Simu ya samsung galaxy s22+ 5g ni simu mpya ya samsung ya mwaka 2022
Galaxy s22+ ni moja ya simu bora iliyotengenezwa kwa ustadi mkubwa kwenye kila nyanja ikiwemo kamera
Kitu kinachofanya bei ya samsung galaxy s22+ kuwa ni zaidi ya shilingi milioni mbili kwa sehemu kubwa ya Tanzania
Fuatilia bei yake, kisha fuatalia kila sifa ya S22+ uone ni namna gani ubora wake unavyoweza kuizidi simu ya iphone 13 pro max
Bei ya Samsung Galaxy S22+ Tanzania
Bei ya samsung galaxy s22+ 5g kwa baadhi ya maduka ya simu ya kinondoni ni shilingi 2,600,000/=
Hii ni bei itakayokupa galaxy ya GB 256 na RAM ya GB 8
Swali ambalo linaweza kuwa kichwani mwa mtu, ni kwa nini simu iuzwe kwa zaidi ya milioni mbili.
Bei kubwa ya hii simu hasa inasababishwa na ubora wake upande wa utendaji, kioo, uimara wa bodi, network nzuri na sifa zingine
Kama unataka kuifahamau Samsung S22+ kiundani basi zisome sifa zake zote ambazo zimeambatanishwa kwenye posti hii.
Sifa za simu ya Samsung Galaxy S22+ 5G
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g and 5g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | Dynamic AMOLED 2X, Refresh rate:120Hz |
Softawre |
|
Memori | UFS 3.1,256GB, 128GB na RAM 8GB |
Kamera | Kamera nne
|
Muundo | Urefu-6.6inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 2,600,000/= |
Upi ubora wa samsung galaxy s22+ 5g
Ubora mkubwa wa galaxy s22+ ni kuwa na chip yenye utendaji mkubwa
Ufanisi mkubwa wa chip unaifanya simu kuwa na uwezo wa juu kwenye kila sehemu
Lakini pia ina kioo kinachoonyesha vitu kwa uzuri sahahi
Ina uwezo wa kutumia aina zote za 5G na ina masafa ya 4G ya kutosha
Samsung s22 haipitihsi maji hata simu ikidumbukia kwenye kina cha maji ya mita moja
Ukitazama upande wa network mpaka kwenye software utaona ni simu ambayo imekamilika
Japokuwa ina changamoto zake chache kama utakavyoona baadae
Uwezo wa Network
Galaxy S22+ inaweza kutumia kila aina ya mtandao wa 4G na 5G
Aina ya 4G inayotumia ni LTE Cat 24
LTE Cat 24 ina spidi ya juu inayofikia 3000Mbps
Ni spidi kubwa sana ambayo hakuna mtandao wa simu nchini Tanzania unaotoa kasi hiyo
Ila ina masafa ya LTE yanayotumika na mitandao yote ya simu hapa nchini
Hivyo kila la laini ya 4G itafanya kazi vizuri.
Pitia huu kurasa kujua, masafa ya mtandao wa LTE ya Tanzania
Ubora wa kioo cha samsung galaxy s22+ 5G
Simu mpya za samsung s-series za 2022 zinatumia kioo cha Dynamic AMOLED 2X
Dynamic AMOLED 2X ni super amoled iliyoboreshwa yenye ongezeko la rangi zaidi
Hivyo kuna uhalisia kiasi cha juu wa vitu kuonekana kwa jinsi vilivyo kwenye mazingira halisi
Ubora wa display yake unaongezewa na uwepo wa HDR10+
Na pia kioo kuwa na resolution ya kiwango kikubwa ya 1080 x 2340 pixels,
Kioo cha samsung galaxy s22+ 5g kina uangavu unaoweza kuonyesha vitu vizuri simu ikiwa inatumika juani
Kwani ina nits zinazofika 1700
Na kizuri zaidi kioo chake kina refresh rate inayoifanya simu kuwa nyepesi na nyororo wakati wa kuscroll
Kwa sababu refresh rate yake ni 120Hz
Nguvu ya processor ya Exynos 2200
Simu ya samsung galaxy s22+ 5G inatumia processor ya Exynos 2200 kufanya kazi zake zote
Kuhusu utendaji exynos 2200 ina nguvu kubwa
Inaweza kucheza gemu za kila aina kwa ubora wa ultra hd bila simu kupata joto
Kwenye app ya geekbench, hii processor ina alama 1161
Na kwenye app ya antutu exynos ina alama 975,340
Ni chip chache sana ambazo zina alama kama hizo
Hii inasababishwa na processor ya simu kutumia muundo wa Cortex X2 kwenye core moja
Na cortex 710 kwenye core tatu
Na pia core ndogo zipo nne na zinatumia muundo wa Cortex-A510
Kwenye linki ifuatayo utatambua, jinsi ya kujua simu yenye processor bora
Uwezo wa betri na chaji
Betri ya samsung galaxy s22+ 5G ina ukubwa wa 4500 mAh aina ya Li-Po
Ukubwa unaosaidia simu kukaa na chaji takribani masaa 97 ikiwa haitumiki mara kwa mara
Ukaaji wa chaji wake si wa kiwango kikubwa kama simu ya oppo find x3 pro
Kwa mujibu wa gsmarena galaxy s22+ inajaa chaji kwa 100% baada ya dakika 62
Ujazaji wa haraka wa chaji kwa sababu simu inakuja na chaji inayopeleka umeme kwa kasi ya wati 25
Ukubwa na aina ya memori
Kuna matoleo mawili ya samsung galaxy s22+ upande wa memrori
Ipo ambayo ina ukubwa wa GB 128 na nyingine yenye ukubwa wa GB 256
Zote zinatumia RAM zenye ukubwa wa GB 8
Ufanisi wa simu huongezeka zaidi RAM ikiwa kubwa
Aina ya memori ambazo simu inatumia ni UFS 3.1
Hizi ni memori ambazo husafirisha data kwa kasi ianyofikia 2900 MB/s
Hivyo simu inawaka kwa haraka na app kufunga kwa urahisi ndani ya sekunde
Uimara wa bodi ya samsung galaxy s22+ 5g
Simu ina bodi ngumu ambayo haipitishi maji ikiwa imezama kwenye kina cha mita moja na nusu
Upande wa nyuma na kwenye kioo kunalindwa na kioo cha Gorilla Glass Victus+
Na upande wa pembeni umewekwa aluminiamu
Pia simu urefu wake na uzito ni wa wastani unaoweza kukaa vizuri kwenye mkono
Ubora wa kamera
Galaxy S22+ ni samsung macho matatu
Ina kamera kwa ajili ya kupiga vitu ambavyo vipo mbali sana yaani Telephoto
Na kamera kwa ajili ya kupiga eneo pana kwa nyuzi ya 120 yaani Ultrawide
Katika picha ambazo zimepigwa na gsmarena simu inatoa picha kwa rangi halisi za vitu
Vitu vinaonekana vitu kwa nyakati zote yaani usiku na mchana
Zitazame hapa, picha zilizopigwa na samsung s22+
Ubora wa Software
Simu inakuja na mfumo endeshi wa Android 12 na One UI 4,1
Kuna ongezeko la vitu ambavyo havipo kwenye android 11
Kwa mfano toleo jipya la android inaweza kukuonyesha app ambazo zinatumia kamera
Hivyo inakuwa ni rahisi kujua app usiyoitambua ambayo inachota taarifa zako
Yapi Madhaifu ya samsung galaxy s22+ 5g
Changamoto kubwa ya galaxy s22+ ni uwezo wake mdogo wa kukaa na chaji
Ukitazama iphone 13 pro max ina betri dogo zaidi ya hii samsung
Lakini iphone inaweza kukaa na chaji masaa 18 simu ikiwa kwenye intaneti
Wakati galaxy s22+ ni masaa 14
Hii simu haiji na chaji
Mnunuaji atalazimika kununua pesa ya ziada kununua chaji yake
Neno la Mwisho
Kama una bajeti inayotosheleza na unapenda simu bora, galaxy hii itakufaa
Kama ukiagiza toka amazon bei ya samsung galaxy s22+ ni ya chini zaidi ya hapa Tanzania
Maoni 2 kuhusu “Bei ya Simu Mpya ya Samsung Galaxy S22+ 5G na sifa zake”
Nashindwa kuingia mtandaoni hii simu nifanyaje!!??
Angalia kama umetengeneza access point