Hii ni orodha ya simu 10 za iphone zenye bei inayoanzia laki mbili mpaka milioni moja na nusu.
Utaona simu za apple iphone za bei rahisi za ambazo zimetoka kuanzia mwaka 2015 mpaka 2022
Pia utafahamu sifa na ubora wa kila iphone iliyopo kwa ufupi.
Itasaidia kuelewa kama simu inafaa kwa wakati uliopo ama la.
Asilimia kubwa ya simu hizi ni used ama zilirudishwa kiwandani na kurekebishwa(refurbished)
iPhone XR
Simu ya apple iPhone XR imetoka mwaka 2018
Ni simu ya 4G yenye kamera moja nzuri inayoweza kuchukua mpaka video za 4k kwa spidi inayofika 60fps
iPhone xr ni simu ambayo haipitshi maji hata ukiizamisha kwenye kina cha mita moja kwa muda wa nusu saaa
Simu ina bodi ngumu yenye vioo vya gorilla glass upande wa nyuma na mbele.
Simu nyingi mpya za android zinazidiwa na iPhone xr kiutendaji.
Sababu kubwa processor yake aina ya Apple A12 Bionic ina nguvu sana.
Kwani ina alama zinazozidi 1000 kwenye geekbench
Simu inaweza kupokea mfumo endeshi mpya wa iOS 15.4.1 bila shida
Bei ya iPhone XR Tanzania
Bei ya iPhone XR yenye ukubwa wa 64GB inafika shilingi 545,670/=
Ni bei ya masoko ya mtandaoni ebay
Ila kwa Tanzania bei yake inaweza ikazidi hapo
Unaweza kuagiza kwa ebay na simu ikakufikia kiurahisi
Bei ya chini ya laki sita inastahili kwa sababu bado simu ina ubora mwingi unaoizidi simu ya Tecno Camon X
iPhone 11
Simu ya iphone 11 ni iphone ambayo ilitoka mwishoni mwa 2019
iPhone 11 haipitishi maji simu ikidumbukia kwenye kina cha mita mbili kwa muda wa nusus saa
Ina bodi ngumu kupasuka kwani inatumia kioo cha gorilla glass
Ina mtandao wa 4G aina ya LTE cat 18 wenye kasi inayofika 1200Mbps
Kioo cha iPhone 11 ni cha ips lcd na resolution yake ni 828 x 1792 pixels
Kiuwezo, simu inazizidi simu za android za daraja kati zote na nyingine za daraja la juu za 2020-2022
Kwa sababu processor yake ya apple a13 bionic nguvu yake ni kubwa
Bei ya iPhone 11 Tanzania
Bei ya iPhone 11 ya GB 64 ni shilingi 847,530.00/= kwa soko la ebay.
Kwa Tanzania hasa maduka ya simu makumbusho bei inaweza kuzidi 900,000/=
Ni bei inayoendana na simu mpya ya Samsung Galaxy A53 5G
Lakini Samsung Galaxy A53 5G inazidiwa na apple iphone 11
iPhone SE 2020
Simu ya iPhone SE 2020 ni simu ndogo ya iphone ya mwaka 2020.
Simu ina utendaji unaoendana na iphone 11.
Ila kuna vitu vimepungua kwenye se 2020
Ila utendaji wake ni mkubwa kuliko redmi note 11 pro plus 5g
Kwa sababu inatumia processor ya apple a13 bionic.
Ni simu ambayo haipitishi maji ikizama kwa kina cha mita moja moja kwa muda wa nusu.
Betri yake ni ndogo na ukaaji wa chaji si mkubwa
Bei ya iphone se 2020
Bei ya iPhone se 2020 ya gb 64 ni shilingi 464,400.00/= kwa masoko ya ebay.
Kwa Tanzania kwenye maduka ya kariakoo bei yake inavuka 600,000/=
iPhone 8
iPhone SE ni simu ya iphone iliyotoka mwaka 2017
Simu inaweza kupokea toleo jipya la iOS 15.4.1 toka toleo la iOS 11
Ni simu nyingine yenye uwezo wa kuzuia maji kupenya.
Betri yake ina ukubwa wa 1821mAh
Na linakaa chaji masaa machache yapatayo 66 kama simu haitumikii mara kwa mara
Kioo chake kina resolution ndogo ya 750 x 1334 pixels
Na bodi yake ni ngumu.
Uwezo wake wa processor unaizidi mbali sana simu ya redmi note 10 na Samsung Galaxy A52S.
Bei ya iPhone 8 Tanzania
Bei ya iphone 8 yenye ukubwa wa 64GB inafika shilingi 397,062.00/= kwa masoko ya ebay
Kwa maduka mengi ya simu ya kariakoo simu haizidi 500,000/=
Na maduka mengine kinondoni bey yake inazidi 600,000/=
iPhone 8 Plus
Simu ya iPhone 8 Plus ni simu ya mwaka 2017 yenye iOS 11
Simu inaweza kupokea mfumo mpya endeshi wa iOS 15.4.1
Processor yake ya apple a11 bionic ina nguvu na inazizidi simu nyingi mpya za android
Betri ya iPhone 8 Plus ni dogo linalokaa masaa machache na chaji
Ukiwa unapiga simu masaa mengi simu itaisha chaji baada ya masaa 21
Kioo cha iphone 8 plus ni cha aina ips lcd chenye resolution 1080 x 1920 pixels
Simu ni fupi upande wa kimo
Bei ya iphone 8 plus Tanzania
Bei ya iPhone 8 plus yenye ukubwa wa 64GB inafika shilingi 464,400.00/= ebay
Ila kwa wauza simu wa maduka ya kariakoo bei kubwa zaidi ya 530,000/=
iPhone XS
Simu ya iPhone XS ni simu ndogo yenye kimo cha inchi 5.8
Simu imetoka mwaka 2018
Inatumia processor yenye nguvu aina ya Apple A12 Bionic.
A12 Bionic inaizidi processor ya snapdragon 695 na dimesnity 1200
Hizi ni processor zilizotumiwa na simu nyingi za androiza daraja kati za mwaka 2020-2022
Betri yake ni dogo na linakaa na chaji masaa machache vilevile
Simu ina iOS 12 na inaweza kupokea toleo la iOS 15.4.1
Kioo cha iPhone xs ni cha oled chenye resolution kubwa ya 1125 x 2436 pixels.
Ni simu ambayo haipitishi maji
Bei ya iPhone XS Tanzania
Bei ya iPhone XS ya ukubwa wa GB 64 inafika shilingi 534,060.00/= ebay
Baadhi ya maduka ya kinondoni bei yake inazidi 600,000/= ila haivuki shilingi 700,000/=
iPhone X
Simu ya iPhone X ni simu yenye kimo cha inchi 5.8 ya mwaka 2017
Simu ina kioo cha OLED chenye resolution kubwa ya 1125 x 2436 pixels
Kioo kina ubora wa kuonyesha vizuri kwa sababu kina hdr10 na dolby vision
Inatumia processor yenye utendaji mkubwa
Processor yake ya Apple A11 Bioni inazipita simu nyingi mpya za android za madaraja ya kati
Betri lake ni dogo na halikai na chaji muda mrefu
iPhone X inaweza kupokea toleo jipya la iOS 15.4.1
Kamera yake si nzuri kwani haina dual pixel pdaf na hairekodi video ya 4K
Bei ya iPhone X Tanzania
Bei ya iPhone x ya ukubwa wa gb 64 inafika shilingi 487,620.00/=
Lakini kwa maduka ya simu dar es salaam bei yake inazidi 700,000/=
iPhone 7
Simu ya iPhone 7 ni iphone ya mwaka 2016
Kimo cha iphone 7 ni kidogo kwani inchi zake 4.7
Simu ina utendaji wa kuridhisha upande wa processor.
Kwani chip ya apple a10 inaizidi mbali chip ya snapdragon 678 iliyomo kwenye Redmi note 10 ya 2021
Ina kamera moja yenye uwezo wa chini kwa sasa
Betri yake ni dogo na halitunzi chaji muda mrefu kwani ukubwa wake ni 1960mAh
Kioo cha iphone 7 ni aina ya ips lcd na kina resolution ndogo
Bei ya iPhone 7 Tanzania
Bei ya iPhone 7 ya ukubwa wa GB 32 ni shilingi 273,996.00/= ebay
Kuna maduka ya kariakoo yanayoiuza simu kwa shilingi laki tatu mpaka laki tatu na nusu
Hii ni simu ambayo wakati wake unaenda kuisha
iPhone 6s
Simu ya iPhone 6S ni simu ya mwaka 2015.
Ina kimo kifupi cha inchi 4.7
Simu haina uwezo wa kuzuia maji kupenya
Kioo cha iphone 6s ni cha aina ya ips lcd chenye resolution ndogo ya 750 x 1334 pixels
Hivyo ubora wake ni mdogo
Utendaji wake ni wa kawaida kwa sababu processor yake inachuana na snapdragon 678
Betri yake haikai na moto muda mrefu kwani ni dogo (1715mAh)
Bei ya iPhone 6s Tanzania
Bei ya iPhone 6s ya ukubwa wa 16GB inafika shilingi 270,000/= kwa Tanzania.
Lakini hii bei ni kubwa.
Kwa sababu iphone 6s ya GB 32 ni shilingi 227,556/= kwenye duka la mtandaoni la ebay
iPhone SE 2022
Simu ya iPhone SE 2022 ni toleo jipya la mwaka 2022 la iPhone
Ni simu yenye kimo kifupi cha inchi 4.7
Utendaji wa simu upande wa processor unazizidi simu karibu zote za android
Kwa sababu iPhone SE 2022 inatumia chip yenye nguvu zaidi kwa sasa ya ya Apple A15 Bionic
Simu ina kamera moja inayoweza kurekodi video za 4k kwa spidi mpaka ya 60fps
Betri yake haikai na chaji muda mrefu.
Ina betri dogo lenye ukubwa wa 2018mAh
Bei ya iPhone SE 2022 Tanzania
Bei ya iPhone SE 2022 inafika shilingi 1,302,642.00/=
Hii ni bei ya SE ya ukubwa GB 64
Maduka mengine hapa Tanzania bei ya simu itakuwa kubwa zaidi ya shilingi 1.3M
Maoni 20 kuhusu “Simu 10 za iPhone za bei rahisi 2022-2024 (Na sifa zake)”
Simu ziko safi japo utendaji kazi wake unatofautiana,je vip kuhusu matoleo ya samsung?
Utendaji unautazama kupitia aina ya chip
Naomba unipunguzie bei ya iphone 6s
Hii hata kwa 250k unaweza kuipata
iPhone gali xan pungux jeeee
Kwahyo iPhone 12promax inapatkan Kwa beigan
USED ni milioni moja na laki tatu
iphone 8 plus sasa hivi unaiuza inabei gani?
Iphone 11 ya mtumba kutoka Dubai ina shiling ngapi ndugu
Nataka iphone 6s
Watu washapigwa sana kwa biasha za mitandaoni,mnanihakikishiaje kuwa nitakapoagiza kupitia mtandao nitapata mzigo wangu? Na je kama sitapata nitapeleka malalamiko yangu wapi?
Jambo zuri kuuliza, tafari pitia Sera yetu ya faragha na disclaimer (kanusho).
https://simunzuri.com/kanusho/
Kwa ambayo wapo far tunaweelekeza kufika kwenye maduka husika wenyewe.
Kwa ambao wananunua AliExpress au eBay hii mitandao ni mgumu Sana kupoteza pesa. Kwa mfano AliExpress wanaishikiria pesa mpaka bidhaa itakapokufikia
Naomba kujua bei ya Iphone11
Naomba bei ya iPhone x
Kwa sasa bei ya iPhone x ya GB 64 ni 550,000
Je niki itaji kufanya kuangiza simu maana kwa asaiv nina iphone6 s” ila naitaji iphone xr kwa hii niliyo nayo aitunzi chaji kwa sana
Mikoani hakuna maduka ya simu hizi?
Mie nipo mara
naomba kujua kama unaiza USED iphone
Kwani izo cm hazipo usid
Ninaomba ufafanuzi wa simu iphone 8 plus kiuwezo, Jinsi ya kuipata niko Moshi, na bei yake, na utumaji wa pesa.