Infinix hot 50i ilitangazwa mwezi septemba na kuingia sokoni rasmi mwezi oktoba 2024
Ni simu ya daraja la chini ila ina maboresho mazuri katika maeneo matatu kama utakavyoona
Bei ya Infinix hot 50i ya GB 128 ni shilingi 310,000 na ya GB 256 inaenda shilingi 350,000
Hii post itakujulisha iwapo simu inafaa kuinunua ama la kwa kuangalia sifa zake za muhimu zaidi kiundani
Twende pamoja.
Sifa za simu ya Infinix Hot 50i
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | IPS LCD, Refresh rate:120Hz |
Softawre |
|
Memori | 256GB,128GB na RAM 6GB,4GB |
Kamera | Kamera MOJA
|
Muundo | Urefu-6.7inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 310,000/= |
Uwezo wa network
Infinix hot 50i ni simu ya 4G na haisapoti eSIM
eSIM ni aina ya laini ambayo haitumii laini za plastiki, bali inakuwa ndani ya simu
Aina ya 4G inayokuja na hii simu ni LTE Cat 7 ambayo kasi yake ya kupakua vitu inafika 300Mbps
Ni kasi kubwa lakini mitandao karibu yote hapa nchini huwa na kasi ya chini ya 100Mbps upande wa 4G
Lakini kama ukiwa kwenye nchi zenye 4G yenye kasi zaidi utaweza kupata kasi hii
Ubora wa kioo cha Infinix hot 50i
Kioo cha infinix hii kina resolution ndogo ambayo sio full hd japo kinaonyesha vizuri
Hii simu imeboreshwa kwenye kiwango cha refresh rate inayofika mpaka 120hz
Kwa bahati mbaya unaweza usione faida ya refresh rate kutokana na aina ya processor inayotumiwa na hii simu
Kwa sababu haina uwezo wa kusukuma fremu nyingi na pia ni nadra kufikia hio refresh rate ya 120hz
Uang’avu wa kioo ni wa wastani kwani kiwango cha nits ni 500
Nits 500 zinasaidia kiasi fulani vitu kuonekana vizuri wakati ukiwa unaitumia simu kwenye mazingira yenye jua jingi
Nguvu ya processor Mediatek helio G81
Hot 50i inatumia processor ya mediatek helio g81 kufanya kazi zake zote
Mediatek helio g81 imegawanyika katika sehemu(cores) nane
Sehemu yenye nguvu kubwa inatumia muundo wa cortex a75 ambao utendaji wake ni wa wastani
Helio G81 inaweza kufanya vitu kwa kasi ya kawaida
Kwa maana inacheza gemu nyingi lakini sio kwa resolution kubwa zenye muonekano mzuri zaidi
Kwa mfano gemu ya PUBG Mobile ikicheza kwenye hii chip inakuwa inacheza kwa frmu chini ya 30fps
Ambazo zinafanya gemu kutokuwa na muonekano mzuri na smooth
Kiujumla ni kwamba processor hii ni kwa ajili ya simu zinazolenga watu wenye matumizi ya kawaida
Na ndio walengwa wa Infinix Hot 50i
Uwezo wa betri na chaji
Kama wewe matumizi yako ni kupiga simu, kutuma sms na kuingia mtandaoni mara chache, betri yake inaweza dumu karibu siku mbili
Kwa sababu betri yake ina ukubwa wa 5000mAh na processor yake haina matumizi makubwa sana ya chaji
Ikizingatiwa imeundwa kwa ajili ya mtumiaji mwenye matumizi ya kawaida
Kasi yake ya kuchaji sio kubwa kwani inapeleka umeme wa wati 18
Hivyo inaweza jaza simu kwa takribani masaa manane
Hata hivyo karibu simu zote madaraja ya chini huwa na kiwango cha chini cha kuchaji simu
Ukubwa na aina ya memori
Kuna matoleo ya aina mbili upande wa memori ambapo kuna yenye ukubwa wa GB 128 NA GB 256
RAM zimegawanyika katika kwenye ukubwa wa GB 6 na GB 4
Kwa mwenye bajeti kubwa ni bora ununue ya GB 256 na RAM GB 6
RAM inasaidia sana kufungua vitu vingi kwa wakati bila kukwama kwama
Lakini RAM ikiwa ndogo simu inakuwa nzito ukiwa umefungua apps nyingi kwa wakati mmoja
Uimara wa bodi ya Infinix Hot 50i
Bodi ya hii simu ni ya plastiki kwenye pande zote na sio titanium kama ilivyo kwa iphone
Sifa mojawapo nzuri ya hot 50i ni uwepo wa waterproof ya viwango ip54
IP54 inamaanisha simu haitopitisha ya kiwango cha kunyunyulizika kwa kizungu inaitwa splash resistant
Kwa hiyo ukizamisha kwenye ndoo yenye maji mengi simu itaharibika ndani ya muda mfupi sana
Kuwa makini
Ni vizuri pia ukanunua na skrini protekta kwa sababu hot 50i haiji na skrini protekta
Kiujumla simu haina bodi imara lakini haishangazi kutokana na aina ya bei
Ubora wa kamera
Infinix Hot 50i ina kamera moja na inapiga picha vizuri kwenye mwanga mwingi
Ila nyakati za usiku kwenye mwanga mdogo ubora wa picha hauvitii
Simu inajitahidi kwenye usahihi wa rangi hasa mazingira ya mwanga mwingi
Kiwango cha noise(chengachenga) sio kikubwa na ni ngumu kuonekana kama hujaikuza picha
Kutokana na nguvu ndogo ya chip, simu inarekodi mwisho video za full hd na sio 4K
Japo kamera yake ina megapixel 48
Ubora wa Software
Simu inakuja na mfumo wa android 14
Hakuna taarifa rasmi iwapo itapokea toleo la Android 15 ambalo ni jipya kwa sasa
Mfumo mwingine unaombatana na Android 14 kwenye hii simu ni XOS 14.5
XOS 14.5 kwa sasa inajaribu kuondoa usumbufu wa notification zinazoweza kukukera wakati ukicheza gemu
Kwa mfano ukiwa unacheza gemu halafu ukapokea meseji ya whatsapp, meseji itaonekana kwa mtindo tofauti ambao hautoziba gemu unalocheza
Washindani wa Infinix Hot 50i
Kwenye miezi ya karibuni kuna simu nyingi zimetoka za bei ndogo
Na zote zinaweza kuwa mbadala wa hot 50i japo sifa nyingi zinaendana
Mshindani wa kwanza ni Redmi 14C, hii inatumia processor sawa na ya infinix ila yenyewe betri lake kubwa zaidi
Bei ya Redmi 14C inashahabiana na infinix hot 50i
Toleo lingine ni la Samsung Galaxy A06 na yenyewe ina utendaji unaoendana na huu
Neno la mwisho
Hii ni simu sahihi sana kwa mwenye bajeti ndogo
Haina vitu vingi vizuri ila inakidihi mahitaji mengi ya mtumiaji wa simu wa kawaida
Lakini kama unataka simu ambayo ipo kamili kila idara hili sio chaguo zuri
Mfano kwenye kamera kuna aina ya lenzi hazipo na haiwezi kurekodi video za 4k
Iwapo unahitaji simu imara sana na yenye ubora mkubwa zaidi huna budi kuongeza bajeti na kutafuta matoleo mengine