Simu aina ya redmi note 8 pro ni simu ambayo imetoka mwaka 2019.
Ni simu ya 4G inayoweza kupokea toleo la Android 11 la mwaka 2021
Toleo android 11 linaifanya simu kuendana na nyakati za sasa
Ikizngatiwa sifa zake nyingi zinapatikana pia kwenye matoleo mapya ya simu za android
Bei ya redmi note 8 pro inapatikana chini ya laki tano kutegemeana na tolea lake
Bei ya Redmi Note 8 Pro Tanzania
Bei ya redmi note 8 pro ya GB 64 na RaM GB 8 inauzwa shilingi 390,000/=
Na redmi ya 128GB yenye ram 6GB inauzwa shilingi 425,000/=
Na toleo la mwisho la 128GB lenye ram ya GB 8 bei yake ni shilingi 450,000/=
Hizi ni bei za aliexpress bei za maduka ya Tanzania ni kubwa.
Sifa zake ziatupa uhalisia wa bei.
Sifa za Redmi note 8 pro
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | IPS LCD, |
Softawre |
|
Memori | UFS 2.1,128GB,64GB,256GB na RAM 8GB,6GB ,4GB |
Kamera | Kamera nne
|
Muundo | Urefu-6.53inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 450,000/= |
Upi ubora wa Simu ya Redmi note 8 pro?
Ubora wa redmi note 8 pro ni kamera yake yenye uwezo wa kurekodi kwa spidi kubwa
Simu ina bodi imara na ngumu kuvunjika
Inakubali kupokea tolea lingine la android
Bei yake ni rafiki na inavumulika kwa wenye bajeti ndogo
Utendaji wake ni wastani unaoweza kufungua applikesheni za aina nyingi
Japokuwa uwezo wake wa network umegawanyika
Uwezo wa Network
Network ya redmi note 8 pro ni ya 4G.
Simu ina masafa machache ya mtandao wenye kasi ya 4G
Aina ya 4G inaweza kudownload spidi inayofikia 600Mbps kama kuna mtandao mzuri
Hii inachangiwa na LTE ya Cat 12
LTE yake inaweza kutumika kwenye mitandao yote ya simu nchini Tanzania
Ubora wa kioo cha Redmi note 8 pro
Kioo cha simu ya redmi note 8 pro ni aina ya ips lcd.
Vioo vya ips lcd vina rangi chache sababu ya contrast ndogo
Kitu kinachofaa bei ya kioo chake kuwa rahisi lakini ubora wa kuonyesha picha si mkubwa kama vioo vya amoled
Ila ubora wa kioo umeboreshwa na resolution kubwa ya pixels 1080 x 2340
Hivyo screen itaonyesha vitu kwa rangi zilizokorea kiasi
Nguvu ya processor Helio G90T
Processor aina ya helio G90T ina core nane.
Core kubwa zinaipa simu uwezo wa kucheza gemu ya Call of Duty: MobileĀ kwa ubora wa 4K
Chip inapata alama za wastani kwenye app zinapima nguvu ya processor na gpu
Kwa mfano app ya antuntu inaipa alama 492 kwenye core moja.
Jua kuwa utendaji mzuri wa simu hupata alama angalau 500
Utendaji wa wastani unatokana na uwezo wa core kubwa kwenye spidi
Uwezo wa core kubwa
Core kubwa zipo mbili ambazo zinatumia muundo wa Cortex A76
Huu ni muundo umetumika kwenye processor aina ya Helio G95
Ila helio g95 ina nguvu zaidi, isipokuwa helio g90t ina spidi ya 2.05GHz
Uwezo wa core ndogo
Simu ina core ndogo sita zinazotumia muundo wa Cortex A55
Cortex A55 inaisadia simu kula chaji kidogo
Ni moja ya muundo unaofanya kazi ndogo kwa matumizi madogo ya betri
Uwezo wa betri na chaji
Ukubwa wa betri ya redmi note 8 pro ni 4500mAh
Uwezo wa betri kukaa na chaji ni masaa 114 ikiwa inatumika mara chache.
Na uimara wa ukaaji wa chaji ni masaa 15 simu ikiwa intaneti muda wote
Ila betri yake inapeleka umeme wa wastani wa wati 18.
Ni kiasi cha umeme kitakochojaza simu kwa masaa mengi yanayoweza fika matatu
Ukubwa na aina ya memori
Kuna matoleo matano ya hii simu kwenye ukubwa wa memori.
Ukubwa wa memori unaanzia GB 64 mpaka GB 256
Na ram zinaanzia GB 4 mpaka GB 8
Memori yake ina kasi kubwa ya kusafirisha data
Kasi kubwa hufanya simu kuwaka kwa haraka na app kufunguka kwa sekunde chache
Hii inasababishwa na aina ya memori ya UFS 2.1 kutumika.
Spidi ya kuandika na kusoma UFS 2.1 inafika 1200MBps
Uimara wa bodi ya Redmi note 8 pro
Upande wa nyuma simu ina kioo cha Gorilla Glass 5
Na pia Gorilla Glass 5 inalinda kioo cha redmi note 8 pro
Kuna majaribio yaliyofanywa na kampuni ya gorilla
Katika majaribio hayo, simu yenye kioo hiki haikuvunjika ilipondosha mara nyingi kwa kimo cha mita 1.2
Haihitaji screen protecto wala kava
Ubora wa kamera
Redmi note 8 pro ni simu ya macho manne
Kamera moja kubwa ya 48MP inatumia autofocus ya PDAF kwenye ulengaji.
Dual pixel pdaf ina ulengaji wa ufanisi mkubwa kuliko PDAF
Kamera zake zinarekodi video za ubora wa aina tatu.
Kwani inarekodi video za full hd kwa spidi ya 30fps mpaka 120fps
Pia inaweza kurekodi video za 4K(Ultra HD) kwa spidi ya 30fps
Na video za HD kwa spidi inayofika 960fps
Na kitu kizuri simu inaweza kuondoa mitikisiko(yaani stabilization) wakati wa kurekodi video
Sababu kamera zinatumia Gyro-EIS
Ubora wa Software
Ukiimiliki simu kwa sasa utakuta Android 9 yenye MIUI 12.5
Lakini simu inakubali kupokea android 11.
Toleo la android 11 limeboreshwa applikesheni zake na mifumo yake.
Kwa mfano, utohaji wa ruhusa za app zinachukua data za simu ni tofauti na Android 9
Pia mfumo endeshi wa android 11 umewekewa app ya kurekodi screen.
Hivyo simu inakupunguzia muda wa kutafuta app ya namna hiyo
Yapi Madhaifu ya Redmi Note 8 Pro
Simu inatumia vioo vyenye uwezo mdogo wa kuonyesha rangi nyingi za kutosha
Kioo chake hakina hdr10 au hdr10+
Inatumia refresh rate ya kawaida hivyo kioo sio chepesi
4G yake ina masafa machache inayofanya baadhi ya mitandao duniani kutokubali 4G
Simu haina uwezo wa kuzuia maji kupenya kwani inakosa viwango vya IP67
Utendaji wa processor unapata shida ya kucheza baadhi ya gemu zenye graphics kubwa kwa ubora wa UHD
Hitimisho
Bei ya redmi note 8 pro inaifanya simu kuwa ya bei nafuu yenye ubora mkubwa
Ila kuna matoleo mapya ya simu yenye uwezo mkubwa kuliko note 8 pro
Mshindani wa simu hii ni redmi 10 na hata samsung galaxy a33