Oppo A17K ni simu iliyotoka mwishoni mwa mwaka 2022 mnamo mwezi oktoba
Ni simu ya daraja nafuu ambayo haihitaji bajeti kubwa kuimiliki
Kwani bei ya oppo A17K haizidi laki tatu na nusu, ni moja ya oppo za bei nafuu
Kikawaida aina hii ya simu hufaa kwa matumizi ya kawaida kama kupiga simu, kuingia instagram nk
Hii inatokana na aina ya memori na chip inayotumiwa na hii simu kama utakavyoona kwenye maelezo yaliyomo
Bei ya Oppo A17K ya GB 64
Oppo A17K kwa sasa inauzwa shilingi laki tatu na elfu thelathini (330,000/=) ikiwa mpya
Kwa ambayo imeshatumika inapatikana chini ya laki tatu
Kwa kulinganisha na oppo zingine bei ya hii simu ipo kwenye kundi la oppo za bei nafuu
Japo kiutendaji haipo kwenye kundi moja kabisa na Oppo Reno8 ambazo ni simu za daraja la kati
Kwa maana usitarajie mambo makubwa sana kutoka kwenye hii kutokana na kuwa na sifa za kawaida
Sifa za Oppo A17K
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | IPS LCD |
Softawre |
|
Memori | eMMC 5.1, 64GB na RAM 3GB |
Kamera | Kamera moja
|
Muundo | Urefu-6.56inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 330,000/= |
Upi ubora wa OPPO A17K
Simu ina betri kubwa inayoweza kukaa na chaji muda mrefu
Inatumia umeme kidogo sana kitu kinachoipa simu uwezo wa kukaa na chaji masaa mengi
Inasapoti mtandao wa 4G japo siku hizi karibu simu zote zina hii teknolojia
Ni simu pana na ndefu inayofanya vitu kuonekana kwa ukubwa
Vitu vingine ni vya kawaida ubora wake sio wa viwango vya juu.
Uwezo wa Network
Hii simu inasapoti mpaka mtandao wa 4G na haina uwezo wa 5G
Aina ya 4G inayosapoti ni LTE Cat 7 yenye kasi ya kupakuwa vitu inayofika 300Mbps
Na kasi ya kupakia(ku-upload) vitu ni 150Mbps
Hizi ni kasi kubwa ambapo kwa hapa Tanzania ni nadra sana kuipata
Na kama kuna mtandao unaotoa hii basi gharama yake ni kubwa na pia ni kasi ya 5G
Ina masafa yote yanayotumiwa na mitandao ya simu nchini hivyo intaneti itashika bila shida
Ubora wa kioo cha Oppo A17K
Hii oppo inatumia kioo cha IPS LCD chenye resolution ya 720 x 1612 pixels
Hii resolution sio kubwa kwani muonekano wa vitu hautokuwa na ubora mkubwa kama ulivyo kwenye vioo vya amoled na oled
Uangavu wake unafika nits 600, ni kiasi cha kuridhisha cha kukupa mwangaza mzuri ili uweze kuona vitu ukiwa unatumia simu juani
Unajua simu ukiwa unatumia nje mahala pasipo kuwa na kivuli inakuwa ni shida kuona kwa ustadi
Ila simu yenye nits nyingi inaepusha hilo tatizo
Nguvu ya processor ya Mediatek Helio G35
OPPO A17K inatumia processor ya mediatek helio g35
Helio G35 imegawanyika katika sehemu 8, na sehemu zote zinatumia muundo unaojulikana kama Cortex A53
Cortex A53 ni muundo wenye nguvu ndogo na ni wa kitambo kwa sasa
Hii inamaanisha nguvu na uharaka wa simu katika utendaji ni mdogo kwa kazi zinazohitaji nguvu kubwa
Ndio maana gemu kama la PUBG linacheza kwa kiwango cha 25fps kwa kutumia mpangilio wa graphics za viwango vya chini
Yaani kama ukicheza kwa ultra hd simu inaweza kuanza kukwama kwama
Uwezo wa betri na chaji
Ukubwa wa betri ya Oppo A17K ni 5000mAh
Ni betri kubwa na ukaaji wa chaji unaweza ukamaliza masaa zaidi ya 10 ukiwa kwenye intaneti muda wote
Haina mfumo unaopeleka umeme kwa kasi kubwa
Kwa maana chaji yake inapeleka taratibu inayoweza chukua masaa mengi mpaka kuchaji kwa 100%
Ukubwa na aina ya memori
Memori ya oppo a17k ipo ya aina moja na yenye ukubwa wa GB 64
Na RAM yake ina ukubwa wa GB 3
Aina ya memori inayotumiwa ni eMMC, ambazo huwa zina kasi ndogo zinaposafirisha data
Hazina kasi kubwa kama ilivyo memori aina za UFS
Siku hizi simu nyingi hutumia memori za UFS, ukubwa wa memori unaweza kukulazimu kuweka memori kadi ya ziada
Kwa sababu apps huwa zinahifadhi data zinazochangia kula memori
Uimara wa bodi ya OPPO A17K
Kwenye upande wa skrini, simu imewekewa skrini protekta
Walau hii inaipa ulinzi simu lakini sio mbaya ukaongezea skrini protekta nyingine
Pia ina ulinzi wa kuzuia maji ya kiwango cha kutiririka kwa kasi ndogo
Kama ukizamisha simu kwenye maji ya kina kirefu, simu itaathirika ndani ya muda mrefu kwani haina IP67
Hivyo umakini unahitajika unapotumia
Ubora wa kamera
Hii simu ina kamera moja tu yenye resolution ndogo ya 8MP
Haina teknolojia ya ulengaji ya PDAF kama ilivyo kwa baadhi ya simu nyingi za bei nafuu
Na inaweza kurekodi video za full hd kwa kiwango cha 30fps
Kiujumla usitarajie ubora mkubwa wa kamera hasa unapopiga picha ukiwa kwenye mwanga hafifu.
Ubora wa Software
Oppo A17K inatumia mfumo endeshi wa Android 12
Kwa sasa kuna toleo jipya la android 14, hakuna uhakika kama itapokea toleo hili jipya au hata la Android 13
Lakini pia OPPO hii inaambatana na mfumo wa ColorOS
ColorOS 12.1 pia inakupa urahisi wa kuinganisha simu na laptop(kompyuta) bila kutumia app nyingine
Washindani wa oppo A17K
Washindani wakubwa wa toleo hili ni simu kutoka Tecno, Infinix, Redmi na Realme
Tecno Spark 10 ina bei na sifa inayoendana na Oppo A17K
Spark 10 inakupa kioo kizuri chenye refresh rate inayofika 90Hz
Na pia ina kamera nzuri yenye resolution inayofika 50MP na yenye PDAF na pia inasapoti chaji yenye kasi inayofika 18W
Kwa mantiki hiyo inaweza ikamfanya mnunuaji kuchagua tecno badala ya hii oppo
Hitimisho
Kwa wapenzi wanaotaka kujaribu simu za OPPO huku wakiwa hawana bajeti kubwa wanaweza kuanza na hii
Lakini ikumbukwe OPPO A17K inalenga watumiaji wasiokuwa na matumizi mengi makubwa na simujanja
Kwa maana kama wewe ni mpenzi sana wa kupiga picha hili linaweza lisiwe chaguo sahihi
Ila kama unataka simu inayotunza moto hii inafaa.
Wazo moja kuhusu “Bei ya sasa ya Oppo A17K na Sifa Zake”
Napataje spea za simu za oppo a7