Simu ya redmi note 9 ilitoka rasmi mwaka 2020
Kwa miaka miwili iliyopita ilikuwa ni moja ya simu nzuri ya daraja la kati.
Lakini uimara wake wa bodi, kamera, chaji na processor zinaipa simu nafasi ya kushindana na simu nyingi mpya za android 11
Bei ya redmi note 9 ni chini ya shilingi laki tano
Ukizielewa kiundani sifa zake, unaweza kushawishika kuitumia kwani zina ubora kwenye sehemu nyingi
Bei ya Redmi Note 9 Tanzania
Bei ya redmi note 9 pro kwenye soko la kidunia ni shilingi 438,858/=
Hii ni redmi yenye ukubwa wa GB 128 na RAM GB 6
Ni bei inayovumilika hasa unapotazama ubora wa sehemu mbali mbali za simu.
Kwa wauza simu ndani ya Tanzania bei yake inaweza kuzidi laki tano.
Kitu cha muhimu, zielewe kiufasaha sifa za simu yoyote kabla ya kununua, ili ujue kama itakidhi mahitaji yako
Sifa za Redmi Note 9
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | IPS LCD, |
Softawre |
|
Memori | 128GB,64GB, na RAM 6GB,3GB,4GB |
Kamera | Kamera nne
|
Muundo | Urefu-6.53inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 438,858/= |
Upi ubora wa simu ya Redmi Note 9
Ubora wa redmi note 9 unapatikana kwenye mfumo wake wa chaji
Simu ina uwezo wa kuchaji simu nyingine
Betri yake ni kubwa inayoweza kutunza chaji muda mrefu
Utendaji wake unaweza kusukuma gemu nyingi za ubora tofauti
Simu inapokea toleo lingine la android ya mwaka 2021
Uwezo wa Network
Simu ina uwezo wa kutumia intaneti za aina zote isipokuwa 5G
Netwrok bands za 4G zinasapoti mitandao yote ya simu ya hapa Tanzania .
Hii ni kwa sababu simu ina network bands zipatazo kumi ikiwemo zile zinazotumika na mitandao ya hapa nchini
Aina ya 4G yake ni LTE Cat 7 yenye spidi inayofikia 300Mbps.
Hiki ni kiwango kinaweza kudownload faili la ukubwa wa 1200MB kwa sekunde chache
Ubora wa kioo cha Redmi Note 9
Kioo cha redmi note 9 ni cha aina ya ips lcd
Kina uangavu wa wastani unaofikia nits 450.
Ukiwa unatumia simu juani unaweza pata shida kuona vitu vya kwenye display
Kiubora, ips lcd ina ubora mdogo ila resolution kubwa inaisidia simu kuonyesha vitu kwa ustadi.
Kwani resolution yake ina pixels 1080 x 2340
Nguvu ya processor ya MediaTek Helio G85
Simu ya redmi note 9 inapewa nguvu na processor ya Helio G85.
Hii ni processor ya daraja la kati yenye core nane.
Ina core zenye nguvu sana na zenye nguvu ndogo
Utendaji wa helio g85 ni wa wastani hasa kwa kutizama data za geekbench na antutu.
Kwenye geekbench processor inapata alama 358
Na antutu inaipa alama 231,800
Nguvu ya wasatani kiutendaji inasababishwa na muundo na uwezo wa core kubwa hasa,
Uwezo wa core kubwa
Kuna core kubwa mbili zenye spidi inayofikia 2.0GHz
Na zinatumia Cotex A75.
Core ya Cortex A75 haina nguvu kubwa sana ukilinganisha na Cortex A78.
Ndio maana kiutendaji processor haipati alama zinazofuka 500 kwenye geekbench.
Huu ni muundo unaoweza kusukuma gemu ya Fortnite kwenye resolution ndogo na kwa spidi ya 30fps
Uwezo wa core ndogo
Core ndogo zipo sita na zina spidi isiyovuka 1.8GHz
Hizi core zimeundwa kwa muundo wenye ufanisi mkubwa katika matumizi madogo ya umeme
Muundo huo ni Cortex A55
Cortex A55 hutumika pale processor inapochakata kazi zinazotumia nguvu ndogo
Uwezo wa betri na chaji
Betri ya redmi note 9 pro ina ukubwa wa 5020mAh
Chaji yake inaweza kueleka ueme unaofikia wati 18.
Huu ni umeme unaoweza kujaza simu kwa za zaidi ya masaa matatu
Wati 18 ni umeme mdogo ukilinganisha na ukubwa wa betri
Betri yake inakaa na chaji masaa 125 kama simu ikiwa inatumika mara chache.
Na ukiwa unatumia intaneti masaa mengi mfululizo simu inaisha chaji baada ya masaa 18.
Fuatilia, uwezo wa simu ya redmi kukaa na chaji(Majaribio ya gsmarena)
Ukubwa na aina ya memori
Simu inakuja katika aina nne upande wamemori
Kuna redmi ya 64GB ram ya 3GB, 64GB ram ya 4GB,128GB ram ya 4GB na 128GB ram ya 6GB
Huu ni ukubwa unaotunza mafaili na video za kutosha
Uimara wa bodi ya Redmi Note 9 Pro
Redmi note 9 pro ina bodi ambazo si imara sana upande wa nyuma
Kwa sababu imetengenezwa kwa plastiki.
Lakini kwenye screen ni kugumu kupasuka na kuchunika.
Hiyo inatokana na simu kuwa na kioo cha gorilla glass 5
Ubora wa kamera
Simu ina kamera zipatazo nne
Kamera kuu ina sensa kubwa ya megapixel 48
Lakini mufmo wake wa kamera hauna dual pixel pdaf wala OIS.
Dual pixel pdaf inaipa kamera ya simu ubora wa kulenga kwa ustadi kitu kinachotembea pindi unapochukua picha au video.
Kamera yake inaweza kurekodi video za aina moja ambayo ni full hd kwa spidi ya 30fps
Ubora wa Software
Simu hii inakuja na android 10 ila inakubali kuwekewa toleo la android 11
Na pia inakuja na MIUI 11 na inakubali MIUI 12.5
MIUI 12.5 ina app nzuri ya kuscreen shot.
Kwani inaweza kuscreenshot kitu kwa urefu unaohitaji hata ukurasa mzima
Yapi Madhaifu ya Redmi Note 9
Utendaji wa redmi note 9 ni wa wastani kwa maana hauna nguvu kubwa sana
Mfumo wake wa kamera hauna OIS
Chaji yake inajaza betri kwa masaa mengi kwa sababu ya spidi ndogo
Simu haitumii kioo cha amoled ambavyo vinaonyesha vitu kwa uangavu mkubwa
4G yake ina bands chache tofauti na simu za redmi zingine
Simu haina kamera ya telephoto wa optical zoom
Neno la Mwisho
Hii simu ni nzuri.
Ila bei yake inaonekana kuwa kubwa kwa mwaka huu.
Kuna simu ya Redmi Note 10 5G inayouzwa chini ya laki nne ina utendaji mkubwa kuliko Note 9
Kwa hiyo kama muuzaji anaiuza chini ya kaki tatu na nusu hapo itakuwa sawa.
Lakini kwa bei ya laki nne utapata simu bora kuliko hii.
Chaguo ni lako.
Wazo moja kuhusu “Ubora na bei ya simu ya Redmi note 9 (2022)”
Nna simu yangu Xiaomi Redmi note 9 128 gb ina tatizo la hi_fi audio ivo nahitaji mteja