Kampuni ya Tecno Mobile imeanza mwaka 2023 kwa kuja na simu mpya ya Tecno Phantom X2 Pro
Kama una mawazo kuwa tecno ni tecno tu hata iweje basi jua simujanja hii ni kali japo bei imechangamka
Kwani bei ya Tecno Phantom X2 Pro ni zaidi ya milioni moja, inashangaza.
Tecno hii ni tofauti na tecno zote ambazo umewahi ona ama kusikia
Kwenye posti hii kuna ufafanuzi wa vitu muhimu vilivyoongeza ubora wa hii simu, fuatilia.
Bei ya Awali ya Tecno Phantom X2 Pro
Tecno Tanzania hawajatangaza bei yake hapa nchini
Ila nchini India bei yake imeainishwa kuwa ni shilingi 1,500,000/= (milioni moja na laki tano) za Tanzania
Ni moja ya simu ya bei kubwa ya Tecno.
Hii inatokana na mambo mengi ikiwemo kutumika kwa moja ya chip yenye nguvu kubwa duniani
Processor hii inaifanya simu kufanya kazi kwa haraka.
Lakini pia hii ni simu ya tecno itakayokuwa inapata matoleo mapya ya Android kwa kipindi cha miaka miwili kuanzia 2023 mapka 2025
Matoleo mapya yanaifanya simu kupokea teknolojia mpya za Android
Sifa za simu ya Tecno Phantom X2 Pro
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g and 5g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | AMOLED, Refresh rate:120Hz |
Softawre |
|
Memori | UFS 3.1, 256GB na RAM 12GB |
Kamera | Kamera tatu
|
Muundo | Urefu-6.8inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 1,500,000/= |
Upi ubora wa Tecno Phantom X2 Pro
Ni simu yenye nguvu kubwa kiutendaji
Phantom X2 Pro ni simu janja inayokubali mtandao wa 5G
Ina ugumu unaoweza kuepusha simu kupasuka inapodondoka
Betri yake ni kubwa na inapeleka chaji kwa kasi
Ina muundo unaovutia kuushika na kimuonekano
Ina aina tatu za kamera zenye kutoa ubora mzuri wa picha
Pamoja na hayo mapungufu ni machache sana kama utakavyoona
Uwezo wa Network
Hii simu inasapoti mitandao yote ikiwemo 5G
Vodacom Tanzania inayo mtandao wa 5G kwa baadhi ya maeneo kwa mkoa wa Dar Es Salaam
Upande wa 4G inatumia LTE aina ya LTE Cat 24.
LTE Cat 24 inaweza kupakua kitu kwa kasi inayofika 3000Mbps ambayo ni sawa na 375MBps
Kwa mfano kama unadownload faili la MB 375 itachukua sekunde moja tu kumalizika
Lakini kasi ya simu inategemea na uwezo wa mtandao wa simu husika.
Ni changamoto kuipata kasi hiyo kwa hapa Tanzania upande wa 4G ila 5G inawezekana
Simu ina masafa yote yanayotumika hapa nchini hivyo mitandao yote itakubali
Ubora wa kioo cha Tecno Phantom X2 Pro
Kioo cha Tecno Phantom X2 Pro ni aina ya AMOLED chenye resolution 1080 x 2400 pixels
Aina hii ya kioo huwa inafanya vitu viwe “sharp” na rangi kuwa yenye kukolea
Vioo vya amoled huwa vinaonyesha vitu kwa rangi zake halisi kwa kiasi kikubwa hasa rangi nyeusi
Kitu kingine ambacho kioo chake inacho ni refresh rate inayofikia 120Hz
Kiwango hiki hufanya simu kuwa nyepesi(smooth) unapokua unatachi kioo kwa kupeleka juu na chini (scroll)
Kwa bahati kioo chake hakina teknolojia ya HDR10 ambayo huboresha vitu na kuvifanya vionekane kwa usahihi kama vinavyoonekana na jicho la binadamu
Ni kitu cha kuzingatia kwa sababu simu nyingi za bei ghari huweka HDR10
Upande wa uangavu, simu ina kiwango kidogo kwani nits zinafika 500.
Ambapo simu kama Redmi Note 10 nits zake zinaenda mpaka 1000.
Nguvu ya processor MediaTek Dimensity 9000
X2 Pro inafungua app kwa haraka na kufungua app nyingi kwa wakati mmoja bila simu kupata shida
Uwezo wake unaiwezesha simu kucheza gemu ya aina yoyote kwa graphics zenye ubora mkubwa
Magemu huwa yanahitaji chipset yenye nguvu
Phantom inatumia processor ya MediaTek Dimensity 9000
Kiuwezo, inaendana na chip iliyotumika kwenye Samsung Galaxy S22 ambayo ni Snapdragon 8 gen 1
Snapdragon 8 gen 1 iko kwenye ligi moja na processor yenye nguvu zaidi duniani kwa sasa kutoka apple (Apple A16 Bionic)
Dimensity 9000 imegewanyika katika sehemu tatu upande wa core
- Core yenye nguvu sana moja (1×3.05 GHz Cortex-X2)
- Core yenye nguvu zipo tatu (3×2.85 GHz Cortex-A710 )
- Na core zenye nguvu ndogo zipo nne (4×1.80 GHz Cortex-A510)
Core zenye nguvu ndogo ni kwa ajili ya matumizi yasiyohitaji nguvu kama kupiga, kutuma sms nk
Inasaidia kupunguza matumizi makubwa ya betri kwani core zenye huwa zinakula chaji nyingi
Uwezo wa betri na chaji
Betri ya Tecno Phantom X2 Pro ina ukubwa wa 5160mAh
Hii betri inakaa na chaji lakini si kwa kiwango kikubwa
Inashangaza betri yenye ujazo wa zaidi 5000mAh kushindwa kutunza chaji kwa masaa 14 simu ikiwa inaperuzi intaneti muda wote
Kwa mujibu wa GSMArena Phantom X2 Pro inadumu kwa muda wa masaa 12 ikiwa inaperuzi muda wote
Chaji ina wati 45 lakini inajaa kwa 39% ndani ya nusu saa, sio muda wa kuridhisha kwa chaji ya 45W
Ila hiyo inachangiwa na betri kuwa kubwa sana pia
Ukubwa na aina ya memori
Simu ya Phantom ina toleo moja yenye ukubwa wa memori 256GB na RAM ya GB 12
Na simu haiji na sehemu ya kuweka memori kadi
GB 256 ni nyingi ila memori ina umuhimu wake pia
Memori inayotumia ni aina ya UFS 3.1 ambazo huwa na kasi inaypfika 1200MBps
Kasi hii inasaidia simu kukopi faili kwa haraka na pia kuendana na kasi ya mtandao wa 5G
5G huwa inadownload vitu kwa kasi hivyo inahitaji memori yenye kasi kubwa pia kusafirisha data
Uimara wa bodi ya Tecno Phantom X2 Pro
Kwenye skrini simu inalindwa na kioo cha Corning Gorilla Victus
Kwa mujibu kampuni ya gorilla, hiki kioo kilijaribiwa kuangushwa kwa urefu wa mita 2 toka juu kwenye eneo baya
Lakini simu haikupasuka.
Na kiuharisia vioo vya gorilla ni himilivu na vigumu kupasuka
Ila upande wa nyuma una plastiki
Kwa bahati mbaya simu haina viwango vya IP vinavyoonyesha uwezo wa kutopitisha maji simu ikizama kwenye maji
Simu zinazouzwa kwa gharama kubwa huwa wanaweka aina hii ya ulinzi
Ulinzi unaokupa uhuru wa kuitumia simu hata kwenye mvua
Ubora wa kamera
Tecno Phantom X2 Pro ina jumla ya Kamera tatu (tecno macho matatu)
Kuna kamera ya kupiga vitu ambavyo vipo mbali sana na kamera ya simu
Kamera hii huitwa Telephoto ina 50MP
Na pia ina kamera ya kupiga eneo pana sana, hii huitwa (Ultrawide)
Na pia ina kamera ya kawaida inayopiga vitu vya karibu na vilivyopo kwenye upana wa wastani
Hii inaitwa Wide na ina 50MP
Kiujumla kamera zake zote zinapiga picha vizuri kwenye mazingira yote ya mwanga hafifu na mchana
Ila inatatizo moja ambalo ni Dynamic Range
Kwneye mwangaza mwingi, rangi ya vitu uhalisia wake unapungua kama maji, rangi ya blue uweupe unazidi
Ama nyakati zingine mtu anatokea anang’aa sana kuliko anavyoonekana
Kamera zake zinaweza kurekodi mpaka video za 4K kwa fremu 30 kwa sekunde
Ubora wa Software
Tecno Phantom X2 Pro inatumia mfumo endesh wa Android 12 na software ya HiOS 12
Android 12 imeshazungumziwa sana
Ila HiOS 12 inakuja na vitu vingi ikiwemo AI Gallery 5.0
AI Gallery 5.0 huu ni mfumo wa utambuzi unaweza kuziweka picha zinazoendana sehemu moja kwa hiyo huhitaji kuzipanga picha bali AI Gallery inaweza fanya hivyo
Huu mfumo unatumia teknolojia ya Artificial Intelligence (Akili bandia kwa kiswahili kisicho rasmi)
Kwa maana simu inakuwa na akili ya kutambua kuwa picha hii ina kitu fulani kinachoendana na kitu kilichopo kwenye picha nyingine
Yapi Madhaifu ya Tecno Phantom X2 Pro
Kasoro kubwa ya hii simu ni kukosekana kwa IP67 au IP68
Ukiona alama za IP67 au IP68 inamaanisha simu haipitishi maji wala vumbi
Tecno wamefuata njia ya iPhone kwa kutoa sehemu ya kuweka memori kadi
Ukaaji wa chaji hauwendani na ukubwa wa betri kwani inazidiwa na simu ya iphone 14 pro ambayo betri yake ni 4300mAh
Kioo(display) chake hakina HDR10+ na uangavu wake ni wa wastani
Neno la Mwisho
Tecno wanaendelea kuimarika na uthibithsho ni toleo la Phantom X2 Pro
Lakini kuna TATIZO.
Bei ya Tecno Phantom X2 Pro inaendana kwa kiasi kikubwa na simu ya Xiaomi 13 Pro
Vitu ambavyo havipo kwenye Phantom hii vinapatikana kwenye Xiaomi 13 Pro
Hii inamaanisha tecno wanaenda kukumbana na ushindani mkubwa kutoka kwa makampuni mengine
Inabidi tecno mobile wajitathmini kuhusu bei za vifaa vyao
Maoni 3 kuhusu “Bei ya Simu ya Tecno Phantom X2 Pro na Ubora Wake (2023)”
Napenda nipate techno phantomx2 pro 256gb
Nipo Congo naipataje île phantomx2 pro
Congo mbali sana ngoja tuangalie utaratibu