Tecno Spark 10C ni toleo jipya la tecno kwa mwaka 2023
Spark 10C ina tofauti ndogo sana na simu ya Tecno Spark 10
Na tofauti yao ipo kwenye camera na software, mengine yanafanana
Bei ya tecno spark 10c inazidi laki tatu na nusu japo kisifa inaleta maswali
Maswali hayo yanatokana na sifa za kiujumla za hii simu japo vipo vya kuvutia.
Bei ya Tecno Spark 10 ya GB 128
Bei ya Tecno Spark yenye GB 128 ni shilingi 410,000/=
Bei inaweza kuwa inasababishwa na kioo pamoja na ukubwa memori
Vipengele vingi vya simu ni vya kawaida ambavyo kwenye simu zingine bei zake ni chini ya laki nne
Kiulanganish, spark 10c inashabiana na Samsung Galaxy A04 ya mwaka 2022
Ni vizuri kuitazama kila kipengele kujua kama simu inakufaa kwa matumizi yako
Sifa za Tecno Spark 10
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | IPS LCD, Refresh rate:90Hz |
Softawre |
|
Memori | 128GB, na RAM 8GB |
Kamera | Kamera MBILI
|
Muundo | Urefu-6.6inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 410,000/= |
Upi ubora wa Tecno Spark 10C
Simu ina kioo chenye refresh rate kubwa inaypfika 90Hz, hivyo ni kizuri kwa magemu
Inakuja na nafasi kubwa ya kuhifadhi mafaili
Ukaaji wa chaji ni mkubwa kwani betri yake ni kubwa pia ina 5000mAh
Inakuja na ram kubwa na inaweza kuongeza ukubwa wa RAM
Inakubali mtandao wa 4G wenye kasi kubwa
Ina muonekano wa kuvutia na ina glasi kwa nyuma
Uwezo wa Network
Tecno spark 10c ni simu ya 4G kwa maana haina 5G
Aina 4G inayotumia ni LTE Cat 7 yenye kasi ya 300mbps ambayo ni sawa na 37.8
Yaani kama unadownload applikesheni ya whatsapp yenye MB 37, simu itamaliza kuipakua kwa sekunde moja tu
Ila jua ni ngumu kupata kasi hii kwenye mitandao ya simu za mkononi kwa hapa Tanzania
Simu ina masafa yote ya 4G yanayotumiwa hapa nchini
Hivyo kila mtando utafanya kazi vizuri
Ubora wa kioo cha Tecno Spark 10C
Kioo cha tecno kina ubora wa kawaida kwa sababu kinatumia teknolojia ya IPS LCD
Na resolution yake ni 720p ambayo iko sawa na spark ya mwaka 2022
Kwa viwango vya sasa resolutuion inayopendekezwa ni 1080p yaani full hd.
Ila haishangazi sana ukizingatia ni simu ya daraja la chini na inawalenga watumiaji wenye matumizi ya kawaida
Kiujumla ubora wa vioo vya IPS LCD huzidiwa na vioo vya amoled
Simu yenye kioo cha amoled ni tecno phantom x2 pro ambayo bei yake inazidi milion
Pitia hapa: Sifa za tecno phantom x2 pro, uijue kinagaubaga
Nguvu ya processor Unisoc Tiger T606
Processor ya unisoc tiger t606 ndio chip inayoiwezesha simu ya spark 10c
Ni chip iliyogawanyika katika sehemu mbili, sehemu ya kwanza ina jumla ya core 2
Hizi ni core zenye nguvu kubwa kwenye hii simu na zinatumia muundo wa Cortex A75
Na kwenye core zenye nguvu ndogo zipo sita zikiwa zinatumia muundo wa Cortex A55
Kwa mgawanyo huu inamaanisha uwezo wa simu kiutendaji ni mdogo
Sio simu nzuri kwa mtu anaependa kucheza gemu kubwa kama za mpira, za mapigano na nyinginezo
Lakini pia ni chip inayotumia umeme kiasi kidogo hivyo betri inakaa muda mrefu na chaji
Uwezo wa betri na chaji
Betri yake ina ukubwa wa 5000mAh hivyo unaweza kutumia muda mrefu bila kuhofu chaji kuisha haraka
Uwezo wa kukaa na chaji ni mkubwa kwa sababu processor yake haitumii umeme mwingi
Spark 10C inakuja na chaji yenye uwezo wa kupeleka umeme wa wati 18
Kwa kipindi cha nyuma kiwango hiki kilikuwa kinachukuliwa kama fast chaji
Ila siku hizi kuna simu zinapeleka mpaka wati 120 zinazojaza simu kwa dakika 17 tu
Na simu za kawaida huwa zinakuja na chaji kuanzia wati 25
Wati 18 ni nzuri ila simu inachukua muda kujaa kwa 100%
Ukubwa na aina ya memori
Tecno spark 10c inakuja na toleo moja tu upande wa memori
Toleo hilo lina ukubwa wa GB 128
Kwa mtumiaji asiependa kupakuwa vitu vingi hili toleo zuri kwake na anaweza asijaze simu yote
Haijaainishwa ni aina ipi ya memori inayotumika na hii simu
Uimara wa bodi ya Tecno Spark 10C
Bodi ya Tecno Spark 10C inakuja na kioo upande wa nyuma
Kioo kinachotumika sio gorilla na hivyo kuna umuhimu wa kutumia kava
Na uzuri tecno simu zake mpya huwa zinakuja makava ukifungua box
Simu hii haina uwezo wa kuzuia maji endapo ikizama kwenye maji ya kina kirefu
Kwa sababu haina viwango vya IP68, hivyo kuwa makini na matumizi yako hasa ukiwa kwenye mvua au ufukweni
Ubora wa kamera
Simu ina kamera mbili kamera kubwa ina megapixel 16 ni tofauti na spark 10 yenye megapixel 50
Ubora wa kamera unaangaliwa kwa vitu vingi sio megapixel pekee kama simu ina mfumo mzuri wa kamera, kamera kuanzia megapixel 10 zinaweza kutoa picha kali
Kama unabisha tazama kamera za iPhone 13 Pro Max ambazo zote zina 12MP
Ziangalie, simu zenye kamera nzuri ikiwepo iphone 13 pro max
Upande wa Tecno Spark 10C haina mfumo mzuri wa kamera kuanzia kamera kuu hata selfie
Hii inapelekea ubora wa picha kuwa mdogo hata nyakati za mchana
Ukiitazama hii picha chini utaona noise(chengachenga) kwa mbali na rangi za majani kuwa mwangaza mwingi kuliko uhalisia
Hii inasababishwa na kamera kukosa angalau HDR10 na uchakataji wa kiwango cha chini wa ISP(processor)
Kwenye video simu inaweza kurekodi video za full hd pekee na haiwezi kurekodi video za 4K
Na pia haina OIS(Optical Image Stabilization) hivyo ukiwa unarekodi video huku unatembea inabidi utulize mkono ili video isitokee ikiwa na mitikisikomitikisiko.
Ubora wa Software
Utofauti mwingine kati ya Tecno Spark 10 na Spark 10C ni upande wa software
Spark 10C inatumia mifumo ya nyuma
Kwani inakuja na Android 12 na HiOS 8
Android 12 ni bado toleo zuri lakini kwa simu mpya inafaa ije na toleo la Android 13
Ikizingatiwa hakuna uhakika kama simu itakuwa inapokea matoleo mapya ya android huko mbeleni
Hata hivyo utaweza kuongeza ukubwa wa RAM mpaka GB 4
Yapi Madhaifu ya Tecno Spark 10C
Katika mrorongo wa matoleo ya Tecno spark 10, tecno spark 10c ina mapungufu mengi
Ubora wa picha ni wa kiwango cha chini
Processor yake ina nguvu ndogo kusukuma vitu vingi na gemu kubwa
Kioo chake hakina HDR10 wala HDR10+
Simu haina 5G ukizingatia kuna simu zina bei kama hii na zinakuja na 5G
Inatumia mfumo endeshi wa kipindi cha nyuma na kuacha mifumo endeshi mipya
Neno la Mwisho
Tecno Spark 10C ni toleo zuri kwa anayependa simujanja inayotunza chaji
Kama unaishi kwenye maeneo yenye umeme usio na uhakika hii simu itakusaidia
Ila kwa mtu anayependa kamera na simu yenye utendaji mkubwa basi hili sio chagua zuri kuwa nalo
Maoni 4 kuhusu “Bei ya Tecno Spark 10C na Sifa Muhimu”
Kwann kamera siyo nzuri
Kwanin? Ina bei kubwa alafu camera yake inauwezo mdogo
Wanashindwa wapi kuweka ubora wa simu kutokana naukubwa wake??
Yangu nimesahau paswadi