Kikawaida kamera nzuri za simu zinatoa picha au video zinaonekana vizuri zikiwa zimepigwa na kurekodiwa kwenye mazingira yenye mwanga mdogo.
Simu ambazo zina ubora mdogo wa kamera huonyesha vitu vilivyopigwa kwenye mwanga mdogo vibaya.
Mara nyingi simu zenye kamera nzuri huwa na teknolojia nzuri ya kulenga(autofocus), teknolojia ya kutuliza kamera(OIS), teknolojia ya optical zoom na processor yenye nguvu.
Kwenye hii post kuna simu tano zenye kamera bora.
Taarifa za ubora wa kamera umeegemea sana kwenye majaribio ya DXOMark na wachambuzi mbalimbali.
Sasa basi ni jambo la msingi kuvifahamu vitu vinavyoangaliwa sana kutambua uwezo wa kamera ya simu.
- Exposure na Contrast
- Rangi
- Autofocus
- Texture
- Noise(Chenga Chenga)
- Utulivu wa kamera wakati wa kurekodi.
Nini hasa maana ya hivi vitu vya kamera na umuhimu wake?
Exposure na Contrast
Exposure inafanunua kiasi cha mwanga kamera inaweza kukusanya.
Kamera inapokusanya mwanga wa kutosha wakati wa upigaji picha ndivyo picha inatokea safi.
Exposure sahihi inatengeneza picha bora.
Vitu vinavyoathiri kamera kwenye ukusanyaji wa mwanga ni Aperture(tundu linalopitisha mwanga).
Itazame simu ya Samsung galaxy s22 ultra kwenye kurasa gsmarena.
Kwenye upande wa kamera utaona kuna kitu kimeandikwa f/1.8.
f/1.8 ni aperture inayotambulisha ukubwa wa aperture inayopitisha mwanga kwenye kamera.
Hiki ni kiasi kikubwa cha aperture, namba zinapokuwa kubwa basi apperture ni ndogo.
Na zinapokuwa ndogo basi apperture ni kubwa hivyo simu inapitisha mwanga mwingi.
Kamera inapaswa iweze kutofautisha rangi na tone.
Yaani iweze kutofautisha rangi tofauti tofauti kutoka nyeusi mpaka nyeupe.
Kitendo hiki kinafahamika kama contrast.
Sasa contrast ikiwa angavu sana itaongeza mwangaza uangavu kwenye picha yote na kufanya rangi za picha na uweupe usiotakiwa.
Na contrast ya kamera ikiwa na giza rangi za picha zitaonekana na uweusi usiohitajika.
Lakini ikiwa na uwiano mzuri kamera inatoa picha iliyo balansi rangi hivyo picha nzuri.
Rangi
Kamera nzuri inatoa picha ama video kama jicho la binadamu linvyoona hiko kitu kwenye mazingira halisi.
Rangi nyeusi inapaswa ionekane kama ilivyo bila kuongeza rangi ama kupunguza.
Baadhi ya smartphone hung’arisha mtu mwenye rangi nyeusi kwa kuongeza rangi zisizohitajika.
Kiuhalisia kamera haipaswi kukoreza sana rangi bali kitu kinachapigwa kinapaswa kutokea kwa rangi zake halisi.
Autofocus
Autofocus ni uwezo wa kamera kulenga kitu kinachopigwa picha kwa usahihi.
Kamera nzuri inaweza kupiga picha kitu kinachotembea na kutokea vizuri.
Chukulia mfano unapiga picha ya mwewe anaetembea.
Ili mwewe atokee vizuri inabidi simu ilenge vizuri.
Inakuwa ni changamoto kuendana na spidi ya mwewe.
Ila simu yenye teknolojia nzuri ya autofocus italenga yenyewe moja kwa moja.
Na kufanya mwewe kutokea vizuri.
Mpaka sasa autofocus inayotumika sana kwenye simu hasa za daraja la chini ni PDAF(Phase Detect AutoFocus).
Simu za madaraja ya juu hutumia Autofocus zilizoboresha ambazo ni dual Pixel PDAF, Multi Direction PDAF na Laser Autofocus
Hata simu zenye camera nzuri zilizopo hapa zinatumia dual Pixel PDAF na Laser Autofocus au Multi Direction PDAF.
Texture
Texture ni ubora wa picha kuonyesha kila kilichopo kwenye kitu kinachopigwa picha.
Kwa mfano ukiwa unampiga picha mtu na ukiizoom uso wa huyo mtu basi kila kitu ikiwemo vipele inapaswa vionekane na matundu ya ngozi.
Ukiona kamera inashindwa kuonyesha baadhi ya vitu wakati wa kuzoom basi kamera ya simu sio nzuri.
Mifano mzuri ni hizi picha mbili ambazo zinafanya ya texture kwenye jicho.
Kama unavyoona picha ya kushoto inaonyesha vitu vingi vya kwenye ngozi ya jicho.
Hii inafanya simu kupiga picha kwa uzuri.
Noise
Kamera ikipiga picha ama kurekodi video inatakiwa kuonyesha vitu vinavyohusika kwa uzuri.
Kamera ikiwa inaongeza vitu ambavyo havipo kwenye kinachopigwa picha hiyo hufahamika kama Noise.
Kwa mfano unapiga picha halafu picha inaonyesha chenga chenga, giza au mwanga uliopitiliza, zote hizo ni noise.
Pia picha au video kuonyesha ukungu ukungu.
Noise ni kitu ambacho kipo kwenye kamera nyingi za simu.
Lakini kiwango cha Noise kikiwa kikubwa tarajia picha mbaya.
Noise hutokea sana pale ambapo simu inakuwa na uwezo mdogo wa kukusanya mwanga wa kutosha hasa usiku.
Na inaposhindwa kutengeneza contrast sahihi.
Utulivu wa kamera(OIS)
Kamera nzuri ya simu huwa haitingishiki pale anayerokodi video akiwa anatembea.
Video inaonekana kutulia.
Kamera za simu zenye uwezo huu huwa zina teknolojia inayofahamika kama OIS.
Kirefu cha OIS ni Optical Image Stabilization.
Na teknolojia ya stabilization inayotumika sana kwenye selfie kamera ni gyro-EIS.
gyro-EIS inafanana na OIS ila gyro EIS inatumia sensa accelerometer.
Simu zote ambazo zipo kwenye orodha ya simu zenye kamera bora zina OIS.
Picha za usiku
Kamera nzuri ina uweozo wa kuonyesha kwa usahihi picha zinapigwa nyakati za usiku.
Kikawaida mwanga wa usiku ni mdogo.
Simu zenye kamera nzuri huwa na aperture kubwa.
Kwa simu yenye aperture kubwa inaweza kukusanya mwanga mwingi usiku.
Mwanga ukishakuwa wa kutosha basi kazi zingine zinaweza fanyika kiustadi.
Siku hizi baadhi ya simu wameboresha kamera kwa kuweka kitu kinafahamika kama AI(Artificial Intelligence)
Sasa basi simu zipi zilizoonyesha ubora kwenye nyanja zilizoainishwa?
Huawei P50 Pro
Simu ya Huawei P50 Pro inatumia teknolojia ya autofocus ya Laser AF na PDAF.
Kukilenga kitu kinachopigwa kiustadi Laser AF hutumia miale kuakisi.
Miale inaskani data kiundani tofauti na Lens.
Kamera kuu ya huawei p50 pro ina resolution ya megapixel 50.
Upitishaji mwanga kwenye simu hii ni wa kutosha kwa sababu aperture yake ina ukubwa wa f/1.8
Muungano wa teknolojia nzuri ya autofocus na apperture unazalisha ubora sahihi kwenye picha.
Picha zinazopigwa na simu ya P50 Pro zinaonyesha kila kitu kwa asilimia kubwa bila kupoteza data nyingi.
Exposure ya simu inabalansi mwanga kwa usahihi.
Hilo linavyofanya kamera kutokuongeza wala kupunguza kitu kwenye picha.
Kwa maana contrast inaonyesha rangi sahihi kwa uhalisia kama jicho la binadamu linavyoona.
Hii ni picha ambayo imepigwa kwa kutumia simu ya huawei p50 pro na GSMarena wakati wa mchana.
Vitu vyote vilivyolengwa na simu vinaonekana .
Rangi ya anga ni bluu kama ilivyo kwenye mazingira halisi.
Rangi ya ardhi yenye barafu haijaathiriwa na mwangaza mkubwa wa jua.
Barafu inaonekana kwa rangi yake asilia nyeupe.
Kamera ya simu haijakoreza magorofa kupitiliza
Kiufupi kamera ya simu inaweka milinganyo mzuri ya contrast na dynamic range.
Nyakati za siku ndizo nyakati sahihi hasa kujua uwezo wa kamera.
Huawei P50 Pro bado inatoa picha kali hata kwenye mazingira ya mwanga mdogo.
Exposure ya simu inaweza kukusanya mwanga wa kutosha unaoweza kuonesha vitu vinavyotakiwa kupiga simu.
Autofocus yake ya Laser AF inasaidia simu kukitambua kitu kinachopigwa picha na kukilenga vizuri.
Laser AF inaweza kuona vitu hata kwenye giza.
Kwenye upande wa texture, vitu vya kwenye picha vinaonekana kiundani hata ukiikuza picha.
Japokuwa kamera kuu inapoteza ubora wa kitu ambacho kipo mbali na kamera.
Mfano huu hapa.
Kwenye ghorofa kwenye sehemu liyozungushiwa duara jekundu ni mashine ambayo ipo mbali na simu juu kabisa.
Picha ikikuzwa kuitazama kiundani kuna ukungu unatengenezeka yaani Noise.
Noise ya simu ni ndogo kwa sababu vitu vingi kwenye eneo hilo vinaonekana kwa uzuri.
Tazama ukuta na hiyo mashine.
Simu nyingi hasa zenye kamera mbovu haziwezi onyesha kila kitu kwenye hilo eneo
Apple iPhone 13 Pro Max
Kamera ya iPhone 13 Pro Max ina utendaji mzuri kwenye kubalansi mwanga kwa maana ya exposure.
Simu ya iPhone 13 Pro Max ina aperture kubwa ya f/1.5
Mwanga unaokusanywa ni mwingi unaoweza kuonyesha picha kiundani kwa uzuri.
Kamera ya iphone 13 pro max inatumia teknolojia ya dual pixel pdaf kwenye kamera kuu.
Ubora wa picha zinazopigwa mchana unaweza ukaendana na Huawei P50 Pro.
Rangi za vitu za kwenye picha za mchana haviathiriwi na mwanga mkubwa wa jua.
Vitu hutokea kwa rangi halisi.
Hii ina maana contrast na dynamic range ya iphone 13 pro max ina mlinganyo na usahihishaji unaofaa kwenye kamera.
Picha iliyopigwa mchana na iPhone 13 Pro Max kutoka kwa gsmarena.
Kamera inaonyesha vitu kwa uhalisia bila kuongeza ama kupunguza.
Huwezi ukaona noise kama ukungu ama chenga chenga kwenye kila kitu kilichotokea kwenye picha.
Ukiikuza picha kuangalia vitu vilivyopo kiundani utaweza kuona kwa uzuri.
Utendaji kwenye texture upande wa vitu vilivyo mbali na kamera ni mkubwa.
Kamera inaonyesha data kwa asilimia kubwa.
iPhone 13 pro max inatoa picha ama video nzuri kwenye mwanga mdogo.
Nyakati za usiku huwa zinasababisha kamera za simu kuzarisha noise hasa ukungu.
iPhone hii ina kiwango kidogo sana cha Noise kwenye mwanga hafifu.
Hata ukijaribu kukuza picha kutathmini texture wakati wa mchana, kitu kilicho mbali na kamera kitaonekana.
Mashine na ukuta kwenye duara jekundu vinaonekana kwa rangi zake na vinaweza kutambulika.
Hakuna ukungu au chenga upande wa kwenye anga.
Lakini nyakati za usiku vitu ambavyo vipo mbali kamera havionekani vizuri kwa sababu kamera ya simu inakusanya mwanga mdogo sana na vinafanya kutokuonekana vizuri.
Kwa kuzingatia standard ya kamera,
iPhone 13 Pro Max ina texture nzuri na noise ndogo nyakati za usiku.
Google Pixel 6 Pro
Simu ya Google pixel 6 pro ina kamera tatu.
Kamera kuu ina 50MP.
Kamera zingine ni Telephoto na ultrawide.
Kwenye kamera kuu kuna aperture ya f/1.9
Google pixel 6 pro inatumia teknolojia mbili za autofocus ambazo ni Laser AF na dual pixel autofocus.
Laser AF na dual pixel autofocus zina ulengaji wenye vipimo sahihi kwa sasa.
Uwezakano ni kuwa laser af imewekwa kutumika usiku au kwenye mwanga mdogo.
Kiasi cha upitishaji mwanga kinazidiwa na simu za iphone 13 pro max na Huwei P50 Pro.
Kamera ya pixel 6 pro ina exposure na contrast zinazosaidia muonekano safi wa picha nyakati za mchana.
Kamera ya pixel 6 pro inazalisha texture nzuri wakati wa mchana.
Kitu cha mbali kikikuzwa picha inaonyesha kila kinachohusika kwenye hiko kitu.
Pia kama ilivyo kwenye simu zingine, wakati wa usiku kamera inatoa picha nzuri.
Ijapokuwa noise zinatokea ila kwa kiwango cha chini.
Utendaji wa kamera kwenye ukusanyaji mwanga unafanya baadhi ya vitu vionekane kwa mbali.
Bado google pixel 6 ni kamera inayoonyesha vitu kwa usahihi usiku.
Exposure ndogo inachangia rangi nyeusi kutawala sana kiasi cha kwamba rangi ya kijani ya majani haionekani vizuri hata picha ikikuzwa.
Vivo X70 Pro+
Simu ya vivo X70 ina kamera nne ambazo ni wide(kamera kuu) 50MP, periscope telephoto 8MP, Telephoto 12MP na ultrawide 50MP.
Vivo x70 pro+ inatumia aina mbili za autofocus ambazo ni PDAF na Laser Af.
Laser AF inapotumika autofocus nyingine pia inahitajika.
Laser AF iko fasta ila ina changamoto ya kulenga kitu ambacho kipo mbali.
Aperture ya kamera inaweza kupitisha mwanga mwingi.
Ina aperture kubwa ya saizi f/1.6
Ubora wa hardware wa kamera ni lazima kamira itatoa picha kali wakati wa mchana na usiku.
X70 Pro ina exposure inabalansi mwanga kwa ustadi sahihi.
Mwanga ambao unafanya kamera kutoa picha zenye rangi zinazoendana na mazingira halisi
Chukulia picha hii iliyopigwa na gsmarena kwa kutumia simu ya vivo x70 pro+.
Rangi ya majani yaliyokauka kwenye mti kushoto yako tofauti na majani kibichi ya kwenye uwanja.
Mwanga wa kutosha unafanya anga kuonekana na rangi ya bluu halisi.
Kamera haiongezi rangi ambazo si halisi na wala haitoi chenga chenga hata ukiikuza picha.
Na upande wa texture kamera inaweza kuonyesha vitu karibu vya kwenye picha kiundani kama ukiikuza.
Xiaomi Mi 11 Ultra
Simu ya xiaomi mi 11 ultra ni moja ya simu yenye kamera tatu.
Kamera hizo ni wide camera 50MP, ultrawide camera 48MP na periscope 48MP.
Kamera za kuu(wide) na periscope zina OIS hivyo video haitotikisika wakati wa kurekodi.
Upande wa autofocus(Ulengaji) imetumia dual pixel pdaf na Laser AF kwenye kamera kuu.
Dual pixel pdaf hukusanya data nyingi za kamera kukilenga kwa usahihi sana kitu kinachopigwa picha ukilinganisha na pdaf.
Na Laser AF inaboresha upigaji picha kwenye mwanga hafifu hasa nyakati za usiku.
Kamera ya ultrawide na telephoto zinatumia pdaf.
Na aperture ya kamera kuu inaukubwa wa f/2.0 ambayo inapitisha mwanga wa kutosha kwenye kamera.
Kamera zingine mbili zinapitisha mwanga mdogo kwa sababu aperture zake ni f/4.1 na f/2.2
Kamera ya mi 11 ultra zinapiga picha safi nyakati za usiku na mchana.
Simu ina exposure nzuri inayoonyesha picha kwa undani na bila kupoteza ubora wa vitu vilivyopo.
Contrast ya kamera inabalansi rangi kwa vipimo vinavyohitajika kwenye nyakati za usiku na mchana.
Tazama picha uliyopigwa na gsmarena kwa kutumia kamera ya xioami mi 11 ultra.
Kamera inatoa picha yenye texture kubwa.
Kwa kitu ambacho kipo na kamera na kamera bado inaweza kuonyesha picha ya hiko kitu pale moja ya sehemu ya vitu vilivyoonekana kwenye picha ikikuzwa.
Tazama picha ya chini.
Vitu vinavyoonekana kwenye picha upande wa kulia kinatambulika kwa urahisi na kiwango cha NOISE ni kidogo sana.
Utendaji wa kamera ya xiomi mi 11 ultra nyakati za usiku ni wa kuridhisha sana.
Vitu vilivyopo kwenye mazingira ambayo picha imepigwa vinaonekana kwa uzuri na kwa kutambulika.
Rangi ya taa inayowakaa na rangi ya giza la usiku hutokea kama ambavyo vionekanavyo kwenye mazingira halisi.
Contrast ya kamera inatofautisha rangi kwa ustadi.
Exposure ya kamera ina ukusanyi wa mwanga unaoweza kuonesha vitu vingi kuonekana kwenye picha
Picha iliyopigwa kutumia xiaomi mi 11 ultra nyakati za usiku na gsmarena.
Simu ina kiwango kidogo cha noise.
Ukiikuza picha kutazama vitu kiundani kuna ukungu wa kiwango kidogo.
Kiwango ambacho hakiwezi kuzuia mtazamaji kutambua vitu vilivyopo pichani.
Simu nyinginezo.
Zipo simu zenye kamera nzuri zinazolingana na huawei p50 pro, xiaomi mi 11 ultra, iphone 13 pro max, vivo x70 pro+, Google pixel 6 pro nk.
Simu zenye kamera nzuri zingine ni iphone 12 pro max, huawei mate 40 pro, oppo find x3 pro.
Chukua muda wako kuzipitia kwenye tovuti xdomark wenyewe wanazitest kamera ya simu kwenye engo nyingi.
Maoni 2 kuhusu “Simu zenye camera nzuri 2022”
We mbn Kila simu una kosoa2
Kwa sababu simu zinazidiana, kitu kimoja kinaweza kupatikana huku na huku mwingine kikawa hakipo na ndio maana kila toleo linakuwa na maboresho.