Mwaka 2022 Oppo imetoa toleo jipya la simu ya kundi la kati.
Simu hiyo ni OPPO A96
Simu mpya ya oppo a96 ina uwezo wa kuzuia vumbi kupenya ndani ya simu
Kitu kinachosaidia simu kudumu muda mrefu
Sifa za simu ya oppo a96 zinashawishi ila kwa wengine zinaweza zisiwavutie.
Hasa ukifuatalia kioo, network na kamera bila kusahau bei yake.
Sifa za Oppo A96 kiufupi
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | IPS LCD, Refresh rate:90Hz |
Softawre |
|
Memori | UFS 2.2, 128GB,256GB na RAM 8GB |
Kamera | Kamera MBILI
|
Muundo | Urefu-6.59inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 766,854.97/= |
Upi ubora wa Simu ya Oppo A96
Ubora mkubwa wa simu ya Oppo A96 ni display(kioo) nzuri kwa ajili ya kucheza gemu.
Simu ina uwezo mkubwa kuchaji betri kwa haraka na utunzaji wa moto wa muda mrefu
Oppo A96 ina viwango vya IP vinaonyesha uwezo wa simu kuzuia maji na vumbi.
Hii ni simu yenye mfumo wa chaji unaoweza chaji kifaa kingine.
Mfumo huo hujulikana kama reverse charging.
Network
Oppo A96 inakubali mtandao wa 4G.
Simu ina network bands 11 pekee kati ya 24
Network bands ambazo zipo kwenye hii simu ni 1, 3, 5, 7, 8, 20, 28, 34, 38, 40 na 41
4g ya oppo a96 inakubali mitandao yote hapa Tanzania.
4G ya hii simu ya oppo ni ya kundi la 13 yaani Cat 13.
Kasi ya juu kabisa ya kudownload ni 390Mbps.
Haina tofauti na simu ya infinix note 11 pro
Ubora wa kioo cha oppo A96
Kioo cha Oppo A96 ni aina ya IPS LCD.
Ni kioo chenye refresh rate ya 90Hz.
Refresh rate kuanzia 90Hz kwenda mbele hufanya simu kuwa nyepesi unapo-scroll au kucheza gemu.
Kioo kina uangavu wa 600nits unaowezesha kioo kuonyesha vitu vizuri ukiwa unatumia simu juani.
Pamoja na uangavu simu ina resolution inayofanya video na picha vionekane kwa ustadi.
Ustadi huo unasababishwa na resolution kubwa ya 1080 x 2412 pixels
Nguvu ya processor Snapdragon 680 4g
Oppo A96 inatumia processor ya Snapdragon 680 4G.
Snapdragon 680 4g ni chip ya kundi la kati yenye core nane.
Ukubwa wa Transistor za hii processor ni 6nm(nanometer)
Nanometer ndogo inamaanisha processor ina transistor nyingi.
Transistor nyingi zinaongeza nguvu ya processor.
Jifunze zaidi kuhusu: nanometer na transistor
Uwezo wa core zenye nguvu sana
Snapdragon 680 ina core nne zenye nguvu sana.
Kila core ina spidi ya 2.4GHz
Core zote zinatumia muundo wa Kryo 265 Gold
Kryo 265 Gold ni jina linalowakilisha core za Cortex A73
Kwa sasa Cortex A73 ina utendaji wa kiwango cha chini ukilinganisha Cortex A76 iliyomo kwenye simu zinazotumia MediaTek Helio A96.
Kwenye Antuntu Snapdragon 680 ina alama 83258
Wakati Helio A96 ina alama 96288
Kiujumla processor ya simu ya oppo a96 haina nguvu kubwa sana.
Uwezo wa core zenye nguvu ndogo
Core zenye nguvu ndogo ni maalumu kwa kufungua apps zisizohitaji nguvu kubwa.
Ubora wa aina hii ya core ni kwenye matumizi madogo ya umeme
Simu ina core 4 zenye nguvu ndogo zenye spidi ya 1.9GHz
Core zote zinatumia muundo wa Kryo 265 Silva ambao ni Cortex A53
Cortex A53 ina nguvu ndogo sana na matumizi yake umeme ni makubwa ukilinganisha na Cortex A55
Cortex A55 imetumika kwenye Helio A96
Uwezakano ni kuwa simu zinazotumia Helio A96 zikawa na nguvu kubwa na matumizi madogo ya betri.
Uwezo wa betri na chaji
Betri ya Oppo A96 ina ukubwa 5000mAh aina ya Li-Po.
Betri ni kubwa inayoifanya simu kukaa na chaji muda mrefu.
Mfumo wa chaji unapeleka umeme wa wati 33.
Kwa mujibu wa Oppo betri inajaa kwa 50% ndani ya dakika 26 tu na inajaa ndani ya dakika 63
Kitu kingine ni simu kuwa na uwezo wa kuchaji simu nyingine.
Simu nyingi zenye betri za 5000mAh hutunza chaji kwa masaa 14 simu ikiwa inatumia intaneti.
Uwezekano wa ukaaji wa chaji muda mrefu unaweza patikana kwenye oppo a96
Ukubwa na aina ya memori
Memori ya oppo a96 ni aina ya UFS 2.2
UFS 2.2 husafirisha data kwa kasi ya 1200MBps.
Kasi inayofanya simu kuwaka na kufungua applikeshi kwa haraka.
Na ukiwa unakopi faili la ukubwa 1200MB simu inaweza maliza kukopi ndani ya sekunde.
Oppo A96 zipo za aina mbili
- Oppo ya 128GB na 8GB RAM
- Oppo ya 256GB na 8GB RAM
Ukubwa wa memori unachangia bei ya simu kuwa kubwa
Ram za hii simu ni aina ya LPDDR4X
LPDDR4X hutumia umeme mdogo kusafirisha data kwa kasi kubwa
Uimara wa bodi ya oppo a96
Bodi ya oppo a96 ni imara na ni ngumu.
Japokuwa imeundwa kwa plastiki lakini inaweza kuzuia vumbi na maji
Kwenye ulinzi wa kioo imetumika glassi ya kawaida.
Haijahainishwa kama ni vioo vya gorilla.
Simu ni nyembamba na uzito wa gramu 191
Urefu na upana wa simu unafiti kwa kiasi kikubwa kwenye mkono.
Simu inakubali laini mbili ndogo
Ubora wa kamera
Kamera za Oppo A96 zipo mbili tu.
Kamera hizo ni kamera kuu(wide) yenye 50MP
Na depth sensor kamera 2MP
Kamera ya Depth hutumika kupima umbali wa kitu kinachopigwa picha
Ni kamera inayosaidia ulengaji mzuri na sio kupiga picha
Kamera za hii simu zinakosa OIS na dual pixel pdaf.
Hivyo ubora wa picha unaweza ukawa wa kawaida nyakati za usiku
Ubora wa video
Kama ilivyotangualiwa kusema, kamera ya oppo a96 si ya kuvutia.
Kamera zake zinaweza kurekodi aina moja ya video kwa spidi ndogo.
Oppo a96 inweza kurekodi video za ubora wa full hd pekee kwa spidi ya 30fps.
Video za Full HD zinaonyesha maudhui vizuri
Lakini kwa ulimwengu wa leo kuna television za 4K.
Video za 4K huwa na ubora mkubwa zaidi.
Ubora wa Software
Pamoja na simu kuzinduliwa mwaka 2022 oppo imekuja na Android 11.
Simu mpya za mwaka 2022 zinakuja na toleo jipya la Android 12
Japokuwa kuna maboresho ya kiusalama kwenye toleo jipya la android, Android 11 ndroid bado ina vitu vizuri vingi.
Oppo A96 pia inawezeshwa na software ya Color 11.1
Color 11 inakuwezesha kuhariri rington za simu na kuzibadilisha kuwa audio za mp3
Pia mfumo wa color 11 una dark mode(rangi nyeusi).
Na color 11 inaweza kujiongeza mwanga kwenye jua kali.
Na kujipunguza mwanga nyakati za usiku au kwenye mwanga mdogo.
Bei ya oppo a96 Tanzania
Bei ya oppo a96 inafika shilingi 770,000/=
Baadhi ya maduka ya kariakoo bei ya oppo a96 ya 256GB ni 750,000/=
Wakati maduka mengine simu inauzwa kwa 850,000/=
Kiujumla bei ya oppo a96 ni kubwa.
Kwa kuzingatia bei, simu ina madhaifu mengi kama utakavyoona
Kwa bei hii unapata Redmi note 10 pro, Samsung Galaxy 52 na Infinix Note 11 Pro na chenji ikabaki
Yapi Madhaifu ya oppo a96
Oppo A96 haitumii vioo vya Gorilla 6 ambavyo ni vigumu kupasuka
Bodi ya simu imeundwa kwa plastiki hivyo simu itahitaji kava
Simu ina bands chache za network ya 4g na haina 5g
Oppo hawajaweka vioo vya amoled vinavyoonyesha vitu kwa rangi halisi kwa kiasi kiukubwa.
Simu inatumia android 11 badala ya android 12
Processor yake ina nguvu ndogo ukilinganisha na simu zinazouzwa 700,000 na kuendelea
Oppo A96 haina kamera ya ultrawide, Macro na Telephoto
Neno la Mwisho
Kwa mtumiaji wa kawaida atafurahi akiwa na simu mpya ya oppo a96
Utendaji wake ni wa kuridhisha.
Lakini sio mbaya kuulizia simu zingine zinazoendana bei na oppo a96
Wazo moja kuhusu “Sifa za Simu mpya ya OPPO A96 (Ubora na Udhaifu)”
Nitakua je kama CM yangu ya oppo kama original nitaitambuaje