Kuelekea mwishoni mwa mwaka 2023 infinix walitoa toleo jingine la simu aina ya Infinix Hot 40
Hili ni baada ya toleo la infinix hot 30 ambvalo limetoka mwaka 2023 pia
Infinix Hot 40 ina tofauti ndogo na watangulizi wake ila kuna utofauti kidogo kwenye mfumo wa software
Bei ya infinix hot 40 kwa hapa Tanzania inazidi shilingi laki tatu kutokana na ukubwa wa memori
Bei yake pia inawezwa kuathiriwa na eneo
Bei ya Infinix Hot 40 ya GB 128
Kwa Tanzania bei ya simu inaanzia shilingi laki tatu na nusu
Bei ni rafiki kiujumla ukilinganisha na ukubwa wa memori
Kwa maana memori inatosheleza kuhifadhi vitu vya kutosha
Na isitoshe inakuja na sehemu ya kuweka memori kadi
Japo ukubwa wa memori haupaswi kuwa kigezo pekee cha kukushawishi kununua simu
kwani kuna baadhi ya sifa hazina ubora mkubwa ila muhimu zingatia mahitaji yako kama yanafikiwa na sifa za simu husika
Sifa za Infinix Hot 40
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | IPS LCD, Refresh rate:90Hz |
Softawre |
|
Memori | 256GB,128GB na RAM 8GB |
Kamera | Kamera tatu
|
Muundo | Urefu-6.78inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 350,000/= |
Upi ubora wa Infinix Hot 40
Hot ina ubora katika maeneo matano ambayo yanweza mfurahisha mtumiaji wa kawaida
Kwanza simu ina mfumo wa chaji wenye kasi ya kujaza betri kwa haraka
Betri yake ni kubwa inaweza kukaa na chaji muda mrefu
Memori ni kubwa na bei ni rafiki kiasi fulani
Kamera yake kubwa ina megapixel nyingi japo hii ni kitu kimoja kati ya vitu vingi vinavyofanya kamera kuwa nzuri
Kwenye upande wa network uwezo wake ni wa wastani kama utakavyoona
Uwezo wa Network
Infinix Hot 40 inasapoti mpaka mtandao wa 4G kwani chip iliyotumika na simu haina uwezo wa 5G
Ndio maana inaweza semwa kwa sasa uwezo wake ni wa kawaida
Ikizingatiwa tayari mitandao ya Tigo, Airtel bila kusahau Vodacom inasapoti 5G kwa baadhi ya maeneo hapa Tanzania
Aina ya 4G ya hii simu ni LTE Cat 7 upande wa kudownload na LTE Cat 13 upande wa ku-upload
Yaani kwa maana kama hii spidi inapatikana kweli, itakuchukua sekunde mbili tu kuweka whatsapp kwenye simu
Kwa bahati mitandao ya simu hapa nchini mara nyingi 4G yao huwa ni ngumu kufika hata 100Mbps hata ukiwa eneo zuri
Kiufupi usitarajie kuipata kasi hii kwa Tanzania
Ukiondoa uwezo wa wastani wa network kuna ubora fulani wa kuridhisha upande wa kioo
Ubora wa kioo cha Infinix Hot 40
Kioo cha Infinix Hot 40 kinatumia teknolojia IPS LCD
Kwa sasa simu nyingi za kundi la kati hutumia vioo vya AMOLED
Kiubora amoled ipo juu hasa kwenye utajiri wa rangi ila kioo orijino cha infinix kinasapoti refresh rate kubwa inayofika 90Hz
Refresh rate inapokuwa kubwa husaidiwa simu kuwa nyepesi unapotachi ama kuperuzi
Changamoto kubwa ya refresh rate ya juu ni matumizi makubwa ya betri
Kama haina umuhimu kwako unaweza izima na kuseti refesh rate ya 60Hz
Ubora wa vitu vingi vya simu ikiwemo refresh rate vinaweza visiwe na maana yoyote kama haufahamu nguvu ya processor ya simu
Maana processor ndio ubongo wa simu janja na kompyuta
Nguvu ya processor Mediatek Helio G88
Hot 40 inatumia processor kutoka kwa kampuni ya Mediatek ya Taiwan
Chip hiyo inaitwa Mediatek helio G88 ambayo imegawanyika katika sehemu mbili ikiwa na jumla ya core nane
Kiutendaji uwezo wake sio mkubwa japo inaweza kucheza magemu mengi ila baadhi utalazimika kucheza kwa ubora wa chini wa graphgics kupata FPS nyingi
Kwa mfano gemu ya PUBG Mobile 2020 inacheza kwa viwango vya wastani wa FPS 30 kwenye ubora wa chini
Ila ukiweka Full HD yaani pixel 1080 fps zinapungua mpaka fps 19
Picha inayotolewa hapa ni kuwa helio g88 inaweza fanya kazi nyingi ila changamoto itakuja unapofungua app nyingi zinazotumia nguvu kubwa
Unaweza kuanga kiundani hapa, uwezo wa mediatek helio g88
Kufaidi uwezo wa mediatek helio g88 betri ya simu inabidi na yenyewe inabidi iwe na uwezo wa kuridhisha
Maana betri ikiwa ndogo simu inaweza wahi kuzimika ukiwa unacheza gemu kwani helio g88 ufanisi wake ni wa wastani
Uwezo wa betri na chaji
Betri ya Infinix Hot 40 ina ukubwa wa 5000mAh
Mara nyingi ukubwa huu unaweza kustahimili kukaa na chaji kwa zaidi ya masaa kumi kutegemeana na matumizi
Betri ikiwa kubwa hufanya simu kuchelewa kujaa kama chaji kasi yake ni ndogo
Chaji ya Hot 40 inaweza kupeleka umeme mpaka wati 33
Wati 33 inaweza kujaza betri ya 5000mAh ndani ya dakika 80
Chaji zenye kasi ndogo huchukuwa zaidi ya masaa matatu kujaza simu
Kwa maana hiyo hata video zako ambazo umeziweka kwenye simu unaweza kuzitazama kwa muda mrefu bila kuhofia chaji kuisha
Ni vizuri ukaelewa mfumo mzima wa memori wa hii simu
Ukubwa na aina ya memori
Infinix Hot 40 imegawanyika sehemu mbili upande wa memori
Kuna yenye ukubwa wa GB 128 na GB 256 na zote zina RAM ya GB 8
Kwa bahati mbaya ni kwamba mfumo wake wa memori ni eMMC
eMMC huwa na kasi ndogo ya kusafirisha data ukilinganisha na mfumo wa UFS
Inaweza leta changamoto ya simu kuwa nzito pindi inapojaa
Siku hizi kampuni nyingi za utengenezaji simu hutumia UFS hata kwa madaraja ya kati na ya chini
Inawezekana labda infinix wanajaribu kupunguza gharama za utengenezaji ndio maana hata bodi ya simu haina vitu vikubwa sana vya kulinganisha na iPhone 15 Pro Max
Uimara wa bodi ya Infinix Hot 40
Njia moja wapo ya kujua uimara wa bodi ya simu ni kwa kutazama viwango vya IP
IP huwa vinaonyesha uwezo wa simu kuzuia maji ndani ya simu kama ikizama kwenye kina fulani
Infinix Hot 40 haina viwango rasmi vya IP ya aina yoyote kama vile IP53
Maana yake ni kuwa mtumiaji anapaswa kuwa makini anapokuwa kwenye mvua ama mazingira yenye maji
Bodi ya infinix hot 40 ina muonekano wa kuvutia hasa mpangilio wake wa kamera zake tatu
Ila muonekano mzuri wa kamera na ubora wa kamera hivyo ni vitu viwili tofauti vya kutofautisha
Ubora wa kamera
Moja ya eneo lenye ubora hafifu kwenye Infinix Hot 40 ni upande wa kamera
Kamera yenye lenzi ya macro ina megapixel 2MP ili kupata picha nzuri kamera inabidi na walau megapixel 8
Kamera kuu ina megapixel 50 ila inakosa mfumo mzuri wa ulengaji angalau PDAF japo pia ni wa kizamani kwani simu za sasa huja na dual pixel pdaf
Ni ngumu kuieleza kamera za hii simu kiundani kwani kuna hazijaelezwa
Upande wa kurekodi video kamera yake inaweza kurekodi mpaka video za full hd kwa kiwango cha 30fps
Haiwezi kurekodi video za 4K
Ubora wa Software
Infinix Hot 40 inatumia mfumo endeshi wa Android 13 na XOS 13.5
XOS 13.5 imejaribu kuiga baadhi ya vitu vya iphone 15 kama dynamic island
Dynamic island huwa inaziba sehemu ya kamera ya mbele na kuonyesha baadhi ya vitu
Kwenye infinix ukiichaji simu basi kiwango cha betri kujaa inakuwa inaonekana kwenye hiyo sehemu ya dynamic island
Washindani wa Infinix Hot 40
Kuna matoleo ya samsung ya bei nafuu ambayo yametoka mwishoni mwa mwaka 2023
Matoleo hayo ni Samsung Galaxy A05 na Samsung Galaxy A05S
Bila jusahau kuna itel ya chini za laki mbili pia zinaweza kuleta ushindani kama simu mbadala ya bei nafuu
Mshindani mwingine ni Redmi 12 na Redmi 12C ambazo bei yake inaendana na hii infinix
Kiujumla machaguo ni mengi kwa sasa
Neno la Mwisho
Bei ya infinix hot 40 ni rafiki hasa ukiangalia ukubwa wa memori
Sio simu nyingi zinaweza kupatikana kwa kima cha laki tatu na memori ikiwa ba ukubwa wa GB 128
Kwa mtumiaji mwenye matumizi ya wastani hatoona shida akiwa anaitumia hii simu
Maoni 5 kuhusu “Bei ya Infinix Hot 40 na Sifa Zake Muhimu”
Mnakopesha
Bado Kwa sasa
Maboresho zaidi upande was camera
MAFIKIRI WABORESHE
Mimi naomba betri liwe 6000 kama hapo mwanzo na finger print ya nyuma