SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

Bei ya Samsung Galaxy A51 na Sifa Zake Muhimu (2023)

Sifa za simu

Sihaba Mikole

July 5, 2023

Simu ya samsung galaxy a51 ina miaka karibu minne tangu imetoka mwaka 2019

Ni simu ya daraja la kati hivyo bado inaweza kutumika bila shida mwaka 2023

Kiujumla ni kwamba sifa nyingi za samsung galaxy a51 zinazizidi baadhi ya simu mpya za mwaka huu

Uzuri ni kuwa bei ya samsung galaxy a51 kwa sasa haifiki laki tano kwa maeneo mengi hapa Tanzania

Bei ya Samsung Galaxy A51 ya GB 128

Kwa hapa Tanzania simu inauzwa kwa shilingi laki nne (420,000)

Kwa bahati mbaya simu ni used kwa maana ni ngumu kwa sasa kuipata ikiwa mpya kabisa

Hivyo ni muhimu kuikagua kwa ustadi kutambua hali yake ya sasa ili usiuziwe kitu ambacho kitakusumbua mbeleni

Ukinunua kwa mtu mkononi unaweza ipata mpaka kwa laki tatu ila umakini unatakiwa

Sifa zake kuanzia kamera, kioo, utendaji na hata memori zinaifanya bei yake ya sasa kuwa shindani na matoleo mapya

Sifa za Samsung Galaxy A51

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g, 4g
Processor(SoC)
  • CPU – Exynos 9611
  • Core Zenye nguvu(4) – 4×2.3 GHz Cortex-A73
  • Core Za kawaida(4) – 4×1.7 GHz Cortex-A53
  • GPU-Mali-G72 MP3
Display(Kioo) Super AMOLED
Softawre
  • Android 10
  • One UI 5
Memori UFS 2, 256GB,128GB,64GB na RAM 8GB,6GB,4GB
Kamera Kamera nne

  1. 48MP,PDAF(wide)
  2. 12MP(ultrawide)
  3. 5MP(macro)
  4. 5MP(depth)
Muundo Urefu-6.5inchi
Chaji na Betri
  • 4000mAh-Li-Po
  • Chaji-15W
Bei ya simu(TSH) 420,000/=

Upi ubora wa Samsung Galaxy A51?

Simu imegawanyika kwenye matoleo mengi ya memori na pia kwa ukubwa RAM

Kama bajeti ni ndogo unapata nafasi ya kuimiliki yenye memori na ram ndogo

Ina kamera inayotoa picha vizuri ukilinganisha pia na baadhi ya simu za mwaka 2023

Inakubali kupokea toleo jipya kabisa la android 13 kitu kinachoipa thamani na uhai wa kutumika muda mrefu

Ina utendaji wa wastani na ukaaji wa chaji ni wa kiwango cha kuridhisha ikiwa mpya

Pamoja na ubora wake ni vizuri ukaifuatilia kwa kila kitu kwa sababu kuna baadhi ya vitu vilivyopo kwenye simu za sasa hii simu haina

Uwezo wa Network

Samsung Galaxy A51 inakubali mpaka mtandao wa 4G kama kiwango cha juu

Haina uwezo wa kutumia teknolojia ya 5g maana ni simu ya kitambo

Aina ya 4G inayotumia ni LTE Cat 12 ambayo kasi yake ya kupakua vitu ni 600Mbps

Na kasi ya kupakia(upload) vitu ni 150Mbps ambayo ni sawa na 18MBps

Kwa maana kama unaweka video ya MB 18 instagram itachukua sekunde moja kumaliza

Hata hivyo kwa Tanzania hakuna mtandao wa simu unaotoa kasi ya 600Mbps mpaka hivi leo ikiwemo mitandao yenye 5G

Mitandao yenye 5G hapa nchini ni Tigo na Vodacom kwa baadhi ya maeneo

Ubora wa kioo cha Samsung Galaxy A51

Kioo halisi cha samsung galaxy a51 ni super amoled

Amoled ni vioo ambavyo vinaundwa na materio yenye kutoa mwingi bila kutumia taa za led

Kitendo hiki husaidia vioo vya amoled kuzalisha rangi halisi kwa kiwango kikubwa hasa rangi nyeusi huwa inakorea sana

Kioo chake kina resolution kubwa ya 1080 x 2400 pixels

Hii inakuhakikishia muonekano nadhifu wa vitu vinavyoonekana kwenye skrini

Kioo cha hii simu inakosa teknolojia zingine kama HDR10

Hata bado ni kioo kizuri

Kwa kuwa ni amoled basi jua kuwa bei ya kioo cha samsung a51 ni kubwa hivyo kuwa makini

Nguvu ya processor Exynoss 9611

Katika kufanya kazi zake Samsung Galaxy A51 inatumia processor ya Exynoss 9611

Imegawanyika katika sehemu mbili

Sehemu ya kwanza inahusisha core zenye nguvu ambazo zipo nne

Core hizo zinatumia muundo wa Cortex A73

Kwa sasa Cortex ni muundo ambao utendaji haupo kwenye kundi la processor zenye nguvu

Ndio maana magemu mengi yanacheza kwa fremu chache kwenye ubora wa juu wa graphics

Na sehemu yenye core ndogo zinatumia muundo wa Cortex A53

Simu za siku hizi zinatumia mfumo ulioboreshwa zaidi wa Cortex A55 wenye matumizi madogo ya betri na utendaji mkubwa

Uwezo wa betri na chaji

Betri ya samsung a51 ina ukubwa wa 4000mAh

Ukaaji wa chaji unachukua masaa 13 simu ikiwa inaperuzi intaneti muda wote

Chaji yake inapeleka umeme mdogo wa wati 15

Hivyo betri inaweza kujaa kwa 100% baada ya masaa masaa mawili na dakika 14

Simu nyingi za android za hivi karibuni zinakuja na chaji yenye uwezo wa kupeleka wati 33

Ambapo kujaa ni swala dakika 70 tu

Kama kasi ya chaji haina tatizo, samsung itakufaa kuwa nayo

Ukubwa na aina ya memori

Samsung Galaxy A51 inatumia memori aina ya UFS ambazo huwa zinasafirisha data kwa kasi

Kuna matoleo yapatayo matano upande wa memori

Kuna yenye GB 64, 128, na 256 pia RAM zipo za GB 4, 6 na 8

Yenye memori bei ni kubwa ambayo inaweza kuzidi laki tano

Na yenye memori ndogo bei yake ni ndogo

Ila simu inaweza kuwahi kujaa kama unadownload app na vitu vingine vingi

Uimara wa bodi ya Samsung Galaxy A51

Bodi ya Samsung Galaxy A51 ni imara kwa kiasi fulani

Kwa maana upande wa mbele imewekewa Gorilla Glass 3

Gorilla Glass 3 ni kigumu kuchunika ila kikianguka kwa kimo fulani kinapasuka kwa uwepesi

Vioo ambavyo huwa na ugumu wa kutopasuka kwa wepesi ni Gorilla glass 5 angalau

Upande wa nyuma simu imewekewa plastiki

Hivyo ni vizuri ukwa unaweka kava mara kwa mara

Ubora wa kamera

Ubora wa kamera ni wa kuridhisha kwa kiasi fulani hasa kamera yake kubwa yenye megapixel 48

Kwenye mwanga picha zinatokea vizuri japo changamoto kidogo kwenye usahihi wa rangi

Inahitaji utaalamu sana kujua kasoro hiyo

Vinginevyo unaweza usiitofautishe ubora wake wa picha na simu ya apple iphone 13 pro max

Aina ya kamera nyingine ambayo ipo ni ya Ultrawide maalumu kwa kupiga eneo kubwa kama vile kiwanja cha mpila kitokee chote

Hata hivyo ni kamera moja tu ndio yenye teknolojia ya ulengaji wa PDAF zingine hazina

Iwapo utapiga picha kitu kinachokimbia kutumia kamera ya ultrawide itakubidi uwe mwepesi sana kupiga picha ili kitokee vizuri

Maana hizi teknolojia za ulengaji husaidia kwenye maswala kama hayo, kulenga kitu moja kwa moja bila wewe kutumia nguvu kubwa

Kitu cha kufurahisha ni kuwa simu inaweza kurekodi video za 4K

Ubora wa Software

Ikiwa mpya samsung a51 inakuja na android 10

Ila ina uwezo wa kupokea toleo jipya kwa sasa ambalo ni Android 13 na One UI 5

Kitendo cha kupata toleo jipya la android kunafanya A51 kuwa simu nzuri hata kwa mwaka 2023

Maana kuna simu zilizotoka mwaka 2019 hazikuwahi kupata matoleo mapya ya android

Washindani wa Samsung Galaxy A51

Washindani wa sasa wa Samsung Galaxy A51 ni Tecno Camon 20

Tecno Camon 20 ina bei inayoendana na hii samsung kwa sasa

Na inatumia processor yenye nguvu inayoweza sukuma gemu nyingi pasipo na shida

Na mshindani mwingine anaeweza kukushawishi kughairi kuinunua ni Redmi Note 12 Pro 5G

Redmi inauzwa chini ya laki tano na ina mtandao wa 5G

Na pia inatumia kioo cha amoled kama ilivyo hii samsung

Neno la Mwisho

Pamoja na ukweli kuwa Samsung Galaxy A51 ni simu ya zamani kitendo cha kupata toleo jipya la android linaipa thamani mpya kwa sasa 2019

Simu hii utaipata ikiwa used kwa uwezekano mkubwa kwa sasa hivyo ikague vizuri

Bei yake ni rafiki na inavumilika kwa watu wengi hapa nchini

Maoni 2 kuhusu “Bei ya Samsung Galaxy A51 na Sifa Zake Muhimu (2023)

  • Samsung A51 ni mzur kwakwel illa kasolo yakke ni kua sijapaona seems ya kulekod wakat unaongea na mtu zaid ya screen record tu ila ni smu mzr na naflaiya maisha kupitia ihii Samsung A51

Maoni na Maswali

Email yako haitochapishwa, kwenye alama * lazima pajazwe ili ukomenti

Related Articles

samsung galaxy note20 thumbnail

Bei ya Samsung Galaxy Note 20 Ultra 5G na Sifa Zake 2023

Simu ya Samsung Galaxy Note 20 Ultra ni samsung ya mwaka 2020 Japo ina miaka ipatayo mitatu tangu itoke ila ni moja samsung kali mpaka wakati huu wa sasa Bei […]

iphone feki 2

Simu Origino ni Zipi na Unazitambuaje? (Hatua za kufuata)

Matoleo ya simu yamekuwa yakitoka mara kwa mara yakiwemo yenye bei kubwa na zinazotamaniwa na watu wengi Aina hizi ya simu huvutia watu wasio waaminifu kutengeneza simu feki zenye ufanano […]

Bei ya sasa ya Samsung Galaxy S10 5G na Sifa Zake

Samsung Galaxy S10 5G ni simu ya mwaka 2019 iliyopo kwenye kundi la daraja la juu kwa wakati huo Ni simu ya mwanzo kuja na teknolojia ya 5g. Japokuwa ina […]

simu za bei rahisi

Simu used za bei rahisi za madaraja ya kati na juu

Kuna simu za bei kubwa ambazo zilizotoka miaka ya nyuma na kwa sasa hazipatikani zikiwa mpya Matoleo yake yalikuwa yanalenga watumiaji wanaopenda vitu vya gharama hivyo kuwa na vitu vingi […]

SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

E-mail : simunzuriblog@gmail.com

Simu: +255 624 213 048

Whatsapp: +255 756 077 262

Kabila, Magu

Mwanza, Tanzania

Company

Find Us On

FB Twitter Instagram