GPS kirefu chake ni Global Positioning System, ni mfumo wa utambuzi wa maeneo ambao unasimamiwa na Marekani
Simujanja karibu zote zina huu mfumo
Una faida kubwa sana hasa kama unajua jinsi ya kutumia gps kwenye simu yako
Inaweza kukulinda na upotevu ama kufuatilia mahala ambapo kifaa chako kipo kama umekipoteza
Pitia: Maana ya GPS na jinsi inavyofanya kazi
Matumizi ya GPS yanahitaji kuwa na app aidha ya ramani au ya kupima umbali, eneo na hata spidi
Hapa utaabarishwa hatua zote muhimu ili uweze tumia gps
Kuwasha GPS
GPS inatakiwa iwe ON ili uweze kuitumia
Kama ikizimwa hakuna app yoyote itakoyeweza pata taarifa za eneo husika
Jinsi ya kuwasha gps ni rahisi
Kwenye simu hutambulika kama “Location”
Swipe(kutachi) kioo chako cha simu kutokea juu ili ije sehemu yenye machaguo ya kuwasha data, wifi, tochi, bluetooth na mengineyo
Katika hayo machaguo kuna chaguo mojawapo limeandikwa “Location” alama yake ni kamshare kuria upande wa juu
Kama umeweza kuiona itachi sehemu husika na hapo utakuwa umeiwasha
Kujua namna ya kuitumia inategemeana na malengo yako kwa sababu ina matumizi mengi
Na kwa maana utalazimika kutumia apps mbalimbali zinazoweza kufanya kazi unayoitaka kwa kutumia GPS
Hivyo tutafafanua jinsi ya kutumia huu mfumo kwa kuangalia baadhi ya matumizi
GPS Kwenye Ramani(eneo ulilopo)
Baada ya kuwasha fungua applikesheni ya ramani kwenye simu za android huitwa Maps
Simu zote zina applikesheni ya google maps
Ukiifungua kitu cha kwanza ramani itakuonyesha eneo ambalo hupo wakati huo
Hata ukiwa unatembea app inaendelea kuonyesha ulipo yaani inabadilika kutokana na unavyohama kutoka sehemu moja kwenda nyingine
Google Maps inaweza kukuonyesha majengo yote ambayo upo jirani nayo wakati huo
Na pia kama kuna vituo vya afya na mashule basi app itakuonyesha hizo taasisi
Kama huijui njia applikesheni itakuelekeza
Kutambua spidi ya chombo chako cha usafiri
Pia unaweza kuitumia gps kama kifaa cha kusoma spidi ya chombo chako cha usafiri
Na unaweza kuitumia kufahamu spidi yako ya kutembea, kukimbia na hata kasi ya baiskeli
Hii itakulazimu kutumia applikesheni za speedometer zinazopatikana play store
Nenda playstore kisha tafuta applikesheni imeandikwa GPS Speedometer ina nembo(PICHA) ya 84MPH
Ukishaingia kwenye simu ifungue na uipe ruhusa ya kutumia gps
Baada ya kuifungua utaona kitufe kimeandikwa Start Trip
Gusa hiko kitufe baada ya hapo utaona spidi ya chombo ambacho unasafiri nacho
Kujua umbali uliotembea na wa eneo unaloenda
GPS ya simu ina uwezo wa kukujulisha umetembea umbali kiasi gani
Na pia inaweza kukuonyesha umbali kutoka eneo ulilopo mpaka unapoenda
Applikesheni nzuri ya kujua umbali uliotembea ni hiyo hiyo ya GPS Speedometer
Kwa sababu inaonyesha umbali pamoja na spidi kwa wakati mmoja
Kadri utakavyokuwa unatembea app inaandika kilomita ambazo umetumia
Hii inaweza kukusaidia kujua urefu unaotembea ama matumizi ya mafuta ya gari unayotumia kutokana na huo urefu
Kama unasafiri kwenda kwenye mkoa mwingine google Maps inaweza kukujulisha muda uliobaki kufika eneo unaloenda kutokana na spidi yako au ya gari ama chombo chochote
Ili uweze kufanikisha hili yafuatayo unapaswa uyafanye.
- Fungua applikesheni ya Google Maps (Maps)
- Upande wa chini kulia kuna alama ya bluu yenye mshale kuelekea kulia, bonyeza hapo
- Itakuja sehemu ya kuweka eneo ulilopo na unaloenda, app itatumia gps ya eneo ulilopo(haina haja ya kujaza)
- Jaza eneo ambalo unaloenda
- Chagua aina ya usafiri (Gari, treni au kwa mguu) hata ukiacha haina shida
- Utaona muda na kilomita za eneo husika
- Chini yake bonyeza “Start”
Baada ya hapo Google Map itakuwa inakuelekeza uelekeo wa kufuata kama binadamu tena kwa sauti ila ya kiingereza
Na itakwambia hilo eneo ukifika
Kutrack simu
GPS inaweza kutumika kuifuatilia simu mara nyingi kukiwa kuna app
Google map inaweza kutumika kujua eneo ambalo mtu anaweza kutumia
Kutokana na maswala ya haki za faragha, hatotuchimba kiundani kwa kuonyesha aina za app zinazotumika kufanya hiyo kazi
Ila kwenye app ya map unaweza kushea eneo ambapo simu ipo muda wote
Unaweza kufuatilia zaidi kwenye tovuti ya google wameelezea kiundani
Hitimisho
Namna ya kutumia gps ni rahisi na inategemea unaitaka kuitumia gps ikusaidie kitu gani
Unapowasha gps itakulazimu utumie app mbalimbali zinazojishughulisha na kitu
Mara nyingi gps inatumika pamoja na applikesheni za ramani kama Google Maps
Maoni 17 kuhusu “Jinsi ya Kutumia GPS kwenye Simu (Hatua kwa Hatua)”
Mungu awape mwanga zaidi
Shukrani
Naomba kufungiwa GPS kwenye power tiller nipo Bahi
Hatuna hiyo huduma kiongozi
Mimi nataka kujua jinsi ya kupima shamba, kujua ukubwa na kuchora ramani
Nine download app ya gps ,nikifungua inaniandikia username ,nikaandika ,password nayo nmeandika lkn inaandika incorrect, nisaidien nifanikishe kujiunga
Jina la app inaitwaje maana kuna app za gps nyingi.
Nahitaji kujua baada ya kufunga gps ktika pikipiki yangu, na tayari nimeweka cm card kwenye gps, Sasa nafanya aje kujua kuitrack
Kuna gps unazitrack kwa kutumia app yao na nyingine kwa kutumia website, kila gps tracker huwa inakuja na maelekezo. Ungetaja brand ya hiyo gps ingekuwa raisi zaidi kueleza kinachofuata
Nahitaj mamba yako mkuu tufanye kazi
namba zote zipo chini kabisa ya peji hii
Mpo vzr wakubwa ila sijaelewa namn yakuitrack sim kam imepotea
Naomba kujua namna ya kutumia GPS kupima eneo mf shamba,kiwanja kwa kutumia simu
Nahitaji nielekezwe namna ya kutumia GPS kulima shamba,kiwanja,Kwa kutumia simu.
Nataka juju’s hapo ya kutafuta simu au no inasomeka wapi na unatumiaje
Sijaelewa ulichoandika
Nataka kujua eneo nililo jenga lina ukubwa gani