Simu ya iPhone 6 Plus ni iPhone ambayo ilitoka mwaka 2014
Umri wa miaka minane tangu itoke unaifanya bei ya iPhone 6 plus iwe chini ya laki tatu
Apple walishasitisha kutengeneza hii simu hivyo smartphone hii utaipata ikiwa used
Swali, je simu hii inafaa kutumika kwa mwaka 2022?
Kiuhalisia bei yake na sifa zake zitakupa jibu sahihi.
Fuatilia kila ufafanuzi uliopo kwenye ukurasa huu
Bei ya iPhone 6 Plus Tanzania
Kwa baadhi ya maduka kinondoni bei ya iphone 6 plus ya GB 64 ni shilingi 230,000/=
Wauza simu wengine wanaiuza mpaka 270,000/=
Kwa sasa hii ni moja ya iPhone za bei rahisi
Bei ndogo inasababishwa na sifa zake kuwa na kiwango cha chini kwa nyakati za sasa
Sifa za Simu ya iPhone 6 Plus
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | IPS LCD, |
Softawre |
|
Memori | 16GB,128GB,64GB na RAM 1GB, |
Kamera | Kamera MOJA
|
Muundo | Urefu-5.5inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 280,000/= |
Upi ubora wa iPhone 6 Plus
Hakuna cha kukizungumzia zaidi kuhusu ubora wa iPhone 6 Plus
Kwa sababu ni simu ambayo ipo chini sana kwa nyakati za leo
Uzuri mkubwa wa hii simu ni kuwa ndogo na fupi
Hivyo kwa wanaochukia simu ndefu basi iPhone hii inawafaa
Lakini ubora wa vitu kiujumla ni mdogo sana
Uwezo wa Network
iPhone 6 Plus ni simu ya 4G yenye masafa mengi
Hivyo hii simu inakubali mitandao ya simu karibu yote duniani
Ila 4G yake ni aina ya LTE Cat 4
Spidi ya juu kabisa ya kudownload vitu kwa LTE Cat 4 ni 150Mbps
Japo mpaka sasa hakuna laini ya simu Tanzania yenye inteneti inayoweza kufika spidi hiyo
Pitia hapa uelewe, maana ya 4G
Ubora wa kioo cha iPhone 6 Plus
Kioo cha iPhone 6 Plus ni cha aina ya IPS LCD chenye resolution ndogo
Kumbuka simu ni ya zamani, mwaka 2014 resolution ya 1080 x 1920 pixels ilikuwa ni kubwa sana
Hii simu haina refresh rate kubwa
Na ubora wa IPS LCD unazidiwa kwa kiasi kikubwa na AMOLED
Hivyo ubora wa uonyeshaji wa picha ni wa kawaida
Nguvu ya processor Apple A8
Apple A8 ndio processor ambayo inaipa nguvu hii simu.
Utendaji wa apple a8 ni mdogo sana
Kwani ina core mbili tu zenye mizunguko michache inayofanya kazi chache
Hivyo usitarajie simu kuweza kufanya kazi kubwa kiufanisi
Kwa mfano app ya geekbench 5 inaipa apple a8 alama 328
Kwa nyakati hizo, hii ilikuwa ni utendaji mkubwa kwani chip ya Samsung Galaxy S5 ina alama 151 kwenye core moja
Kumbuka Galaxy S5 na iPhone 6 Plus zilikuwa zinashindana sokoni
Uwezo wa betri na chaji
Betri ya iPhone 6 Plus ni dogo sana
Ukubwa wa betri yake ni 2915mAh
Ukubwa huu wa betri unaweza kudumu kwa masaa 24 kama ukiwa unaongea na simu mara kwa mara
Na ukiwa unaperuzi intaneti betri inadumu kwa masaa 9 tu
Kama ukiwa unatazama video za instagram au youtube masaa ya betri yatapungua zaidi
Chaji yake inapeleka umeme mdogo wa wati 11
Ukubwa na aina ya memori
Kuna matoleo matatu ya hii iphone ambayo yote yana RAM ya 1GB
Kuna iphone ya GB 16, 64 na 128GB
Memori za 64gb na 128gb zinaweza kuhifadhi app na mafaili mengi
Kwa bahati mbaya udogo wa RAM unaipa simu kikomo cha kuhimili matumizi ya app nyingi kwa wakati mmoja
Uimara wa bodi ya iPhone 6 Plus
Bodi ya simu ya iPhone 6 Plus imetengenezwa na gorilla glass upande wa mbele
Ila upande wa nyuma simu imewekewa alumiamu
Lakini Gorilla zilizotengenezwa chini ya mwaka 2016 sio imara sana
Hivyo kuwa na kava na protector ni muhimu sana
Na uzuri kimo cha simu ni inchi 5.5
Hivyo ni nyepesi kubeba na inajaa kwenye mkono
Ubora wa kamera
iPhone 6 plus ina kamera moja tu upande wa nyuma
Na selfie kamera pia ipo moja
Ubora wake wa kamera unazidiwa na matoleo mapya ya simu za daraja la kati kuanzia 2019 hadi sasa
Pamoja na hivyo kamera yake inaweza kurekodi video za 4K kwa kasi ya 30fps
Na uzuri simu inatumia OIS kutuliza video wakati wa kurekodi huku ukiwa unatembea
Ubora wa Software
Nyakati za nyuma, app za simu zilikuwa haziwezi kuwasiliana kwenye mfumo wa iOS
Lakini ilipokuja iOS 8 mwaka 2014 hiko kitu kikaanzishwa
Mfumo huo uliwezesha kufanya vitu viwili kwa wakati mmoja kwenye kifaa kingine
Kwa mfano, ukiwa unaongea na simu ilikuwa ni ngumu kuandika sms
Basi iOS 8 iliwezesha simu kuungana kompyuta ya MAC
Na kisha ukawa unatumia kompyuta kujibu sms na simu ikiwa inatumika kuongea na mtu
Ila ni vitu vya kawaida siku hizi
Lakini pia simu inakubali mpaka iOS toleo la 12
Yapi Madhaifu ya iPhone 6 Plus
Ukilinganisha na simu mpya nyingi za sasa iPhone ina mapungufu mengi
Lakini ni vizuri ukilinganisha iPhone 6 Plus na Samsung Galaxy S5 au S6
Simu haijatumia kioo kizuri cha OLED au amoled
Wakati Galaxy S5 ilitoka kabla lakini tayari ilikuwa na kioo cha amoled
Simu haikuwa na uwezo wa kuzuia maji kupenya
Kwani hakuna sehemu ambayo imeainisha simu kuwa na IP67
Neno la Mwisho
Bei ya iPhone 6 Plus ni ndogo inayoweza kukuvuta kuimiliki simu
Lakini hii simu haipokei maboresho ya kupokea mfumo endeshi mpya wa iOS 15
Huko mbeleni kuna apps nyingi hazitofanya kazi
Kwa mfano app ya Whatsapp haitafanya kazi kwenye matoleo ya iPhone 6 muda si mrefu
Ni vizuri ukaangalia matoleo ya mbele ya iPhone zenye bei ndogo
Maoni 11 kuhusu “Bei ya Simu ya iPhone 6 Plus na Sifa zake Muhimu (2022)”
Swali langu nauliza jee hii simuyangu inaweza kuala kusumbua lini?
iPhone inapokea mpaka tolea iOS 12.5, na inapokea security updates hivyo inaweza chukua muda kidogo mpaka ianze kuacha kutumia WhatsApp na app zingine
Je sim yangu itaanza sumbua kuazia muda gani
Ndo mkomeeeee
iphone 6 hazitofanya whatsapp tena mwaka gani
kiukweli nisimu nzur san me niwape hongela sana compuni ya iphon
Sm yangu ni iPhone 6prus s nayo ita fungiwa WhasApp
Simu Gani ya iphone nyingine tofauti na iphone plus yenye bei ya chini??
iPhone 7 na zenyewe bei yake inavumilika
Je. mwaka gani iphone 6s WhatsApp itaacha kufanya kazi wakati kuna baadhi ya raia wanazimiliki sana na je. Kbla awajafanya ivo watatoa taarifa na kuwapa muda watumiaji wa iphone 6s
Aise kwanini inafika mda WhatsApp isitumike