Tangu mwishoni mwa mwaka 2023 mpaka mwaka huu 2024 Vivo imeachia matoleo mengi ya simu
Katika matoleo hayo yapo ya bei ndogo, bei ya kati na bei kubwa
Kwa maana inalenga watumiaji wa simu wenye hali zote za kiuchumi
Hivyo basi hapa tunakuletea simu mpya za vivo na bei zake ambazo zimetoka kati ya desemba 2023 na mwaka 2024
Kuna simu zipatazo 15 kwenye orodha na nyingi ni nzuri kwa kiasi kikubwa
1. Vivo V30 Pro
Bei ya Vivo V30 Pro: 1,300,000/= ,Ukubwa wa Memori: 256GB, RAM: 8GB
Simu ya Vivo V30 Pro ni simu iliyotoka februari 2024
Inatumia processor yenye nguvu ya wastani, chip hiyo ni Mediatek dimensity 8200
Kioo chake cha amoled kina utajiri wa rangi na kina HDR10+
Hii ni moja ya simu yenye kamera inayopiga nzuri kwenye kamera zote tatu
Betri yake ina ukubwa wa 5000mAh na kasi yake ya chaji ni wati 80
2. Vivo Y100t
Bei ya Vivo Y100t: 600,000/= ,Ukubwa wa Memori: 256GB, RAM: 8GB
Simu ya Vivo Y100t iliingia rasmi februari 2024 kama ilivyo kwa Vivo V30 Pro
Inatumia chip ya dimensity 8200
Bei yake ni ndogo ukilinganisha na Vivo Y100t inatokana na aina ya kioo chake na hata kamera
Kwani ina kamera mbili lakini kamera moja ndio nzuri zaidi
Na pia kioo chake sio cha Amoled bali ni IPS LCD ila hakina HDR10+
3. Vivo IQOO Neo9 Pro
Bei ya Vivo IQOO Neo9 Pro: 1,300,000/= ,Ukubwa wa Memori: 256GB, RAM: 8GB
Hii ni simu ambayo na yenyewe imetoka mwezi februari 2024
Inatumia chip yenye nguvu kubwa kiutendaji ya Snapdragon 8 Gen 2
Kioo chake ni cha aina ya LTPO AMOLED na refresh rate yake ni kubwa inayofika 144Hz
Chaji yake inapeleka umeme wa kujaza betri ndani ya dakika 20 kutokana na kuwa na kasi ya wati 120
Ila ina kamera mbili tu huku kamera kubwa ikiwa na uwezo wa kurekodi video za 4K
4. Vivo Y200e
Bei ya Vivo Y200e: 630,000/= ,Ukubwa wa Memori: 128GB, RAM: 6GB
Simu ya Vivo Y200e iliingia sokoni mwaka 2024 mwezi wa februari
Ina utendaji wa juu wa kuridhisha japo sio mkubwa sana kama IQOO Neo9 Pro
Hii inatokana na kutumia processor ya Snapdragon 4 Gen 2
Ina jumla ya kamera mbili tu huku kamera kubwa ikiwa na megapixel 50
Chaji yake inapeleka umeme wa wati 44
5. Vivo V30
Bei ya Vivo V30: 1,100,000/= ,Ukubwa wa Memori: 256GB, RAM: 8GB
Kamera za Vivo V30 zipo tatu ambazo ni ultrawide, wide na ya tatu haijaainishwa
Utendaji wake ni wa kuridhisha kwa sababu inatumia chip ya Snapdragon 7 Gen 3
Betri yake ina ukubwa wa 5000mAh wakati huo chaji yake inapeleka umeme wa wati 80 unaoweza jaza simu kwa 100% ndani ya dakika 40
Kioo chake ni cha amoled na kina HDR10+
6. Vivo Y100(IDN)
Bei ya Vivo Y100(IDN): 630,000/= ,Ukubwa wa Memori: 128GB, RAM: 8GB
Hii ni simu ambayo ilitoka mwezi januari mwaka 2024
Ni simu yenye sifa nzuri katika nyanja za utendaji, kioo na hata chaji na betri
Kioo chake kina HDR10+ na pia ni cha aina ya AMOLED
Chajji yake ina wati 80 inayojaza betri kwa dakika 45 pekee
Betri yake ina ukubwa wa 5000mAh hivyo inakaa na moto muda mrefu
7. Vivo Y28
Bei ya Vivo Y28: 450,000/= ,Ukubwa wa Memori: 128GB, RAM: 4GB
Hii ni simu ya daraja la kati iliyotoka mwezi januari 2024
Utendaji wake ni wa wastani kutokana na kutumia chip ya mediatek dimensity 6020
Ubora wa kioo chake sio mkubwa kwa sababu resolution yake ni 720 x 1612 pixels
Kamera zake zipo mbili na zinarekodi video za full hd pekee na sio 4K
Betri yake ni kubwa ila kasi ya chaji yake ni wati 15 hivyo inachukua muda kujaa
8. Vivo G2
Bei ya Vivo G2: 450,000/= ,Ukubwa wa Memori: 128GB, RAM: 4GB
Vivo G2 ni simu nyingine ya mwaka 2024 ambayo imetoka januari
Hii simu ina utendaji wa wastani na kuna baadhi ya sifa zina ubora wa chini
Kwa mfano kioo chake ni cha IPS LCD ambacho resolution yake ni ndogo
Kamera yake inaweza kurekodi video za full hd kwa kiwango cha 30fps
Na yenyewe ina betri kubwa ila chaji haina kasi kubwa kwani inapeleka umeme wa wati 15
9. Vivo V30 Lite
Bei ya Vivo V30 Lite: 1,400,000/= ,Ukubwa wa Memori: 256GB, RAM: 8GB
Simu ya Vivo V30 Lite ni simu ya mwaka 2023 iliyotoka desemba
Kwa maana hivyo bado ni simu mpya kwa mwaka 2024
Utendaji wake ni wa kiwango cha kati hii kwa sababu inatumia processor ya Snapdragon 695 5G
Chaji yake inapeleka umeme wa wati 44 hivyo betri lake la wati 4800mAh inajaa kwa haraka
Hii simu ina kamera tatu yaani macho matatu na moja ya kamera ina OIS kwa utulivu wakati wa kurekodi video ukiwa unatembea
10. Vivo IQOO Neo9
Bei ya Vivo IQOO Neo9: 1,200,000/= ,Ukubwa wa Memori: 256GB, RAM: 8GB
Simu ya Vivo IQOO Neo9 ni simu ya vivo iliyotoka desemba 2023
Utendaji wake ni mkubwa kwani inatumia chip yenye nguvu ya Snapdragon 8 Gen 2
Ina jumla ya kamera mbili huku kubwa ikiwa na megapixel 50 na OIS
Chaji yake ya wati 120 inajaza simu kwa 40% ndani ya dakika 9
Na betri lake lina ukubwa wa 5160mAh
11. Vivo S18 Pro
Bei ya Vivo S18 Pro: 1,200,000/= ,Ukubwa wa Memori: 256GB, RAM: 8GB
Vivo S18 Pro ni simu nyingine kali ya vivo ya mwaka 2023 ila ilitoka mwezi desemba
Inatumia processor yenye nguvu ya Mediatek Dimensity 9200+
Kioo chake ni cha AMOLED na kina refresh rate ya 120Hz
Kamera zake tatu na zinaweza kurekodi video za 4K
Chaji yake inapeleka umeme mpaka wa wati 80 na betri yake ina 5000mAh
12. Vivo S18
Bei ya Vivo S18: 850,000/= ,Ukubwa wa Memori: 256GB, RAM: 8GB
Kwenye desemba 22 mwaka 2024 ndio mwaka ambao simu ya Vivo S18 iliingia rasmi sokoni
Nguvu ya kiutendaji ni ya kuridhisha japo sio kama simu ya Vivo S18 kwa sababu yenyewe inatumia chip ya Snapdragon 7 Gen 3
Pia kioo chake ni kizuri kwani cha Amoled
Ina kamera mbili tu na kamera kubwa ina megapixel 50
Chaji yake inapeleka umeme mwingi wa wati 80 na betri yake ina 5000mAh
13. Vivo S18e
Bei ya Vivo S18e: 780,000/= ,Ukubwa wa Memori: 256GB, RAM: 8GB
Simu ya Vivo S18e ni simu ya daraja la kati ambayo ilitambulishwa mwezi desemba na kuanza kupatikana rasmi januari 2024
Inatumia chip ya Mediatek Dimensity 7200 ambayo nguvu yake ni ya wastani
Betri yake ina ukubwa wa 4800mAh na chaji ni wati 80
Ina kamera mbili tu huku kamera kubwa ina megapixel 50
Kioo chake ni cha amoled chenye refresh rate ya 120Hz
14. Vivo Y36i
Bei ya Vivo Y36i: 450,000/= ,Ukubwa wa Memori: 128GB, RAM: 4GB
Hii ni simu ya daraja la kati ambayo ilianza kupatikana mwezi januari 2024 ila ilitangazwa mwezi desemba 2023
Inatumia processor ya Mediatek dimensity 6020
Ina kamera moja tu yenye megapixel 13 na ulengaji wa PDAF
Hii kamera inaweza kurekodi video za full hd yaani 1080
Ukubwa wa betri ni 5000mAh na chaji ina kasi ya wati 15
Maoni 3 kuhusu “Simu 14 mpya za Vivo za ubora mkubwa na bei zake (2024)”
Kwann mikoa ya kusini,hizi simu hazipatikani?…
Vivo ziko pow ila maboresho kwenye kamera na makava na speak zake zipatikane kiulahis mwanza
Vivo S18 NIPO KAGERA MULEBA