Simu ya tecno camon 11 ni simu ambayo imetoka mwaka 2018.
Bei ya tecno camon 11 ni chini ya shilingi laki mbili.
Ni simu ambayo haiendani na nyakati za sasa
Utafahamu ubora wake kwa kuzijua sifa za simu husika
Bei ya tecno camon 11 Tanzania
Bei ya tecno camon 11 ya 32GB kwenye maduka ya Tigo ni shilingi 319,999/=
Ila sasa kiuhalisia simu haistahili kuuzwa kwa zaidi ya laki mbili
Unataka kujua sababu?
Zisome kila sifa ya camon 11
Sifa za tecno camon 11
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | IPS LCD, |
Softawre |
|
Memori | eMMC 5.1, 64GB,32GB na 3GB,4GB |
Kamera | Kamera nne
|
Muundo | Urefu-6.2inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 320,000/= |
Upi ubora wa tecno camon 11
Kiuhalisia simu ya tecno cammon sio simu nzuri.
Kwa maana ina vitu vilivyo chini ya ubora kwa asilimia kubwa
Kikubwa ni kuwa ni simu ya 4G yenye spidi ya kuridhisha kama utakavyoona kwenye kipengele cha network
Mambo mingine yana ubora wa chini
Uwezo wa Network
Simu ya tecno camon 11 inatumia 4G aina ya LTE Cat 7
LTE Cat 7 inaweza kudownload faili kwa spidi inayofika 300Mbps
Hivyo kama mitandao ya simu inatoa spidi hii basi mafaili makubwa yatamalizika kudownload muda mfupi
Simu ina masafa ya mtandao wa 4G ya aina tisa
Na ina masafa yote yanayotumika na mitandao ya simu Tanzania
Ubora wa kioo cha tecno camon 11
Kioo cha tecno camon 11 ni cha aina ya IPS LCD.
Hiki ni kioo kizuri kama kinakuwa na resolution kubwa
Ila camon 11 ina resolution ndogo ya 720 x 1500 pixels
Hivyo ubora wa kioo kuonyesha vitu kwa ustadi ni wa wastani
Kiubora, vioo vya amoled vinaizidi mbali vioo vya ips lcd.
Ndio maana simu kama camon 18 premier inakuwa na bei kubwa
Nguvu ya processor MediaTek Helio A22
Simu ya tecno camon 11 inatumia processor ya MediaTek Helio A22
Helio A22 ina jumla ya core nne.
Hizi ni core ndogo ambazo hutumika kufanya kazi ndogo
Kwa sababu zinatumia muundo wa Cortex A53
Ni muundo unaoifanya simu kuwa na nguvu ndogo ya kiutendaji
Kwenye geekbench helio a22 ina alama 161
Hii inafanya simu kupata shida wakati wa kucheza gemu kama Call of Duty: Mobile
Uwezo wa betri na chaji
Simu ina betri lenye ujazo mdogo wa 3750mAh
Hivyo ukaaji wa chaji ni mdogo
Na simu haina chaji yenye kasi.
Tarajia simu kuchukua masaa mengi kujaza betri dogo la 3750 mAh
Ukubwa na aina ya memori
Kuna matoleo mawili ya camon 11 upande wa memori.
Kuna tecno ya GB 32 na Tecno ya GB 64
Utendaji nndogo wa simu unachangiwa na memori ya eMMC 5.1 iliyopo kwenye simu hii
kwa sababu memori eMMC zina kasi ndogo ya kusafirisha data ukifananisha na memori za UFS
Bei yake inaweza kuwa kubwa zaidi kutokana na ukubwa wa memori
Uimara wa bodi ya tecno camon 11
Bodi ya tecno camon 11 si imara kwa sababu imeundwa kwa plastiki upande wa nyuma
Bodi za plastiki zina kawaida ya kuchunika rangi kadri umri wa simu unavyoenda
Na pia haijawekewa ulinzi wa kioo cha gorilla upande wa mbele
Hivyo kava na screen protector inahitajika kuimarisha ulinzi wa simu
Bila hivyo simu ikidondoka kimo kirefu inaweza kuvunjika
Ubora wa kamera
Simu ina kamera mbili pekee upande wa nyuma.
Kamera kubwa ina resolution ya 13MP na inatumia teknolojia ya ulengaji ya kawaida sana
Kwa hiyo ubora wa picha wa kitu kinachotembea unaweza kuwa mdogo
Kiujumla mfumo wake wa kamera sio wa kuvutia.’
Simu haiwezi kurekodi video za 4k bali inarekodi video za full hd pekee.
Anayerekodi video anapaswa kutuliza mkono kwa sababu simu inakosa OIS
Ubora wa Software
Tecno camon 11 inakuja na toleo la android 8.1
Ni toleo ambalo bado linakubali apps nyingi za play store
Japokuwa kwa sasa kuna toleo jipya android 12
Kwa bahati mbaya simu haipokei toleo lingine la android
Yapi Madhaifu ya tecno camon 11
Simu ina mapungufu kwenye kila kitu unachokifahamu kinachounda simu
Ukianza na memori haina kasi inayoongeza ufanisi wa kiutendaji
Kamera zake hazitoi picha za kuvutia
Kioo chake kina resolution ndogo
Utendaji wa simu ni mdogo kutokana na kuwa na kutumia chip yenye nguvu ndogo
Neno la Mwisho
Tecno Camon 11 inamfaa mtumiaji mwenye bajeti ndogo sana ya simu
Kwani hata mtumiaji mpya anaweza kupata simu nzuri kwa bei ya chini ya laki tatu
Kwa mpenzi wa magemu hatofaurahia kutumia simu
Kuna simu ya bei nafuu ya redmi 9a na pia tecno spark 8 pro yenye utendaji wa kuridhisha
Wazo moja kuhusu “Bei ya Simu ya Tecno Camon 11 na Sifa Zake (2022)”
Badilisha izo simu make so powa an