Kama ilivyotarajiwa hapo awali kuhusu ujio wa simu mpya za iphone kwa mwaka huu 2023
Moja ya simu hiyo ni iPhone 15 Pro ambayo imeongezewa utendaji
Kiumuonekano hauwezi kutofautisha sana na matoleo ya mwaka uliopita
Na pia hakuna mabadiliko makubwa sana ya kuweza kuruka kutoka iphone 14 pro mpaka kwenye hii iphone mpya
Ndio maana hata bei ya iphone 15 pro ina ufanano na matoleo yaliyopita
Iangazie kwenye kila nyanja ujue vitu vipya ambavyo vimekuja na hii simu.
Bei ya iPhone 15 Pro ya GB 256 Tanzania
Bei halisi ya iPhone 15 Pro yenye ukubwa wa GB 256 ni shilingi 2,800,000(milioni mbili na laki nane)
Kwa Tanzania bei yake inaweza kufika milioni tatu kutokana na gharama zingine
Maboresho makubwa yaliyopo kwenye iphone mpya ni kwenye uchezaji wa gemu na utendaji kiujumla
Pia kwa mara ya kwanza apple wamelazimika kuweka muundo wa chaji wa USB Type C ambazo hutumika sana kwenye simu za android
Hii ilitokana na mapendekezo yaliyotolewa na umoja wa ulaya kuzitaka kampuni za utengenezaji wa simu kuwa na muundo mmoja wa chaji usiolazimisha watumiaji kununua chaji za aina tofauti.
Sifa za iPhone 15 Pro
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g and 5g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | LTPO Super Retina XDR OLED, Refresh rate:120Hz |
Softawre |
|
Memori | NMVe,, 256GB,128GB, 1TB na RAM 8GB |
Kamera | Kamera TATU
|
Muundo | Urefu-6.1inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 2,800,000/= |
Upi ubora wa iPhone 15 Pro
Simu inakuja na processor mpya na yenye nguvu ukilinganisha processor zilizotumika kwenye simu zilizopo sokoni kwa sasa
Chaji zinazotumika kwenye simu za android zinaweza kuichaji hii simu bila shida na kwa spidi kubwa
Kioo chake kina refresh rate kubwa na uwezo wa kuonyesha vitu kwa muonekano mzuri
Hii ni simu ngumu ambayo haitumii vioo kama ilivyo matoelo ya awali
iPhone za mwaka 2023 zinatumia RAM kubwa tofauti na miaka iliyopita ambapo RAM ya simu zimekuwa ni ndogo yaani GB 6.
Ni simu ngumu hata ikiingia kwenye maji
Ni simu inayosapoti eSIM ambapo kwa Tanzania mitandao ya Vodacom na Airtel wanayo hii huduma
Kufahamu eSIM, ufafanuzi huu hapa: Maana ya eSIM kwa lugha nyepesi
Kuna mengi kwenye hii simu kama utakavyoona mbeleni
Uwezo wa Network
iPhone 15 Pro ni simu ya 5G na inasapoti aina zingine za network
Inaweza kutumia aina zote za 5G ikiwemo ya mmWave
5G ya mmWave ndio yenye kasi kubwa zaidi kwanza ambayo inapatikana sana marekani
Kwa bahati mbaya yenyewe inahitaji minara mingi ili imfikie mtumiaji
Kwa sababu masafa yake hayaendi umbali mfreu kama ilivyo 5G nyingine
Kwa hapa Tanzania mitandao yenye b5G ni Airtel, Vodacom na Tigo
Na zote zinatumia masafa ya kati na mafupi
Ubora wa kioo cha iPhone 15 Pro
Kioo cha iPhone 15 Pro ni cha aina ya LTPO OLED, apple wenyewe wanakiita LTPO Super Retina XDR OLED
LTPO kirefu chake ni Low Temperature Crystalline Oxide kazi yake kubwa ni kudhibiti kiwango cha refresh rate
Kioo cha iphone 15 pro kina refresh rate ya 120Hz
Kama kioo kikiwa kinaonyesha vitu muda wote kwa kiwango cha refresh rate kubwa hata kwenye hali ambayo haihitaji refresh rate kubwa basi betri itawahi kuisha
Uwepo wa LTPO unasaidia kutumika kwa refreshbrate kubwa kwenye nyakati inapohitajika
Pia kioo chake kina kiwango kikubwa cha reslution ambayo ni 1179 x 2556 pixels
Uzuri ni kuwa simu ina teknolojia ya dolby vision na hdr10, vitu vinavyoongeza kina cha rangi kwenye kioo
Hivyo vitu vingi vinaweza kuonekana kwa rangi zake halisi bila kupoteza ubora wake
Nguvu ya processor Apple A17 Pro
Simu inatumia processormpya ya Apple A17 Pro ambayo imegawanyika katika sehemu sita
Sehemu mbili za mwanzo inahusisha core zenye utendaji mkubwa
Mara hufanya kazi pale simu inapokuwa inatumia app zinazohitaji nguvu kubwa mfano magemu
Na sehemu ya pili inahusisha core zenye nguvu ndogo ama wastani ambazo zipo nne
Hizi hutumika wakati simu inafungua apps zinazohitaji nguvu ndogo ama ya kawaida mfano kutuma meseji ama kupiga simu au kuangalia video za instagram
Mtindo huu unaongeza ufanisi wa matumizi mazuri ya betri
App ya kupima nguvu za processor inayoitwa Geekbench inaonyesha kuwa Apple A17 Pro ina alama zipatazo 2500
Hii inaashiria apple a17 pro ndio chip ya simu yenye nguvu zaidi kuliko zingine kwa sasa
Uwezo wa betri na chaji
Betri ya iPhone 15 Pro kwenye makaratsi ni ndogo
Ila kwa jinsi apple wanavyounda simu zao ukaaji wa chaji huwa ni wa masaa mengi
Hata hivyo iPhone 15 Pro ukaaji wa chaji sio mkubwa ukilinganisha na toleo la iPhone 15 Plus
Tuchukulie data kutoka kwenye tovuti ya tomsguide, ambapo iphone 15 pro imeweza kukaa na chaji kwa masaa 11 kwenye majaribio mbalimbali ikiwemo intaneti
Sio kiwango kikubwa kama ilivyo kwa iPhone 15 Pro Max ambayo chaji yake inaenda mpaka masaa 13
Simu pia inasapoti wireless chaji, kasi yake sio kubwa kama simu ya Infinix Note 30 Premier inayopeleka umeme wa wati 50W
Wakati iphone 15 pro inapeleka umeme wa chaji wa wati 15 kama kiwango cha juu.
Ukubwa na aina ya memori
Simu inakuja na aina NNE za upande wa kubwa wa memori huku zote zikiwa na RAM ya GB 8
Kuna iPhone 15 Pro ya GB 128, 256, 512 na 1TB
Aina ya memori simu inayotumia ni NVMe ambayo usafirishaji wake wa data ni mkubwa
Yaani kama unakopi kitu kutoka kwenye kompyuta ya mac kwenda kwenye simu utaona faili linamalizika kukopi kwa haraka
Uimara wa bodi ya iPhone 15 Pro
Kitu kikubwa ambacho apple wamekinadi sana ni madini mapya yaliyotumika kuundia bodi
Madini hayo hutwa titanium, inasemwa kuwa madini haya huwa ni magumu
Tukipata undani wa uimara kwenye hii simu tutakutaarifu
Kama ilivyo kwa matoleo ya iphone ya zamani, hii pia haipitishi maji kwani ina viwango vya IP68
Kama simu ikizama kwenye cha mita 6 kwa muda wa nusu saa simu haitoathiriwa na maji
Ubora wa kamera
Hii simu ina kamera zipatazo tatu yaani macho matatu
Kuna kamera moja kwa ajili ya kupiga eneo pana hufahamika kama Ultrawide
Na nyingine kwa ajili ya kupiga kitu ambacho kipo mbali kamera hii huitwa telephoto
Kuna maboresho upande wa kamera ya telephoto, apple wameongeza kiwango cha kuweza kuzoom
Simu hii inaweza kuzoom mpaka mara tano bila kupoteza ubora wa picha
Bado ni kiwango cha chini ukifananisha na simu ya Samsung Galaxy S23 Ultra
Ubora wa picha hauna tofauti na iPhone 14 Pro japokuwa kuna mifumo imeboreshwa ya kuchakata ubora wa picha
Tutajadili ubora wa picha wa hii simu kiundani katika makala zingine
Ubora wa Software
Unaijua NameDrop, muundo wa kushea namba kati ya simu mbili kwa kugusisha sehemu ya juu
Huu ni muundo ambao umekuja kwenye iOS 17
Sio kitu kigeni kwenye simu za Android japo Google waliachana na hiki kitu
Sina uhakika kama itakuwa na mafanikio kwenye iphone
Kiujumla iPhone 15 Pro inatumia mfumo endeshi wa iOS 17
iOS 17 umeweka kwa kiasi kikubwa teknolojia ya Artificial Intelligence(AI) kwa maana isiyo rasmi Akili bandia
Washindani wa iPhone 15 Pro
Washindani wakubwa wa iphone 15 Pro kwanza ni iPhone 14 Pro
Kama ilivyoelezwa awali kuna tofauti ndogo sana kiasi cha kwamba mtumiaji wa kawaida anaweza asione kipya
Kwa sasa iPhone 14 Pro inaenda kuuzwa kwa bei ya chini ya toleo jipya
Mshindani mwingine ni Samsung Galaxy S23+
Japokuwa iphone ina nguvu zaidi kiutendaji lakini kwenye uhalisia hakuna tofauti ya wazi kiutendaji kati ya hizi simu mbili
Samsung inakuja na betri kubwa na kamera nzuri zaidi naweza kusema
Neno la Mwisho
Kwa mtu mwenye simu ya iPhone 14 Plus akinunua iPhone 15 Pro ataona utofauti kubwa
Ila kwa mtu ambaye ana iPhone 14 Pro Max anaweza asione tofauti kubwa
Mwitikio wa matoleo ya iPhone 15 haujawa mkubwa kama miaka iliyopita
Hata hivyo hii ni simu kali na nzuri kwa mwenye bajeti inayotosheleza
Wazo moja kuhusu “Bei ya iPhone 15 Pro na Sifa Zake Muhimu”
Nahitaji hiyo simu ya iPhone 15 nimeona inaubora