Simu ya Redmi 10A iliiingia sokoni mwaka 2022
Ni aina ya simu inayolenga watu wenye matumizi ya kawaida kama sio machache
Hivyo bei ya Redmi 10A ni chini ya laki tatu kwa hapa Tanzania
Kutokana na aina ya sifa ilizo nazo haifai kuuzwa kwa bei inayozidi laki tatu
Fuatilia kiundani kutambua jinsi sifa zake zinavyofanya bei yake kuwa ndogo na ujue kama inakufaa ama haikufahi
Bei ya Redmi 10A ya GB 64
Redmi 10A yenye ukubwa wa GB 64 inapatikana kwa shilingi 250,000
Hii ni bei ya mwaka 2023
Redmi 10A zenye ukubwa zaidi ya huo bei inakuwa zaidi ya hapo
Baadhi ya vitu vinavyofanya bei kuwa ndogo ni ubora mdogo kwenye kamera, utendaji na hata kioo
Hata hivyo, kwa mtumiaji wa kawaida simu inayoweza kukidhi mahitaji yake na anaweza asione shida yoyote
Tatizo tu linakuja kwa mtu anayetaka simu ya kupiga picha nzuri ndio atakutana na changamoto kwenye kamera
Sifa za Redmi 10A
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | IPS LCD |
Softawre |
|
Memori | eMMC 5.1,128GB,64GB,32GB na RAM 3GB,6GB,4GB |
Kamera | Kamera moja
|
Muundo | Urefu-6.5inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 250,000/= |
Upi ubora wa Redmi 10A
Inakuja na machaguo matatu moja ikiwa na memori kubwa yenye kutosheleza kuhifadhi vitu vingi
Uzuri ni kuwa bei yake inavumilika
Ina ukaaji wa chaji wa masaa mengi kwa sababu ya betri kubwa na utendaji unaotumia moto kidogo
Ni moja ya simu ya 4G yenye bei ndogo
Kama ilivyoelezwa mwanzoni, redmi 10a ni ya daraja la chini, vitu vingi vilivyopo havina ubora mkubwa
Yapo mambo yanayoweza kukidhi mahitaji yako kama ukiziangalia sifa zingine kiundani
Uwezo wa Network
Redmi 10A inasapoti mpaka mtandao wa 4G kama kiwango cha juu
4G ina kasi ya wastani inayofika 300Mbps ya kupakuwa vitu
Aina hii 4G huitwa LTE Cat 7
Kasi ya kawaida ila kwa Tanzania hakuna mtandao wenye kasi hii kwa upande wa 4G
Hii inamaanisha kwa mazingira ya nchini simu bado inafaa
Kwa maana kasi za mitandao ya simu huwa ni chini 100Mbps hata kama eneo lina watu wachache wanaotumia intaneti
Ubora wa kioo cha Redmi 10A
Ubora wa kioo cha redmi ni wa kawaida kutokana na kutumika kwa teknolojia ya IPS LCD
IPS LCD haina ubora mkubwa wa uwasilishwaji wa rangi ukilinganisha na vioo vya AMOLED
Kama ukitazama picha moja kwenye simu yenye kioo cha lcd na amoled, amoled, picha huonekana vizuri sana
Mbali na kuwa na kioo cha IPS LCD, na resolution sio kubwa ambayo ni 720 x 1600 pixels
Uangavu wake pia ni wa kiwango kidogo cha nits 400
Kwa maana kwenye jua kali sana mwanga kwenye kioo unakuwa sio wa kiwango cha kuonesha vitu vizuri
Nguvu ya processor Mediatek Helio G25
Nguvu ya processor mediatek helio g25 kwa ajili ya kufanya kazi kwenye vitu vinavyotumia nguvu ndogo
Linapokuja swala la vitu vinavyotumia nguvu kubwa hii simu haitokupa kitu kizuri
Nguvu ndogo ya processor yake ina sababishwa na kutumiwa kwa muundo aina ya Cortex A53 kwenye core zote nane
Cortex A53 ni muundo unaowekwa kwenye chip kwa ajili ya kutumia umeme kidogo kwa gharama ya utendaji wa chini
Ndio maana hii simu inakaa na chaji muda mrefu
Kwa mtu ambaye matumizi yake ni kupiga simu na intaneti kidogo haitaji sana processor yenye nguvu kubwa
Ila kumbuka processor ndio ubongo wa simu ikiwa duni vitu vingine vyote vinakuwa chini moja kwa moja
Uwezo wa betri na chaji
Chaji ya Redmi 10A ina uwezo wa kupeleka chaji kwa kasi ya wati 10
Ni kiwango kinachozaja betri ya 5000mAh kwa masaa yanayozidi matatu
Betri yake ya 5000mAh ina ukaaji wa masaa mengi yanazidi 14 kama hutumii intaneti mara kwa mara
Pia soc yake inatumia umeme kidogo sana na vifaa vingine vina matumizi madogo
Hivyo kwa mtu anaeishi maeneo yenye changamoto ya umeme hii simu ni msaada mzuri
Ukubwa na aina ya memori
Kuna matoleo ya aina sita kwenye upande wa memori na ram
Kiwango kikubwa cha RAM ni GB 6 na memori ya kuhifadhi vitu ni GB 128
Kwa bahati mbaya bei inaongezeka kutokana na ukubwa wa memori
Kama utakuwa ni mtu wa kupakuwa sana mafaili, memori ya GB 128 inafaa zaidi
Iwapo kipato ni changamoto sana basi ya GB 32 inatosheleza kwa sababu bei yake ni 170,000
Uimara wa bodi ya Redmi 10A
Bodi ya redmi 10a ni ya plastiki
Haina uimara wa kuzuia maji kama simu ikiingia ndani ya maji
Kwani haina viwango IP vinavyoainisha uwezo wa kuzuia maji pindi simu ikizamishwa kwenye kina fulani
Kiujumla ni muhimu kuweka skrini protekta kwa sababu simu haina ulinzi wa aina yoyote ya kioo
Hivyo kuimarisha simu ikae muda mrefu huna budi kuwa na kava na protekta ya skrini
Ubora wa kamera
Hii simu haina mfumo mzuri wa kamera kiujumla
Ina kamera moja tu yenye megapixel 13 huku ikiwa na ulengaji wa kiwango duni ya AF
Hivyo ubora wa picha hasa kwenye mwanga hafifu sio mzuri
Upande wa video kamera yake inaweza kurekodi video za full hd pekee yake kwa kiwango cha 30fps
Hii inatokana na aina ya processor kutokuwa na nguvu ya kutosha kuchakata data za kutosha
Ubora wa Software
Redmi 10A inatumia android 11 na haina uwezo wa kupokea toleo jipya la android 13
Hata kwenye matoleo ya android ya miaka ya karibuni kumekuwa hakuna tofauti kubwa sana
Tena kwa redmi unaweza usione tofauti yoyote
Mbali na android 11 simu inakuja na mfumo wa android 12.5
MIUI ina vitu vingi kwa mfano app yake ku-screenshot inaweza kuchukua peji kwa urefu unaotaka wewe
Kwa sababu yenyewe inaruhusu ku-scroll
Kitu utakachochukia kwenye MIUI ni matangazo japo sio yale ya kukela
Ila karibu app zote za MIUI huwa zina matangazo
Washindani wa Redmi 10A
Mshindani wa kwanza Redmi 10A ni infinix hot 20i
Infinix hot 20i imetumia vitu vyote vilivyotumika kwenye redmi 10a
Ila hot 20i inakuja na android 12 yaani toleo la mbele ya android
Na bei ya infinix ni sawa na ya redmi
Bingwa mwingine ni Samsung Galaxy A04
Japo yenyewe bei yake ipo juu kidogo ila inaruhusu kupokea android 13 ambalo ni jipya
Kwenye simu hakuna kitu cha muhimu kama kupata sapoti ya software
Neno la Mwisho
Redmi 10A ina bei ya kizarendo ila usitarajie makubwa sana
Kiukweli na kiuharisia simu nzuri kwenye kampuni yoyote huuzwa bei kubwa angalau laki tatu kwenda mbele
Ila kama hii simu unamnunulia mtu mfano mama au baba ambaye kijijini hili ni chaguo zuri kwake
Maoni 3 kuhusu “Bei ya Sasa ya Redmi 10A na Sifa Muhimu”
Je naweza kulipa kidogo kidogo mpaka mimalize
Ni mm Aly ukasha saluwa maoni yanga Ni kuwa je inawezekana kilipia simu kidogo kidogo mpaka mimalize ndio niweze kutumiwa simu yangu ndani ya miez mitatu
Unapatikana mkoa gani