Samsung watakuwa wanatoa matoleo mapya ya Android kwa kipindi cha miaka 7 kwenye simu zote mpya za s-series
Miaka ya nyuma simu za samsung zilikuwa zinapata maboresh kwa muda mfupi sana
Yaana kama ukinunua galaxy yenye android 10 toleo la mwisho utakalopata ni android 12
Lakini kwa sasa Simu inakuja na Android 14 hivyo ukinunua utaweza kupata mpaka toleo la android 21
Vitu vingne vya kuvutia vya hii simu ni uwepo wa mifumo ya Akili Bandia(artificial inteligence)
Kwa mfano inaweza kubadilisha lugha kiingereza kuwa kwa kiswahili wakati mtu anaekupigia simu akiwa anaongea kiingereza
Inaondoa mipaka ya lugha kwenye mawasiliano
Washindani wa Samsung Galaxy S24+
Karibu simu zote za madaraja ya juu yanaweza kutoa ushindani mkali kwa toleo hili la Samsung
Mfano Apple iPhone 15 Pro Max ni kikwazo kikubwa kwa samsung hasa soko la China na USA
Samsung imeshindwa kufanya vizuri kwenye soko la China kwa miaka mingi
Huawei na iPhone ndizo zinazotawala kule
Kwa marekani, karibu ya 60% ya watumiaji wa simu wanatumia iPhone
Neno la Mwisho
Kama bajeti yako haina uwezo wa kumiliki Samsung Galaxy S24 Ultra basi mbadala mzuri S24 Plus
Sifa za Samsung Galaxy S24+ hazina tofauti sana na ile galaxy kubwa
Haina haja ya kuwaza sana kama unaweza kununua simu yenye bei ya milioni mbili kama ilivyo kwa hii samsung