Kampuni ya Xiaomi toka China ilitangaza ujio wa Redmi Note 12 mnamo mwezi januari mwaka 2023
Ni toleo baada ya simu ya daraja la kati Redmi Note 11 hivyo kuna maboresho kiasi fulani
Maborsho yanayoifanya bei ya Redmi Note 12 kutokuzidi shilingi laki tano kutegemeana na ukubwa wa memori
Kwenye posti hii utazifahamu sifa zake zote muhimu na simu kutoka kwenye kampuni zingine zinazoendana kisifa na hii redmi
Bei ya Redmi Note 12 ya GB 128
Kwa Tanzania Redmi yenye ukubwa wa memori ya GB 128 inapatikana kwa kiasi cha shilingi 490,000/=
Ukizitazama sifa za simu hii na kulinganisha na simu zingine utagundua bei yeke ni nafuu
Ni mara chache kama sio ngumu kupata toleo la simu yenye kioo cha amoled, 5g, chaji yenye kasi na mfumo memori wenye nguvu kwa bei ya chini ya laki tano
Unaweza kuliona hili kwenye mfano wa simu ya Samsung Galaxy A34, ina bei kubwa.
Sifa za Redmi Note 12
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g and 5g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | AMOLED, Refresh rate:120Hz |
Softawre |
|
Memori | UFS 2.2, 256GB,128GB na RAM 8GB,6GB,4GB |
Kamera | Kamera TATU
|
Muundo | Urefu-6.67inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 490,000/= |
Upi ubora wa Redmi Note 12
Simu ina kioo chenye refresh rate inayozidi 100Hz
Inakuja na chaji yenye kasi kubwa ya kupereka chaji
Betri yake inakaa na chaji masaa mengi kwani ni kubwa
Kamera zake zinatoa picha nzuri bila kuharibu uhalisia wa rangi halisi za vitu vilivyopigwa picha
Ina utendaji mkubwa wa kuweza kila aina ya appliksheni bila shida
Kioo chake kina uwezo wa kuonyesha rangi nyingi kiasi cha kwamba vitu vingi vitaonekana kwa uhalisia wake
Ni simu ndefu na inakuja na kioo cha kinachoweza kuzuia michubuko
Japo simu ina kamera nzuri kwa kiasi kikubwa ila kuna kasoro kiasi ambayo utaiona baadae
Uwezo wa Network
Redmi note 12 inasapoti mtandao mpaka wa 5G
Inasapoti masafa ya 5g yapatayo matano ila yote ni masafa ya chini yaani low bands 5G
Ambapo inakuwa na tofauti ndogo na 4G kwenye spidi na uharaka wa muitikio(latency)
Faida ya masafa ya chini upande wa 5G ni kupenya kwenye kuta bila shida
5G yenye kasi kubwa (masafa ya juu) hukumbana na ugumu wa mawimbi kupenya kirahisi
Hivyo kasi hupungua ukiwa ndani ya nyumba
Kwa mitandao ya Vodacom na Tigo wana Masafa ya Kati
Upande wa 4G inakubali 4G aina ya LTE Cat 18 yenye kasi inayofika 2500Mbps
Ubora wa kioo cha Redmi Note 12
Kioo cha Redmi Note 12 ni aina ya AMOLED ambacho kina refresh rate ya 120Hz
Kiwango cha refresh rate ya 120Hz kinaifanya simu kuwa na mwitikio wa haraka wakati unagusa
Na hivyo hufanya kuscroll(kugusa simu kwa kupeleka juu na chini) kuwa mzuri hasa ukiwa unaperuzi vitu
Ubora wake wa kioo unaongezewa na uwepo wa kiwango kikubwa cha resolution ya 1080 x 2400 pixels
Ujazo mkubwa unasaidia simu kuwa na mkorezo mzuri wa rangi zilizokorea vizrui bila kuwa na muonekano wa kupauka
Kioo kina uangavu unaosaidia vitu kuonekana vizuri ukiwa unaitumia kwenye jua
Kwani kiwango chake cha uangavu kwa kipimo cha nits kinafika 1200
Kwenye kuchunika simu inaweza kustahimili kwa sababu ina skrini protekta ya toleo la Gorilla 3
Nguvu ya processor Snapdragon 4 Gen 1
Kiutendaji simu ina nguvu ya kufungua applikesheni za aina nyingi kutokana na kutumia processor ya Snapdragon 4 Gen 1
Snapdragon 4 Gen 1 imegawanyika katika sehemu mbili ambapo sehemu yenye nguvu ina core mbili zenye kasi inayofika 2.0GHz
Muundo wa hizi unaotumia ni Cortex A78 ambayo nguvu yake ni kubwa na pia ulaji wa chaji ni wa kiwango kidogo
Hata hivyo utendaji wa snapdragon 4 gen 1 ni wa wastani ukilinganisha na simu za Samsung Galaxy S23 au iPhone 14 Pro Max
Ila ni utendaji endapo utaieka kwenye kundi moja na Tecno Spark 10 pro
Upande wa kucheza magemu simu ina utendaji wa wastani
Kutokana na gemu kubwa nyingi kama PUBG kucheza kwa 30fps kwenye resolution kubwa
Ila iwapo utaseti resolution ndogo za graphics kiwango cha fremu kitapanda kwa gharama ya kupungua ubora wa picha
Uwezo wa betri na chaji
Betri ya Redmi Note 12 ina ujazo wa 5000mAh na aina ya Li-Po
Ukiwa unaperuzi intaneti masaa yote simu itadumu kwa kipindi cha muda wa masaa 13
Inakuja na chaji yenye kasi ya wati 33 ambayo inachukua dakika 68 tu kujaza simu kutoka 0% mpaka 100%
Kiwastani utunzaji wa chaji ni kiwango cha kawaida hasa ukiilinganisha hii simu na Samsung Galaxy 34 ambayo inakaa zaidi ya masaa hayo.
Uwezekano ni kwamba mfumo wake wa software ukawa unachangia matumizi ya ziada ya chaji
Hata hivyo masaa kumi na tatu ukiwa kwenye intaneti ni mengi
Na ukizingaitia simu inawahi kujaa chaji kwa dakika chache
Ukubwa na aina ya memori
Simu ipo na matoleo mawili upande wa memori
Aina ya memori iliyotumika ni UFS 2.2 ambayo kasi ya kusafirisha data inafika 1200MBps
Hivyo ukiwasha simu itawahi kuwaka na app kufunguka kwa haraka
Unaweza kupata redmi ya GB 128 kwa RAM ya 4GB au 6GB
Na pia yenye GB 256 mabayo RAM yake ni 8GB
Yenye memori kubwa bei yake ni kubwa vile vile kwa mtumiaji ambaye GB 128 ni ndogo atalazimika kuongeza pesa ya ziada kupata ya GB 256
Uimara wa bodi ya Redmi Note 12
Upande wa nyuma simu ina plastiki na mbele kuna kioo cha gorilla 3
Gorilla 3 ni kioo imara kuzuia michubuko ila sio kupasuka, ukiangusha simu kwenye eneo baya simu inapasuka
Ila kama umeweka funduo na simu kwenye mfuko mmoja kukwaruzika hakutotokea
N i tofauti na vioo vya Gorilla 5 au Victus
Maji ya kiwango cha kuchuruzika hayawezi kupenya ndani ya simu kwa sababu ina viwango vya IP53
Hivyo ukiizamisha ndani ya kina cha mita moja maji yatapenya ndani ya simu kwa muda mfupi
Kiujumla, umakini unahitajika kwani uimara wake sio sawa na simu kama Xiaomi 13 Pro
Ubora wa kamera
Idadi ya kamera kwenye redmi note 12 zipo tatu huku kamera kubwa ikiwa na megapixel 48
Kamera nyingine ni kwa ajili ya kupiga eneo pana inafahamika kama ultrawide na ina megapixel 8
Na kamera ya mwisho kwa ajili ya kupiga kitu kilicho karibu sana na kamera ina megapixel 2 na hufahamika kama macro
Nyakati za mchana ambapo mwanga ni wa kutosha picha zinatokea vizuri
Kuna kiwango kidogo cha noise kinaonekana kama ukiikuza simu kidogo
Ila uhalisia wa rangi za vitu vilivyopigwa picha ni wa kiwango cha kuridhisha
Kamera yake inaweza kurekodi video za full hd pekee kutokana na processor yake kutokuwa na uwezo wa kuchakata video za 4K
Ubora wa Software
Redmi Note 12 inakuja na Android 12 na mfumo wa MIUI 14
Ukiwa na MIUI utakutana na mfumo wa kuscan app pindi ukimaliza kuidownload kutoka play store
Mfumo huo unalenga kutambua uwepo wa virusi kwenye app inayowekwa
Kitu kimoja ambacho kitakukela kwenye MIUI ni swala la matangazo
Kuna matangazo japo si ya kukera kama yale yanayokuja kwa mtindo wa notification
Calculator ya MIUI ina sehemu ya kutazama thamani za sarafu mbalimbali duniani
Washindani wa Redmi Note 12
Jambo ngumu ni kupata simu yenye sifa sawa na redmi note 12 kwa bei ya chini ya laki tano
Ila wapo washindani wenye sifa za ziada zinazokosekana kwenye Redmi Note 12 kwa bei zinazokaribiana kwa kiasi
Kuna Samsung Galaxy A33 5G.
Samsung Galaxy A33 5G ni samsung isiyopitisha maji ukiizamisha kwenye maji ya kina cha mita moja kwa muda wa nusu saa
Na pia ina kioo kigumu kupasuka cha Gorilla 5, na bei yake ni shilingi laki sita na sabini
Mshindani mwingine ni Xiaomi Pocco X5
Pocco X5 inakaribiana vitu vingi na redmi note 12 japo redmi inaizidi kidogo kwenye utendaji
Poco bei yake ni ndogo zaidi na inapatikana chini ya laki tano na bado pia ni simu ya 5G
Neno la Mwisho
Yote ya Yote ni kuwa sifa za redmi note 12 inaifanya kuwa ni simu ya 5g yenye bei ndogo
Mtumiaji anayependa simujanja yenye nguvu ya kuridhisha hawezi kusita kuimiliki hii
Iwapo unahitaji vitu vingine vya ziada zaidi basi kuna washindani wake wenye bei zinazokaribiana kiasi fulani
Maoni 5 kuhusu “Bei ya Redmi Note 12 na Sifa Zake Muhimu”
Kiukwel xm ni nzur lakn bei ghali xana afadhal ingekua 400,000
Inategemeana na maduka Mimi nimenunua 420,000tzs Kwa Xiaomi agent
Kweli cm n nzur tatzo n bei yake kuwa kubwa
Cm ninzuri mm nmeikubali Sana sema Bei kwangu nikubwa Sana Bora
Natumia iko poa Sana mwenyewe anahitaji Niko makambako nichek 0757525170