SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

Bei ya Tecno Spark 20 na Sifa Zake Muhimu

Sifa za simu

Sihaba Mikole

January 30, 2024

Tecno Spark 20 ni toleo la Tecno lilotoka mwishoni mwa mwaka 2023 hivyo ni simu inayofaa hata kwa mwaka 2024

Bei ya Tecno Spark 20 yenye ukubwa wa memori ya GB 256 inaenda mpaka shilingi laki nne na nusu

Ubora wa hii simu unaendana kwa kiasi kikubwa na simu ya Samsung Galaxy A05s ya mwaka 2023

Kuna sifa zipatazo tano zinazoweza kumvutia mteja kuinunua hii simu

Hivyo basi hii posti itaangazia vipengele vya kamera, betri na chaji, utendajia, uwezo wa network na uimara wa bodi ya simu

Kabla ya yote ni muhimu ukajua sifa za jumla za Tecno Spark 20 kama zilivyoainishwa kwenye jedwari

Sifa za Tecno Spark 20

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g, 4g
Processor(SoC)
  • CPU – Mediatek Helio G85
  • Core Zenye nguvu(2) – 2×2.0 GHz Cortex-A75
  • Core Za kawaida(6) – 6×1.8 GHz Cortex-A55
  • GPU-Mali-G52 MC2
Display(Kioo) IPS LCD, Refresh rate:90Hz
Softawre
  • Android 13
  • HIOS 13
Memori 256GB na RAM 8GB
Kamera Kamera MBILI

  1. 50MP,PDAF(wide)
  2. 0.08MP
Muundo Urefu-6.6inchi
Chaji na Betri
  • 5000mAh-Li-Po
  • Chaji-18W
Bei ya simu(TSH) 450,000/=

Uwezo wa network

Hii inasapoti mpaka mtandao wa 4G aina ya LTE Cat 7

LTE Cat 7 ina kasi ya juu ya kupakua vitu inayofika 300Mbps

Kwa sasa unaweza kuipata kasi hii kama simu inasapoti mtandao wa 5G

Kwani 4G ni nadra kuipata kasi hiyo kwa sasa hapa nchini

Iwapo mtandao wa simu husika unaweza kukupa kasi ya 300Mbps basi utaweza kupakua faili la MB 74 kwa sekunde mbili

Ila kumbuka hilo linategemea kama 4G ya mtandao husika inakupa kasi hiyo

Ubora wa kamera

Hii simu inakuja na kamera mbili ila kiuhalisia ina kamera moja

Kamera yenyewe ina ukubwa wa megapixel 50

Mfumo wake wa kamera unatumia teknolojia ya ulengaji ya PDAF

PDAF ina uhalaka katika kukitambua kitu kinachopigwa picha

Hivyo muonekano ni wa kutilia kama ukiwa unapiga picha kitu kinachotembea

Ubora wa picha ni wa kuvutia hasa nyakati za mchana

Haina tofauti na ubora ambao upo kwenye simu ya Tecno Spark 10 Pro

Ubora wa kioo

Hii simu inatumia kioo cha IPS LCD chenye resolution ya 720×1612 pixels

Hioo sio resolution kubwa hivyo muonekano wa vitu utakuwa na ubora duni ukifananisha na vioo vya AMOLED

Uzuri wa kipekee kwenye skrini ya Spark 20 ni uwepo wa refresh rate kubwa inayofika 90Hz

Ila hii kwa sasa imekuwa ikiwekwa kwenye simu nyingi za madaraja ya kati

Uzuri wa refresh rate kubwa ni simu kuwa nyepesi na nzuri kwa kucheza magemu

Kwa bahati mbaya ni kuwa simu ikiwa inatumia refresh rate kubwa muda wote hutumia kiwango kikubwa cha chaji

Hivyo kwenye mfumo wa HIOS uliopo kwenye Tecno unaruhusu kubadilisha refesh rate na kuweka ndogo

Uwezo wa Betri na chaji

Betri ya Tecno Spark 20 ina ukubwa wa 5000mAh

Ni betri kubwa hivyo ukiwa unatumia intaneti muda wote inaweza kustahimili kukaa na chaji kwa muda wa masaa 10

Na hata ukiwa unacheza magemu betri inaweza kudumu kwa muda wa masaa saba

Upande wa chaji simu inasapoti chaji mpaka ya wati 18

Hii ni chaji yenye kasi ya wastani sio kama zile simu zenye kasi ya wati 30

Hivyo simu inaweza kuchukua muda kidogo kujaa kwani betri ya mAh 5000 ni kubwa

Hata hivyo kuna faida pia kuwa na simu yeny kasi ya kuchaji ya wastani

Uwezo wa kiutendaji

Ukitaka kujua uwezo wa simu kiutendaji ni kwa kutazama aina ya processor(chipu) iliyotumika

Spark 20 inatumia chip ya Mediatek Helio G85 ambayo imegawanyika sehemu mbili zenye jumla ya core nane

Kuna core mbili zenye nguvu kubwa ambazo zinatumia muundo wa Cortex A75

Kwenye kucheza magemu, chip inacheza kwa muonekano mkubwa kwenye baadhi ya magemu

Kwa mfano gemu la PUBG Mobile inacheza kwa FPS 45 Kwenye muonekano wa Ultra HD

Muonekano mzuri zaidi huifanya processor kutumia nguvu kubwa

Kama chip ikiwa ni dhaifu sana inacheza kwa kuganda ganda

Utendaji wa hii chip unaendana na chip ya Snapdragon 680 4G iliyotumika kwenye simu za Oppo A96 na Xiaomi Redmi Note 11

Hivyo utendaji wa Spark 20 unastahili kuiweka simu kwenye kundi la kati

Uimara wa bodi ya simu

Simu ya Tecno Spark 20 ina viwango vya IP vinavyoashiria uwezo wa simu kutopitisha maji

Japokuwa haina viwango vya IP67 au IP68 ambavyo huashiria kuwa simu hata ikizama kwenye kina cha mita 1.5 kwa muda wa nusu saa maji hayawezi kupenya

Viwango hivi utavikuta kwenye simu mfano wa Samsung Galaxy S24 Ultra ama iPhone 15 Pro Max

Ni maji ya rasha rasha ndio yanayoweza kutoingia ndani ya simu

Haiwezo kustahimili kama ikizama kwenye maji mengi

Uwepo wa IP-rating ni maboresho makubwa kwenye simu za Tecno

Kwani nyingi za zamani hazikuwa zinawekwa ulinzi wa kuzuia maji

Washindani wa Tecno Spark 20

Kwa kutazama nguvu ya utendaji na bei ya tecno spark 20, washindani sahihi wa simu ni Samsung Galaxy A05s, Oppo A96 na Redmi 10C

Galaxy A05s ina kitu cha ziada kwenye skrini kwani resolution yake ni kubwa

Wakati Redmi 10C inapatikana bei rafiki

Kiufupi ni kwamba kuna simu zipatazo kama 20 kutoka kwa makampuni ya Oppo, Xiaomi, Motorola, Samsung, Vivo, Honor na Tecno yenyewe ambazo zinaweza kuwa mbadala

Kwa bahati mbaya au nzuri bidhaa za makampuni upatikanaji wake hapa nchini una changamoto

Kitu kinachoipa tecno faida.

Neno la mwisho

Kwa wanaopenda simu zenye memori kubwa ili kuhifadhi vitu vingi hii inaweza ikawa chaguo zuri

Bei yake inavumilika na kwa kiasi kikubwa kinaendana na sifa za simu husika

Ila sio mbaya pia ukatazama matoleo yanayorandana kisifa

Maoni 2 kuhusu “Bei ya Tecno Spark 20 na Sifa Zake Muhimu

Maoni na Maswali

Email yako haitochapishwa, kwenye alama * lazima pajazwe ili ukomenti

Fuatilia Zaidi

No Featured Image

Bei ya Samsung Galaxy A25 na Sifa zake

Simu ya Samsung Galaxy A25 ilitoka rasmi mnamo mwezi desemba 2023 Ni simu ya daraja ambayo bei yake kwa Tanzania ni shilingi laki saba (700,000/=), hii ikiwa ni bei ya […]

Bei ya Tecno Spark 20 Pro+ na Sifa zake

Simu ya Tecno Spark 20 Pro+ ilitoka rasmi desemba ya mwaka 2023 ila kwa Tanzania imeanza kupatikana miezi ya karibuni Kwa Tanzania bei ya juu kabisa ya Tecno Spark 20 […]

nokia thumbnail

Simu mpya za Nokia zilizotoka 2023-2024 na bei zake

Kwa mwaka 2024, kampuni ya HMD Global inayotengeneza simu za Nokia hawajatoa toleo jipya mpaka sasa machi 2024 Taarifa kutoka vyanzo mbalimbali zinasema HMD inatarajia kutoa matoleo 17 mwaka 2024 […]

simu mpya

Simu mpya kali 20 na bei zake kwa mwaka 2024

Hii ni orodha ya simu mpya ambazo zimetoka mwaka 2024 ama mwishoni mwa mwaka 2023 kutoka kwa kampuni zipatazo 11 Ni orodha inayohusisha simu za daraja la kati na la […]

SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

E-mail : simunzuriblog@gmail.com

Simu: +255 683 420 543

Whatsapp: +255 756 077 262

Kabila, Magu

Mwanza, Tanzania

Company

Find Us On

FB Twitter Instagram