Kama umeshawahi kutumia simu za tecno na hukuwahi kuridhishwa na ubora wa kamera basi Tecno Phantom X inaweza kukubadilisha.
Tecno Phantom X ni moja ya tecno yenye camera nzuri kaitka upigaji picha na kurekodi video
Inazipita Tecno nyingi zilizopo sokoni
Ila kiuhalisia haiwezi kuwekwa kwenye kundi la simu zenye kamera nzuri na ubora mkubwa
Ubora wake unashindana zaidi na smartphone za Infinix
Kwenye hii posti utaona ubora wa picha ambazo Phantom X imezipiga na ufafanuzi wa kamera zake tatu
Utaona uwezo wa phantom x katika kupiga picha nyakati za mchana na usiku
Idadi na aina ya kamera za Tecno Phantom X
Simu ya tecno phantom x ni tecno macho matatu kwa maana ina aina tatu za kamera
Kamera hizo ni
- Wide (kamera kuu) yenye resolution ya 50MP
- Telephoto yenye resolution ya 13MP
- Ultrawide ya nyuzi 120 na resolution ya 8MP
Kamera ya Telephoto hutumika kupiga vitu ambavyo vipo mbali sana na kamera
Huwa zinatoa picha bila kupoteza ubora (kwa maana pixels) ukilinganisha na zoom ya app ya kamera
Ultrawide huwa inapiga picha eneo pana mfano kama unataka uwanja wa mpira uonekane wote basi utatumia kamera ya ultrawide
Kamera ya wide ni ile kamera ya kawaida ambayo ndio hutumika zaidi
Ukitazama resolution ya moja ya kamera ina 50MP.
Wingi wa megapixel si kigezo kinachoelezea ubora wa kamera ikiwemo phantom x
Kamera za iphone huwa zina megapixel 12 tu ila huwa zinatoa picha kali
Bali kuna vitu vya muhimu vinayoisaidia simu kutoa picha safi
Vitu vya muhimu vilivyopo kwenye kamera ya Tecno Phantom X
Kama kuna kitu cha msingi cha kutazama kwenye kamera basi ni aina ya ulengaji (autofocus)
Na uwepo wa HDR
Phantom X ina ulengaji ulio mzuri wa kutambua kukilenga kitu kwa ustadi
Hiyo inatokana na simu kuwa na autofocus ya Dual Pixel PDAF na Laser AF
Autofocus husaidia kutambua kinachopigwa kama kipo kwenye eneo linalotakiwa (focus)
Simu yenye dual pixel pdaf hutoa picha zinazoonekana vizuri ambazo zimepigwa kwenye mwanga mdogo
Na pia dual pixel pdaf hutoa picha vizuri ukiwa unapiga kitu kinachotembea kwa haraka mfano ukiwa unampiga picha ndege angani
Kwa sababu dual pixel pdaf huwa iko fasta kutambua na kukilenga kitu
Laser AF hutumia miale kutambua kinachopigwa picha.
Kamera hii inaweza kuona kitu hata kwenye giza
Uwepo wa HDR
Kamera ya tecno phantom x ina hdr ya kawaida na sio ile ya HDR10 au HDR10+
Umuhimu wa HDR ni kuboresha muonekano wa vitu vinavyopigwa picha au kurekodiwa
Lengo kubwa ni muonekano wa picha uendane na jinsi kitu kinavyoonekana na jicho la mwanadamu kwenye mazingira halisi.
Na huwa inasaidia sana kuonyesha vitu vizuri kwenye mwanga mdogo
Uwepo wa Optical Zoom
Optical zoom ni aina zoom(kukuza picha) inayotumia lenzi za kamera
Optical zoom ya phantom x inaweza kukuza kitu mara mbili
Ni ndogo ukilinganisha na Samsung Galaxy S22 ambayo inakuza kitu mara tatu
Japokuwa app ya simu (digital zoom) inaweza kuza kitu mara 30 lakini huwa zinapoteza ubora
Optical zoom haipotezi ubora pindi itumikapo
Uwezo wa kukusanya mwanga
Uwezo wa ukusanyaji mwanga hupimwa kwa kutazama ukubwa wa tundu unaopitisha mwanga kwenda kwenye lenzi
Hii hufahamika kama aperture vipimo vyake huandikwa f/{namba }
Mfano Tecno Phantom X aperture yake ni f/1.9
Hivyo upitishaji mwanga ni wa kiwango cha kulidhisha
Namba ikiwa kubwa maana yake mwanga unaopita ni mdogo na ikiwa ndogo maana yake simu inapitisha mwanga mwingi
Simu ikiwa inapitisha mwanga mwingi na picha hutokea vizuri pia
Muundo wa app ya Camera ya Tecno phantom X
App ya phantom x ukiifungua utakuta imeandikwa AI Camera
Hii ni kamera ya wide ile yenye 50MP
App ina machaguo mengi ikiwemo uwezo wa kuzima HDR kama huitaji
Na pia ina kitu kinaitwa Super Night Mode
Ambayo inafaa kutumika kama mwanga ukiwa mdogo
Yenyewe inatumia algorithms(kanuni) ambazo zinaweza isaidia kamera kutoa picha vizuri nyakati za usiku
Ubora wa picha nyakati za Mchana
Kamera ya tecno phantom x inatoa picha nzuri kimuonekano
Upande wa rangi inajitahidi kwa kiasi kikubwa kuonyesha rangi sahihi
Hivyo tatizo la overexposure si kubwa sana
Changamoto kubwa japo ina overexposure ndogo, ila inaifanya kamera kutoonyesha rangi kwa uzuri.
Ukiizoom picha mara moja ubora wa muonekano wa vitu unapungua ubora kiasi tofauti na picha iliyopigwa na iphone 13 pro max kwenye eneo hilo
Itazame hapa na ulinganishe: Picha ya jengo iliyopigwa kwa iPhone 13 pro Max
Ila kitu cha msingi ambacho ni kizuri zaidi ni uwezo wake wa kutofautisha rangi za vitu
Tazama upande wa kichaka kulia mwa mti
Picha inaoonyesha kivuri hakijaweza kuzuia rangi za majani kupotea
Baadhi ya kamera hupoteza kabisa uhalisia pale sehemu inapokuwa na giza tofauti na jinsi kitu kinavyoonekana
Ila hii imejitahidi kwa hilo
Japokuwa simu ina noise(vitu vinavyochafua ubora wa picha) zinazoweza onekana kwa uwazi
Selfie camera(kamera za mbele zipo mbili) inajitahidi kuonyesha vitu vizuri
Ila kwenye mwanga mkali selfie camera ya tecno phantom x inakumbana kuzidi kwa uwiano wa contrast
Kwa maana muangaza unakuwa mwingi mpaka unapoteza rangi halisi ya kitu
Hizo sehemu ambazo zimezungushiwa zimekuwa nyeupe badala ya nyekundu (pinki nadhani)
Hili tatizo hujulukana kama overxposure
Kama kamera za selfie zingekuwa na HDR hilo tatizo lingepunguzwa
Ila kiujumla kamera hii ni nzuri kwa kulinganisha na simu nyingi za tecno
Ubora wa picha nyakati za usiku
Kamera kubwa ya tecno inaonyesha vitu vilivyopo kwenye picha kwa uzuri kiasi fulani
Kama ilivyo kawaida changamoto ya noises zipo kwa nyakati za usiku
Noise(vitu visivyohitajika kama ukungu) kwa kamera za simu huwa zipo
Ila simu zenye kamera kali zaidi huonekana kwa kiwango kidogo
Kama picha inavyoonekana, karibu vitu vyote vinaokena kwa uzuri
Ili upate ubora mzuri itakubidi utumie Super Night Mode
Vinginevyo ubora wa picha unaweza usiwe mkubwa sana
Ubora wa kamera za Ultrawide na Telephoto
Uwezo wa kamera hizi mbili ni wa kiwango cha chini kiujumla
Upande wa kamera wa ultrawide hautoi picha nzuri
Hii inawezekana ikawa inachangiwa na resolution yake ya 8MP
Lakini Redmi Note 10 ina kamera ya ultrawide yenye 8MP lakini ubora wake ni wa kuridhisha
Ubora wa Video
Tecno Phantom X inaweza kurekodi video za ubora aina mbili
Yaani video za Full HD na 4K (UHD)
Inarekodi video za 4K kwa kiwango cha fremu 30 na 60 kwa sekunde
Ila seldie kamera inarekodi video za full hd pekee
Unaweza tazama hapa
Ila kwa bahati mbaya simu inakosa teknolojia ya OIS
OIS (Optical Image Stabilization) huondoa mitikisiko wakati wa kurekodi huku ukiwa unatembea
Hivyo video hutulia
Bei ya Tecno Phantom X
Kikawaida simu ikiwa na kamera nzuri basi bei yake huchangamka pia
Kwa kuwa Tecno Phantom X ni tecno yenye camera nzuri basi bei yake haiwezi kuwa sawa na tecno zingine
Kwani bei yake inazidi milioni moja
Japokuwa kuna vitu vingine pia ambavyo huchangia bei kuwa juu.
Fuatilia: Ubora na bei ya Tecno Phantom X