Hii ni orodha inayohusisha simu kumi za Motorola ambazo zimetoka kati ya mwaka 2021 na 2022
Motorola ambazo zimetokea kwenye list bei zake zinaanzia laki tatu kwenda mbele
Nyingi ya simu janja za motorola zilizopo ni za daraja la kati
Hivyo bei haitafanana na simu nyingi za bei rahisi unazozifahamu na hata kisifa
Tuziangazie kila motorola iliyopo kiundani na bei yake madukani
Motorola Moto G62 5G
Simu ya Motorola Moto G62 5G ni simu ambayo imeingia sokoni mwezi juni mwaka 2022
Ni simu ambayo inakubali mtandao wa 5G ya masafa ya kati
Utendaji wake ni wa wastani kwa sababu inatumia processor ya Snapdragon 480+ 5G
Kioo cha moto G62 5G sio cha amoled bali ni cha IPS LCD ambacho kina resolution 1080 x 2400 pixels
Simu inakuja na mfumo endeshi mpya wa Android 12 ambao umeboresha ufanisi kwenye usalama
Ukaaji wa chaji unaweza kudumu kwa masaa zaidi ya 15 simu ikiwa inatumia intaneti
Hii inatokana na betri lake kuwa na ukubwa wa 5000mAh
Upande wa kamera simu pia ina jitahidi japo kwa kiwango cha kawaida
Kwa sababu kamera zake tatu zote haziwezi kurekodi video za 4K na hazina dual pixel pdaf
Bei ya Motorola Moto G62 5G
Hii simu imezinduliwa hivi karibuni nchini Brazil
Na bado haijasambaa katika masoko ya nchi zingine duniani
Hivyo bei yake haijainishwa kwa sasa
Motorola Moto G82
Simu janja ya motorola moto G82 ni simu ya 5G ambayo inatumia mfumo endeshi wa Android 12
Ni simu yenye nguvu kubwa ya utendaji
Hilo linasababishwa na simu kutumia chip ya Snapdragon 695 5G
Snapdragon 695 5G inaweza kufanya kila kazi ya simu inayohitaji kiufasaha ikiwemo kucheza magemu yanayohitaji nguvu kubwa
Kioo chake kinaonyesha vitu kiustadi kwa sababu ni kioo cha amoled na resolution ya 1080 x 2400 pixels
Kioo hiki kina refresh rate ya 120 inayoifanya simu kuwa nyepesi
Moto G82 ina kamera tatu ambapo kamera kuu ina OIS na PDAF kwa ajili ya ulengaji sahihi
OIS husaidia kamera kutulia wakati wa kurekodi video huku ukiwa unatembea
Bei ya Motorola Moto G82
Bei ya Motorola Moto G82 yenye ukubwa wa GB 128 ni 1,208,551.01/=
Hii ni bei ya duka la mtandaoni la Amazon
Kiujumla bei ni kubwa sana ukilinganisha na simu nyingine zinazotumia Snapdragon 695 5G
Motorola Edge 30
Simu ya Motorola Edge 30 ni simu ambayo imetoka mwanzoni mwa mwezi wa tano mwaka 2022
Ni simu mpya ya motorola inayotumia Android 12
Edge 30 ina utendaji wenye nguvu kwa sababu mfumo wake wa memori ni wa aina ya UFS
Na pia inatumia processor ambayo ina nguvu ya kufungua app za kila aina
Chip hiyo ni Snapdragon 778G+ 5G
Hii processor inaifanya simu kuwa na network ya 5G
Ukaaji wa chaji si mkubwa sana kwani betri yake ina ukubwa wa 4020mAh
Simu ina kioo chenye ufanisi mkubwa kutokana na kuwa na refresh rate inayofika 144Hz
Na pia kioo chake cha amoled kina rangi nyini na resolution kubwa
Bei ya Motorola Edge 30
Bei ya Motorola Edge yenye ukubwa wa GB 128 na RAM GB 8 ni shilingi 1,727,171.94/=
Bei inaedana na ubora wa simu kiasi fulani hasa ukitazama mfumo mzima wa kamera
Kwani kamera zake zinatumia teknolojia nzuri ya ulengaji ya Omnidirection PDAF
Ambayo iko shap kutambua kinachopigwa picha
Motorola Edge 30 Pro
Motorola Edge 30 Pro ni moja ya simu bora ya Android yenye uwezo mkubwa kwenye kila nyanja
Simu hii ina utendaji wenye nguvu kutokana na kutumia processor ya Snapdragon 8 gen 1
Kitu kinachofanya simu kuweza kufungua kila aina ya app kiurahisi bila kukwama
Inatumia kioo cha OLED chenye uwezo wa kuonyesha rangi bilioni moja
Vitu vingi vitaonekana kwa rangi zake halisi
Mfumo wake wa kamera unaweza kutoa picha nzuri nyakati za usiku na mchana
Hiyo inachangiwa na kamera zake kuwa na Omnidirection PDAF na OIS
Simu inatumia betri kubwa inayokaa na chaji masaa mengi
Kwani betri yake ina ukubwa wa 4800mAh
Hii ni moja ya simu inayojaa chaji kwa haraka kwani chaji inapeleka umeme wa wati 68
Bei ya Motorola Edge 30 Pro
Kwa kutazama sifa chache za Edge 30 Pro unaweza ukajua bei yake itakuwaje
Bei ya Motorola Edge 30 Pro ya ukubwa wa GB 512 na RAM ya GB 8 ni shilingi 2,346,701.00 za Tanzania
Hii ni simu ambayo ipo kundi moja na Samsung Galaxy S22 na iPhone 13 Pro Max
Motorola Moto G52
Motorola Moto G52 ni simu ya 4G ambayo imetoka mwaka 2022 mwezi Aprili
Utendaji wa simu ni wa wastani
Kwani simu inatumia processor ya daraja la kati aina ya Snapdragon 680 4G
Kioo chake ni chepesi kuperuzi kwani kina resolution ya 90Hz na ni cha Amoled
Simu ina kamera ambazo zinaweza kurekodi video za ubora wa full hd pekee
Na kamera zote hazijawekewa OIS
Kasi ya upelekaji chaji ni mkubwa
Kwani chaji inapeleka umeme wa wati 30 hivyo betri lake la 5000mAh linaweza kujaa ndani ya dakika 80
Bei ya Motorola G52
Hii ni android ya daraja la kati huvyo bei yake sio kubwa kama Motorola Edge 30 Pro
Kwani bei ya Motorola G52 ni shilingi 732,170.71
Hii ni bri G52 ya GB 128 na RAM ya GB 4
Motorola Moto E32s
Hii ni simu nyingine ya 4G ambayo imetoka mwaka 2022 mnamo mwezi juni
Motorola Moto E32S inakuja na android toleo la 12
Ni simu ya daraja la chini ambayo utendaji wake si mkubwa
Hii inatokana na Moto E32s kutumia chip ya Mediatek Helio G37
Nguvu ya Mediatek Helio G37 huwa ni ndogo hasa kama unatumia app nyingi sana kwa wakati moja
Kutumika kwa Helio G37 kunaifanya simu kuwa na kioo ambacho kina resolution ndogo ya 720 x 1600 pixels
Na pia processor inailazimisha simu kutumia kioo cha IPS LCD
Na hata kamera zake tatu si za kuvutia sana hivyo utoaji wa picha utakuwa wa kawaida
Ila kitu kizuri hii simu lazima ikae na chaji muda mrefu
Kwa sababu betri yake ina ukubwa wa 5000mAh
Bei ya Motorola Moto E32S
Bei ya Motorola Moto E32S ya ukubwa wa GB 64 inaanzia shilingi 370,309.42
Bei ndogo inatokana na ubora wa chini wa simu husika
Motorola Edge 20 Pro
Motorola Edge 20 Pro ni simu ya mwaka 2021 hivyo ina Android 11
Ni simu kali mpaka wakati huu na inachuana na simu za android nyingi mpya
Kwani utendaji wake ni wa kiwango cha juu kutokana na kutumia processor ya Snapdragon 870 5G
Kutokana na kuwa na chip yenye nguvu inafanya simu kuwa na kioo chenye resolution kubwa ya 1080 x 2400 pixels
Na pia inaipa uwezo kioo chake kuonyesha rangi nyingi
Ndio maana kioo chake cha OLED kinaweza kuonyesha rangi zipatazo bilioni moja
Simu ni ngumu kuvunjika kwani kina kioo cha gorilla 5
Tazama hapa majaribio ya kuvunja simu yenye kioo cha Gorilla 5
Upande wa betri na chaji simu ipo vizuri kwa kiasi kikubwa
Chaji yake inajaza betri mapema mno
Ikizingatiwa betri yake ina ukubwa wa wastani wa 4500mAh
Bei ya Motorola Edge 20 Pro
Simu yoyote ikitumia processor yenye uwezo mkubwa bei lazima iwe kubwa pia
Hivyo bei ya Motorola Edge 20 Pro ni shilingi za Tanzania 1,173,350.50
Motorola Edge 20
Motorola Edge 20 ni moja ya simu bora ya daraja la kati ambayo ilitoka 2021
Ubora wake unachagizwa na kutumika kwa processor ya Snapdragon 778G 5G
Kitu kinachoipa simu uwezo wa kutumia mtandao wa 5G
Na pia chip inaifanya kioo cha simu kuwa na resolution kubwa 1080 x 2400 pixels
Ila kioo chake si imara sana kwa sababu kina Gorilla 3 ambacho huwa ni kigumu kuchunika
Ina kioo cha OLED na betri kubwa ya 4500mAh
Kamera zake zinaweza piga picha kitu cha mbali kwa sababu kuna kamera aina ya Telephoto
Bei ya Motorola Edge 20
Bei ya Motorola Edge 20 ya GB 128 ni shilingi 1,173,350.50
Bei inaendana kwa kiasi kikubwa na ubora wa simu yenyewe
Motorola Moto G Power
Motorola Moto G Power ni motorola ya daraja la kati ya mwaka 2020
Utendaji wake si mkubwa sana kwa sababu inatumia chip ya Snapdragon 665
Hivyo vitu vingi vya hii simu pia vitakuwa na utendaji wa kawaida
Kwa mfano, kioo cha simu kinatumia IPS LCD chenye resolution ya 1080 x 2300 pixels
Na hata kamera ubora wake ni wa kawaida japo simu inaweza kurekodi mpaka video za 4k
Ila ukaaji wa chaji ni mkubwa
Kwa sababu betri ya Moto G Power ina ukubwa wa 5000mAh
Bei ya Motorola Moto G Power
Bei ya Motorola Moto G Power inaanzia shilingi 450,459.93
Motorola Moto G Power 2022
Motorola Moto G Power 2022 ni simu ya daraja la chini ambayo imetoka mwishoni mwa 2021
Inafanana vitu vingi Motorola Moto E32S
Kwani simu zote imetumia chip ya MediaTek Helio G37
Kutokan na simu kuwa na uwezo mdogo inafanya simu kuwa na bei ndogo pia
Kwani motorola nyingi zina bei kubwa
Bei ya Motorola Moto G Power 2022
Bei ya motorola moto g power 2022 ya ukubwa wa GB 64 ni shilingi 300,000
Ni moja ya motorola ya bei nafuu
Maoni 4 kuhusu “Simu 10 Nzuri za Motorola na Bei Zake (2022)”
Mm nimenunua Motorola but mpKa sasa sjapata cover Wala protector
Naomba kusaidiwa japo kujua sehemu gani nitapata hizo plz
Kiushahuri nunua kupitia AliExpress
Naomba nifahamishe sehemu ambayo naweza kupata protector and cover ya simu coz until now kila nnapoenda sibahati naambiwa hakuna kabisa plz naomba msaaada
Ok ngoja nifuatilie