SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

Bei ya Tecno Phantom X na Sifa Zake (2022)

Sifa za simu

Sihaba Mikole

April 17, 2022

Tecno Phantom X ni simu yenye kamera nzuri baina ya tecno nyingi ambazo zimewahi kutoka

Hii ni smartphone ya mwaka 2021 yenye ubora unaozishinda simu mpya nyingi  za 2022

Ubora wa kamera na utendaji umeifanya bei ya Tecno Phantom X kuzidi milioni moja

simu ya teno phantom x upande wa nyuma na mbele

Bei inayoleta utata linapokuja swala la sifa zake.

Hii inatokana na uwepo wa simu zingine bora zaidi zenye bei ya chini ya milioni moja

Bei ya Tecno Phantom X Tanzania

Bei ya phantom x kwenye maduka mengi ya simu ni shilingi 1,100,000/=

Phantom X ni simu kali kutoka tecno

Hii ni simu ya flagship (simu ambazo kampuni inaweka nguvu nyingi)

Simu ina sifa nzuri nyingi

Japo zipo baadhi ambazo zinaonyesha simu kuwa ya gharama kuliko uhalisia

Sifa za Tecno Phantom X

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g, 4g
Processor(SoC)
  • CPU – Mediatek Helio G95
  • Core Zenye nguvu(2) – 2×2.05 GHz Cortex-A76
  • Core Za kawaida(6) – 6×2.0 GHz Cortex-A55
  • GPU-Mali-G76 MC4
Display(Kioo) Super AMOLED, Refresh rate:90Hz
Softawre
  • Android 11
Memori 256GB na RAM 8GB
Kamera Kamera nne

  1. 48MP,dual pixel PDAF(wide)
  2. 13MP(telephoto)
  3. 8MP(ultrawide)
Muundo Urefu-6.7inchi
Chaji na Betri
  • 4700mAh-Li-Po
  • Chaji-33W
Bei ya simu(TSH) 1,100,000/=

Upi ubora wa Tecno phantom x

Simu ina utendaji mkubwa kutokana na kuwa na processor ya daraja la kati.

Kamera zake zinatumia teknolojia za kisasa za ulengaji

Ina mfumo wa chaji unaopeleka chaji kwa kasi inayojaza betri kwa haraka

taarifa ya tecno phantom x kwa picha

Betri lake ni kubwa linalokaa na chaji muda mrefu

Ni simu ndefu na inayonyesha vitu kwa uzuri

Kioo chake ni chepesi kwa sababu ya kuwa na refresh rate kubwa.

Tuchimbe kiundani kutathmini ubora kwenye vipengele vingine

Uwezo wa Network

Simu ya tecno phantom x ni simu ya 4G inayokubali intaneti ya 4G ya mitandao yote Tanzania

Inatumia 4G aina ya LTE Cat 12

Kasi ya kudownload ya LTE cat 12 inafika 600Mbps

network ya tecno phantom x

600Mbps ni sawa na 75MBps

Kwa maana mtandao wa simu wenye spidi kubwa utaifanya simu kudownload faili la ukubwa 75MB kwa sekunde moja

Japo hakuna kampuni linalotoa huduma ya intaneti yenye kasi hii hapa nchini

Ubora wa kioo cha Tecno phantom x

Kioo cha tecno ni kizuri na kinaoonyesha vitu kwa rangi zinazokaribiana na uhalisia wa mazingira.

Picha na video zinaonekana vizuri kwa sababu simu ina kioo cha super amoled.

Kioo kilichowezeshwa refresh rate inayofika 90Hz.

Ukiwa unaperuzi sms ama picha kioo huwa kinaenda kwa haraka

Na refresh rate kubwa inaifanya simu kuwa nyepesi wakati wa kucheza gemu.

Ubora wa kioo unaonegezeka zaidi ikiwa resolution kubwa.

Phantom X kioo chake kina resolution yenye pixels nyingi kiasi cha 1080×2340

Nguvu ya processor ya Helio G95

Simu ya tecno phantom x ina ulengaji wenye nguvu ya kuridhisha

Ni simu inayoweza kucheza gemu yenye graphics nyingi ya Call of Duty: Mobile kwa ubora wa Ultra hd.

Simu inacheza gemu hilo kwa spidi ya 38fps

Nguvu kubwa inachangiwa na processor ya Helio G95

Ni processor ya daraja la kati yenye core nane zilizogawanyika sehemu mbili.

Kuna core kubwa na core ndogo kabisa

Uwezo wa core kubwa

Nguvu kubwa ya hii chip inasabishwa na kutumia muundo wa Cortex A76

Utendaji wa core zenye Cortex A76 unazingatia matumizi kidogo ya umeme kwa kazi kubwa

Japokuwa kiuwezo, Cortex A76 inaachwa kwa mbali na muundo wa Cortex A78

Cortex A78 inafanya kazi kubwa na kwa matumizi madogo zaidi ya betri

Uwezo wa Core kubwa za helio g95 ambazo zipo mbili ni wa wastani.

Kwa sababu kuna baadhi ya magemu kama Fortnite yanacheza kwa resolution ndogo

Uwezo wa core ndogo

Processor ina core ndogo sita ambazo hutumika simu ikiwa inafanya kazi zinazohitaji nguvu ndogo.

Uwezo wa core ndogo hupimwa kwa kuangalia matumizi madogo ya umeme

Processor ya helio g95 zina core ndogo zenye muundo wa Cortex A55

Huu ni moja ya muundo unakula umeme mdogo sana

Uwezo wa betri na chaji

Betri ya tecno phantom x ina ukubwa wa 4700mAh.’

Kwenye majaribio mbalimbali, betri yake inakaa na chaji masaa 122 simu ikiwa inatumika mara chache

Na simu ikiwa kwenye intaneti, betri inaweza kuisha baada masaa yanayokaribia 15

Chaji ya simu inapeleka umeme mwingi.

Kwani kasi yake inafikia wati 33

Kwa mujibu wa Tecno, wati 33 inaweza kujaza betri kwa 70% kwa nusu saa tu

Ukubwa na aina ya memori

Kuna toleo moja la phantom x

Na toleo lenyewe lina memori ya GB 250 na RAM ya GB 8.

Tecno hawajainisha aina ya memori ya simu, lakini inaweza ikawa memori za UFS

Uimara wa bodi ya Tecno phantom x

Simu ina bodi imara na ngumu kuvunjika

Kwa sababu upande wa kioo umewekewa vioo vya gorilla glass 5

Na upabde wa nyuma simu ina kioo cha gorilla glass 5

Gorilla glass 5 huwa ni vioo vigumu kupasuka pindi simu ikianguka kwa urefu wa kimo cha mita 1.2

Na glassi huepusha simu na mikwaruzo

Ubora wa kamera

Tecno phantom x ina kamera mbili upande wa nyuma

Kamera yake kuu ni nzuri

Kwani imewezeshwa teknolojia ya ulengaji ya dual pixel pdaf.

dual pixel pdaf inafanya simu kutoa picha safi hasa kitu kinachopigwa picha kikiwa kwenye mwendo.

tecno phantom x upande wa kamera

Pia ina autofocus nyingine aina ya Laser AF

Laser AF inaisaidia simu kulenga kwa usahihi endapo picha inachukuliwa usiku au kwenye mwanga mdogo

Kwani ni aina ya autofocus inayotoa mwanga unaoweza kuona vitu usiku

Kamera zake zinaweza rekodi video mpaka za 4K kwa spidi ya 60fps

Ubora wa Software

Simu inakuja na android 11

Mfumo endeshi wa android 11 una applikesheni ya kuscreen na kurekodi screen

Hivyo hutohitaji app ya ziada.

Ukitaka kujua vitu vilivyomo kwenye android 11, pitia linki hii

Ni mfumo unaokupa uwezo wa kudhibiti app linapokuja aina ya data app inazozichukua

Yapi Madhaifu ya Tecno phantom x

Kasoro kubwa inayoonekana wazi ni uwezo wa processor.

Vitu vilivyomo kwenye tecno phantom x vingekuwa na utendaji mkubwa zaidi kama simu ingekuwa na chip yenye nguvu.

Simu ambazo bei yake inafika milioni huwa zinakuwa na chip ya simu yenye nguvu

Tecno walipaswa waweke angalau chip MediaTek Dimensity 1200 au Snapdragon 695 5g

Kasoro nyingine ni simu kutokuwa na 5G

Na jambo lingine ni simu kukosa uwezo wa kuzuia maji kupenya.

Simu kama samsung galaxy a52 ambayo haivuki laki nane ina viwango vya IP67

Ambavyo vinaonyesha uwezo wa simu kuzuia maji kupenya

Neno la Mwisho

Ukiondoa uwezo mdogo wa processor, Phantom X ni simu nzuri ya daraja la kati.

Japokuwa bei ni kubwa lakini ina sifa za kuvutia nyingi

Bei ya tecno phantom x inaweza kunua simu ya redmi note 11 pro+ 5g na chenji ikabaki

Redmi note 11 pro+ 5g ina utendaji wa processor wenye nguvu kuliko phantom x

Maoni na Maswali

Email yako haitochapishwa, kwenye alama * lazima pajazwe ili ukomenti

SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

E-mail : simunzuriblog@gmail.com

Simu: +255 683 420 543

Whatsapp: +255 756 077 262

Kabila, Magu

Mwanza, Tanzania

Company

Find Us On

FB Twitter Instagram