Kama unahitaji kumiliki Vivo ya bei rahisi kwa mwaka 2022 Vivo Y21 inaweza ikawa chagua zuri.
Ila linapokuja ubora wa simu, utendaji wake ni wa chini kwa kuzingatia memori na chip
Simu ya Vivo Y21 ina memori kubwa hata hivyo.
Baadhi ya sifa zake zinakidhi pakubwa mahitaji ya mtumiaji wa simu
Pitia taarifa zote zilizopo kwenye post hii uifahamu vizuri simu.
Bei ya vivo Y21 Taznania
Bei ya vivo y21 inatofautiana kulingana na ukubwa wa memori na ram
Vivo y21 ya gb 64 inauzwa shilingi 410,000/= mpaka 450,000/=
Ni bei ya maduka ya simu kariakoo mitaa ya agrey
Na vivo y21 ya gb 128 bei yake inafika 490,000/=
Bei inaonekana ni kubwa kwa Tanzania ukilinganisha bei ya simu nchini India
Kwani India bei ya juu kabisa ni shilingi 426,884/=
Kiuhalisia sifa za vivo y21 zinaifanya bei yake kuwa kubwa kuliko ubora wa simu yenyewe
Sifa za Vivo Y21
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | IPS LCD, |
Softawre |
|
Memori | eMMC 5.1, 128GB,64GB na RAM 4GB |
Kamera | Kamera mbili (macho mawili)
|
Muundo | Urefu-6.51inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 450,000/= |
Upi ubora wa Simu ya Vivo Y21
Simu ina betri kubwa inayoweza kukaa na chaji kwa masaa mengi ya kutosha
Memori yake inaweza kuhifadhi mafaili mengi
Mfumo wake wa gps una aina nne za gps
Simu ina sehemu ya memori kadi na pia ina redio
Katika nyanja zingine ubora umegwanyika kama utavyoona.
Ni vizuri ukaielewa simu ya Y21 kwa kuzingatia mahitaji yako
Uwezo wa Network
Simu hii ya Vivo inauwezo wa kukubali mtandao wa 4G
Aina ya 4G yake ni LTE Cat 7
4G ya LTE cat 7 inaweza kudownlod faili kwa spidi ya juu inayofikia 300Mbps
Endapo mtandao wa simu unakupa spidi hii, basi vivo y21 itadownload faili la 13ooMB kwa sekunde 39
Si laini zote za simu Tanzania zinakubali intaneti ya kasi(4G) kwenye hii simu.
Kwa sababu ina bands za 4G saba pekee
Ubora wa kioo cha Vivo Y21
Kioo cha vivo y21 ni aina ya IPS LCD.
Kiubora, kioo cha ips lcd kinaundwa na rangi chache.
Kitu kinachofanya baadhi ya vitu kuonekana kwa rangi zisizo halisi hasa rangi nyeusi
Resolution yake ina ukubwa wa kawaida(standard)
Kwani ina pixels 720×1600, vitu vitaonekana kwa ubora mzuri
Nguvu ya processor ya Helio P35
Processor ya Helio P35 ina core nane
Katika core nane kuna core nne zenye spidi kubwa na core nne zenye spidi ndogo
Spidi kubwa inafikia 2.35GHz, na ndogo inafikia 1.8GHz
Core zote zina muundo wa Cortex A53
Kiuhalisia muundo wa cortex a53 ni kwa ajili ya kufanya kazi ndogndogo
Kwa hiyo vivo y21 ni simu yenye utendaji wa chini sana kwenye kurekodi video za resolution kubwa.
Na hata kucheza magemu ya simu yenye graphics nyingi(tegemea simu kupata moto)
Uwezo wa betri na chaji
Chaji ya vivo y21 inaweza kupeleka umeme kwa kasi inayofikia wati 18
Hii ni kasi ya wastani.
Kwa umeme huo betri yake inaweza kujaa kwa masaa yanayofikia matatu.
Kwa sababu betri yake ina ukubwa wa 5000mAh
Hivyo ukilinganisha nguvu ya chaji na ukubwa wa betri, itachukua dakika nyingi sana simu kujaa chaji
Ukubwa na aina ya memori
Vivo y21 ina memori aina eMMC 5.1
Kabla ya mwaka 2015, memori za eMMC 5.1 ndio memori zilizokuwa na kasi zaidi.
Lakini baada ya ujio wa aina mpya ya UFS, zimeifanya eMMC kupitwa na wakati
Kuna aina mbili za Y21 upande wa memori
Ipo vivo y21 ya 64GB, RAM 4GB na 128GB, 4GB RAM
Uimara wa bodi ya Vivo Y21
Bodi ya vivo y21 imetengenezwa kwa plastiki.
Bodi za plastiki huwa ni nyepesi kupasuka iwapo simu ikianguaka kwa kimo cha mita mbili.
Na ni bodi zenye changamoto ya rangi kuchunik kadri muda unavyokwenda
Kuongeza ulinzi mtumiaji atalazimika kuweka kava na screen protectot.
Simu ni ndevu na nyepesi kubeba
Kwani uzito wake unafikia gramu 182
Ubora wa kamera
Kuna kamera mbili tu kwenye simu ya vivo y21
Kamera kuu ina sensa ya megapixel 13
Wakati kamera ya macro ina 5MP
Kamera aina ya macro hutumika kupiga picha au video ya kitu cha karibu sana na kamera.
Kwa mfano ukitaka kumpiga picha sisimizi na aonekane kwa ukubwa basi kamera ya macro ndio inafaa zaidi
Na kamera yake kubwa ina ya teknolojia ya ulengaji ya PDAF ambayo si nzuri sana kama multdirection pdaf
Ubora wa Video
Kamera ya hii simu inaweza kurekodi video zenye ubora wa aina moja pekee
Kama unarekodi video utapata video zenye ubora wa full hd(1080) kwa spidi ya 30fps
Hivyo usitarajie kupata video za 4k na 8k kwa spidi ya 60fps
Sababu kubwa ya kushindwa kurekodi video za 4k ni nguvu ndogo ya processor ya simu
Ubora wa Software
Vivo y21 ni simu ya android 11 yenye software ya vivo Funtouch 11.1
Mfumo wa android 11 una applikesheni ya kurekodi screen ya simu,
Ukiwa nayo utapunguza gharama ya bando la kudownload applikesheni za kurekodi screen.
Wakati functouch 11.1 inaiwezesha simu kuongeza ukubwa wa memori ya ram.
Funtouch ina muundo wa kuvutia wa multi tasking(kutumia app nyingi kwa wakati mmoja)
Kwani inazipangilia apps kwa muundo wa row(grids)
Inatengeneza urahisi wa kuhama kutoka app moja mpaka nyingine
Yapi Madhaifu ya Vivo Y21
Kwa kutazama bei yake na sifa zake, simu inakosa vitu vingi sana ambavyo vipo kwenye simu nyingi za laki nne mpaka laki tano.
Kwanza, uwezo wa processor ni wa chini na utendaji wake una nguvu ndogo.
Kioo chake kina resolution ndogo kwani simu ya bei hii hutumia resolution za Full HD Plus(1080×2600)
Chaji yake inapleka umeme kidogo wakati simu ya redmi note 10 inapeleka umeme wa 33W
Bodi ya simu ni ya plastiki na simu haina viwango vya IP53(kuzuia vumbi)
Kamera zake hazirekodi video zenye resolution kubwa zaidi
Kioo chake kina refresh rate ya kawaida na hakina teknolojia ya HDR10
Neno la Mwisho
Bei halisi ya vivo y21 ilipaswa iwe chini ya 300,000 au isizidi 350,000 kama samsung a03s
Kama utapata chini ya hapo utakuwa umeipata kwa bei stahiki
Lakini kuuzwa juu ya laki nne inaifanya kuwa simu ya gharama sana kuliko ubora
Hiyo ni bei ya simu ya redmi note 10 ambayo ina utendaji mkubwa kuliko y21
Lakini sio mbaya kujaribu kitu tofautii(uzuri wa Functouch)
Maoni 3 kuhusu “Bei ya Simu ya Vivo Y21 na Sifa Zake (2022)”
Sim n nzur sana kiukwel ila je kama kioo cha kamera kimechafuka camera inaonekana kama Haina ubora je unaweza kubadilisha kioo cha camera mfano mm cm yang camera ya nyuma ikipiga picha unakua na ukungu sana je naweza kubadisha kioo cha camera ya nyuma ya mbele ipo saw.
Naweza kubadili kioo cha camera ya nyuma maana nikioiga picha inatoka yenye ukungu nahic n kioo cha camera kimechafuka je uweza wa kubadili upo?
Sina hakika