Hii ni orodha ya simu kumi za Realme za bei rahisi kwa mwaka 2022
Kwenye orodha utazifahamu realme za daraja la chini na la kati
Kuna simu za realme zilizotoka mwaka 2020, 2021 na realme mpya za mwaka 2022
Ubora wa kila realme iliyopo na bei zake zitakuongoza kupata chaguo zuri linaloendana na unachokihitaji
Baadhi ya simu za Realme za bei rahisi
Simu ya Realme C31
Simu mpya ya realme c31 imetoka mwishoni mwa mwezi machi mwaka 2022.
Ni simu yenye kioo cha aina ya ips lcd kilicho na resolution ndogo ya 720×1600 pixels
Utendaji wa simu ni mzuri kwani inatumia processor ya daraja la kati aina ya Unisoc Tiger T612
Simu inaweza kukaa na chaji masaa yanayozidi 14(data ikiwa on) kwa sababu ya kuwa na betri kubwa la 5000mAh
Ina mfumo wa memori wenye kasi aina ya UFS 2.1 unaongeza nguvu ya utendaji wa simu
Simu ina bodi imara na kioo kigumu kuchunika sababu imewekewa kioo aina ya panda
Ni realme ya macho matatu yenye kamera zenye ubora mdogo sana
Bei ya realme c31
Bei halisi ya realme c31 ya ukubwa wa GB 32 ni shilingi 305,000/=
Na bei ya realme c31 ya ukubwa wa GB 64 ni shilingi 335,325.19/=
Bei ya simu inavumulika ila upatikanaji wake nchini Tanzania ni mdogo
Hivyo ni vizuri ukainunua simu aliexpress kama ikiwezekana
Simu ya Realme Narzo 50i
Simu ya realme narzo 50i ni simu ya bei nafuu ya android ya mwaka 2021
Simu ina utendaji mdogo kutokana na aina ya processor inayotumia
Ina kamera moja tu ambayo resolution yake sio kubwa
Uwezo wa kukaa na chaji muda mrefu ni mkubwa kwani betri lake ni la 5000mAh
Ina bands chache za mtandao wa 4G
Kioo cha realme narzo 50i ni cha aina ya ips lcd na kina resolution ndogo vilevile
Kiujumla ni simu inayomfaa mtumiaji anayeanza kutumia simu janja
Bei ya realme narzo 50i
Bei halisi ya realme narzo 50i ni shilingi 228,630.81/=
Hii ni kwa narzo 50i ya ukubwa GB 32
Kama utanunua Tanzania bei inaweza kuzidi 250,000/=
Realme C21Y
Simu ya realme c21y ni simu ya mwaka 2021 yenye toleo la android 11
Simu ina utendaji wa wastani kutokana na kutumia processor ya daraja la kati aina ya Unisoc T610
Kamera zake tatu ni za kuridhisha japokuwa ni kamera moja tu yenye teknolojia ya ulengaji wa PDAF
Simu inakuja na betri kubwa ya ujazo wa 5000mAh
Kioo cha realme c21 ni cha aina ya IPS LCD chenye resolution ndogo ya 720 x 1600 pixels
Ila hii simu imeundwa kwa plastiki upande wa nyuma na kwenye frem
Bei ya Realme C21Y
Bei ya Realme C21Y yenye ukubwa wa GB 32 ni shilingi 327,881.09/=
Bei inaendana na ubora wa simu na sifa zake.
Ukibahatika kuipata Tanzania bei yake inaweza kuwa zaidi ya hiyo
Simu ya Realme C11
Realme C11 ni simu ya mwaka 2020 yenye toleo la android 10
Utendaji wa simu si mkubwa kutokana na kutumia memori aina ya eMMC na chip ya MediaTek Helio G35
Kioo cha realme c11 kinatumia teknolojia ya ips lcd ambacho huwa na rangi chache.
Lakini pia kioo kina resolution ndogo ya 720×1560 pixels
Linapokuja swala chaji, simu ina uwezo wa kukaa na betri muda mwingi (betri la 5000mAh)
Simu ina kamera mbili tu ambazo zina ubora wa chini katika upigaji picha
Bei ya Realme C11
Bei ya realme c11 ambayo ina ukubwa GB 32 ni shilingi 226,134.94/=
Realme C11 ina matoleo mawili yanayotofautiana ukubwa wa ram
Hivyo bei zake zitakuwa hazitofautiani sana
Simu ya Realme 9 5G
Simu mpya ya realme 9 5g ni simu ya macho manne inayotumia toleo la android 11.
Ni simu ambayo imeingia sokoni mwezi machi 2022
Simu inakubali 4G ya mitandao yote Tanzania kwa sababu ina network bands za 4G zipatazo 12
Processor yake aina ya dimensity 810 inaifanya simu kuwa na uwezo mkubwa wa kufungua app yoyote
Realme 9 5G ni simu inayokubali mtandao wa 5G
Kioo cha Realme 9 5g kina resolution kubwa ya 1080×2400 na ni cha ips lcd chenye refresh rate ya 90Hz
Ina betri kubwa la 5000mAh
Hivyo simu inakaa na chaji muda mrefu wakati huo utendaji ni mkubwa
Bei ya Realme 9 5G
Bei halisi ya Realme 9 5G yenye ukubwa wa GB 64 na RAM ya GB 4 ni shilingi 487,745.73/=
Toleo la GB 128 bei yake inazidi laki tano na nusu.
Elewa kuwa hii ni simu ya daraja la kati ndio maana bei yake ipo juu kidogo
Simu ya Realme narzo 50
Simu ya realme narzo 50 ni simu ya 4G mpya ambayo imetoka mwezi machi 2022
Realme narzo 50 ina kioo chepesi wakati wa kuperuzi kwani kimewekewa refresh rate inayofika 120Hz
Kioo cha narzo 50 ni cha aina ya ips lcd kilichoboreshwa kwa kuwekewa resolution ya 1080×2412 pixels
Simu inaweza kusukuma kila aina ya app kwa sababu inatumia processor yenye nguvu aina ya MediaTek Helio G96
Betri yake ina ukubwa wa 5000mAh na hivyo inaweza kukaa na chaji masaa mengi
Na kizuri simu inawahi kujaa kwa haraka, ina fast chaji inayopeleka umeme kwa kasi inayofikia wati 33
Ni simu ya android 11 inazungukwa na kamera tatu upande wa nyuma
Ila ubora wa kamera sio mkubwa na inaweza kurekodi video za aina ya full hd pekee.
Bei ya Realme narzo 50
Bei ya realme narzo 50 toleo la gb 64 na ram ya GB 4 ni shilingi 396,293.41/=
Na realme ya ukubwa wa GB 128 na RAM ya GB 6 bei yake stahiki haizidi 487,745.73/=
Ila kwa bei za realme Tanzania inazidi laki tano
Simu ya Realme C35
Realme C35 ni simu ya macho matatu yenye android 11 ambayo imetoka mwaka 2022 (Ni simu mpya)
Utendaji wa simu unaweza kufungua app nyingi kwa wepesi kwa sababu ya kutumia processor ya uwezo wa kati ya Unisoc Tiger T616
Ina kamera tatu, kamera kuu ni nzuri zaidi kwa sababu ina PDAF.
Ila PDAF haifikii kiubora teknolojia ya ulengaji ya dual pixel pdaf.
Betri yake ni kubwa (5000mAh) ila chaji yake haipeleki umeme mwingi sana (18W)
Kioo cha realme c35 ni cha ips lcd chenye uangavu mdogo wa 480nits
Ila koo kina resolution nzuri ya 1080 x 2408
Bei ya Realme C35
Bei ya realme c35 ya ukubwa wa GB 64 na RAM GB 4 ni shilingi 466,257.60/=
Kwa ukubwa zaidi ya huo bei yake inaweza kuzidi laki tano
Simu ya Realme C25Y
Simu ya realme c25y ni simu ambayo imetoka mnamo mwaka 2021.
Ina utendaji wa wastani kwa sababu ina processor ya Unisoc T610 na memori za eMMC 5.1
Ina kioo cha ips lcd kilicho na resolution ndogo ya 720 x 1600 pixels
Simu imeundwa kwa plastiki hivyo si simu imara sana
Ina kamera tatu na kamera kubwa ina resolution ya 50MP
Lakini ubora wake si mkubwa kwa sababu hakuna dual pixel pdaf na OIS
Pia kamera zake hazirekodi video kubwa za 4k
Simu ina betri kubwa la 5000mAh na betri inayochaji kwa spidi inayofikia wati 18
Bei ya Realme C25Y
Bei ya halisi ya realme c25y ni shilingi 335,325.19/=
Hii ni bei ya realme c25y ya gb 64 yenye ram 4G
Lakini ushishangae bei kupanda zaidi ya laki tatu na nusu kwa maduka ya simu dar es salaam
Simu ya Realme C25
Simu ya realme c25 ni simu ya android 11 ya mwaka 2021
Ni simu yenye betri kubwa sana la ujazo wa 6000mAh
Hivyo inaweza kukaa na chaji masaa mengi
Hilo pia linachangiwa na utendaji wa wastani unaochangiwa na processor ya daraja la kati ya Helio G70
Ina 4G yenye bands chache ila inakubali mitandao mingi ya simu nchini
Kioo cha realme c25 ni cha IPS LCD ambacho kina resolution ndogo 720 x 1600 pixels
Betri yake inapeleka umeme wa wastani unaofikia wati 18
Ubora wa kamera ni wa kawaida kwani kamera zake zinarekodi video za full hd pekee na kwa spidi ndogo ya 30fps
Bei ya Realme C25
Bei ya realme c25 yenye ukubwa wa GB 64 ni shilingi 353,102.71/=
Bei inaweza kuongezeka kama hautonunua simu mtandaoni
Kwani maduka ya simu mengi ya Tanzania wanaiuza simu kwa bei ya juu kidogo
Simu ya Realme Narzo 50A
Simu ya realme narzo ni simu ya mwaka 2021 yenye android 11.
Betri ya narzo 50a ina ukubwa wa 6000mAh.
Tegemea simu kukaa na chaji muda mrefu.
Utendaji wake ni wa wastani na wa kuridhisha, inatumia chip ya MediaTek Helio G85
Kioo cha realme narzo 50a ni cha aina ya IPS LCD chenye resolution ndogo ya 720×1600
Ni realme ya macho matatu ambayo haina mfumo mzuri sana wa kamera.
Kwa sababu kamera kubwa inatumia PDAF ambayo inazidiwa na dual pixel pdaf
Na pia kamera zake zinarekodi video za ubora wa full hd pekee yake kwa spidi ya 30fps
Bei ya realme Narzo 50A
Bei ya narzo 50a ya ukubwa wa GB 64 ni shilingi 365,809.30/=
Hizi ni bei za India.
Hivyo kwa Tanzania bei yake inaweza kuzidi 400,000/=
Maoni 3 kuhusu “Simu za Realme za bei rahisi 2022 (na ubora wake)”
Kwanini msitafte mawakala kila mkoa ili kurahisisha upatikanaji wake kwa urahisi
Bei yake kioo
Bei zake za vioo sifahamu, sijui unaulizia toleo lipi