Simu ya Tecno Pova 5G ni simu ya 5G kutoka tecno
Hii ni moja ya simu ya daraja la kati ya mwaka 2021 inayoweza kuchuana na simu nyingi za redmi
Hivyo uwezo wake wa utendaji unaifanya bei ya tecno 5G kuwa zaidi ya laki sita
Itakulazimu kufamu sifa zake na ubora wake kamera, kioo, bodi, processor na network ili ujiridhishe kama bei yake inakidhi vigezo
Ufafanuzi wote unapatikana kwenye hii posti
Bei ya Tecno Pova 5G Tanzania
Bei ya tecno pova 5g ya ukubwa wa GB 128 na RAM ya GB 8 ni shilingi 670,000/=
Pova 5G ni tofauti na Tecno Pova ya kawaida
Kiubora 5G ina vitu vingi vizuri hasa kwa kutazama uotfauti wa sifa za tecno pova 5g na tecno pova
Sifa za simu ya Tecno Pova 5G
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g and 5g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | IPS LCD, Refresh rate:120Hz |
Softawre |
|
Memori | UFS 3.1, 128GB na RAM 8GB |
Kamera | Kamera tatu (tecno macho matatu)
|
Muundo | Urefu-6.9 inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 670,000/= |
Upi ubora wa Tecno Pova 5G
Ubora wa tecno pova 5g unapatikana kwa kiasi kikubwa kwenye utendaji
Kwa sababu simu inatumia processor ambayo ina nguvu kutoka kwa kampuni ya mediatek
Ina ubora wa kuweleka upande wa kioo
Kutokana na kioo kuwa na resolution kubwa
Ina uwezo mkubwa wa kukaa na chaji masaa kwa maana betri yake ni kubwa sana
Simu ina mfumo wa memori unaopeleka data kwa kasi kubwa ya kusafirisha
Kasi kubwa inaimarisha utendaji wa simu
Uwezo wa Network
Tecno pova 5g inasapoti mtandao wa 5G na 4G kwa pamoja
Aina ya 4G simu inayotumia ni LTE Cat 18
Kasi ya LTE Cat 18 ni 1200 Mbps ambayo ni sawa na 150MBps
Kwa maana faili la ukubwa wa 1500MB litadownloadiwa kwa sekunde kumi
Kwa bahati mbaya hakuna mtandao wa simu unaotoa kasi hiyo hapa Tanzania
Lakini cha muhimu ni kuwa simu inakubali 4G ya mitandao yote Tanzania
Ubora wa kioo cha Tecno Pova 5G
Kioo cha tecno pova 5g ni cha aina ya IPS LCD
Kiubora, ips inaachwa mbali na vioo aina ya amoled ambavyo unaweza vimetumika kwenye simu ya tecno camon 18 premier
Ila kitendo cha kio chake kuwa na resolution ya 1080 x 2460 kinaongeza ubora wa screen kuonyesha vitu vizuri
Na kioo pia ni chepesi kutokana na kuwa na refresh rate ya 120Hz
Refresh rate kubwa huwa inafaa sana kucheza gemu
Japokuwa ulaji wa chaji huongezeka
Nguvu ya processor MediaTek Dimensity 900
Pova 5G inatumia chip ya mediatek dimensity 900 kufanya kazi zote zinazofanywa na simu
Dimensity 900 ni processor ya simu ya daraja la kati yenye idadi ya core nane (octa core)
Utendaji wake ni mkubwa
Kwenye app ya geekbench dimensity 900 ina alama 711 kwenye core moja
Alama hizi ni nyingi kuliko zile za Helio G80 ya samsung galaxy a32
Utendaji mkubwa wa chip unachangiwa na uwezo wa kimuundo wa core kubwa na core ndogo
Uwezo wa core kubwa
Tecno hii yenye dimensity 900 ina core zenye nguvu kubwa zipatazo mbili
Kila core inafanya kazi kwa spidi inayofika 2.4 GHz
Hii inamaanisha processor yake ina mizunguko bilioni 2.4 kwa sekunde
Kila mzunguko mmoja unaweza kufanya kazi nne
Hivyo chip inaifanya simu kuweza kufungua app nyingi za kila aina kwa wakati mmoja kirahisi
Kwani muundo wa core zake ni Cortex A78 ambao ina matumizi madogo ya umeme kwa utendaji mkubwa
Uwezo wa core ndogo
Processor ina core sita zenye uwezo mdogo
Spidi ya kila core haizidi 2.0 GHz
Na zinatumia core aina ya Cortex A55
Hizi ni core ambazo zinatumia umeme mdogo sana
Na utendaji ni wa chini
Huwa ni maalumu kwa ajili ya shughuli ndogondogo simu inazofanya
Uwezo wa betri na chaji
Betri ya tecno pova ina ukubwa wa 6000mAh
Ukubwa huu unaipa simu nafasi ya kukaa na chaji masaa ya kutosha kuliko kawaida
Ila simu inaweza chukua masaa zaidi ya matatu kujaa
Kwa sababu chaji yake haina kasi kubwa ya kupeleka chaji
Kasi yake ni 18W
Ukubwa na aina ya memori
Kuna toleo la aina moja tu la pova 5g upande wa memori
Ukubwa wa tecno hii ni GB 128 na RAM ya GB 8
Aina ya memori simu inayotumia ni UFS 3.1
Kasi ya UFS 3.1 kwa kusoma data ni 2100MBps na kuandika data ni 1200MBps
Spidi hiyo inafanya simu kufungua app kwa haraka
Hivi karibuni samsung imetangaza ujio aina ya memori yenye kasi zaidi ya UFS 4.0
Uimara wa bodi yaTecno Pova 5G
Kiujumla bodi ya pova 5g inatumia plastiki upande wa nyuma na pembeni
Ila tecno haijatumia vioo vya gorilla kuzuia simu kuvunjika
Hivyo ni muhimu kuweka kava na screen protector
Simu ni ndefu na urefu wake ni inchi 6.9
Kwa mtu anaependa simu ndefu basi tecno hii itamfurahisha kwa kiasi kikubwa
Ubora wa kamera
Tecno Pova 5G ni tecno macho yenye kamera moja tu iliyowekewa PDAF
PDAF iko taratibu kutambua kitu kinachopigwa picha ukilinganisha na dual pixel pdaf
Kamera mbili zilizabaki zina resolution ndogo
Na nyingine haitoi picha nzuri kabisa
Kamera hiyo ni aina ya QVGA
Kamera zake zinaweza kurekodi video za full hd pekee kwa spidi ya 30fps
Japokuwa dimensity 900 inaweza kuchakata video za 4K bila shida
Ubora wa Software
Simu inakuja na androdi toleo la 11 na mfumo wa HIOS 8.0
HIOS 8.0 una mpangilio wenye icon kubwa upande wa notification
Pia mpangilio wa settings una icons unaorahisisha mtumiaji kufanya uchaguzi mzuri
Pia ina app ambayo inaonyesha hali hewa ya eneo ulilopo mubashara kabisa
Yapi Madhaifu ya Tecno Pova 5G
Tecno Pova 5G ina mfumo mbovu wa kamera
Kamera zake haziwezi kurekodi video za 4K
Pia kamera zake mbili zina uwezo mdogo wa kutoa picha nzuri
Simu haiwezi kupiga picha eneo pana sana kwa kuwa hakuna kamera ya ultrawide
Kioo cha tecno kinaonyesha rangi chache kwa kuwa ni cha ips lcd
Simu haina uwezo wa kuzuia maji kwa sababu hakuna viwango vya IP-Ratings
Neno la Mwisho
Kwa mtumiaji anayejali utendaji wa simu pekee tecno pova 5g itakupa pafomansi kubwa
Hivyo bei yake ni rafiki
Lakini pia kwa bei hiyo hiyo unapata simu ya Redmi note 11 pro plus 5g ambayo ina vitu vya ziada