Simu ya Infinix Smart 6 ni simu ya mwaka 2021 hivyo ni miaka miwili imepita
Kipindi imetoka ilikuwa inauzwa kwa bei nafuu
Kwa maana hiyo bei ya infinix smart 6 kwa mwaka 2023 haizidi laki mbili na nusu.
Ni simu ambayo inamlenga mtumiaji asiyehitaji mambo mengi
Ndio maana ukitazama sifa zake utakutakana na vitu ambavyo vina ubora wa kawaida sana
Bei ya Infinix Smart 6 ya GB 32
Infinix Smart 6 ambayo ukubwa wake ni GB 32 na RAM ya GB 2 inauzwa shilingi 250,000/=
Bei hiyo itatofautiana kutokana na maduka kwa hapa Tanzania
Sehemu zingine simu inapatikana chini ya hapo
Utakapoamua kuimiliki hii simu usitarajie kupata ubora mkubwa kama uliopo kwenye simu mpya za samsung galaxy au tecno za bei kubwa
Ni simu kwa ajili ya matumizi madogo madogo yaani inafaa kuwapa wazazi
Sifa za Infinix Smart 6
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | IPS LCD |
Softawre |
|
Memori | 64GB,32GB na RAM ,3GB,2GB |
Kamera | Kamera nne
|
Muundo | Urefu-6.6inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 250,000/= |
Upi ubora wa Infinix Smart 6
Hii ni simu inayokaa na chaji muda mrefu kwani ina betri kubwa
Na pia ina chip yenye matumizi madogo ya betri
Ni simu ya bei nafuu yenye mtandao wa 4G
Baadhi ya simu za bei nafuu huishia kuweka 3G pekee yake
Ni simu ndefu inayokupa muonekano mkubwa wa vitu
Kama ni mtu unayependa kusoma vitabu, maandishi yake yataonekana kwa ukubwa stahiki
Mambo mengine ni ya viwango vya kawaida kama ilivyotangulia kuelezwa
Uwezo wa Network
Infinix Smart 6 inasapoti mitandao yote mpaka 4G kasoro 5g
Aina ya 4G inayotumia ni LTE Cat 7 yenye kasi ya kudownload 300Mbps sawa na 37.5MBps
Kwa maana kama unaweka whatsapp kwenye simu itachukua sekunde mbili simu kuiweka hiyo app
Spidi hii sio rahisi kuipata kwa nchini kwetu, ila pia ukifananisha na simu nyingine unaona kabisa uwezo wa network sio mkubwa kivile
Inakubali masafa yote ya simu yaliyopo nchini
Hivyo hakuna laini ya simu itakayokwama kutumika
Ubora wa kioo cha Infinix Smat 6
Kioo Cha Infinix smart ni IPS LCD chenye resolution ya 720 x 1600 pixels
Kiwango Cha resolution sio kikubwa na pia vioo LCD huwa sio vizuri hasa kikiwa na resolution
Kwa maana hiyo muonekano wa rangi za vitu hautokuwa wa kuvutia kama ilivyo kwenye vioo vya amoled.
Uangavu wa kioo unafika mpaka nits 500
Hii inamaanisha vitu vinaonekana kwa uzuri kiasi ukiwa unaitumia simu kwenye mazingira yenye miale mingi ya jua
Kioo Cha hii simu Haina vitu vingine kama HDR, refresh rate kubwa nk
Nguvu ya processor Unisoc SC9863A
Simu inatumia processor ya unisoc sc9863a katika kufanya kazi zote
Hii processor imegawanyika sehemu mbili na zote zinatumia muundo wenye nguvu ndogo
Muundo huo wa core huitwa Cortex A55.
Hii chip inakosa nguvu kubwa japo Ina core zinazofika mane
Simu ikiwa na mafaili mengi na app nyingi zikiwa zinajifungua kwa pamoja usishangae ukakutana na simu kuwa nzito
Hii chip sio nziri kwa mpenzi wa magemu makubwa ya mapigano
Hiki kitu kinaifanya simu iwe inamfaa mtu anayetumia simu kwa shughuri za kawaida
Uwezo wa betri na chaji
Betri ya Infinix smart 6 Ina ukubwa wa 5000mAh
Ina chaji inayopeleka umeme kwa Kasi ya wastani ya wati 10
Kwa sababu betri ni kubwa, spidi ya chaji inaijaza betri kwa masaa yanayozidi matatu
Kutokana na simu kuwa na chip yenye nguvu ndogo na kioo chenye resolution ndogo ukaaji wa chaji ni mkubwa.
Simu ikiwa inatumia intaneti inaweza kukaa kwa masaa zaidi ya 14
Ukubwa na aina ya memori
Infinix Smart 6 IPO za aina mbili upande wa memori
Ndogo kabisa Ina GB 32 na Ram ya GB 2
Wakati kubwa Ina GB 64 na Ram ya GB 3
Ni vizuri ukachukua yenye GB 64 kwa sababu ya GB 32 ni ndogo na RAM yake itakuletea shida mbeleni
Mfumo wa android hutumia RAM nyingi na kumbuka kuna kiwango Cha memori kinatumiwa na mfumo endeshi pamoja na app zinazokuja na simu.
Hivyo utakuta kuna kiwango kikubwa Cha memori hutoweza kukitumia
Uimara wa bodi ya Infinix Smat 6
Bodi ya hi simu imeundwa kwa plastiki upande wa nyuma na pembeni
Na Haina viwango vya IP vinavyoonyesha uwezo wa simu kuzuia maji na vumbi kuingia ndani ya simu
Bodi za plastiki wakati mwingine huwa ni rahisi kupoteza rangi zake
Ni vizuri ukawa unatumia kava muda mwingi kuitunza thamani ya simu
Pia ni vizuri kuweka screen protekta kwa sababu simu Haina vioo vigumu kama vya gorilla
Ubora wa kamera
Kamera za Infinix smart 6 zipo mbili ila kiuhakisia kuna kamera moja
Kwa sababu lenzi ya kamera ya pili kazi yake huwa ni kupima kiundani kitu kinachotakiwa kupigwa picha na umbali wa kamera ulipo
Kamera hizi huitwa depth, huwa hazina umuhimu miaka ya Sasa
Kamera ya kubwa Ina megapixel 8 huku ikiwa Haina ulengaji wa PDAF
Kama unampiga picha mtu anayekimbia au gari, picha yake inaweza isitokee vizuri
Mfumo mzima wa kamera sio wa kuridhisha kiuhakisia
Upande wa video kamera zinaweza kurekodi video za full hd pekee
Na pia hakuna OIS kitendo kitachohitaji kutuliza mkono wakati unarekodi kitu huku ukiwa unatembea
Ubora wa Software
Hii simu ingekuwa ni nzito kupitiliza kama ingekuwa inatumia mfumo endeshi wa Android unaotumiwa na simu zingine.
Kuepuka Hilo, Infinix Smart 6 imewekewa mfumo wa Android 11 Go Edition
Go Edition ni mfumo wa android unaowekwa kwenye simu zenye ram na processor zenye nguvu ndogo
Mfumo unasaidia kiasi Fulani hivyo simu kuwa nzito itakuwa ni kwa kiasi kidogo.
Android Go Edition inakuja na vitu ambavyo vimepunguzwa
washindani wa Infinix Smat 6
Kama wewe ni mnunuaji basi inabidi uzifuatilie baadhi ya simu zinazoendana sifa
Simu hizi zina bei zinazoendana na sifa zinazopishana kidogo
Baadhi ni nzuri kuliko smart 6.
Simu hizi ni Samsung Galaxy A02, Redmi 9A, Samsung Galaxy A10 na Tecno Spark 8C
Kwenye hiyo kuna zenye sifa nzuri zaidi na bei ya kuvumilika
Neno la Mwisho
Iwapo wewe matumizi yako ni kupiga simu, kuingia Whatsapp, YouTube, kuwasiliana n wati mbalimbali, hii simu itakupunguzia mzigo wa kumiliki simu janja.
Ila kama kipaumbele chako ni kamera, memori kubwa, magemu na kazi zingine nzito ni Bora ukatafuta chagua mbadala
Tena simunzuri.com imefafanua matoleo mengi na sio mbaya ukauliza nasi tutakujibu kwa kadri ya uwezo wetu.
Maoni 10 kuhusu “Bei ya Infinix Smart 6 na Sifa za Muhimu 2023”
Ndo haina fingerprint
Inayo
Mimi simu yangu ni Inifinx smart 6 Lakin nikichaji inakaa mpk masaa hata sita na haijai shida INAWEZA ikawa ni Nini Maana chaji nimenunua juzi juzi na ni mpya
Inaweza ikawa ina wati ndogo
MImi naitaka wapi wanauziaga
mimi naitaka nipatie wapi
Jamani mim na infinx hot 8lakini ina ganda mala kwamala adi ina jizima na kuj washa niifanueje iludi kama zaman
Hii ni shida ya memori na vifaa vingine kadri muda unavyoenda ndio ubora hupungua, hot 8 si simu nzuri kiivyo kama umesoma maelezo
Me nahitaji infinixy hot 11
Nataka kufaham hii sim Infinix smart 6 inakaa na chaji Kwa muda Gani?