Kwa mwaka 2023 infinix wameingiza matoleo mapya ya simu zipatazo tisa
Matoleo hayo yamegawanyika katika makundi kama matatu kwa kuzingatia bei zake na ubora wake
Utakutana na infinix zenye ubora wa chini, kati na ubora wa juu
Hivyo kwenye hii orodha kuna simu mpya za infinix za mwaka 2023 na bei zake kwa Tanzania
Infinix Note 30 Pro
Infinix note 30 Pro ni simu ya daraja la kati ambayo imetoka mwezi mei
Ina urefu wa inchi 6.67 na ina kioo kizuri aina ya amoled chenye refresh rate ya 120Hz
Hii ni simu inayoweza kuchaji kwa njia ya wireless kwa maana unachaji simu bila kutumia waya wa usb
Fahamu Zaidi: Ubora na uwezo wa infinix note 30 Pro
Kamera yake ina lenzi kubwa ya megapixel 108 na upigaji wa picha ni wa kuridhisha
Betri yake inakaa na chaji muda mrefu kwani ukubwa wake ni 5000mAh
Na pia inakuja na chaji yenye wati 68 inayoweza kujaza simu kwa 80% ndani ya nusu saa
Bei ya Infinix Note 30 Pro
Kwa Tanzania simu inauzwa kiasi cha shilingi 700,000/=
Kwa maeneo mengine inaweza kupatikana chini ya bei tajwa
Bei yake inaendana na ubora wa simu kiujumla
Infinix Note 30
Simu ya Infinix Note 30 imetoka pamoja na note 30 pro kwa maana zote ni za mwezi mei
Utendaji wa note 30 ni wa wastani kwa sababu inatumia processor ya Helio G99
Ina kio aina ya IPS LCD chenye refresh rate inayofika 120Hz
Ubora wa kamera sio mkubwa sana kama simu iliyotangulia
Kasi ya chaji ni wati 45 na yenyewe inajaza betri yake ya 5000mAh ndani ya muda mfupi
Unaweza kupata infinix ya GB 128 au ya GB 256 kwenye upande wa memori
Hii ni simu ya 4G, haina 5G kama ilivyo kwa note 30 5g
Hapa, kuna maelezo ya kina kuhusu infinix note 30
Bei ya Infinix Note 30
Infinix Note 30 ya GB 256 inapatikana kwa kiasi cha shilingi laki sita
Kama hiki kiwango ni kigumu kulipa kwa mkupuo yapo maduka ambayo yanakopesha
Ila lazima utoe kianzio ili ukopeshwe
Infinix Note 30 5G
Simu nyingine ya Infinix iliyotoka mwezi mei mwaka 2023
Ni simu ya 5G
Kwa haraka haraka unaweza kudhani Infinix note 30 5G ni bora zaidi kutokana na utendaji mkubwa kuliko infinix note 30 pro
Kiuhalisia infinix note 30 pro ni nzuri zaidi
Kwa sababu note 30 5G inatumia kioo cha ips lcd, ina kamera yenye megapixel 64
Inakuja na chaji yenye wati 45 ambayo inajaza betri kwa muda mfupi pia
Ila haina mfumo wa kuchaji simu bila kutumia waya
Bei ya Infinix Note 30 5G
Bei ya Infinix Note 30 5G ni shilingi 450,000/= kwa hapa Tanzania
Simu nyingi za 5G bei huanzia laki nne, hizi ni zile zenye kiwango cha kawaida
Infinix Note 30 VIP
Katika matoleo ya note 30 toleo la infinix note 30 VIP ndio toleo bora zaidi
Kwani infinix note 30 vip inatumia processor yenye nguvu kubwa hivyo inaipa uwezo wa ziada
Kwa mfano kamera yake inaweza kurekodi mpaka video za 4K ambazo huo na muonekano mzuri na uliokorea vizuri
Na yenyewe ina mfumo wa wireless chaji kwa maana kuchaji bila kutumia waya
Kasi ya wireless chaji ni kubwa sana humu kutokana na uwezo wa kupeleka chaji kwa wati 50
Hii inafanya simu iweze kuchaji kwa 50% ndani ya nusu saa
Chaji nyingi za wireless huwa zinapeleka kiwango kidogo ila infinix wamejitahidi
Kiufupi simu ina vitu bora vingi na hii ni simu nzuri zaidi ya infinix mpaka sasa
Unaweza kuijua zaidi kwa kutazama hii video ya Youtube.
Bei ya Infinix Note 30 VIP
Kwa kuwa ubora wa infinix note 30 vip unazizidi simu nyingi zilizopo humu hivyo bei yake lazima iwe kubwa kiasi
Infinix Note 30 VIP inauzwa kwa shilingi 860,000 ya GB 256
Kwa kuringanisha simu na bei naweza nikasema ni bei rafiki kwa kiasi kikubwa
Infinix Hot 30
Infinix Hot 30 ni simu yenye uwezo wa wastani ambayo imetoka mwezi machi 2023
Ina jumla ya kamera zipatazo mbili ambapo kubwa ina megapixel 50 ila kiubora wa picha sio wa kiwango kikubwa
Betri lake ni kubwa lina 5000mAh
Chaji yake inapeleka umeme wa wati 33 ambayo inajaza simu kwa 50% ndani ya nusu saa
Inatumia kioo cha ips lcd chenye refresh rate ya 90Hz
Na pia inakuja na android toleo la 13 ambalo bado ni jipya kwani android 14 bado haijatoka rasmi
Bei ya Infinix Hot 30
Infinix Hot 30 ya GB 256 kwa Tanzania inauzwa kwa shilingi 450,000
Hata hivyo kuna toleo moja tu upande wa memori ambalo lina RAM ya GB 8 na memori ya GB 256
Infinix Hot 30i
Hii ni simu nyingine ambayo imetoka mwezi machi pamoja na hot 30
Simu mbili zina ufanano wa kiwango kikubwa utofauti upo kwenye sehemu chache
Hot 30i ina kamera yenye kiwango cha chini na ukubwa wake ni megapixel 13
Pia inatumia android 12 na hakuna uhakika wa kupata toleo lifuatalo la android 13
Memori yake ni GB 128 na RAM yake ni GB 4
Ni ndogo ukilinganisha na hot 30 lakini bado upo uwezekano wa kuhifadhi mafaili mengi ya kutosha
Pia chaji ina kasi ya kawaida ambayo umeme wake ni wati 18
Bei ya Infinix Hot 30i
Kwa kuwa tayari umeona kuna vitu vimepunguzwa hivyo bei yake hii ni ndogo zaidi
Infinix Hot 30i inauzwa kwa kiasi cha shilingi 350,000 kwa Tanzania
Infinix Hot 30 play
Unataka simu yenye betri kubwa sana lenye 6000mAh bila kujali mambo mengine?
Basi Inifinix Hot 30 Play inakupa suruhisho hilo
Hivyo utakuwa na simu inayokaa na chaji kwa muda mrefu kama sio masiku
Kiutendaji simu haina nguvu kubwa kwani processor yake ni ndogo ambayo ni Mediatek Helio G37
Kioo chake kina reslution ndogo ya 720 x 1640 pixels na aina ya IPS LCD ila refresh rate yake inafika 90Hz
Pia inatumia toleo la sasa la android ambayo ni android 13
Na chaji yake inapeleka umeme wa kiwango cha wastani cha wati 18
Bei ya Infinix Hot 30 Play
Bei ya Hot 30 Play kwa hapa Tanzania ni shilingi 380,000/=
Kiuhalisia hii inaizidi kidogo hot 30i
Infinix Smart 7
Simu ya infinix smart 7 iliingia sokoni mwezi wa pili mwaka 2023
Hii ni simu ya daraja la chini hivyo haina vitu vingi vizuri kama ilivyo kwa matoleo ya note na hot
Utendaji wa smart 7 ni mdogo kwa sababu inatumia processor yenye nguvu ndogo
Kamera zipo mbili na inarekodi video za full hd
Ila kiubora wa kamera ni kiwango cha kawaida kama sio cha chini
Ina betri kubwa na inakaa na chaji masaa mengi kwa sababu simu haitumii nguvu kubwa
Ila chaji yake inapeleka kiwango kidogo cha umeme wa wati 10
Kwa maana tegemea betri kuchukua masaa mengi mpaka kujaa
Bei ya Infinix Smart 7
Infinix Smart 7 ni infinix ya bei nafuu kwenye hii orodha iliyopo
Inauzwa shilingi 220,000/= hapa Tanzania
Ni simu inayofaa kwa mtumiaji anaejali matumizi ya chaji
Infinix Smart 7 Plus
Simu nyingine yenye betri kubwa ya 6000mAh ni Infinix Smart 7 Plus
Hii simu inafanana vitu vingi smart 7
Hivyo hakuna vitu vingi vya kuvifafanua kiundani
Kwani pia ni simu ya kundi la daraja la chini
Bei ya Infinix Smart 7 Plus
Bei ya Infinix Smart 7 Plus ya GB 3 na memori ya 64 ni shilingi 210,000/=
Bei hazitofautiani sana
Hitimisho
Una machaguo tisa upande wa infinix kwa mwaka 2023
Uchaguzi wa moja ya simu itategemeana na kiasi cha pesa kilichopo mfukoni
Ukiwa na bajeti ya kutosha unapata infinix nzuri tofauti na apo utapata infinix ya kusukuma siku
Kubwa zaidi ni aina ya matumizi ndio itakupa muongozo wa simu ipi ya infinix ya kununua mwaka 2023
Maoni 18 kuhusu “Orodha ya Simu Mpya za Infinix na bei zake 2023”
Names kupataje utalatibu w Juanita mzingo inche za inje
Simu mnakuwa mnaziwekearam kubwa huku hazina uwezo
Kama ipi Kwa mfano?
Simi anapatikana mkoa gani
Simu ni zuri na zinaubora sana ila camera huwa ni this kuharibika so kama company you have to chake on that
Mngekua mnatupa update za Bei za simu zenu kila mwezi ili mtu akitoka nyumbani ajue anakiasi gani na anakwenda kununua simu gani
Nataka hiyo infinix smart 7 plus
Mimi nataka infinix note 30 sasa naipataje?
Mim naona unaweza ukanunua smartphone kwa bei kubwa halafu isiwe na uwezo kwani hili mnalionaje?
Kikubwa unapotaka kununua simu Kwa kuangalia uwezo zingatia processor iliyotumika. Hii inakupa picha juu ya uwezo WA simu
Nahitaji sm ya mkopo naomba muongozo na kianzia cha kila sm
Naipataje simu ya kulipiya kidogo kidogo
Infinix hot 11 pray kwa Sasa ni shingap?harafu vipi mbona zinajamu hizo za hot 11 pray?
Hizi sio powerful sana
Hiyo infikix kwa mkopo shingapi
Huduma hii hatuna Kwa sasa
Jaman mim sina hela
Pambana kiongozi
Nahijaji mko wapi