SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

Simu Mpya za Google Pixel 2024 na bei zake

Simu Mpya

Sihaba Mikole

September 1, 2024

Kuna matoleo yapatayo manne ya simu mpya za google ambayo yametoka mwaka 2024

Matoleo yote yanatofoautiana kwa kiasi fulani kwenye muundo na baadhi ya vitu kama utakavyoona

Hivyo, bei zake pia zinatofatiana na pixel yenye bei ndogo inaanzia milioni mbili na nusu

Yap, bei ni ghari ila kama ni mfutuliaji na mtumiaji sana wa simu utakuwa unaelewa ubora wa simu za google

Simu zenyewe ni hizi.

  1. Google Pixel 9
  2. Google Pixel 9 Pro
  3. Google 9 Pro XL
  4. Google Pixel 9 Pro Fold

Tuiangalie moja baada ya nyingine

Google Pixel 9

Bei ya Google Pixel 9: 2,500,000/= ,Ukubwa wa Memori: 128GB, RAM:  12GB

Hii ni google pixel yenye urefu mdogo wa inchi 6.3

Utendaji wake ni mzuri kwani ina chip ya Tensor G4

Ina jumla ya kamera mbili zinazoweza kurekodi video za 4K

pixel 9

Kioo chake(skrini) ni cha oled chenye refresh rate ya 120Hz na teknolojia ya hdr10+

Betri yake ni kubwa ya 4700mAh na inadumu kwa masaa kama 11 ukiwa kwenye intaneti muda wote

Google Pixel 9 Pro

Bei ya Google Pixel 9 Pro: 3,200,000/= ,Ukubwa wa Memori: 128GB, RAM:  16GB

Google Pixel 9 Pro na yenyewe urefu wake ni inchi 6.3

Inasapoti chaji ya wati 27 hivyo betri yake ya mAh 4700 inajaa kwa muda mfupi

pixel 9 pro

Ina kioo cha ltpo oled ambacho kina faida ya kudhibiti refresh rate kulingana na aina ya matumizi

Hii simu ina kamera tatu ambapo kamera mbili zina megapixel 48, na nyingine ina megapixel 50

Inapewa nguvu na processor ya Google Tensor G4

Google Pixel 9 Pro XL

Bei ya Google Pixel 9 Pro XL: 3,700,000/= ,Ukubwa wa Memori: 256GB, RAM:  16GB

Hii ndio simu ndefu zaidi ina inchi zipatazo 6.8

Na kamera zake zipo tatu, moja ina megapxel 50 zingine zina megapixel 48

pixel 9 pro xl

Inarekodi hadi video za 8K, ambazo zinakuwa na uangavu mkubwa na mzuri

Betri yake ni kubwa ya mAh 5050

Inakaa na chaji takribani masaa 12 ukiwa unatumia intaneti muda wote

Google Pixel 9 Pro Fold

Bei ya Google Pixel 9: 8,000,000/= ,Ukubwa wa Memori: 256GB, RAM:  16GB

Ukiangalia bei utaona kuwa hii ndio pixel yenye bei kubwa sana kuliko kawaida

Hii ni bei ambayo unanunua kiwanja na kuanza ujenzi taratibu

Maana yake hii ni simu inayolenga watu wenye wenye kipato kikubwa zaidi

pixel 9 pro fold

Katika utendaji utendaji na kamera simu ina ufanano tu wa sehemu na simu zilizotangulia

Tena pixel 9 pro na XL zina kamera kubwa zaidi

Utofauti wa bei unasababishwa na muundo wa simu kuwa wa kujikunja wenye kioo kipana

Tena kioo chenyewe ni cha LTPO OLED ambayo vina ubora mkubwa na gharama kubwa pia

Maoni 11 kuhusu “Simu Mpya za Google Pixel 2024 na bei zake

Maoni na Maswali

Email yako haitochapishwa, kwenye alama * lazima pajazwe ili ukomenti

Fuatilia Zaidi

Hizi ndizo simu zenye uwezo mkubwa wa betri kupitiliza

Kuna teknolojia mpya ya betri imezipa betri za simu uwezo mkubwa sana Kwa sababu ya hii teknolojia simu zinakaa mpaka SIKU NNE bila kuchaji Na si siku nne ukiwa unaitumia […]

Bei ya Google Pixel 11 Pro na Sifa Zake

Google Pixel 11 Pro imewasili Lakini kuna jambo moja litakalokufanya ufikilie kununua hii simu. Jambo hilo ni bei yake. Bei ya Google Pixel 11 Pro ni shilingi milioni 3 kwa […]

Simu za Google Pixel sahihi za kununua (2026)

Hapa Tanzania Google Pixel imeshika kwa sasa Ni simu zilizovuta wengi na kununua kama vipofu Matokeo yake wengine wameibuka kununua Google Pixel ambazo hazifai kwa sasa Baadhi za Google zina […]

-google pixel 10 pro

Simu mpya za Google Pixel 10 na bei zake (ubora na sifa)

Mbabe wa kamera upande wa simu ametoa matoleo mapya Si mwingine bali ni Google Pixel 10 Google Pixel 10 unaweza kuiona kuwa haina tofauti na Pixel 9 Lakini haipo hivyo […]

SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani
TUFUATE
Youtube Facebook Instagram twitter

E-mail : simunzuriblog@gmail.com

Simu: 0756 077262 au 0683 420543

Whatsapp: +255 756 077 262

Kabila, Magu

Mwanza, Tanzania

Company